Yussuf Manji, Omba Toba

Yussuf Manji, Omba Toba

Waislamu kwa kuombeana mabaya hamjambo! kila kukicha albadirr! hivi mnafikiri Mungu ni wa kuhukumu tu? kazi kubwa ya Mungu ni kusamehe jamani. Ndio maana ktk Ukristo tunaambiwa tusamehe 7 mara 70
...mbona yule mungu wenu hamkumsamehe mara hizo, mpaka mkamtundika mtini tena kwa dhambi zenu ! Acha kuleta kichaa chako pilipili kichaa
 
Yussuf Manji, ni matumaini yangu kuwa ujumbe huu utakufikia popote ulipo.

Binafsi kama Muislam mwenzako nnachukuwa fursa hii kukukumbusha kuwa hakuna kitu bora kama kukiri na kukubali makosa yako na kuomba toba.

Toba nnayokushauri kuiomba hapa, si kwa serikali wala kwa watawala. Toba nnayokukumbusha mimi kuiomba ni kwa Mola wako Muumba mbingu na ardhi.

Manji uliwakosea sana Waislam kipindi cha nyuma kiasi, kwa kutumia fedha zako kununulia viwanja vya wakf vya Waislam, na kuwa mkaidi kila uliposemeshwa kuhusu hilo.

Viwanja hivyo ambavyo historia inaonyesha kuwa vilikuwa vijengwe chuo kikuu cha kwanza Tanganyika (hilo halikufanyika lakini hilo ni simulizi jingine kabisa ambalo Alama Mohamed Said anaweza kulisimulia vizuri zaidi).

Ulifatwa na Waislam wakikuomba kuwa mkataba ulioingia na BAKWATA ni wa kidhalimu na haufai lakini kwa ukaidi wako hukuwasikiliza na uliwatoa njiani na kuendelea na mkataba wako.

Sakata la viwanja hivyo lilipelekea Waislam kufungwa, kupigwa na kujeruhiwa mpaka walipoona kuwa hawakuwezi kwa ajili ya kutumia fedha zako na nguvu ya baadhi ya waliokuwa BAKWATA, Waislam wakafikia maamuzi makali ya kuwa sasa wanakushtaki kwa Mwenyeezi Mungu.

Miaka imepita ukidhani kuwa shtaka hilo halina meno kwako, lakini leo tunashuhudia ukigeukwa kila upande.

Aibu ya kushikwa na kuwekwa ndani pekee si ndogo kwa mtu wa "caliber" yako. Licha ya kupimwa na kukutwa kuwa u mlevi wa madawa, tumeona sakata la Oysterbay likikutia hasara kubwa sana, tumeona wafanyakazi wako wakifungiwa kuingia kwenye ofisi zao, tunasikia akaunti zako zinafungiwa kila kukicha.

Kama hiyo haitoshi, tunasikia umepatwa na matatizo ya moyo. Mwenyezi Mungu anasema katika Qur'an tukufu:

Qur'an 2:10. Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi. Basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uwongo. Maelezo

Kwa yote hayo bado tu hujashtuka ni kwanini yakukute yote hayo? Nakusihi, zingine zote ni sababu lakini ukweli unabaki kuwa ukweli, Waislam wameitikiwa dua zao dhidi yako.

Yussuf Manji tunakutaka usiwe katika wale ambao:

Qur'an 2:7. Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao, na juu ya macho yao pana kifuniko. Basi watapata adhabu kubwa. Maelezo

Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe na hachoki kusamehe, tunakutaka uombe toba kwa mola wako, umtake radhi, uwatake radhi na Waislam na uwarudishie viwanja vyao na mali zao, tena usithubutu kuvirudisha kwa wale wale waliokuuzia, itakuwa haina maana kabisa. Virudishe kwenye taasisi za Kiislam zenye kumuogopa Mwenyezi Mungu au tumia viwanja hivyo hivyo kuanzisha Manji Islamic Trust Fund na uiendeshe mwenyewe kwa manufaa ya Waislam.

Fata nasaha hizo uone mambo yatavyokunyookea.

Jikumbushe:

Maimamu kumsomea Manji Ahla-badri

Mjue Sheikh Ponda Issa Ponda na Kundecha

Waislamu wataka jengo lao toka Quality Group | Bongo5.com

MKATAMBUGA: WAISLAMU WAMELOGWA NA NANI?

Manji hakuna wakukuokoa katika haya na hayatokwisha ukifanya dharau isipokuwa wewe mwenyewe, anza kwa kumrudia Allah na kumuomba toba.

Na Mwenyeezi Mungu ndiye ajuwae zaidi.
Du kazi ipo,makosa binafsi na toba wapi na wapi,ina maana asingechukua hivyo viwanja ,Manji yasingempata haya yanayompata sasa?kwa maana nyingine Manji kafikwa na hayo sababu ya kupora viwanja vya Waislamu?Je Rugemalira,Singh,Malinzi,Kaburu nao wamepora viwanja vya Waislamu?
 
Aiseeeeeh,

Kumbe na hii dini ya warabu pori nayo mnaombea watu wapatwe na mabaya!? Tena, maimamu ndiyo walimuombea mabaya huyo Manji!?

Daaaaah, basi tena.

Kweli , dini zote ni uchwara na unafiki mtupu.
 
MANJI afie jela tu
 
Binafsi nahisi Manji ni sehemu ndogo sana ya tatizo juu ya Waislam, lakini kwa maoni yangu tatizo kubwa ni hii taasisi inayosimamia mali na maendeleo ya waislam wa Tanzania, nayo ni Bakwata,

Na je kipi kinawakosesha kufanya university sasa hivi? Just wondering ?

Taasisi za Roman Catholic sijasikia majaribu haya, si kwamba hayapo, bali wameweza kusimamia haki juu ya waumini wao na sio matumbo yao..

Je unasemaje juu ya hilo Auntie Faiza?
 
Wewe kutokuona haina maana kuwa hawapo na inawezekana huwaoni kwa sababu tu ya ushamba wako. Kwani mzee Bakhresa ana digrii ngapi mkuu?! Mbona kawaajiri wengi tu katika hao wanaojifanya wamesoma sana (watu wa kanisa) na wanamwita bosi wakimuona?

Haya mkuu nimekuelewa
 
Mkuu USIANGALIE UPANDE MMOJA
BORA YA HUYO MANJI HADI LEO YUPO KTK ADHABU YA DUNIA
KULIKO ALIEKUA SHEKH MKUU NA NDO ALIEKUA MHUSIKA MKUU NAE ASHATANGULIA MBELE YA HAKI
ALBADIR AU QUNUUT IKISOMWA HIO MKUU HUA HAICHAGUI
ANGEKUA HAI MCHUNGAJI MTIKILA UNGEMUULIZA
WEWE TEMBEZA TU HILO DOMO LAKO NA ALFJIR HII
MA MTU YANAKUANGALIA TU,,
JIANGALIE NA HALI YAKO KWANZA

Sent from Calculator Phone vesion007

Pemba na Zanzibar nzima mmemsindwa Lipumba na hizo dua zenu ,anazidi kupeta tu
 
Aiseeeeeh,

Kumbe na hii dini ya warabu pori nayo mnaombea watu wapatwe na mabaya!? Tena, maimamu ndiyo walimuombea mabaya huyo Manji!?

Daaaaah, basi tena.

Kweli , dini zote ni uchwara na unafiki mtupu.
Bora dini ya warabu pori au dini ya wazungu mwitu wanaofunga ndoa dume kwa dume??

Sent from Calculator Phone vesion007
 
Duh naona uzi umeshageuzwa wa kidini tena..... sasa imekuwa uislam vs ukristo.... kaz kweli kweli
 
Atubu na madhambi ya kuhonga waamuzi ili simba ionewe uwanjani.ipewe kadi za njano na nyekundu bila sababu.Hiyo ni dhambi kubwa inayo mwandama manji na haiwezi kumuacha salama daima
 
Bora dini ya warabu pori au dini ya wazungu mwitu wanaofunga ndoa dume kwa dume??

Sent from Calculator Phone vesion007

Zote ni ugulagula tu.
Hata warabu wanatindua makinikia kati ya wanaume kwa wanaume na ushahidi upo kuwa hata wao washikishana ukuta.
 
Yussuf Manji, ni matumaini yangu kuwa ujumbe huu utakufikia popote ulipo.

Binafsi kama Muislam mwenzako nnachukuwa fursa hii kukukumbusha kuwa hakuna kitu bora kama kukiri na kukubali makosa yako na kuomba toba.

Toba nnayokushauri kuiomba hapa, si kwa serikali wala kwa watawala. Toba nnayokukumbusha mimi kuiomba ni kwa Mola wako Muumba mbingu na ardhi.

