Yuko wapi kijana mtanashati January Makamba?

Yuko wapi kijana mtanashati January Makamba?

ALIPE FEDHA YA CHAMA ALIZOIBA. mwakajana alikuwa anapokea fedha toka kwa taasisi mbalimbali ili azipeleke kwenye majimbo yaliyokuwa na shida. yeye akazitumia kuhudumia kambi yake ya uraisi . AMEAMBIWA ALIPE MABILIONI HAYO.
 
...Makamba alipaswa kuwa wizara ya Mambo ya nje au Waziri Mkuu..

Performances za akina Pinda na Majaliwa sasa zinapelekea baadhi ya watu kuamini kabisa kwamba kila mtu anaweza kuwa Waziri Mkuu.Haiwezekani.

Makamba pale alipowekwa tu bado anapwaya. Haitoshangaza sana kama atapumzishwa katika reshuffle inayoweza kutokea muda wowote katika safari yetu hii ya mwendokasi.
 
Zinapita siku, wiki, miezi na hata mwaka unaisha sasa bila kumwona au kumsikia Kijana Machachari na makini Januari Makamba katika duru hizi za siasa ya awamu ya tano.
Kwa wanaomtambua Makamba wanaelewa uwezo wake wa kucheza na siasa za Tanzania kama alivyo Lowassa enzi za ujana wake. Ni kijana ambaye hutulia pale ambapo hupatwa na misukosuko ya kisiasa na kujipanga upyaa. Pamoja na kwamba mimi ni moja ya watu wasioipenda CCM lakini Makamba ni hazina safi ambayo hata ukienda upinzani utampata mmoja au wawili wanaofanana naee.

Nakumbuka sote tulioshiriki katika uchaguzi wa mwaka jana tulivyo ona mipango ya ushindi wa Magufuli chini ya kijana huyu. Lakini sijui kimetokea nini mpaka kijana huyu machachari kupotezwa kwenye siasa na kutuipwa wizara mfu.

Niseme wazi kwamba pamoja na figisufigisu za kijana huyu mwaka jana lakini ni Hazina pekee ya mipango iliyosalia CCM. Hakuna kijana ambaye unaweza mfananisha na Makamba ndani ya CCM leo, sio Mwigulu wala Kigwangala. Huwezi msikia Makamba katika mihemko na mwendokasi wa hovyohovyo.
Najua wengi wanamlaumu Makamba kwa Bomoabomoa ya mabondeni ilivyofanyika, lakini ukweli ni kwamba bomoa bomoa ile ilifanywa na Lukuvi na Majaliwa.

Magufuli ameshindwa kumtumia Kijana huyu katika wizara kubwa hapa nchini na hii ndio inawezakuwa sababua kuyumba kwa serikali yake. Makamba alipaswa kuwa wizara ya Mambo ya nje au Waziri Mkuu.

Je huu ni mwanzo wa kufifia kwa Makamba katika siasa?
Makamba alikosa nini hasa kwa mtukufu Rais mpaka akapewa wizara ile?

Is makamba political Banned???

Karibuni kwenye mjadalaa, matusi, vijembe, hekima na busara ni haki yako, sio uchochezi.
No one is indispensable under the sun (JFK)
 
Kwenye Chama Chetu Makamba ni nguzo kuu ya mipango. Yule jamaa ni smart sana... Mara zote anajua anachofanya!

Kukaa kwake kimya kunanifanya niendelee kuamini kwamba yuko makini sana kisiasa! Hafungamani na style yoyote wala hali za dharura kirahisi-hafuati mkumbo! The guy is well focused with own Modus Operandi...

Anafanana sana kitabia na Zitto Kabwe na ni akili kubwa pekee zinazowaelewa hawa jamaa.

Natamani sana kuwa smart kama January Makamba. He is my roll model!

Mark Hilary

January Makamba is not a smart as you think; he is an opportunist.

Ni sawa na kumuona fisi anakula mifupa ya paa, ukamsifia kuwa ni muindaji mzuri!
 
Wadau muwe mnajadili watu wa maana. Makando kando mengine yaacheni huko huko yaliko.
 
Performances za akina Pinda na Majaliwa sasa zinapelekea baadhi ya watu kuamini kabisa kwamba kila mtu anaweza kuwa Waziri Mkuu.Haiwezekani.

Makamba pale alipowekwa tu bado anapwaya. Haitoshangaza sana kama atapumzishwa katika reshuffle inayoweza kutokea muda wowote katika safari yetu hii ya mwendokasi.
Ruka uwezavyo huyo ndo rais 2025., utanikumbuka mkuu kimya kingi kina kishindo



Kyene kyaka mkighanile une...
 
alikua mstari wa mbele kwenye kampeni nilijuwa atapata cheo zaid ya wazir mkuu
 
Kwa mliokuwa kwenye ziara ya Rais magufuli Zanzibar, Je Mh J.makamba alikuwepo? Naamini lile lilikuwa jukwaa lake kuonekana nimeangalia picha sijamuona imekuwaje?
 
Kwa mliokuwa kwenye ziara ya Rais magufuli Zanzibar, Je Mh J.makamba alikuwepo? Naamini lile lilikuwa jukwaa lake kuonekana nimeangalia picha sijamuona imekuwaje?

Alikuwepo na alisema anamsaidia muheshimwa kurudisha basi (ambalo serikali iliyopita ilikuwa inaliendesha nje ya barabara) barabarani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom