Watanzania hivi karibuni tumeshuhudia makundi mawili makubwa yanayo utaka Urais ie Kundi la Mafisadi kwa upande mmoja na kundi la Wapinga ufisadi. Kundi la mafisadi lilanonekana lilijipanga muda mrefu na lina fedha nyingi ambazo limekua likizitumia ili mgombea wao aweze kuibukaa mshindi wa kuiwakilisha CCM kama mgombea. Kundi la Wapinga ufisadi nalo limejikita katika kutetea uzalendo zaid.
Sasa kwakua kuna kila dalili kwamba Chadema haitaweza kutwaa nchi, na kwakua kuna mkinzano mkubwa kati ya makundi haya mawili mimi nashauri kwamba Rais ajaye wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atoke Zanzibar.
Hii itakua imeyakata kilimilimi makundi haya ambayo yameacha kufanya kazi za kujenga nchi kwa kuwaza Urais tu. Pia hii itafanya Zanzibar nayo itoe walau Rais wa pili wa Muungano maana zaidi ya Mwinyi hakuna mwingine aliyetoka Zanzibar.
Hii itakua safi kama vile Mtaange wa kugombea Uspika kati ya Chenge (akiwakilisha kundi la mafisadi) na Sita aliyewakilisha kundi la kupinga ufisadi.
CCM ilitumia busara na kuyapiga chini makundi yote na kumchagua mwanamama. Naona CCM pia inaweza kumpata com[promise candidate kwa kumtoa mgombea Zanzibar.
Hii imekaaje wadau?
Tumekuwa tukiwaweka chini ndugu zetu wa Zanzibar kama vile hawawezi kugombea na kushida bila kupendelewa kama kuna mgombea mzuri atashinda na kama kuna watoa rushwa wazuiwe kugombea. Huwezi kutumia udikteta kupata demokrasia!. Kama CCM wana yote hayo na bado watu mnafikiria kuwapigia kura basi msilalamike umasikini wala rushwa maana nyie ndiyo tatizo na si makundi bali Watanzania wasio badilika mtaendelea na umasikini mpaka mbadilishe chama au chama kibadilike. Wakati wa mwinyi rushwa ilikuwepo sana na wakati wa mkapa ikaongezeka hivyo hata raisi atoke wapi rushwa na uzembe hautaisha CCM mpaka uoga wa kupoteza madaraka uingie