Zanzibar iwe mkoa wa Tanzania

Zanzibar iwe mkoa wa Tanzania

Status
Not open for further replies.
Huu muungano it seems hata wazee wenyewe walikuwa na attitude. Kwa nini waliungana na still zbar ikamaintain serikali na tanganyika haikuwa na serikali? Madaraka ni focus ya kisirisiri ya watu wengi sana na ni toka enzi
 
Watu kama huyo anaetoa maoni si hasha wanaamini nyerere ni rais hadi leo.

Wewe maoni yako ni yapi?Kwa taarifa yako tu maoni yake ni maoni ya watanganyika wengi.Kama Znz haitaua utaifa wake kama Tanganyika ilivyofanya kwa zaidi ya miaka 50 sasa kutokana na ubinafsi wao(wa znz) bac itakuwa ngumu sana kwa watanganyika kukubali kuendelea na muungano wa aina hii!Simply ni kwamba kama hakuna nchi moja,muungano can go to hell !!!!!
 
Asante kamanda kwa ku-upload hii video.
Inawezekana kabisa walitoa hayo mapendekezo hawajawahi kuisoma katika ya Zanzibar.

Pengine hata hawajui kama kuna katiba ya Zanzibar inayotambua Zanzibar kama nchi.

Mnapoteza muda kuongea muungano mfu. Ikitokea mkiongelea muungano ongeleeni in past tense.

[video=youtube_share;Vhs8BMxY4Fg]http://youtu.be/Vhs8BMxY4Fg[/video]
 
Imemshinda nyerere kuifanya mkoa ataifanya yeye aliekuwa hujui hata maana yw nchii nini nenda kamulize Pinda(waziri mkuu) aliposema zanzibar sinchi na kam wasema zanzibar akamulize Benad Membe (waziri waambo ya njee) hiyo TANGANYIKA MPYA(iliozaliwa 1964) Umoja wa Mataifa watumia kiti cha nani,then utasema Zanzibar iwe mkoa ila kabla kuwa mkoa nayeye tukampime akili

Maneno ya namna hii yanafurahisha sana kwa kuwa yanaharkisha kurudi kwa Tanganyika yetu iliyopotea katika hali ya utata. Kama Zanzibar haitaki kuwa mkoa/wilaya, basi, serikali tatu haziepukiki.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Kuna watu wanafaidika nao hivyo hawataki uvunjike piga ua!! Wanasahau kuwa huwezi kumlazimisha mtu kitu kama hakitaki. Wazanzibari wameonyesha dhahiri hawautaki sasa bara tunawalazimisha kwa nini? Hivi mtu akija nyumbani kwako anaweza akakulazimisha ufanye kitu usichotaka!!
Wanasahau kuwa Zanzibar ilikuwepo kabla ya Tanzania. Wanasahu kuwa hata Tanganyika ilikuwa part ya Zanzibar.

Mimi nauliza hivi huu muungano una faida zipi kwa wote hata ukae ujadiliwe miaka nenda miaka rudi?
 
Atakuwa ni jambazi.
 
hiyo iko pouwa xana , znz itoe mikoa miwili tu 😛EMBA na UNGUJA, kisha tuunde na kanda maalumu ya kipolisi .
 
Wanasahau kuwa Zanzibar ilikuwepo kabla ya Tanzania. Wanasahu kuwa hata Tanganyika ilikuwa part ya Zanzibar.

Mimi nauliza hivi huu muungano una faida zipi kwa wote hata ukae ujadiliwe miaka nenda miaka rudi?

Twaona aibu tu kuuvunja kwakuwa tuvimbelembele kwenye Shirikisho la Afrika Mashariki pia twataka tuonekanike tumedumu kwenye Muungano muda mrefu ....Kimsingi hauna faida yoyote ....sijui security au mambo ya miaka ya kugombea uhuru hayapo siku hizi.....

Vunja muungano weka sheria ya Uhuru wa movement Tanganyika na Zanzibar ila vigezo vya utamaduni vizingatiwe ila havita tusumbua sana maana nasi tutakuwa watalii (nguo fupi ruksa kwa dada zetu)
 
Sumbawanga.
BAADHI ya wajumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, wametaka katika katiba ijayo kuwe na muundo wa Serikali moja, huku Zanzibar ikiwa ni moja ya mikoa ya nchi ya Tanzania na iwapo Wazanzibari watakataa, waruhusiwe kujitenga.

Mmoja wa wajumbe wa baraza hilo la Katiba Wilaya ya Kalambo, Afred Ntinda mkazi wa kata ya Mwazye kijiji cha Mpenje alisema hayo jana wakati akichangia maoni katika kikao cha baraza hilo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya wilaya mjini hapa.

Mpenje alisema kuwa mfumo wa sasa wa Serikali mbili una kasoro nyingi na umeshindwa kutatua kero za Muungano hivyo hautakiwi kuendelea kuwepo wakati ule wa Serikali tatu hawezi kulinda muungano huo kwa kuwa Serikali hizo zinaweza kuongozwa na marais kutoka vyama tofauti vya siasa na wenye mitizamo isiyolingana hivyo kuna hatari ya muungano kuvunjika.

“Sisi huku bara kuwa na Serikali moja si tatizo wengi wataridhia, nafikiri kuna tatizo katika upokeaji wa maoni kwa wenzetu wa Zanzibar.

Source: Zanzibar iwe mkoa wa Tanzania - Habari Ya Ndani - mwananchi.co.tz

Binafsi naunga mkono hoja! Zanzibar ina watu wachache kuliko hata mkoa wa Mbeya, inatoa wapi sifa ya kuwa nchi. Iwe tu mkoa wa Tanzania.

Ili iwe nchi we unataka iwe na watu wangapi?
 
haya basi Tanganyika iwe wilaya ya Zanzibar
Wanasahau kuwa Zanzibar ilikuwepo kabla ya Tanzania. Wanasahu kuwa hata Tanganyika ilikuwa part ya Zanzibar.

Mimi nauliza hivi huu muungano una faida zipi kwa wote hata ukae ujadiliwe miaka nenda miaka rudi?
 
haya ndo madhara ya mabaraza yaliyobemendwa. hvi kunawatu hawaelewi hali ya kisiasa ilivyosasa kati ya ZNZ na BARA. Nivyema watu wakazungumzia mambo yanayowezekana kufanyika jaman.
Huyu mdau ametoa maoni take. Bahati mbaya wengi we nu humu mngetaka aseme mnachokiwaza ninyi. Tena yeye amekuwa na busara zaidi kwa kutoa options mbili, tuwe nchi moja tukishindwa tutengane. Je ni kweli yote haya hayawezekani?
 
Wewe maoni yako ni yapi?Kwa taarifa yako tu maoni yake ni maoni ya watanganyika wengi.Kama Znz haitaua utaifa wake kama Tanganyika ilivyofanya kwa zaidi ya miaka 50 sasa kutokana na ubinafsi wao(wa znz) bac itakuwa ngumu sana kwa watanganyika kukubali kuendelea na muungano wa aina hii!Simply ni kwamba kama hakuna nchi moja,muungano can go to hell !!!!!

Kwa waz'br muungano c lazima labda kwa watanganyika.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom