Manji versus Mengi.....in a courtroom...........


Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,609
Points
2,000
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,609 2,000
Mengi amenivunjia heshima - Manji
• Hakimu apokea vielelezo visivyo halisi mahakamani

na Happiness Katabazi


MFANYABIASHARA maarufu nchini, Yusuf Manji (35), jana aliieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kuwa kashfa zilizotolewa na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Reginald Mengi kuwa yeye ni Fisadi Papa zimemvunjia heshima na kupoteza uaminifu wake mbele ya wabunge.
Aidha Hakimu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, anayesikiliza kesi hiyo inayovuta hisia za wengi nchini, Aloyce Katemana, alikubali kupokea vielelezo vya hati ya barua ya mwaliko wa Kamati ya Bunge zisizo halisi, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Manji alitoa nyaraka nane zisizo halisi (Original) ambazo ni mialiko ya shughuli za kiserikali ya ndani na nje ya nchi zilizodai kumtaka awe mgeni rasmi na kutoa hotuba mbalimbali za masuala ya kiuchumi.
Pia alitoa magazeti ya This Day na Kulikoni pamoja na DVD, ambavyo vyote vilipokelewa na mahakama kufanya jumla ya vielelezo vilivyopokelewa kufikia tisa.
Manji ambaye jana ilikuwa ni mara yake ya kwanza kupanda kizimbani hapo, alitoa maelezo hayo wakati akitoa ushahidi wake juu ya kesi hiyo.
Mfanyabiashara alikuwa akitoa ushahidi wake huku akiongozwa na jopo la mawakili maarufu wa kujitegemea nchini: Mabere Marando, Dk. Ringo Tenga, Richard Rweyongeza, Sam Mapande na Beatus Malima.
Manji ambaye anadai alipwe fidia ya sh moja kwa madai ya kukashfiwa na Mengi, aliwasili mahakamani na msafara wa magari mbalimbali likiwemo gari aina ya fuso lilobeba lundo la magazeti ambayo yanadaiwa kuchapisha habari iliyomnukuu Mengi akimkashifu ambayo yaliwasilishwa mahakamani hapo kama kielelezo.
Katika ushahidi wake, Manji alidai Aprili 23-27 mwaka 2009, Mengi kwa kutumia kituo cha televisheni cha ITV, alitoa madai kuwa Manji na wafanyabiashara wengine kuwa ni mafisadi papa, wanahamisha rasilimali za taifa kupeleka nje ya nchi na kwamba wameshiriki kikamilifu katika ufisadi wa ununuzi wa magari ya JWTZ, rada, mradi wa makaa ya mawe wa Mchuchuma, mifuko ya hifadhi ya jamii ya PSPF na NSSF, Dowans na Richmond.
Kwa mujibu wa Manji, Mengi alidai zabuni hizo walizipata kwa rushwa na fedha walizonazo zimetokana na ufisadi.
Mkanda wa kipindi hicho maalum, ulionyeshwa mahakamani hapo kama kielelezo cha ushahidi.
“Mheshimiwa hakimu kupitia matamshi hayo ya mdaiwa (Mengi) kwenye kipindi hicho maalum, kwa kweli, kimenivunjia heshima ndani ya familia yangu, wafanyakazi wangu zaidi ya 4,000, wafanyabiashara wenzangu wa ndani na nje ya nchi na jamii iliniona kama mtu mchafu na wabunge wamepoteza imani na mimi kwa ajili ya matamshi hayo.
“Na kuthibitisha kuwa wabunge hawana imani na mimi hasa wabunge waliokuwa wabunge wa Bunge lilopita….Kamati ya Uchumi ya Bunge, ilinialika kwenye moja ya kikao chao nikatoe hotuba lakini cha ajabu nilivyofika kwenye kikao hicho, kuna baadhi ya wabunge wa kamati hiyo walinikataza kutoa hotuba yangu kwa sababu ni mtu mchafu kwenye jamii na Mengi alikwishanitaja hadharani kuwa mimi ni Fisadi Papa, nililazimika kuondoka kwenye mkutano huo na kurejea nyumbani kwa aibu,” alisema Manji.
Aliendelea, “Kashfa zilizoelekezwa na mdaiwa kwangu, si za kweli kabisa kwani sijawahi kujihusisha na biashara za rada, Dowans, Richmond, ununuzi wa magari ya jeshi, kuhamisha fedha nchini kuzipeleka nje ya nchi na wala sijawahi kushtakiwa kwa kutoa rushwa ili nipate tenda za serikali na hadi nina umri huu sijawahi kutoa fedha zangu mfukoni kujenga nyumba hata moja hapa nchini wala nje ya nchi…hapa jijini naishi kwenye nyumba ya familia pale Upanga na Marekani kuna nyumba ya familia aliyoiacha marehemu baba yangu Meibou Manji,” alidai Manji.
Wakili Marando alipomhoji Manji anatafsri vipi neno Fisadi Papa aliloitwa na Mengi; Manji alijibu kuwa analitafsiri kwamba yeye ni mtu anayekabiliwa na skendo na kwamba papa ni aina ya samaki mkubwa aishie baharini na kukana kwamba yeye siyo samaki aina ya papa bali ni binadamu.
Hakimu Katemana aliahirisha usikilizaji wa kesi hiyo hadi leo asubuhi ambapo Manji ataendelea kutoa ushahidi wake na baadaye kuhojiwa na mawakili wa Mengi.
Mapema mwaka juzi, Manji alimfungulia kesi ya madai ya kashfa Mengi na kituo cha televisheni cha ITV akitaka amlipe fidia ya shilingi moja kwa madai kuwa alitumia televisheni yake kumkashfu kwa kumuita ‘Fisadi Papa’ na mmoja wa watu wanaopora rasilimali za taifa.
 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,609
Points
2,000
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,609 2,000
Manji apanda kizimbani Kisutu Send to a friend Thursday, 03 February 2011 21:32 0diggsdigg

Tausi Ally
MFANYABIASHARA maarufu nchini, Yusuf Manji, jana alipanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kutoa ushahidi katika kesi aliyomfungulia Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Regild Mengi na kumdai fidia Sh1.

Lakini katika kile kilichothibitisha kukua kwa teknolojia, Manji alitoa sehemu kubwa ya ushahidi kwa kuonyesha mkanda wa video badala ya kuzungumza.

Mkanda huo wa picha wa (DVD) ulionyesha hotuba ya Mengi wakati akizungumza na waandishi wa habari na kumtaja Manji kuwa miongoni mwa mafisadi papa wanaoihujumu nchi.

Mkanda huo ulionyeshwa katika mahakama ya wazi, mbele ya Hakimu Mkazi Aloyce Katemana, wakati Manji akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo iliyokuwa kivutio cha aina yake jana mahakamani hapo.

Katika mkanda huo Mwenyekiti huyo wa Makampuni ya IPP, alionekana na kusikika akiwataja watu watano wanaotuhumiwa kuhusika na ufisadi mkubwa nchini na kuitaka serikali iwashughulikie haraka ili kuinusuru nchi isiyumbishwe nao.

Katika hotuba yake hiyo pamoja na Manji, Mengi aliwataja mafisadi wengine aliowaita papa kuwa ni pamoja na Mbunge wa Igunga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC-CCM) na Halmashauri Kuu ya Chama hicho (NEC-CCM) Taifa, Rostam Aziz. Wengine ni wafanyabiashara, Tanil Somaiya, Jeetu Patel na Subash Patel, ambao alisema wanatuhumiwa kuiba mabilioni ya wananchi na kuzihamishia nje ya nchi. 


Baada ya kumaliza kuonyesha mkanda huo (DVD) mahakamani hapo, Manji aliiomba mahakama iipokee DVD hiyo kama moja ya kielelezo cha ushahidi wake katika kesi hiyo.

Mbali na mkanda huo, katika ushahidi wake Manji pia alitoa nyaraka mbalimbali ikiwemo mikataba yake ya kazi pamoja na vyeti vya shule na vyuo mbalimbali alivyosoma na kuvionesha mahakamani hapo kama vielelezo vya ushahidi kwenye kesi hiyo.

Katika ushahidi huo Manji alidai kuwa tuhuma zilizotolewa na Mengi dhidi yake zilimshushia heshima kwa taifa, familia yake, wafanyakazi wake na wabunge kwa kuwa waliamini yaliyosemwa na Mengi.

Alidai kuwa baada ya Mengi kutoa tuhuma hizo ambazo alidai kuwa yeye(Manji) ni Fisadi Papa, alialikwa kwenye mkutano (public conference) ambao ulishirikisha wabunge kutoa hotuba, lakini kutokana na tuhuma zilizotolewa na Mengi aliambiwa kuwa hotuba yake imefutwa kwa sababu ‘si mtu mzuri kwa Tanzania' hivyo akawa mgeni wa kawaida hatua ambayo ilimnyanyasa.

Akiendelea kutoa ushahidi wake, Manji alidai kuwa yeye hausiki katika kashfa inayohusu kampuni ya Richmond, ambayo ilitiliana saini na Shirika la Umeme nchini (Tanesco) mkataba tata wa kufua umeme wa dharura.

Pia alidai ahusiki katika kashfa nyingine ya akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) kwenye Benki Kuu ya Tanzania (BoT), wala kampuni ya Dowans Tanzania Limited iliyorithi mkataba tata wa Richmond.

Alidai pia hahusiki katika ununuzi wa helikopta na magari ya jeshi, ndege ya Rais, rada, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Pensheni ya Watumishi wa Umma (PSPF), Bahati Nasibu ya Taifa na Mradi wa Makaa ya Mawe wa Mchuchuma kama ilivyodaiwa.

Hata hivyo, Hakimu Katemana ameiahirisha kesi hiyo hadi leo ambapo Manji ataendelea kutoa ushahidi wake.

Kufunguliwa kwa kesi
April 29, 2009, Manji alimfugulia kesi Mengi pamoja na Kituo cha runinga cha ITV kinachomilikiwa na Mwenyekiti huyo wa IPP akidai alipwe fidia ya Sh1 kama fidia ya kumkashifu kwa kumwita fisadi papa pamoja na wafanyabiashara wengine.

Manji alifungua kesi hiyo katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, Dar es Salaam kupitia kampuni ya muwakili ya Muganda, Kamugisha na Bwana.

Wakili John Kamugisha, aliyemwakilisha Manji wakati wa kufungua kesi hiyo alipoulizwa sababu ya mteja wake kudai shilingi moja kama fidia, alisema mteja wake huyo (Manji) anaamini kuwa heshima na utu vina thamani kuliko fedha. Kwa mujibu wa Kamugisha kesi hiyo ni ya kwanza kudai kiwango kidogo cha fedha na kwamba ilitarajiwa kuwashangaza wengi.

Katika kesi hiyo Manjia anadai kuwa Mengi kupitia kipindi maalumu cha ITV kilichorushwa April 23, 2009 mara baada ya taarifa ya habari ya saa mbili usiku alimkashifu kwa kutoa matamshi yanayomdhalilisha.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Comments
0 #1 S.T 2011-02-04 08:00 We manji na wenzako ni maafisadi papa, ukweli unauma, wezi wakubwa nyinyi. Ali[NENO BAYA]sea Mengi ni kuwataja wahindi tu kama maafisadi papa kitu kilichopelekea watu wengine kutafsiri ni ubaguzi wa rangi..Na kunao maafisadi papa wengine ambao si wa kundi hili, nao imenipasa kuwajumuisha hapa, akiwemo Mramba, Andrew Chenge na Daniel Yona
Quote
 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,609
Points
2,000
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,609 2,000
Manji, Mengi wavutana mahakamani
• Kisa ni nyaraka za Kagoda

na Happiness Katabazi


JOPO la mawakili wa kujitegemea wanaomtetea mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji (35), jana walipambana kwa kutumia hoja za kisheria ili kuishawishi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, ikubaliane na pingamizi lao la kutaka nyaraka zilizowasilishwa na mdaiwa Reginald Mengi zisitumike katika kesi hiyo.
Jopo hilo lililosheheni mawakili wa kujitegemea maarufu linaloongozwa na Mabere Marando, Dk. Ringo Tenga, Sam Mapande, Richard Rweyongeza na Beatus Malima mbele ya Hakimu Mkazi Aloyce Katema waliiambia mahakama kuwa juzi mawakili wa mdaiwa Mengi ambao ni Michael Ngaro na Deo Ringia, waliwapatia nyaraka hizo ambazo walidai Mengi atazitumia kujitetea wakati ukifika.
Sababu zilizotolewa na Marando kutaka nyaraka hizo zisitumike ni kwamba hazihusiani na kesi hiyo ambayo mteja wake Manji anataka Mengi amlipe fidia ya shilingi moja.
Kwa mara nyingine tena jana Manji alifika mahakamani hapo.
Marando alisema sababu nyingine ambayo wanataka nyaraka hizo zilizoletwa na mawakili wa Mengi zitupwe na mahakama ni kwa sababu nyaraka hizo ni kivuli.
Kadhalika zinaonyesha ni mali ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na ofisi ya Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (takukuru) na kwamba nyaraka hizo licha ya kuwa ni vivuli lakini pia hazionyeshi kama zimethibitishwa kisheria (certified copy).
"Sheria ya ushahidi ya mwaka 2002, inamtaka mtu alete nyaraka halisi mahakamani kama ushahidi na kama hana nyaraka halisi mdai au mdaiwa anaruhusiwa kuomba upande wa pili wa kesi hiyo umpatie nyaraka halisi ili aweze kuzitoa mahakamani kama ushahidi.
"Lakini hawa mawakili wa Mengi hawajatuomba nyaraka halisi hadi sasa na pia walitakiwa hizo nyaraka wazilete mapema mahakamani kabla ya kesi haijaanza kusikilizwa.
Marando pia alishangazwa na nyaraka hizo zinazoonyesha zimetolewa na ofisi ya AG na TAKUKURU kufikishwa mahakamani bila kibali cha mamlaka hizo wala kuonyesha kama alilipia ada ya kupata nyaraka hizo.
Akisoma moja ya nyaraka hizo ambayo ni mkataba ulioingiwa baina ya Kagoda Agriculture Ltd na Quality Group Finance Ltd, Marando alieleza kuwa mkataba huo uliiingiwa na makampuni hayo na si mteja wao (Manji) na kwamba wao ni mawakili wanaomtetea mlalamikaji binafsi na wala si mawakili wa makampuni yanayomilikiwa na mteja wao.
Katika hilo, wakili huyo wa Manji alimshauri Mengi kama anataka kutumia nyaraka ni vyema akafungua kesi nyingine dhidi ya makampuni ya Manji.
Hata hivyo ilipofika upande wa wakili wa Mengi, Ngaro, kujibu hoja hizo aliieleza mahakama kuwa hayuko kwenye nafasi nzuri ya kujibu hizo hoja hivyo kuomba muda wa kwenda kuwasiliana kwanza na mteja wake (Mengi) ambaye yuko safarini mkoani Arusha.
Ombi hilo la Ngaro lilikubaliwa na Hakimu Mkazi Katemana ambaye aliahirisha usikilizaji wa kesi hiyo inayovuta hisia za watu wengu hadi Februali 1.
Mapema mwaka juzi, Manji alimfungulia kesi ya madai ya kashfa Mengi na kituo cha televisheni cha ITV akitaka amlipe fidia ya shilingi moja kwa madai kuwa Mengi alitumia televisheni yake kumkashifu kwa kumuita ‘Fisadi Papa' na kwamba mmoja wa watu wanaopora rasilimali za Tanzania.
 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,609
Points
2,000
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,609 2,000
Wakili wa Manji akataa ushahidi wa Mengi Friday, 04 February 2011 21:27

Tausi Ally
WAKILI wa mfanyabiashara, Yusuph Manji, Mabere Marando, ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kufuta nyaraka zilizowasilishwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi kwa kuwa haziendani na sheria za mahakama.

Marando alitoa ombi hilo, jana mbele ya Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana wakati alipokuwa akisikiliza kesi ya madai ya Sh1 ambayo Manji aliifungua dhidi ya Mengi.

Marando alidai sheria inakataa nakala zisizo halisi na kwamba kuna sheria, inayoruhusu upande wa Mengi kuomba kibali kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo.

"Na kama waraka unahusu serikali unatakiwa ufanyiwe marekebisho na ofisa aliyetoa nyaraka hizo, na kwamba inatakiwa zilipiwe, lakini upande wa Mengi, haujafanya vitu hivyo,"alidai Marando.

Alidai kutokana na hoja hizo, nyaraka zote zilizopelekwa mahakamani hapo na upande wa utetezi hazina msingi, na kwamba ziondolewe mahakamani kwa kuwa zinawapotezea muda.

Marando pia aliutaka upande wa utetezi ueleze umezipata wapi risiti za malipo za serikali kuhusu Kampuni ya Quality Finance Cooparation Group na ni nani aliwapa.

"Kuna mkataba kuhusu Quality Finance Cooparation Group na Kagoda Agriculture, lakini haumuhusu Manji kwa sababu kesi hii inahusu udhalilishaji wa mtu na mtu na siyo mtu na kampuni,"alidai Marando.
Baada ya Marando kutoa hoja hizo, Wakili wa Mengi Michael Ngaro aliiomba mahakama iiahirishe kesi hiyo ili aweze kuwasiliana na mteja wake Mengi.

Hakimu Katemana alikubaliana na ombi hilo na kuiahirisha kesi hiyo hadi Februari 11, mwaka huu.
Wakati yote hayo yakiendelea mahakamani, Manji aliyekuwa amevalia suti nadhifu, alikuwa akisikiliza kwa makini.

Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji, juzi alipanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kutoa ushahidi katika kesi aliyomfungulia Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi na kumdai fidia Sh1,lakini katika kile kilichothibitisha kukua kwa teknolojia, Manji alitoa sehemu kubwa ya ushahidi kwa kuonyesha mkanda wa video badala ya kuzungumza.


Mkanda huo wa picha za (DVD), ulionyesha hotuba ya Mengi wakati akizungumza na waandishi wa habari na kumtaja Manji kuwa miongoni mwa mafisadi papa wanaoihujumu nchi.

Mkanda huo, ulionyeshwa katika mahakama ya wazi, mbele ya Hakimu Mkazi Aloyce Katemana, wakati Manji akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo, iliyokuwa kivutio cha aina yake jana mahakamani hapo.

Katika mkanda huo, Mwenyekiti huyo wa Makampuni ya IPP, alionekana na kusikika akiwataja watu watano wanaotuhumiwa kuhusika na ufisadi mkubwa nchini na kuitaka serikali iwashughulikie haraka ili kuinusuru nchi isiyumbishwe nao. Mbali ya Manji, Mengi aliwataja mafisadi papa kuwa ni Mbunge wa Igunga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC-CCM) na Halmashauri Kuu ya Chama hicho (NEC-CCM) Taifa, Rostam Aziz.

Wengine ni wafanyabiashara, Tanil Somaiya, Jeetu Patel na Subash Patel, ambao alisema wanatuhumiwa kuiba mabilioni ya wananchi na kuzihamishia nje ya nchi.

April 29, 2009, Manji alimfugulia kesi Mengi pamoja na kituo cha runinga cha ITV kinachomilikiwa na Mwenyekiti huyo, akidai alipwe fidia ya Sh1 kama fidia ya kumkashifu kwa kumwita fisadi papa pamoja na wafanyabiashara wengine.

Manji alifungua kesi hiyo, katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, Dar es Salaam kupitia kampuni ya muwakili ya Muganda, Kamugisha na Bwana.

Wakili John Kamugisha, aliyemwakilisha Manji wakati wa kufungua kesi hiyo alipoulizwa sababu ya mteja wake kudai shilingi moja kama fidia, alisema mteja wake huyo (Manji) anaamini kuwa heshima na utu vina thamani kuliko fedha.

 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,609
Points
2,000
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,609 2,000
PHP:
"Kuna mkataba kuhusu Quality Finance Cooparation Group na Kagoda Agriculture, lakini haumuhusu Manji kwa sababu kesi hii inahusu udhalilishaji wa mtu na mtu na siyo mtu na kampuni,"alidai Marando. Baada ya Marando kutoa hoja hizo, Wakili wa Mengi Michael Ngaro aliiomba mahakama iiahirishe kesi hiyo ili aweze kuwasiliana na mteja wake Mengi.
This is rubbish ......................huwezi ukadai mteja wako ni safi halafu matendo yake ndani ya kampuni zake na kwningineko hutaki achunguzwe............................katika makosa ambayo manji amefanya ni hili............................kumpa nafasi Mengi kuanika maovu yake hadharani................................this was a colossal error of judgment on part of Manji...................
 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,609
Points
2,000
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,609 2,000
PHP:
Alidai kutokana na hoja hizo, nyaraka zote zilizopelekwa mahakamani hapo na upande wa utetezi hazina msingi, na kwamba ziondolewe mahakamani kwa kuwa zinawapotezea muda.
Haitoshi kusema hazina msingi nyaraka hizo ni muhimu kutoa hoja kwa nini unafikiria hazina msingi?
 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,609
Points
2,000
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,609 2,000
Code:
Marando pia aliutaka upande wa utetezi ueleze umezipata wapi risiti za malipo za serikali kuhusu Kampuni ya Quality Finance Cooparation Group na ni nani aliwapa.
Risiti walikozitoa siyo suala la msingi na ni nani amewapa halihusiki kwenye kesi ila la muhimu ni je risiti hizo ni za kweli? Maswali ya marando yanadhihirisha kuwa ni za kweli.......................maana hahoji uhalali wa ushahidi tajwa?
 
drphone

drphone

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2009
Messages
3,561
Points
1,225
drphone

drphone

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2009
3,561 1,225
sasa kudai fidia ya sh 1 na kuingia na jopo la mawakili wakubwa kwa kesi ya kudai fidia ya sh 1 wapi na wapi je namdharau mengi kwamba ana pesa wakati huo huo anamwogopa ndomana ya kukodi mawakili wengi
 
B

Bajabiri

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Messages
9,743
Points
0
B

Bajabiri

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2011
9,743 0
wahindi wanaigeuza hii nch wanavyotaka!
 
tzjamani

tzjamani

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2010
Messages
996
Points
0
tzjamani

tzjamani

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2010
996 0
Marando naye vipi anatetea mambo kama haya?
 
shanature

shanature

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2010
Messages
739
Points
225
shanature

shanature

JF-Expert Member
Joined Nov 15, 2010
739 225
dili hilo la mhindi manji kwa wanasheria,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,anadhalilisha nchi yetu na wasomi wetu,,,,,,,,,,iwaje mtukama marando aingie kwenyekesi ya sh1,,...hivi huyo mteja wake atakuwa anamlipa hela halili ya jasho lake au ndio anadhihirisha wizi mtupu............sh1,,ufungue kesi kwani nani atashindwa kulipa anataka kuichafua sheria na katiba ya nchi huyu manji,,,,,,,,kwanza kuna sheria japo sikumbuki vizuri katika business law,,,kuwa kesi ya madai au fidia lazima iendane na viwango(gharama)kuanzia kiasi fulani mahakama fulani iweje hiyo ya sh1!ichezee kodi zetu watanzania,,,,,jaji kulipwa na watu kupoteza nguvu kazi kwa ajili ya upuuzi!!!!!sh1!!!,,mtumishi wa serikali analipwa mshahara na kodi yangu,,,,,anasikiliza kesi ya kipuuzi.................hakimu mzima,,
 
N

Nalonga

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2010
Messages
219
Points
195
N

Nalonga

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2010
219 195
dili hilo la mhindi manji kwa wanasheria,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,anadhalilisha nchi yetu na wasomi wetu,,,,,,,,,,iwaje mtukama marando aingie kwenyekesi ya sh1,,...hivi huyo mteja wake atakuwa anamlipa hela halili ya jasho lake au ndio anadhihirisha wizi mtupu............sh1,,ufungue kesi kwani nani atashindwa kulipa anataka kuichafua sheria na katiba ya nchi huyu manji,,,,,,,,kwanza kuna sheria japo sikumbuki vizuri katika business law,,,kuwa kesi ya madai au fidia lazima iendane na viwango(gharama)kuanzia kiasi fulani mahakama fulani iweje hiyo ya sh1!ichezee kodi zetu watanzania,,,,,jaji kulipwa na watu kupoteza nguvu kazi kwa ajili ya upuuzi!!!!!sh1!!!,,mtumishi wa serikali analipwa mshahara na kodi yangu,,,,,anasikiliza kesi ya kipuuzi.................hakimu mzima,,
Mkuu hiyo shilingi 1,ya fidia ambayo yeye anademand ni katika kuonyesha kwamba pesa sio inshu kwake, anachotaka ni Mshtakiwa amwombe radhi for seven consecutive days katika same media ambayo alitumia kumtangaza kama fisadi papa hilo ndio dai la msingi kwake.Pia mahakama itaamua kama atashinda kesi ni fidia kiasi gani alipwe na si hio shilingi moja.
 
S

superfisadi

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2009
Messages
553
Points
195
S

superfisadi

JF-Expert Member
Joined May 22, 2009
553 195
hivi inawezekana kampuni yako ikafanya ufisadi lakini wewe ukawa safi acha tumuone hakimu atahukumu vipi?
 
Somoche

Somoche

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Messages
4,164
Points
2,000
Somoche

Somoche

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2010
4,164 2,000
Manji wewe ni fisadi TEMBO nyie wahindi mmeibia sana hii nchi lakini ipo siku wenyewe tutawachenjia na hapo mtatafta pa kutokea msipaone SIKU HIYO INAKUJA!
 
Mwanamageuko

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2010
Messages
4,645
Points
2,000
Mwanamageuko

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2010
4,645 2,000
dili hilo la mhindi manji kwa wanasheria,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,anadhalilisha nchi yetu na wasomi wetu,,,,,,,,,,iwaje mtukama marando aingie kwenyekesi ya sh1,,...hivi huyo mteja wake atakuwa anamlipa hela halili ya jasho lake au ndio anadhihirisha wizi mtupu............sh1,,ufungue kesi kwani nani atashindwa kulipa anataka kuichafua sheria na katiba ya nchi huyu manji,,,,,,,,kwanza kuna sheria japo sikumbuki vizuri katika business law,,,kuwa kesi ya madai au fidia lazima iendane na viwango(gharama)kuanzia kiasi fulani mahakama fulani iweje hiyo ya sh1!ichezee kodi zetu watanzania,,,,,jaji kulipwa na watu kupoteza nguvu kazi kwa ajili ya upuuzi!!!!!sh1!!!,,mtumishi wa serikali analipwa mshahara na kodi yangu,,,,,anasikiliza kesi ya kipuuzi.................hakimu mzima,,
Tatizo la watanzania ni kutotaka kujua mambo! Fidia ya Sh1 haiwahusu mawakili, je hamjui kwamba ukishindwa kesi kuna gharama za kesi? (bill of cost) na kama ikitokea Mengi akashindwa na Manji basi mjue zigo la malipo ya hao mawakili linamrudia huyo Mengi wenu, ambae nae hana tofauti na huyo Manji wenu! wote ni mafisadi na wamesigana kimaslahi ndio maana mnayaona haya. vinginevyo wangekuwa kimya kama walivyokuwa awali wakifanya biashara pamoja.
 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,609
Points
2,000
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,609 2,000
KESI YA MANJI Vs MENGI: Korti yatupa nyaraka za Mengi


na Happiness Katabazi


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imevikataa vielelezo vya utetezi vilivyowasilishwa na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Ltd, Reginald Mengi, katika kesi aliyofunguliwa na mfanyabiashara Yusuf Manji.
Uamuzi wa kuvikataa vielelezo hivyo vinavyojumuisha nyaraka 14 zikiwamo zinazoihusu kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd ulitolewa mahakamani hapo jana na Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana.
Katika kesi hiyo, Manji anamlalamikia Mengi kwa madai ya kumkashfu akimdai fidia ya shilingi moja kwa kumuita fisadi papa.
Hakimu Katemana alisema amefikia uamuzi huo baada ya kusikiliza hoja za kisheria zilizowasilishwa mbele yake na pande zote mbili kwa siku mbili tofauti.
Akisoma uamuzi wake huo, alisema anakubaliana na hoja za kisheria zilizowasilishwa awali na jopo la mawakili wa mlalamikaji ambao wanaongozwa na Mabere Marando, Richard Rweyongeza, Dk. Ringo Tenga na Beatus Malima kwamba mahakama hiyo itupilie mbali maombi ya mdaiwa (Mengi) ya kutaka nyaraka hizo zikiwemo nyaraka vivuli ambazo zinaonyesha ni mali ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na mkataba baina kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd na Quality Finance Corporation Ltd.
"Kwa kauli moja mahakama hii inatupilia mbali ombi la mdaiwa (Mengi) kwa sababu nyaraka hizo anazotaka kuzitumia kutolea ushahidi hazihusiani na kesi hii kabisa, na pia nyaraka hizo ni vivuli."
Baada ya Hakimu Katemana kumaliza kusoma uamuzi wake, Wakili wa mdaiwa Michael Ngaro anayesaidiwa na Deo Lingia aliinuka kwenye kiti alichokuwa ameketi na kuieleza mahakama kuwa uamuzi wa hakimu huyo haukuwa wa kushtukiza.
Wakili Ngaro alidai kuwa kitendo cha hakimu huyo kuzikataa nyaraka hizo ni wazi sasa kimesababisha mteja wake asizitumie nyaraka hizo kama ushahidi wakati siku atakapoitwa na mahakama hiyo kujitetea na kwamba wanaomba nakala ya uamuzi huo na ili kwenda kuupinga Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Hata hivyo hoja hiyo ya wakili Ngaro ya kutaka kwenda Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa Mahakama ya Kisutu, ulipingwa vikali na mawakili wa mlalamikaji ambao walimwomba Ngaro asiipotezee muda mahakama hiyo kwani katika mabadiliko ya sheria yaliyofanywa na Bunge mwaka 2002 yanakataza kuyakatia rufaa maamuzi madogo (ruling) yanayotolewa na mahakama za chini kabla kesi ya msingi haijamalizika.
Hata hivyo hoja hiyo ya mawakili wa Manji, ilimfanya wakili wa Mengi kuwasilisha ombi jipya la kuiomba mahakama itumie busara zake kwani siku itakapofika mteja wake kuja kujitetea atakosa nyaraka.
Baada ya ombi hilo, Katemana aliahirisha shauri hilo hadi Februari 15 mwaka huu ambapo atatoa uamuzi.
Mapema asubuhi jana wakili wa Mengi, alianza kujibu hoja za mawakili wa mlalamikaji zilizowasilishwa mahakamani hapo Februali 4, mwaka huu, aliomba nyaraka za mteja wake zipokelewe na pingamizi la Manji kutaka nyaraka hizo zisipokelewe litupwe.
 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,609
Points
2,000
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,609 2,000
Mahakama yakataa vielelezo 14 vya Mengi dhidi ya Manji
Friday, 11 February 2011 20:59

Tausi Ally
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imetupitilia mbali nyaraka 14 zilizowasilishwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, kwa sababu hazina msingi.

Katika nyaraka hizo 14 zilizotupiliwa mbali na Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana, upo mkataba kuhusu Kampuni ya Quality Finance Cooparation Group na Kagoda Agriculture.

Akitoa uamuzi huo jana, katika kesi ya madai ya Sh1 iliyofunguliwa na Yusuf Manji dhidi ya Mengi, Katemana alisema anazitupilia mbali nyaraka hizo kwa sababu hazimhusu Manji na hazina kibali kutoka kwa ofisa wa serikali.

Uamuzi huo ulifuatia Wakili wa Manji, Mabere Marando, kuomba mahakama kufuta nyaraka hizo zilizowasilishwa na Mengi kwa sababu haziendani na sheria za mahakama.

Marando alidai kuwa, sheria inakataa nakala zisizo halisi, lakini ipo sheria ambayo inaruhusu kuomba kibali ambacho ilitakiwa upande wa Mengi wakipeleke kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo.

"Na kama waraka unahusu serikali, unatakiwa ufanyiwe marekebisho na ofisa aliyetoa nyaraka hizo na inatakiwa zilipiwe, lakini upande wa Mengi vitu hivyo vyote havijafanyika," alidai Marando.

Aliongeza kudai kuwa, kutokana na hoja hizo, nyaraka zote zilizopelekwa mahakamani hapo na upande wa Mengi hazina msingi, ziondolewe mahakamani na kwamba, zinawapotezea muda kwa kuwa haziendani na sheria.

Pia, Marando aliutaka upande wa Mengi ueleze ulikozipata risiti za malipo za serikali kuhusu Kampuni ya Quality Finance Cooparation Group na aliyempa.

"Kuna mkataba kuhusu Quality Finance Cooparation Group na Kagoda Agriculture, lakini haumhusu Manji kwa sababu kesi hii inahusu udhalilishaji mtu na mtu sio mtu na kampuni," alidai Marando.

Baada ya Marando kutoa hoja hizo, Wakili wa Mengi, Michael Ngaro, alizipinga hoja hizo zilizotolewa na jopo la mawakili wa Manji, Marando, Richard Rweyongeza na Ringo Tenga kwa madai kuwa, vielelezo hivyo vilitolewa wakati usio muafaka na aliomba mahakama isubiri muda ambao shahidi husika atafika kuthibitisha mahakamani.

Lakini akina Marando walipinga hoja hiyo na Hakimu Katemana alifikia uamuzi wa kuvitupilia mbali vielelezo hivyo.

Baaada ya kutolewa uamuzi huo, Ngalo aliomba mahakama kutumia busara kumruhusu aweze kukata rufani Mahakama Kuu dhidi ya uamuzi huo.

Wakati yote hayo yakiendelea mahakamani hapo, Manji alikuwa amekaa akisikiliza kwa makini.

Awali, mahakama hiyo ya Kisutu ilishuhudia mkanda wa video (DVD) wa hotuba ya Mengi wakati akizungumza na waandishi wa habari na alimtaja Manji kuwa ni miongoni mwa mafisadi Papa wanaohujumu nchi.

Watuhumiwa wengine waliotajwa kwenye mkanda huo na Mengi kuwa mafisadi papa, ni Mbunge wa Igunga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC-CCM) na Halmashauri Kuu ya Chama hicho (NEC-CCM) Taifa, Rostam Aziz.

Wengine ni wafanyabiashara, Tanil Somaiya, Jeetu Patel na Subash Pate
 
Drifter

Drifter

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2010
Messages
2,094
Points
2,000
Drifter

Drifter

JF-Expert Member
Joined Jan 4, 2010
2,094 2,000
hivi inawezekana kampuni yako ikafanya ufisadi lakini wewe ukawa safi acha tumuone hakimu atahukumu vipi?
Huu ndio mkakati mama wa kifisadi walioletewa viongozi wetu na hawa ma-mafia wenye asili ya kigeni: unaunda kampuni kibao ili kutenganisha uwepo wa mmiliki (personal entity) na uwepo wa kampuni (corporate entity) na hivyo kuendesha hujuma bila kuwajibika kama mtu binafsi. Wanasheria wanaweza kutuelimisha zaidi kuhusu hili. Rostam ndiye kinara wa mkakati huo na, pengine, ndio kura yake ya turufu inayomweka ndani ya CC ya chama tawala-ambacho hivi sasa kinaendeshwa kama kikundi cha mafiosi.
 

Forum statistics

Threads 1,295,922
Members 498,479
Posts 31,228,141
Top