Yussuf Manji, Omba Toba

Yussuf Manji, Omba Toba

wauzaji hawakupigwa albadir? mbona hadi leo ndiyo wenye jukumu la kutangaza mwezi umeandama nakugawa tende za msaada toka arabuni?
Waliouza Viwanja hamkuwaombea Dua, Mnamuombea mnunuzi aliyeuziwa na viongozi wenu!! Wauzaji hadi Leo hamkuwahi hata kuwapeleka MAHAKAMANI!!Na ndo hao wagawa tende na nyama misikiti zitokazo Arabuni, Maajabu ya Muda haya
 
Faiza Fox wapeleke MAHAKAMANI waliouza eneo menu LA Wakfu, Na kama Dua Wasomeee hao waliouza sio mnunuzi, Msitake kumsimanga Manji kwa utajiri wake. Kesi anazokabiliana Nazi MAHAKAMANI hazihusiani na Zile Dua zenu, Kama zilishindwa kuwateketeza waliouza Viwanja vyenu vya Wakfu, Vitawezaje kumteketeza mnunuzi? Mungu humlinda MTU mwenye Haki.
 
Wangewasomea Dua waliouza Kiwanja chao cha Wakfu, Wao walimsomea mnunuzi wa Kiwanja Chao aliyeuziwa kwa halali kabisa!! Wakawaacha wauzaji wakiendelea kugawa tende na nyama misikitini toka Uarabuni na kutangaza mwandamo wa mwezi.!!! Haya ni maajabu kabisa!! Toeni taarifa waliouza Sasa hivi wapo wapi na wanafanya nini?
 
Faiza Fox wapeleke MAHAKAMANI waliouza eneo menu LA Wakfu, Na kama Dua Wasomeee hao waliouza sio mnunuzi, Msitake kumsimanga Manji kwa utajiri wake. Kesi anazokabiliana Nazi MAHAKAMANI hazihusiani na Zile Dua zenu, Kama zilishindwa kuwateketeza waliouza Viwanja vyenu vya Wakfu, Vitawezaje kumteketeza mnunuzi? Mungu humlinda MTU mwenye Haki.
Mkuu USIANGALIE UPANDE MMOJA
BORA YA HUYO MANJI HADI LEO YUPO KTK ADHABU YA DUNIA
KULIKO ALIEKUA SHEKH MKUU NA NDO ALIEKUA MHUSIKA MKUU NAE ASHATANGULIA MBELE YA HAKI
ALBADIR AU QUNUUT IKISOMWA HIO MKUU HUA HAICHAGUI
ANGEKUA HAI MCHUNGAJI MTIKILA UNGEMUULIZA
WEWE TEMBEZA TU HILO DOMO LAKO NA ALFJIR HII
MA MTU YANAKUANGALIA TU,,
JIANGALIE NA HALI YAKO KWANZA

Sent from Calculator Phone vesion007
 
Kwanza kesi ya Manji inayomkabili sasa hivi wala haihusiani na dua zenu mlizomsomea, Manji anatuhumiwa kukutwa na Sare za Jeshi, Kwahiyo unataka kusema kama Manji angewarudishia kile Kiwanja chenu cha Wakfu hizi kesi asingekamatwa nazo?Hivyo Mungu wenu angeweza kumlinda Manji aendelee kuhujumu Nchi? Usiusianishe kesi ya Manji na Zile Dua zenu

Qur'an 28:
55. Na wanapo sikia upuuzi hujitenga nao na husema: Sisi tuna vitendo vyetu, na nyinyi mna vitendo vyenu. Salamun Alaikum, Amani juu yenu! Sisi hatutaki kujibizana na wajinga.
 
Yussuf Manji, ni matumaini yangu kuwa ujumbe huu utakufikia popote ulipo.

Binafsi kama Muislam mwenzako nnachukuwa fursa hii kukukumbusha kuwa hakuna kitu bora kama kukiri na kukubali makosa yako na kuomba toba.

