Yussuf Manji ni Muislam na aliwakosea Waislam na ni wajibu wetu kukumbushana.
Toba ni kwa yeyote.
Huo ni uongo Manji hakudhulumu BAKWATA ndiyo waliowadhulumu. Hata hivyo yampatayo Manji yengempata tu awe ameshitakiwa kwa Mungu au hajashitakiwa as long as haonewiHakuna anaeomba mabaya isipokuwa Mwenyezi Mungu kaahidi, anayedhulumu huzidishiwa hasara.
Manji hakuombewa mabaya, Manji kashtakiwa kwa Mwenyezi Mungu.
Na sasa tunamkumbusha aombe toba.
Hiyo ni SHERIA na siyo kakanuni !!Siyo kanuni yao
Mimi nilijifundisha kung fu hapo YWCA Dar 70s.
Manji alitakiwa ajitambue na sio jeuri ya Pesa kwa waislamu wenzake.. Hivi leo watu wachache kama ilivyotokea kwa Bakwata watangaze kuuza mali yoyote ya wakfu, wewe kama unajitambua unaweza kununua kweli.? Ilhali unajua kuwa mali ikitolewa kwa ajili ya Umma au Wakfu ni haramu mtu kununua. Manji aliangalia faida zaidi ya mali kuliko hasara kwa waislamu kupoteza mali zaoFaiza elewa Manj sio wa kulaumiwa asilimia 100. Bakwata na hao masheikh ndio wa kulaumiwa kwani Mali nyingi za waislam inayosimamiwa na bakwata zimeuzwa kinyemela.
Kumbe mtu akikulia vibaya unampa za uso?Mimi nilijifundisha kung fu hapo YWCA Dar 70s.
Wanaojilipua na kufanya vitendo vya kigaidi ni hatari zaidi ya Manji.Waombeeni hao nao wapate Mikosi na mabalaa ili wapotee kwenye uso wa dunia ya wastaarabu.
Yussuf Manji, ni matumaini yangu kuwa ujumbe huu utakufikia popote ulipo.
Binafsi kama Muislam mwenzako nnachukuwa fursa hii kukukumbusha kuwa hakuna kitu bora kama kukiri na kukubali makosa yako na kuomba toba.
Toba nnayokushauri kuiomba hapa, si kwa serikali wala kwa watawala. Toba nnayokukukumbusha mimi kuiomba ni kwa Mola wako Muumba mbingu na ardhi.
Manji uliwakosea sana Waislam kipindi cha nyuma kiasi, kwa kutumia fedha zako kununulia viwanja vya wakf vya Waislam, na kuwa mkaidi kila uliposemeshwa kuhusu hilo.
Viwanja hivyo ambavyo historia inaonyesha kuwa vilikuwa vijengwe chuo kikuu cha kwanza Tanganyika (hilo halikufanyika lakini hilo ni simulizi jingine kabisa ambalo Alama Mohamed Said anaweza kulisimulia vizuri zaidi).
Ulifatwa na Waislam wakikuomba kuwa mkataba ulioingia na BAKWATA ni wa kidhalimu na haufai lakini kwa ukaidi wako hukuwasikiliza na uliwatoa njiani na kuendelea na mkataba wako.
Sakata la viwanja hivyo lilipelekea Waislam kufungwa, kupigwa na kujeruhiwa mpaka walipoona kuwa hawakuwezi kwa ajili ya kutumia fedha zako na nguvu ya baadhi ya waliokuwa BAKWATA, Waislam wakafikia maamuzi makali ya kuwa sasa wanakushtaki kwa Mwenyeezi Mungu.
Miaka imepita ukidhani kuwa shtaka hilo halina meno kwako, lakini leo tunashuhudia ukigeukwa kila upande.
Aibu ya kushikwa na kuwekwa ndani pekee si ndogo kwa mtu wa "caliber" yako. Licha ya kupimwa na kukutwa kuwa u mlevi wa madawa, tumeona sakata la Oysterbay likikutia hasara kubwa sana, tumeona wafanyakazi wako wakifungiwa kuingia kwenye ofisi zao, tunasikia akaunti zako zinafungiwa kila kukicha.
Kama hiyo haitoshi, tunasikia umepatwa na matatizo ya moyo. Mwenyezi Mungu anasema katika Qur'an tukufu:
Qur'an 2:10. Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi. Basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uwongo. Maelezo
Kwa yote hayo bado tu hujashtuka ni kwanini yakukute yote hayo? Nakusihi, zingine zote ni sababu lakini ukweli unabaki kuwa ukweli, Waislam wameitikiwa dua zao dhidi yako.
Yussuf Manji tunakutaka usiwe katika wale ambao:
Qur'an 2:7. Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao, na juu ya macho yao pana kifuniko. Basi watapata adhabu kubwa. Maelezo
Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni wingi wa kusamehe na hachoki kusamehe, tunakutaka uombe toba kwa mola wako, umtake radhi, uwatake radhi na Waislam na uwarudishie viwanja vyao na mali zao, tena usithubutu kuvirudisha kwa wale wale waliokuuzia, itakuwa haina maana kabisa. Virudishe kwenye taasisi za Kiislam zenye kumuogopa Mwenyezi Mungu au tumia viwanja hivyo hivyo kuanzisha Manji Islamic Trust Fund na uiendeshe mwenyewe kwa manufaa ya Waislam.
Fata nasaha hizo uone mambo yatavyokunyookea.
Jikumbushe:
Maimamu kumsomea Manji Ahla-badri
Mjue Sheikh Ponda Issa Ponda na Kundecha
Waislamu wataka jengo lao toka Quality Group | Bongo5.com
MKATAMBUGA: WAISLAMU WAMELOGWA NA NANI?
Manji hakuna wakukuokoa katika haya na hayatokwisha ukifanya dharau isipokuwa wewe mwenyewe, anza kwa kumrudia Allah na kumuomba toba.
Na Mwenyeezi Mungu ndiye ajuwae zaidi.
Kwa hiyo wewe unashauri fanye nini badala ya kuomba toba?akiomba toba sasa si anakubali kosa afu mwanzoni alikataa nini
Ujumbe mzuri na si kwa Manji tu na kwa waislam wote wasiojielewa, na wako wengi mali na vyeo vianawadanganya thank you sister.Yussuf Manji, ni matumaini yangu kuwa ujumbe huu utakufikia popote ulipo.