Hiyo sio hoja ya msingi kwani Zanzibar ilikuwepo kabla ya muungano na wala zanzibar haitegemei misaada kutoka bara kujiendesha kumbuka kama zanzibar inapata 4.5% hili ikiwa ni gawanyo la kodi ya VAT na misaada kutoka nje na mpaka wawakilishi wapige kelele ndio tupate.Hisa za Zanzibar 11% kuanzishwa kwa EAC ambazo baada ya kuvunjika zilitumika kuanzisha BOT mpaka muda huu Zanzibar haijapata gawanyo lake,sasa najiuliza Wazanzibar wao ndio wanaowanyonya watanganyika au watanganyika ndio wanaowanyonya wazanzibar ,maana tunaona leo makusanyo yote ya VAT na income tax yanaingizwa katika hazina kuu ya JMT na sio SMZ.
Sisi tunasema Wazanzibar kwa muungano huu bora basi,kwani ni muungano uliohodhi vyanzo vyote vya mapato ya nchi yetu mfano BOT,VAT,INCOME TAX,ANGA,BANDARI KUU, MISAADA KUTOKA NJE,KUJIUNGA NA MATAIFA YA NJE.Na kichekesho zaidi hakuna hata mzanzibar mmoja aliewahi kuongoza vitengo hivi