Toba nnayokushauri kuiomba hapa, si kwa serikali wala kwa watawala. Toba nnayokukumbusha mimi kuiomba ni kwa Mola wako Muumba mbingu na ardhi.

Manji uliwakosea sana Waislam kipindi cha nyuma kiasi, kwa kutumia fedha zako kununulia viwanja vya wakf vya Waislam, na kuwa mkaidi kila uliposemeshwa kuhusu hilo.

Viwanja hivyo ambavyo historia inaonyesha kuwa vilikuwa vijengwe chuo kikuu cha kwanza Tanganyika (hilo halikufanyika lakini hilo ni simulizi jingine kabisa ambalo Alama Mohamed Said anaweza kulisimulia vizuri zaidi).

Ulifatwa na Waislam wakikuomba kuwa mkataba ulioingia na BAKWATA ni wa kidhalimu na haufai lakini kwa ukaidi wako hukuwasikiliza na uliwatoa njiani na kuendelea na mkataba wako.

Sakata la viwanja hivyo lilipelekea Waislam kufungwa, kupigwa na kujeruhiwa mpaka walipoona kuwa hawakuwezi kwa ajili ya kutumia fedha zako na nguvu ya baadhi ya waliokuwa BAKWATA, Waislam wakafikia maamuzi makali ya kuwa sasa wanakushtaki kwa Mwenyeezi Mungu.

Miaka imepita ukidhani kuwa shtaka hilo halina meno kwako, lakini leo tunashuhudia ukigeukwa kila upande.

Aibu ya kushikwa na kuwekwa ndani pekee si ndogo kwa mtu wa "caliber" yako. Licha ya kupimwa na kukutwa kuwa u mlevi wa madawa, tumeona sakata la Oysterbay likikutia hasara kubwa sana, tumeona wafanyakazi wako wakifungiwa kuingia kwenye ofisi zao, tunasikia akaunti zako zinafungiwa kila kukicha.

Kama hiyo haitoshi, tunasikia umepatwa na matatizo ya moyo. Mwenyezi Mungu anasema katika Qur'an tukufu:

Qur'an 2:10. Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi. Basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uwongo. Maelezo

Kwa yote hayo bado tu hujashtuka ni kwanini yakukute yote hayo? Nakusihi, zingine zote ni sababu lakini ukweli unabaki kuwa ukweli, Waislam wameitikiwa dua zao dhidi yako.

Yussuf Manji tunakutaka usiwe katika wale ambao:

Qur'an 2:7. Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao, na juu ya macho yao pana kifuniko. Basi watapata adhabu kubwa. Maelezo

Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe na hachoki kusamehe, tunakutaka uombe toba kwa mola wako, umtake radhi, uwatake radhi na Waislam na uwarudishie viwanja vyao na mali zao, tena usithubutu kuvirudisha kwa wale wale waliokuuzia, itakuwa haina maana kabisa. Virudishe kwenye taasisi za Kiislam zenye kumuogopa Mwenyezi Mungu au tumia viwanja hivyo hivyo kuanzisha Manji Islamic Trust Fund na uiendeshe mwenyewe kwa manufaa ya Waislam.

Fata nasaha hizo uone mambo yatavyokunyookea.

Jikumbushe:

Maimamu kumsomea Manji Ahla-badri

Mjue Sheikh Ponda Issa Ponda na Kundecha

Waislamu wataka jengo lao toka Quality Group | Bongo5.com

MKATAMBUGA: WAISLAMU WAMELOGWA NA NANI?

Manji hakuna wakukuokoa katika haya na hayatokwisha ukifanya dharau isipokuwa wewe mwenyewe, anza kwa kumrudia Allah na kumuomba toba.

Na Mwenyeezi Mungu ndiye ajuwae zaidi.
Yanaendelea mateso juu yake,malipo hapa hapa duniani alikuwa anafurahi waislam walipokuwa wanakaa gerezani Leo zamu yake
 
Acha mikwara.