Manji uliwakosea sana Waislam kipindi cha nyuma kiasi, kwa kutumia fedha zako kununulia viwanja vya wakf vya Waislam, na kuwa mkaidi kila uliposemeshwa kuhusu hilo.

Viwanja hivyo ambavyo historia inaonyesha kuwa vilikuwa vijengwe chuo kikuu cha kwanza Tanganyika (hilo halikufanyika lakini hilo ni simulizi jingine kabisa ambalo Alama Mohamed Said anaweza kulisimulia vizuri zaidi).

Ulifatwa na Waislam wakikuomba kuwa mkataba ulioingia na BAKWATA ni wa kidhalimu na haufai lakini kwa ukaidi wako hukuwasikiliza na uliwatoa njiani na kuendelea na mkataba wako.

Sakata la viwanja hivyo lilipelekea Waislam kufungwa, kupigwa na kujeruhiwa mpaka walipoona kuwa hawakuwezi kwa ajili ya kutumia fedha zako na nguvu ya baadhi ya waliokuwa BAKWATA, Waislam wakafikia maamuzi makali ya kuwa sasa wanakushtaki kwa Mwenyeezi Mungu.

Miaka imepita ukidhani kuwa shtaka hilo halina meno kwako, lakini leo tunashuhudia ukigeukwa kila upande.

Aibu ya kushikwa na kuwekwa ndani pekee si ndogo kwa mtu wa "caliber" yako. Licha ya kupimwa na kukutwa kuwa u mlevi wa madawa, tumeona sakata la Oysterbay likikutia hasara kubwa sana, tumeona wafanyakazi wako wakifungiwa kuingia kwenye ofisi zao, tunasikia akaunti zako zinafungiwa kila kukicha.

Kama hiyo haitoshi, tunasikia umepatwa na matatizo ya moyo. Mwenyezi Mungu anasema katika Qur'an tukufu:

Qur'an 2:10. Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi. Basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uwongo. Maelezo

Kwa yote hayo bado tu hujashtuka ni kwanini yakukute yote hayo? Nakusihi, zingine zote ni sababu lakini ukweli unabaki kuwa ukweli, Waislam wameitikiwa dua zao dhidi yako.

Yussuf Manji tunakutaka usiwe katika wale ambao:

Qur'an 2:7. Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao, na juu ya macho yao pana kifuniko. Basi watapata adhabu kubwa. Maelezo

Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe na hachoki kusamehe, tunakutaka uombe toba kwa mola wako, umtake radhi, uwatake radhi na Waislam na uwarudishie viwanja vyao na mali zao, tena usithubutu kuvirudisha kwa wale wale waliokuuzia, itakuwa haina maana kabisa. Virudishe kwenye taasisi za Kiislam zenye kumuogopa Mwenyezi Mungu au tumia viwanja hivyo hivyo kuanzisha Manji Islamic Trust Fund na uiendeshe mwenyewe kwa manufaa ya Waislam.

Fata nasaha hizo uone mambo yatavyokunyookea.

Jikumbushe:

Maimamu kumsomea Manji Ahla-badri

Mjue Sheikh Ponda Issa Ponda na Kundecha

Waislamu wataka jengo lao toka Quality Group | Bongo5.com

MKATAMBUGA: WAISLAMU WAMELOGWA NA NANI?

Manji hakuna wakukuokoa katika haya na hayatokwisha ukifanya dharau isipokuwa wewe mwenyewe, anza kwa kumrudia Allah na kumuomba toba.

Na Mwenyeezi Mungu ndiye ajuwae zaidi.
Allah amsamehe makosa yake huko alipo na amuweke mahali anapostahili
 
Bakwata inalaumiwa sana, kwanini kusiwe na umoja mwingine au upo ila sio maarufu kama bakwata??
 
Yusuf Manji amekufa na kuzikwa Canada kwa hiyo roho yako imefurahi sasa.
 
Yusuf Manji amekufa na kuzikwa Canada lwa hiyo roho yako imefurahi sasa.
Inna li Llahi wa inna Ilayhi Rajiun.

Kufa siyo tatizo, ni haki ya kila binaadam. Labda wewe unafikiria utabaki bila kufa?

Marehem hasemwi. Huombewa rehma tu, ndiyo maana anakuwa na title ya "marehem".
 
Kufa ni jambo la lazima haina hata haja ya utabiri...
Vipi baada ya kufa mmepata hilo eneo lenu?
Baada ya kumsomea albadili na kumshitakia kwa mungu wenu mmepata hilo eneo?
 
Back
Top Bottom