Kama tuhuma hii ni kweli, then this is The End of Zitto. Karma Ndio Itamaliza Kila Kitu!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,504
113,618
Wanabodi,

Mimi ni muumini wa kitu kinachoitwa "karma" ambayo ndio hukumu pekee ya haki hapa duniani!. Hii karma wakati wa kuhukumu, haina huruma kwa sababu hukumu zake ni za haki, unaweza kulipa mema, au kupigwa na mapigo ya kufidia uovu!.

Karma ni powers of 'cause and effects' ambapo ukitenda mema, utalipwa mema, na ukitenda uovu utaadhibiwa kwa uovu wako.

Chadema walipomtimua Zitto kwa tuhuma za usaliti, nilisema humu kama kweli Zitto ni msaliti, then 'karma itamshughulikia Zitto na kumuadhibu, lakini kama Chadema haikumtendea haki Zitto, then Chadema itaadhibiwa kwa hukumu kali ya 'karma'.

Ni muda mrefu kumekuwa kukitolewa tuhuma mbalimbali kumhusu Zitto na zote kwa sababu ni tuhuma tuu, ama hukanushwa, au kupanguliwa kisha maisha yanaendelea.

Sasa kuna hii tuhuma mpya nimeisoma kumhusu Zitto.


Mpaka sasa, tuhuma hii, haijakanushwa na Zitto mwenyewe, wala haijakanushwa Ikulu, na huku hilo gazeti lilitochapisha tuhuma hiyo, likiachwa kuendelea kupeta!. Mwana Halisi lilipochapisha tuhuma kama hiyo, kesho yake tuu Ikulu iliiytisha press conference kukanusha na haikupita wiki, lilifungwa kifungo cha milele hadi leo!.Sasa kama tuhuma hii ni kweli, then kwa mujibu wa reference ya 'karma', Zitto ni kweli atakuwa ni msaliti, na sasa kiuhakika kabisa bila kupepesa macho, wala kumung'unya maneno, "Huu sasa ndio mwisho rasmi wa Zitto Zuberi Kabwe!".Nimesema huu ndio mwisho rasmi wa Zitto kwa sababu kuna watu kwanye jamii yetu, wamejaaliwa karama mbalimbali hivyo kuwa ni watu very powerful kwa nguvu ya 'karma' ya mema yao!. Sasa inapotokea mtu akatofautiana nao kwenye public, hadi kufikia kunyoosheana nao vidole kwenye media!, kama tuhuma hizo alizomsingizia Mengi ni kweli, then atasalimika, lakini kama sii kweli, that is the end of him!.Kitendo cha Zitto kumsingizia Mengi, jambo kubwa kama hili (if he really did this), then this is the end of Zitto.Hakuna hata mtu mmoja ambaye aliwahi kukorofishana na Mengi publicly akabaki salama!.This is the list ya watangulizi wa Zitto angalia walifanya nini na nini kiliwatokea!.[/SIZE]
  1. Alipishana kauli na wamiliki wa DTV na CTN kuhusu haki za kuonyesha kombe la dunia, vituo hivi vyote vimekufa.
  2. Alipishana kauli na Shabir Dewji kuhusu wahindi kupendelewa, Shabir Dewji aliswekwa lupango na sijui siku hizi yuko wapi?!.
  3. Alipishana kauli na Katibu Mkuu, Mambo ya Ndani, Silvanus Adel alipomtoa Dewji lupango, Adel alimwaga unga wake!.
  4. Alipishana kauli na mmiliki wa Gazeti la Mtanzania, Generali Ulimwengu, kwa gazeti hilo kutoa siri kuwa Mengi anadaiwa na mabenki. Generali alifutiwa uraia na gazeti la Mtanzania likafilisika hadi kuuzwa!.
  5. Alipisha kauli na Lowasa, Mengi akiwa Mwenyekiti wa NEMCI, Lowasa akang'oka!.
  6. Alipishana kauli na Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Shamin Khan, shamim aling'olewa!.
  7. Alipishana kauli na Waziri wa Utawala Bora, Wilson Masilingi, kuhusu "mchezo mchafu" wa ubinafsishaji wa Kilimanjaro Hotel, Masilingi aling'olewa!.
  8. Alipishana kauli na Iddi Simba kwenye mambo ya Uzawa, Iddi Simba alimwagwa!.
  9. Alipishana kauli na Basil Mramba akiwa waziri wa fedha kuhusu kodi ya Jack Pot Bingo, Mramba aling'oka!.
  10. Alipishana kauli na Adam Malima, almanusura Adam, yangemkuta, Sitta akamuombea msamaha!, ndio salama yake!.
  11. Alipishana kauli na Tido kuhusu TV inayolipwa na kodi za wananchi kugombea matangazo na TV binafsi!, Tido aling'oka!.
  12. Alipishana kauli na Waziri wa Mambo ya ndani, kuhusu 'mademu!', Masha, Masha kang'olewa!.
  13. Alipishana kauli na Mmiliki wa Channel Ten, Franco Tramontano, kugombea mademu fulani mamiss, Franco alikamatwa na kutupwa selo akisubiri deportation ya interpol
  14. Hakimu mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Sabas kiwango, alizuia Tramontano asiwe deported, Kiwanga akamwaga unga!.
  15. Akapishana kauli na Rostam Aziz, kwenye issue ya 'fisadi papa na fisadi nyangumi', Rostam alitimuliwa ubunge na sasa ameikimbia nchi!,
  16. Alipishana kauli na Balozi wa Uingereza kwenye kashfa ya Silvadale!, Balozi wa Uingerezwa aliondoshwa!.
  17. Alipishana kauli na Yusuph Manji, kuhusu Manji kuifilisi mifuko ya hifadhi za jamii, sasa soon Manji atafilisiwa!.
  18. Manji alipomfungulia Mengi kesi ya kumdai shilingi 1!, Wakili wa Manji, Sabas Kiwango alipishana kauli na Mengi, Kiwango akasitishwa uwakili!.
  19. Akapishana kauli na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Muhondo kuhusu wawekezaji wazawa kwenye issue ya gesi asilia, Prof. Muhongo katimuliwa uwaziri.
  20. Alipishana kauli na Mkurugenzi Mkuu, TPDC, Yona Kilaghane kuhusu kuweka masharti nafuu wazawa kumiliki vitalu vya gesi, Kilaghane ametimuliwa TPDC!.
  21. Alipishana kauli na wandeshaji wa Kipindi cha "Kiti Moto", Kiti Moto kilikufa.
  22. Alipishana kauli na 'mtangazaji mmoja maarufu' ambaye Mengi alimtaka ajiunge na ITV, huyo mtangazaji akagoma, mpaka leo huyo mtangazaji ni 'majalala', hoin bin taaban na hajawahi kupata tena ajira popote!.
  23. Alipishana kauli na kundi za Ze Comedy, by then lilikuwa na big impact ya watu kuacha shughuli zao kuiwahi Ze Comedy, sasa sasa hawana impact tena!.
  24. Sasa ndio amepishana kauli na Ziito Kabwe, tusubiri nini kitamtokea Zitto and it is soon!.
  25. And the List goes on...
NB. NB. Kama yote yanayosemwa kumhusu Zitto sii kweli kuwa ni msaliti, na haya Zitto aliyoyasema kumhusu Mengi ni kweli, then Zitto ataendelea kudunda na ACT yate itazidi kuja juu 'karma' sasa itaishughulikia Chadema hali kadhalika itamshughulikia tena Mzee Mengi kama ilivyokwisha mshughulikia kwa mengine kule nyuma!.

Uzuri wa karma, ikikushughulikia na kuanguka chini, ukimaliza kukulipa deni la adhabu ya karma ambayo huwa ni kupata mapigo, then unaweza kusimama tena, kunyanyuka na kuendelea kung'ara!.

Jinsi 'karma' inavyofanya kazi, kila tendo jema binadamu analo tenda, linaproduce positive energy ambayo inakurudia mara dufu kwa kukunyooshea mambo yako na kukuletea mafanikio. Kila jambo baya binadamu analotenda, lina produce a negative energy ambayo ikikurudia inakuletea majanga.

Hivyo hata ukiwa ni mtu mbaya lakini ulitenda mema mengi, then kiwango cha mema yako kinaweza kufunika mabaya yako yote, hivyo yeyote atakayekutibua, karma yako inamshughulikia ipasavyo. Uzuri wa Karma, ni haki bin haki, hakuna kuonewa, ni just what goes around comes around, na malipo ya karma ni hapa hapa duniani!. Ubaya wa karma, adhabu yake ni transfarable up to four generations, hivyo kuna watu mambo yao yanawanyookea kwa mema ya wazazi wao, na kuna watu wanapigika kwa mapigo ya wazazi wao!.

Cha muhimu katika maisha yako haya mafupi hapa duniani, jitahidi kutenda wema sana kadri ya uwezo wako ili kudunduliza akiba kubwa ya positive energy kwa watoto wako!, ni bora kuwekeza kwenye wema kuliko kwenye utajiri!, ndio maana mnaweza kushangaa watu wakatili ajabu na wenye roho mbaya za ajabu lakini bado wanafanikiwa!, na watu wenye roho nzuri na wema wa ajabu, wakiishi katika mateso makubwa na umasikini uliotopea!.

Wazungu wanaijua 'karma' kama 'destiny'.

Pasco

Update. Majibu ya Zitto.

Katika gazeti la Taifa Imara la tarehe 23 Machi 2015 kulikuwa na habari yenye kichwa cha maneno ' Zitto amchongea Mengi kwa JK?' Habari hiyo ilibeba maudhui ya 'post' iliyoandikwa katika mtandao wa Mwana Halisi online.

Habari hiyo inaonyesha kuwa Mimi nilikutana na Rais kwa msaada wa watu mbalimbali na katika kikao hicho inadaiwa nilisema kuwa Mengi ndiye aliyechochea wabunge kuishughikia Serikali ya Rais Kikwete ili ianguke.

Ni vema ifahamike kuwa gazeti la Taifa Imara linamilikiwa na Bwana James Rugemalira wa kashfa ya Escrow na kuendeshwa na Bwana Prince Bagenda aliye organise press conference ya mmoja wa mawaziri waliofukuzwa kazi kwa kashfa hiyo. Vile vile chanzo cha habari hiyo ni mtandao wa Mwana Halisi online ambao unaendeshwa mmiliki wa Mawio gazeti ambalo kila wiki lina habari za kutunga dhidi yangu na chama cha ACT Wazalendo.

Habari hiyo ni ya kutunga yenye fitna zenye lengo la kuchonganisha watu. Naomba kufafanua ifuatavyo

1 Taarifa Maalumu ya Kamati ya PAC kuhusu ufisadi wa tshs 306 bilioni za Escrow hauhusiki na Bwana Reginald Mengi kwa namna yeyote ile. Mengi sio mbunge, sio mjumbe wa PAC na hakushawishi PAC kwa namna yeyote ile. Wezi wa Escrow wasitapetape kutafuta mchawi wakati mchawi ni wizi wao wenyewe. Porojo za kwamba Mengi alihonga wabunge ili kuishughulikia Serikali zinabaki porojo tu. Ila kama kuna mtu ana chembe ya ushahidi wa jambo hilo apeleke kwenye vyombo vya dola kwa hatua kuliko kurudia rudia porojo hizo kwenye vyombo vya habari.

2 Sihitaji kutumia watu ili kukutana na Rais Jakaya Kikwete kwani ninaweza kukutana naye kwa taratibu za kawaida kabisa za kiserikali. Hadithi ya kwamba nimeomba watu wanikutanishe na Rais inaonyesha namna mwandishi alivyoshindwa kutunga uongo wake. Katika kukutana kwangu na Rais kikazi sijawahi hata mara moja kuzungumzia watu. Hivyo kusema nilikwenda Ikulu kumzungumzia Bwana Mengi ni kunidharau na kuidhalilisha Taasisi ya Urais.

3 Nimemwelekeza mwanasheria wangu achukue hatua za kisheria dhidi ya Gazeti la Taifa Imara na vilevile Gazeti la Mawio kwa mfululizo wa habari za kutunga uongo dhidi yangu kila kukicha. Nimeagiza tupeleke mashtaka kwenda Baraza la Habari Tanzania ili magazeti hayo yathibitishe habari zao.

Zitto Kabwe
Kiongozi wa ACT Wazalendo
Angalizo: Kuna nyuzi nyingine ni info pack, hivyo ikipandishwa inakuwa imeshiba datas na kujitosheleza, naomba muichukulie tuu kama umesoma habari ya gazeti, huwezi kumuuliza chochote mwandishi wa habari hiyo.

Samahani kwa kutochangia uzi huu, wala kujibu hoja yoyote kuhusu "Karma", ila wale wenye kuguswa na kupenda kujua zaidi kuhusu 'Karma', nimepandisha uzi maalum kuhusu karma, wele wenye maswali kuhusu karma, nitayajibu hapa
[h=3]Topic: "The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki[/h]Pia nimewahi kupandisha nyuzi nyingine mbili kuhusu karma.
Opinion: Kung'atuka Kwa Zitto, Chadema, Msishangilie Subirieni "Karma!".

"Bora Katiba", Tuikubali!, Tusiichukie CCM!, Kwa Sababu Itahukumiwa na "Karma!".

Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Kila Kitu. Wengi wanazo


Pasco
 
Zitto mtoto wa kigoma kauingia mji kwa pupa,anaishi kwa kuuza maneno na kutaka madaraka makubwa.Tangu alipohongwa tsh 50m na DG wa CHC ili amtoe uwaziri wa fedha Mkulo ili CHC isivunjwe sina hamu naye,pia mwaka jana kwenda nyumbani kwa Membe kufanya kikao Nape na Kinana wakiwepo
 
Hivi kwamaana iyo Mengi ni Mungu anayeioshi dunaian ambaye kila mgusaye lazima ataharibikiwa??
Pasco nafkri ulikuwa unatafuta namna ya kuonyesha Zitto kakosea baada ya taarifa ya habari ya jana lkn pia ayo uliyounganisha wee hapa na wahanga wa matukio yaliyopita sio sahihi.

zito akishindwa atashhindwa kwa mengi wala sio aya ya Mengi.....................kwan huyu mengi anao usafi gani hasa??
 
Last edited by a moderator:
Wafanyabiashara wanatuvuruga, hakuna mgogoro hapo naona ni huano wa makundi ya wagombea urais na kwa kuwa wafanyabiashara wanaamua nani wamuweke hivyo kila mtu anamgombea wake ndo maana wanalumbana wao kupitia wanansiasa njaa
 
Mlio karibu na Zitto mwambieni Sifa anazozipenda Sana kuwazidi wanawake zitamtokea puani!!!!

Si Mara moja hata JK mwenyewe amewahi lalamika ingali Zzk akiwa CDM kwamba huyo kijana ni mnafiki na anamfwata fwata Sana.... JK alisema, "huyu kijana anamatatizo gani? si ajenge chama chake?"

Zitto ni mnafiki na ndumilakuwili Wa viwango vya juu Sana!!! maji aliyoyaingia ni kina kirefu Sana kwake soon atazama!!!

Watu Kama akina Mbowe....Lipumba.... Mbatia..... Dr. Slaa Zitto si saizi yake kabisa ila kwakuwa anapewa Sifa za kijinga na wapuuzi wenzie anaamini anaweza pambana na yeyote na sasa amemwingia Mengi!!!!

Huyo dogo malezi na jamii aliyokulia inaonekana ni yakitumwa iliyokosa nidhamu na adabu.....


Very soon ataona outcome ya Upuuzi wake......
 
Last edited by a moderator:
serikali itajitutumua soon kumlinda zitto kwa kulifungia gazette kuandika uongo na ikulu itakanusha na hata ziito atakanusha, subiri! lakini kwa vyovyote vile uhaini ni suala baya sana srikali hapa ingekuwa imechukuwa hatua lakini kujivuta huku kunatia mashaka. kuna mahali hapako vizuri ama hawakutarajia haya ya zitto kumchongea mengi kuvuja hivyo wanajiandaa kujibu kwa maana wameshtukizwa au ............................
 
Wafanyabiashara wanatuvuruga, hakuna mgogoro hapo naona ni huano wa makundi ya wagombea urais na kwa kuwa wafanyabiashara wanaamua nani wamuweke hivyo kila mtu anamgombea wake ndo maana wanalumbana wao kupitia wanansiasa njaa

wanatuvurugaje sasa? mengi ametaka ufafanuzi kutoka kwa serikali kwa taarifa iliyochapishwa ikimuhusisha na uhaini (kuiangusha serikali kila mara) na aliyetoa taarifa hizo kwa serikali (rais) ni zitto. Mengi anataka ufafanuzi taarifa hiyo ni sawa kuachwa bila kuchukuliwa hatua ili yeye awe salama kwa maana nyingine anataka asafishwe, sasa hapo kuna kuyumbishwa gani?
 
Pasco mimi na wewe tunajuana vyema mkuu maana hapa JF tumeanza wote . Hebu come out clean hapa au hata sirini sema ugomvi wako na Chadema ni upi ?
 
Back
Top Bottom