Siyo mikwara mkuu. Huyu Manji kuna kipindi kibri chake kilizidi. Hivyo viwanja anavyoongelea mtoa mada huyu jamaa alishirikiana na mafisadi wa BAKWATA kuvihujumu. Wale wazee wa njaa pale BAKWATA walimuuzia viwanja vya wakfu kinyume na sheria ya Kiislam inayokataza kuuza viwanja vya wakfu. Kwa ufisadi huu na kukataa kwake kuvirudisha kwa Waislam hata baada ya kuambiwa ni sawa tu haya yanayomkuta hivi sasa. Haki ya mtu daima haipotei. What goes around comes around! Time will tell.
 
Hayo maombi mabaya mlitakiwa kuyaelekeza bakwata sio kwa mtu aliyeuziwa kihalali

Hakuuziwa kihalali mkuu bali walishirikiana wote kufanya ufisadi. Ni kama ile mikataba ya kinyonyaji ya madini japo inaonekana halali katika macho ya sheria lakini kuna uharamu na ufisadi mkubwa nyuma yake.
 
Wakumbushe na wale wanaofanya Mazoezi ya Karate na Ugaidi wafanye toba maana wanainajisi dunia.

Nadhani utakuwa unawazungumzia wale magaidi wa kule Dodoma waliowaua wale watafiti wa udongo baada ya mchungaji kupitia kipaza sauti kuwakusanya kijiji kizima kwenda kufanya mauaji. Hivi kesi yao iliishia wapi wale?!! Maana sijaisikia tena toka wakati ule. Kuna magaidi wengi tu huko madhabahuni lakini hutosikia wakifikishwa mahakamani.
 
Mimi nilijifundisha kung fu hapo YWCA Dar 70s.

Dada muulize Faru Dume mwenye posti namba 44 na 50 akupe mrejesho wa kesi ya wale magaidi walioua watafiti wa udongo kule Dodoma wakiongozwa na mchungaji wao aliyewaita kwa kipaza sauti kwenda kuzimaliza roho zisizo na hatia.
 
Hivi kwanini waislam mnapenda kulalama sana? Hiyo EAMWS si mlishindwa wenyewe kuanzisha kwa upunguani wa viongozi? Leo mnamtupia lawama nani?

Usikurupuke kujibu kama hujui nini kinachojadiliwa. Soma mada kwa umakini na utoe majibu au maelezo ya kile kilichoandikwa. Si vizuri kujitoa ufahamu na kujitia utaalamu ambao hauna. Wakati mwingine kunyamaza ni busara na bora zaidi. Kumbuka, anyamazaye kimya amesalimika.
 

Qur'an 28:
55. Na wanapo sikia upuuzi hujitenga nao na husema: Sisi tuna vitendo vyetu, na nyinyi mna vitendo vyenu. Salamun Alaikum, Amani juu yenu! Sisi hatutaki kujibizana na wajinga.
Angalia usije ukawa wewe ndiye mjinga
 
Naona umevimbiwa na mihogo hapo msoga

Wewe Mmawia chuki zako kwa chama cha kimakinikia angalia wapi unazielekeza. Wakati mwingine unakosea! Kama hapa unapinga hoja za FF kwa sababu tu ni mwanachama wa chama cha makinikia japo hoja yake yake ni ya kweli kabisa kuwa Manji kwa kushirikiana na mafisadi wenzake wa Bakwata wamehujumu mali za Waislam. Katika hoja hii hakuna ushabiki wa kisiasa au Simba na Yanga: Manji kawakosea Waislam na anavuna alichopanda ukiamini sawa usipoamini sawa.
 
Wasio waislam tuachieni mambo yetu kila dini ina mfumo wake FaizaFoxy ametoa rai positive kwa muislam mwenzake, ni juu ya huyo mlengwa kukubali au kukataa, ila labda na sisi tumuombe Allah amsamehe, ila kwa makosa ya ''dhulma'' short cut ni kurudisha kwanza, all n all Allah knows the best
 
Back
Top Bottom