Zamu ya Zanzibar Urais 2015? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zamu ya Zanzibar Urais 2015?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Nov 19, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,774
  Likes Received: 419,795
  Trophy Points: 280
  Kuna mambo manne ambayo yananifanya nitofautiane na wengi ambao wamewatabiria akinamama wa bara Uraisi 2015 au hata mmbara mwingineyo yeyote yule. Kwa mtazamo wangu hili kamwe halitatokea. kwa maono yafuatayo.....

  Matukio haya ndiyo yanayoniongoza kusema hivyo;-

  a) Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi masuala ya Muungano, Mheshimiwa Seif Khatibu alikuwa wa kwanza kulipiga hili baragumu kuwa hii sasa ni zamu ya Mzanzibari kuwa Raisi baada ya Kikwete...............Khatibu ni mtu ambaye yupo karibu sana na JK na kwa hiyo ni rahisi sana kujua kauli hiyo ilitokea wapi...............Kwa maoni yangu Khatibu alitumiwa na JK kupima upepo wa kisiasa unavuma vipi.............

  b) Maamuzi ya makusudi ya kupendelea makundi maalumu yaliyofanywa na Kamati Kuu ya CCM chini ya uongozi wa JK ndani ya CCM katika kipindi cha miaka mitano iliyopita..................Haya ni pamoja na kuwazibia wabara kugombea uenyekiti wa UVCCM na kumnufaisha mzenji....Masauni.ambaye hata hivyo alikwenda kuwadhalilisha kwa kukosa sifa za kuwa kijana wa miaka 35 au chini ya hapo na kuwa na vyeti vya kughushi vya umri wake wa kuzaliwa............................

  Vile vile uteuzi wa wanawake watatu kugombea nafasi ya uspika na kuyaondoa majina yote ya wanaumme kwa visingizio vya gender-balance...........Matukio haya mawili yaashiria udikteta ndani ya CCM kuchukua sura ifuatayo mwaka 2015:-

  Pamoja na kuwa CC ya CCM itaruhusu wagombea wote kutoka kila kona ya nchi kugombea Uraisi lakini majina yatakayorudi ni matatu tu kutoka visiwani kwa minajili ya kile ambacho JK atasema ni kuwaenzi wazanzibari..................na ya kuwa bila ya kuchukua hatua za makusudi hawatakuwa na nafasi za kutoa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania....................

  Usishangae kama nyuso mpya za visiwani zitaingizwa kwenye baraza la mawaziri litakalotangazwa hivi karibuni kwa minajili ya kuwajenga wazanzibari fulani fulani........kwa lengo la kuwaongezea sifa za kuukwaa uraisi.........na wengi wao watakuwa ni vijana ili huko mbele waseme tena hawa mbona ni vijana haswa na wengi tutakubali hizo ghiliba na kushangilia bila ya kujua malengo haswa nini............

  Hivyo mkakati wa JK katika ni nani kumkabidhi nchi wabara andikeni mmeumia..................labda kura zisichakachuliwe na mmbara atatokea upinzani kuliongoza taifa hili..................

  Lakini hilo nalo JK atahakikisha kamwe halitokei kwa sababu atakwamisha mabadiliko yoyote katika muundo wa NEC hadi baada ya uchaguzi wa 2015 ili kujenga mazingira ya mzanzibara aweze kutumia idara ya usalama wa taifa na NEC kutwaa madaraka isivyo halali na kinyume na sheria..............kama ambavyo yeye kajisimika madarakani bila ridhaa ya wapigakura na hivyo kuvunja katiba ya nchi hii.............

  Habari njema ni kuwa CCM itagawanyika vipande vitatu vya kupinga maamuzi ya CC na upinzani utanufaika sana na wageni kutoka CCM.........na hapo kauli ya Baba wa taifa itakuwa imetimia ya kuwa ili CCM ishindwe kutwaa madaraka ni lazima ivunjike vipande vipande yenyewe.............................

  Hivyo ukombozi wa kweli wa mtanzania unategemea sana JK afanye makosa haya comes 2015...................Eeeeeeeeeeeeeeehh mwenyezi Mungu mwongoze huko gizani nasi tupate unafuu wa kiuchumi na shida hizi zipungue za kudhulumiwa na mafisadi wa CCM......................

  Haya ni maono yangu na ya kwako je..................waonaje mustakabali wa Taifa in 2015?
   
 2. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,198
  Trophy Points: 280
  Kwani Zanzibar kuna mkristo, Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete ...................nafikiri nimeeleweka.
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hata mimi nilitaka nikumbushie hilo ila naikahofu nisije nikaitwa mdini.

  Kunda trend ambayo ccm haipendi ionekane inaifuta lakini wakristo na waislam wanapeana zamu kuwa mgombea urais wa ccm.
  Hilo halina ubishi.

