Yussuf Manji, Omba Toba

Yussuf Manji, Omba Toba

KWANINI UNAMSHAMBULIA MUISILAAM MWENZETU?HUONI KAMA UNAWAPA WAKRISTU NGUVU YA KUUZOOFISHA UISLAMU?KWANINI HUKUSEMA HAYA KULE FARAGHANI

Faragha gani mkuu? Yaani dada yetu akaongee na Manji faraghani!! Hiyo hapana mkuu!!!
 
Wewe Mmawia chuki zako kwa chama cha kimakinikia angalia wapi unazielekeza. Wakati mwingine unakosea! Kama hapa unapinga hoja za FF kwa sababu tu ni mwanachama wa chama cha makinikia japo hoja yake yake ni ya kweli kabisa kuwa Manji kwa kushirikiana na mafisadi wenzake wa Bakwata wamehujumu mali za Waislam. Katika hoja hii hakuna ushabiki wa kisiasa au Simba na Yanga: Manji kawakosea Waislam na anavuna alichopanda ukiamini sawa usipoamini sawa.
Siwezi kuamini porojo za kimakinikia

In God we trust
 
ni Vema , akaomba Radhi na akaamua kuanzisha MAnji Trust, na pia kama ulivoshauri dada ni kwamba ASIVIRUDISHE BAKWATA WATAVIUZA TENA! Ahakikishe yeye mwenye awe msimamizi wa kuvielndeleza! Pole Mnji! Nakuombea kwa Mwenye ez Mungu akuzindue na uombe Toba ya kweli nae akuswameh! HAKUNA MKAMIFU :WAKHULIKA ALINSAANA DHAI'FAA" amemuumba mwanadamu Dhaif, basi Mola Mwingi wa kuswameh akuswameh baada ya wewe kuomba Toba!

MLILIE MOLA WAKO ASAA AKAKUSIKIA! ALLAHUMMA INNA KAAFUWWUN TUHIBBUL AFUA FAAFUANNA! Mwenye ez Mungu hupenda kuombwa toba! In sha ALLAh ni mWingi wa Kuswameh
 
Hayo maombi mabaya mlitakiwa kuyaelekeza bakwata sio kwa mtu aliyeuziwa kihalali
Yeye ndo anashawishi watu na hela zake. Kuna mahali Bakwata waliweka bango kuwa wanauza ? Mbinu hizo hizo ndo alitumia kuwarubuni Manispaa Kino wampe coco beach.
 
Duuu....madrassa niwe Kibarua wako..wa kukubebea Quran au???

Kama amesoma madrasa na ana hela ya kufa mtu hawezi kukuajiri wewe na PhD yako?! Mbona wapo wengi tu na shule zao lakini mabosi wao wanaowaweka mjini wengine hata darasa la saba hawakumaliza.
 
Kama amesoma madrasa na ana hela ya kufa mtu hawezi kukuajiri wewe na PhD yako?! Mbona wapo wengi tu na shule zao lakini mabosi wao wanaowaweka mjini wengine hata darasa la saba hawakumaliza.


Sawa ila sijawai ona...........Mwenye..........
 
Hili si la kisiasa mkuu na mimi namuona yupo sahihi na japo nakichukia kile chama chao lakini kwa hapa naunga mkono hoja.
Hujakatazwa kuamini unachokiamini kwa dhati nami siwezi kuwa bendera fuata upepo kisa kasema kikongwe Fayza Fox

In God we trust
 
Waliouza Viwanja hamkuwaombea Dua, Mnamuombea mnunuzi aliyeuziwa na viongozi wenu!! Wauzaji hadi Leo hamkuwahi hata kuwapeleka MAHAKAMANI!!Na ndo hao wagawa tende na nyama misikiti zitokazo Arabuni, Maajabu ya Muda haya
'Buyer be aware !'
 
Yussuf Manji, ni matumaini yangu kuwa ujumbe huu utakufikia popote ulipo.

Binafsi kama Muislam mwenzako nnachukuwa fursa hii kukukumbusha kuwa hakuna kitu bora kama kukiri na kukubali makosa yako na kuomba toba.

Toba nnayokushauri kuiomba hapa, si kwa serikali wala kwa watawala. Toba nnayokukumbusha mimi kuiomba ni kwa Mola wako Muumba mbingu na ardhi.

Manji uliwakosea sana Waislam kipindi cha nyuma kiasi, kwa kutumia fedha zako kununulia viwanja vya wakf vya Waislam, na kuwa mkaidi kila uliposemeshwa kuhusu hilo.

Viwanja hivyo ambavyo historia inaonyesha kuwa vilikuwa vijengwe chuo kikuu cha kwanza Tanganyika (hilo halikufanyika lakini hilo ni simulizi jingine kabisa ambalo Alama Mohamed Said anaweza kulisimulia vizuri zaidi).

Ulifatwa na Waislam wakikuomba kuwa mkataba ulioingia na BAKWATA ni wa kidhalimu na haufai lakini kwa ukaidi wako hukuwasikiliza na uliwatoa njiani na kuendelea na mkataba wako.

Sakata la viwanja hivyo lilipelekea Waislam kufungwa, kupigwa na kujeruhiwa mpaka walipoona kuwa hawakuwezi kwa ajili ya kutumia fedha zako na nguvu ya baadhi ya waliokuwa BAKWATA, Waislam wakafikia maamuzi makali ya kuwa sasa wanakushtaki kwa Mwenyeezi Mungu.

Miaka imepita ukidhani kuwa shtaka hilo halina meno kwako, lakini leo tunashuhudia ukigeukwa kila upande.

Aibu ya kushikwa na kuwekwa ndani pekee si ndogo kwa mtu wa "caliber" yako. Licha ya kupimwa na kukutwa kuwa u mlevi wa madawa, tumeona sakata la Oysterbay likikutia hasara kubwa sana, tumeona wafanyakazi wako wakifungiwa kuingia kwenye ofisi zao, tunasikia akaunti zako zinafungiwa kila kukicha.

Kama hiyo haitoshi, tunasikia umepatwa na matatizo ya moyo. Mwenyezi Mungu anasema katika Qur'an tukufu:

Qur'an 2:10. Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi. Basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uwongo. Maelezo

Kwa yote hayo bado tu hujashtuka ni kwanini yakukute yote hayo? Nakusihi, zingine zote ni sababu lakini ukweli unabaki kuwa ukweli, Waislam wameitikiwa dua zao dhidi yako.

Yussuf Manji tunakutaka usiwe katika wale ambao:

Qur'an 2:7. Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao, na juu ya macho yao pana kifuniko. Basi watapata adhabu kubwa. Maelezo

Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe na hachoki kusamehe, tunakutaka uombe toba kwa mola wako, umtake radhi, uwatake radhi na Waislam na uwarudishie viwanja vyao na mali zao, tena usithubutu kuvirudisha kwa wale wale waliokuuzia, itakuwa haina maana kabisa. Virudishe kwenye taasisi za Kiislam zenye kumuogopa Mwenyezi Mungu au tumia viwanja hivyo hivyo kuanzisha Manji Islamic Trust Fund na uiendeshe mwenyewe kwa manufaa ya Waislam.

Fata nasaha hizo uone mambo yatavyokunyookea.

Jikumbushe:

Maimamu kumsomea Manji Ahla-badri

Mjue Sheikh Ponda Issa Ponda na Kundecha

Waislamu wataka jengo lao toka Quality Group | Bongo5.com

MKATAMBUGA: WAISLAMU WAMELOGWA NA NANI?

Manji hakuna wakukuokoa katika haya na hayatokwisha ukifanya dharau isipokuwa wewe mwenyewe, anza kwa kumrudia Allah na kumuomba toba.

Na Mwenyeezi Mungu ndiye ajuwae zaidi.
Sema Alichokosa.
 
Kwanza kesi ya Manji inayomkabili sasa hivi wala haihusiani na dua zenu mlizomsomea, Manji anatuhumiwa kukutwa na Sare za Jeshi, Kwahiyo unataka kusema kama Manji angewarudishia kile Kiwanja chenu cha Wakfu hizi kesi asingekamatwa nazo?Hivyo Mungu wenu angeweza kumlinda Manji aendelee kuhujumu Nchi? Usiusianishe kesi ya Manji na Zile Dua zenu
We muabudu sanamu utaelewa nini, kama umeshindwa kutofautisha Mungu na sanamu !
 
Sawa ila sijawai ona...........Mwenye..........

Wewe kutokuona haina maana kuwa hawapo na inawezekana huwaoni kwa sababu tu ya ushamba wako. Kwani mzee Bakhresa ana digrii ngapi mkuu?! Mbona kawaajiri wengi tu katika hao wanaojifanya wamesoma sana (watu wa kanisa) na wanamwita bosi wakimuona?
 
Back
Top Bottom