Yusuf Manji amshitaki Reginald Mengi, adai fidia Sh1/-

Yusuf Manji amshitaki Reginald Mengi, adai fidia Sh1/-

Fidia hutolewa kutokana na hasara ambayo mlengwa ameipata. Kwa Manji anaweza kuwa amechafuliwa kwa jamii lakini hakuna hasara ambayo ameipata kifedha.

Kudai fidia ya shelingi moja ina nguvu sana, maana inaonyesha hataki kufaidika na huyo Mengi.

Madhara yake ni kwamba Mengi akishindwa atalipa hiyo shilingi moja na gharama zote za kuendesha hiyo case kwa pande zote.

Kama kutokana na maneno ya Mengi kungelikuwa na watu wengi ambao wangesusia bidhaa za Manji hapo ndipo angeweza kudai fidia kubwa.
 
Hii habari imethibitishwa ? au bado ni tetesi
 
Hii ni habari njema sana

Huu nio muda muafaka, Tunacho takiwa kutambua ni kwamba hii si kesi ya Mengi na mafisadi, ni kesi yetu wote walala hoi wa Tanzania juu ya mafisadi ambao wamekuwa wakitufisadi watanzania wote na kutufanya tuishi maisha ya shida kiasi hiki.

Wito: kwa wana sheria wote, huu ndio muda wa kuonyesha uzalendo na mapenzi kwa nchi yenu, unganeni na kushikama kuhakikisha hawa mafisadi wanapata iliyo stahiki yao.

Wahadhiri wa sheria pote na hasa Mlimani, hapa ndo muda wa kuonyesha usomi wenu, kumbukeni hicho kimshahara mnachopata cha namba ya viatu kiini chake ni kwamba mafisadi wamesabbaisha uchumi wa nchi yetu uishie mifukoni mwao. Muungeni mkono mzalendo Mengi, kwa bure.. kwa kuchangia elimu yenu mliyo jaliwa kuhakikisha sheria inafuata mkondo wake, na ufisadi unakomeshwa.

Mahakimu:
Kumbukeni nanyi ni watanzania, shida zetu ni zenu, ama ndugu zenu, msikubali katu kupindisha sheria kwa kupewa tumakombo na hawa mafisadi. Fateni haki ili ujambazi huu ukomeshwe. Hamuhitaji kufanya kazi ya ziada zaidi ya kuwa waungwana kwa kukataa kupokea chochote na kusimamia haki.

Kama wote tukishiriki kwa moyo mmoja, nina uhakika, hizi kesi zitatusaidia kupata kile tulicho kihitaji.

Iteni wote wenye ushahidi, Yupo kamanda wetu Dr Slaa, yote yakitendewa haki, ukombozi wa Tanzania utakuwa umekamilika.

MUNGU WABARIKI WATANZANIA, WAPE ROHO YA UZALENDO, KILA MTU KWA NAFASI YAKE ASIKUBALI KUNUNULIWA ILI HAKI YETU IRUDI NA TUFURAHIE ASALI NA MAZIWA YA NCHI YETU TANZANIA ULIYO TUJALIA.
 
"Hapa ni patamu sasa, hatimaye kilio cha wana JF kuwa mafisadi watangulie mahakamani ili ushahidi utolewe hatimaye majibu yamepatiakana, kinachotakiwa si mawazo kama ya Mpita njia eti "Better wapi Mkuu... hivi ni vita vya mafahari, sisi nyasi tutaendelea kuumia tu" inabidi tuyatafakari kwa ukaribu. Je ni kweli kuwa hivi ni vita visivyotuhusu sisi wapiganaji dhidi ya ufisadi na mafisadi? Mimi naamini mengi yatajulikana huko huko mahakamani, manake hata mzee slaa alitamani mno hili litokee katika ile orodha yake ya mafisadi lakini halikutokea, madamu limetokea sasa yote yana mwisho."
****************************

Great Thinker:

Nakubaliana nawe. Kwenda mahakamani kina Manji ndiyo hasa inafaa na Mengi mwenyewe aliwaambia kabla -- kwamba waende mahakamani.

Badala yake wakawa wana-enlist watu kama vile Sophia Simba (mmesoma makala kuhusu yeye ktk M.Halisi leo?) na Profesa Lipumba ambaye ni spent force.

Kwanza namuuliza huyo Lipumba: kama ufisadi siyo agenda yake katika upinzani, agenda yake ni nini? Atueleze, na situtajie muafaka ambao amefail totally!
 
Wito: kwa wana sheria wote, huu ndio muda wa kuonyesha uzalendo na mapenzi kwa nchi yenu, unganeni na kushikama kuhakikisha hawa mafisadi wanapata iliyo stahiki yao.
.
Thubutu hawa wanasheria wetu, uzalendo utatoka wapi? hata wanafikiria ulaji zaidi. Tuombe Mwenyezi Mungu atuepushe na ufisadi huu
 
Kaamua kutumia haki yake y akisheria kuomba nominal damages - haina maana kuwa shilingi moja ndiyo thamani yake , bali anachotaka ni kusafishwa jina lake analoona Mengi kalichafua kupitia vyombo vyake vya habari.

