Yuko wapi yule dereva "Giriki" wa basi la Tawaqal?

Sijui Ulikua una maana gani "kuwazuga kwa taa"

Ila ni kweli michezo ya kuchoma ways/balbu za taa za breki za nyuma ilikuwepo. Hasa Kitonga na Pale uwanja wa ndege(njia ya Tukuyu kuelekea kyela) na madereva wengi walichomeshwa kwa mtindo huo
 
Sijui Ulikua una maana gani "kuwazuga kwa taa"

Ila ni kweli michezo ya kuchoma ways/balbu za taa za breki za nyuma ilikuwepo. Hasa Kitonga na Pale uwanja wa ndege(njia ya Tukuyu kuelekea kyela) na madereva wengi walichomeshwa kwa mtindo huo
Yah, nilikua na maana kama ulivyoeleza wewe, dereva wa nyuma akiangalia za Giriki anao kama Giriki ajashika breki na yeye anaamua kufunguka, kumbe Giriki kapunguza mwendo mbele kuna kona kali sema taa za breki haziwaki.
 
Atamzuga nani wakati watu wapo hiyo road kila siku wanajua hadi wapi kuna shimo na wapi hakuna shimo na leo yupo dar kesho mbeya kipi ambacho kitakua kigeni kwake Mkuu hao wanayajua hadi magari ya kampuni za coca au bia ambayo yalikua yanatoka mbeya wanapishana kila siku kona za hiyovi anakwambia Kona mbili zijazo tutakutana na roli la coca kwa sababu wapo humo kila siku na muda wa magari ya kampuni zingine wanajua pia ila wewe ukiambiwa utashangaa kweli...
 
Hakika maisha yanakwenda mbio sana maana mabasi yake yalitesa sana miaka ya 80 na mmiliki wake alioneka kama mtu aliekwisha yaweza maisha.
Tajiri wa Scandinavian mzee Abdullah awali alikuwa dereva wa malori baadae akafungua gereji yake pale Kurasini kisha akaanza biashara ya mabasi.

Baadae mawaziri wakaingiza mabasi yai kwenye hii kampuni na wakawa wanajaza mafuta kutoka hifadhi ya serikali bomu liliporipuka kampuni ikafirisiwa.

Mzee Abdullah route yake ilikuwa ni Dsm - Iringa tu ambayo ilisimamiwa na Bob Said.

Washirika wengine walikuwa Sumaye, Dr Kigoda, Prof Mark nk!
 
Nadhani huyu tajiri alikuwa anaishi Mbeya mjini. Nakumbuka miaka ya 97 nilionyeshwa nyumba yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…