  Zanzibar kiongozi mkristo ni nani?
   
 4. c

  chibhitoke Member

  #4
  Nov 19, 2010
  Joined: Jun 1, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rais 2015 lazima awe mkristo..................................huo ndo utaratibu uliopo though haujaandikwa popote
   
 5. n

  nyaronga Member

  #5
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Imefika wakati tuache ya karne ya 20, jamani tuanze kumpata rais kwa uwezo wa kuongoza nchi katika karne hii ya 21. Hivi watanzania tukoje jamani,?

  Competence and delivery capability, mwaka 2015, hatutakuwa na mtu kuwekwa na chama tu, alafu anauza sura, alafu eti rais, huu nu upuuzi mtupu, by then, watanzania wengi watakuwa wamekomaa na wamechoka na maumivu ya kiuchumi ya kula vumbi ya miaka hii kumi.
   
 6. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #6
  Nov 19, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,198
  Trophy Points: 280
  Zanzibar kutoa rais wa muungano wasubiri labda hadi 2025 kama bado kutakuwa na muungano vinginevyo ndiyo imetoka hawatatoa milele quote my words.
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Nov 19, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,774
  Likes Received: 419,795
  Trophy Points: 280
  Mawazo mazuri lakini ni kitu gani cha kumzuia JK kutekeleza mkakati wake kupitia CC ya CCM ya kutorudisha jina la mbara ambaye atakuwa ni mkristu na kuwalazimisha wana-CCM kuwa wachague kati ya majina ya wazanzibara watatu? Akijua NEC na mashushushu watamlinda mgombea huyo kwa kuchakachua kura kama walivyomlinda yeye?
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Nov 19, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,774
  Likes Received: 419,795
  Trophy Points: 280
  Hiyo dhima ni nzuri lakini kwenye tanuru la CCM chini ya himaya ya JK wanayo?............ au ni sisi tu tulioko mtaani..................
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Nov 19, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,774
  Likes Received: 419,795
  Trophy Points: 280
  Kama Mzee Sita aliyekuwepo madarakani amechakachuliwa sembuse huyo mbara ambaye hata sura haijajulikana?
   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Nov 19, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,774
  Likes Received: 419,795
  Trophy Points: 280
  Swali ni zuri lakini lengo la JK kwani huyo Mzanzibara awe mkristu au awe...........................
   
 11. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #11
  Nov 19, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kitu kimoja mnasahau. Nguvu ya umma. Sidhani CCM itakuwa katika hali ya kulazimisha matakwa yake kwa Watanzania mwaka 2015.
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Nov 19, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,774
  Likes Received: 419,795
  Trophy Points: 280
  Mawazo mazuri nguvu ya wananchi ikisubiri hadi 2015 itakuwa imechelewa.......lazima vuguvugu la kudai mabadiliko lianze sasa.............tupate katiba mpya, NEC mpya.......n.k.......kabla ya uchaguzi ujao..........hapo nguvu ya umma itakuwa imeshika hatamu vinginevyo kutakuwa na vurugu na umwagaji wa damu usio wa lazima hata kidogo.......tukisaidie kizazi kijacho kuwa na maisha bora sasa...........
   
 13. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #13
  Nov 19, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  ...ukristo,uislamu,ukristo ,uislamu,...(sequence n series)
   
 14. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #14
  Nov 19, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kama akilazimisha hivyo basi jk atakuwa anaichimbia ccm kaburi.
   
 15. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #15
  Nov 19, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,792
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  2015 Atakua mkristo lutheran maana hajawahi kuwa rais
   
 16. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #16
  Nov 19, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Vipi kuhusu wapagani na freemasons?
  Hawapo kwenye ratiba?
   
 17. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #17
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kama kamati kuu ya ccm haitabadilika basi mtarajie rais lowasa au mshenzi mwingine yeyote kutoka kwa wana mtandao.
  Tatizo hapa si dini bali ni hawa wendawazimu walioko ndani ya kamati kuu kwani wanaweza kuweka hata jiwe na likapita ili mradi maslahi yao yalindwe tu.
   
 18. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #18
  Nov 19, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Zanzibar walivurunda wenyewe! Zamu yao ilikuwa mwaka 2005 (Salim) lakini wakamkataa.! hii laana itawaandama maisha. By the way kama Kikwete 2005 alisema ni zamu ya waislam, ni nini kitakachowazuia wakristo kusema 2015 ni zamu yao? Nakuhakikishia hata Muddy atoke kaburini 2015 wakristo hawatakubali tena mwislam apewe urais!
   
 19. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #19
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  basi kama ni kupeana zamu ya urais ni sawa lkn naomba iwe rais wa jamhuri akitoka zanzibar.. rais wa zanzibar atoke bara & vice versa
   
 20. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #20
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135


  Jina lako linaendana na ulichokipost
   
Loading...