So this clown Manji is claiming defamation of character. As is if there is any character left to defame!! These dudes are lucky they live in a banana republic...
 
So this clown Manji is claiming defamation of character. As is if there is any character left to defame!! These dudes are lucky they live in a banana republic...
Thats the irony!
Si serikali wamemkaripia Mengi wakampa kichwa..na sasa akifungua kesi huoni ni kama pia serikali wamempa some kind of assurance kuwa he has a claim - anachafuliwa kwa kutajwa na Mengi?
 
Naona Manji hana haja ya pesa za mengi bali heshima yake. Swala hapo sio hiyo sh. 1 bali ndugu Mengi aombe radhi katika vyombo vyake vya habari kwa muda wa siku saba.
 
kwi kwi comedi drama... tusubiri kesi... hii itatuchekesha wengi.

Maybe Mr Mengi ana evidence kwi kwi

Kwa taarifa yako Mengi akizidiwa mahakamani atasema pia kwamba Manji alipenyeza hela... Mengi anajua drama mzee.
 
Je ni kweli kuwa hivi ni vita visivyotuhusu sisi wapiganaji dhidi ya ufisadi na mafisadi? Mimi naamini mengi yatajulikana huko huko mahakamani, manake hata mzee slaa alitamani mno hili litokee katika ile orodha yake ya mafisadi lakini halikutokea, madamu limetokea sasa yote yana mwisho."
Nadhani tulipaswa kuwafikisha sisi mahakamani na si kuwafanya waop ndio waende. katika mazingira kama haya, masuala kuhusu ufisadi hayatakuwa main agenda, kesi ni ya kadshfa na masuala ya ufisadi yataibuka kama sehemu ya utetezi. Ilitakiwa zifunguliwe kesi za ufisadi perse na ngoma ichezwe around ufisadi pekee
 
Muhindi amemuonyesha Mengi jeuri ,sasa hapo ni kujiuliza Je Mengi ataitoa shilingi, tunaifahamu power ya Shilingi pale Bungeni ,ingawa wengine mmeonyesha dharau,ikiwa hii ni kweli basi Mengi hana muda atapata presha ,maana hii ni jeuri ya jeuri kwa wanaofahamu uungwana.
 
Manji ameenda mahakamani amefanya jambo jema.. kwa sababu huko atatueleza kwanini yeye arudishe fedha za Kagoda ambazo zilichotwa kwa wizi? Mahakama itabidi iite ushahidi wa Kagoda.... na kutaka Mwanyika na wenzie wawe mashahidi upande wa Mengi..

Hili wala siyo gumu.. Hili siyo suala la Manji kama wengi wanavyofikiria ni katika kutaka kuifunua Kagoda....

that is whats up.. didn't I say time is up? It is.. Namshauri na Rostam afanye hivyo hivyo.. pleaaasse!!!
 
Manji leo amefungua kesi mahakama ya kisutu akidai amekashifiwa na Mengi. Anamtaka Mengi amlipe fidia ya sh1 kwa kumkashifu na kuandaa kipindu maalum cha kumuomba radi ambacho atakuwa akikirusha (mengi) mfululizo kwa siku saba

Kumbe suala sasa ni kuonyeshana jeuri!!!! Mi nilisema sasa vyombo vya habari vimekuwa kumbi za mipasho, haingii akilini mtu afungue kesi afu adai TSH. 1, huyu Manji hana adabu na ameikosea heshima Mahakama yetu na jopo zima la majaji, wanasheria na hata watunga sheria zenyewe (wabunge) na Bunge limekosewa heshima basi na sisi wananchi tumekosewa heshima.

We unajua gharama za kuendesha kesi zilivyo ikiwemo muda unaotumika kuwalipa huma resource...yeye anapeleka madai ya kipuuzi namna hiyo ama sasa wanyonge tukae chonjo. Hii jamani inamaana gani kwenye duru za sheria..huyu Manji anatufanya sisi watanzania mafala sio???? Naomba moderate weka private forum inayoruhusu wachangiaji kuwatusi hawa mahuruni wa Ufisadi bila bugudha...INAKERA KWELI MAMBO MENGINE.
 
naomba wanasheria wanisaidie ila mimi naelewa hivi;

mengi itabidi aithibitishie mahakama kuwa manji ni fisad. katka mojawapo ya threads humu na kwenye vyombo vya habar kuna shutuma za mengi (na sie) kwa manji. mojawapo ni kuhusu kagoda. shida ni ushahid kuwa mikononi mwa serikali kama kina dpp na takukuru etc. hao watamsaidiaje mengi kuwa manji kweli kafanya madudu? kwamba vitu kama kagoda ni ufisad? na manji kahusika? lasivyo mengi atatoa wapi ushahid wa kukubalika mahakaman?

manji itabidi aithibitishie mahakama kuwa yeye si fisad? kama jibu ni ndio itabid aithibitishie mahakama jins mambo ya kagoda etc yasivyoaiathiri nchi. kwamba madudu hayo si ufisad. ni rahis kuona jins kaz isivyo rahis kwake
 
Kumbe suala sasa ni kuonyeshana jeuri!!!! Mi nilisema sasa vyombo vya habari vimekuwa kumbi za mipasho, haingii akilini mtu afungue kesi afu adai TSH. 1, huyu Manji hana adabu na ameikosea heshima Mahakama yetu na jopo zima la majaji, wanasheria na hata watunga sheria zenyewe (wabunge) na Bunge limekosewa heshima basi na sisi wananchi tumekosewa heshima.

We unajua gharama za kuendesha kesi zilivyo ikiwemo muda unaotumika kuwalipa huma resource...yeye anapeleka madai ya kipuuzi namna hiyo ama sasa wanyonge tukae chonjo. Hii jamani inamaana gani kwenye duru za sheria..huyu Manji anatufanya sisi watanzania mafala sio???? Naomba moderate weka private forum inayoruhusu wachangiaji kuwatusi hawa mahuruni wa Ufisadi bila bugudha...INAKERA KWELI MAMBO MENGINE.
Ndugu hujaiona jeuri hapo ,ila kwa kukumegea kidogo ,Muindi wetu anamdhalilisha tajiri wetu ,kwa maana Mengi hana uwezo wa kumlipa Manjibhai kitita cha mamilioni kama tulivyozoea wengine wakidai fedha kibao kwa kuzalilishwa ,hivyo ameona mengi kauwezo kake ni kadogo sana na akiweka dau la mamilioni Mengi atauza kila kitu na hatatimiza dai,hivyo amempa kiwango cha chini kabisa cha Shilingi moja na kuombwa radhi kupitia hivyo vyombo vyake kwa mida ya siku saba na zikimaliza hizo siku saba hajatimiza hayo atamfunga jela.
 
Manji ameenda mahakamani amefanya jambo jema.. kwa sababu huko atatueleza kwanini yeye arudishe fedha za Kagoda ambazo zilichotwa kwa wizi? Mahakama itabidi iite ushahidi wa Kagoda.... na kutaka Mwanyika na wenzie wawe mashahidi upande wa Mengi..

Hili wala siyo gumu.. Hili siyo suala la Manji kama wengi wanavyofikiria ni katika kutaka kuifunua Kagoda....

that is whats up.. didn't I say time is up? It is.. Namshauri na Rostam afanye hivyo hivyo.. pleaaasse!!!
This surely going to be a very ineresting match to watch. Kwa wale waliokwepa kupeleka kesi za Manji mahakamani sasa ndio wakati wa mahakama kupembua pumba na mchele.Kwa vyovyote vile Mengi hakutoa shutuma za Mafisadi "PAPA" bila kujitayarisha.
 
Hii kesi haitaendelea kwani hapa naona Kagoda inajulikana kwa kuwa kuna ushaidi wa wazi kuwa manji amerudisha pesa za Kagoda amabao najua hata ikiwa vipi serikali haitaweza kumuuliza Mengi ameupata wapi kwani wananchi watajua serikali hipo pamoja na mafisadi.

Na kwakuwa Kagoda ni ya RA atakubali hata kidogo liharibu jina lake, tusubiri tuone huu ndio mwanzo wa kujua yote kwani kukana pesa uliyorudisha ni kazi kubwa, kama hukuiba ulirudisha ya nini? Naona hakushauriana na wenzake kakurupuka tu na kufungua kesi mahakamani bila kujari hatima yake kwake na kilichokuwa kinatafutwa.

Jukwaa la kufungua kagoda na uchafu mwingine ndio hilo.
 

Mahakama itabidi iite ushahidi wa Kagoda.... na kutaka Mwanyika na wenzie wawe mashahidi upande wa Mengi..

Kesi ya Mengi na Manji, mahakama haiwezi kuita shahidi aje kumsaidia Mengi ua Manji.

Manji akishatoa vielelezo vya vipengele vya madai (elements of the course of action) kwamba Mengi kanichafua, mzigo unahamia kwa Mengi, sio kwa mahakama, kwa Mengi, kuthibitisha uchafu wa Manji au kuthibitisha kwamba hakusema Manji fisadi papa.

Au unasemaje, ewe mkufunzi wa sheria wa jamvi, Mkuu Mwanakijiji?
 
Back
Top Bottom