January Makamba na jumba bovu

Hassani

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
710
1,147
Nimepita kwenye account za Januari Makamba,Matusi na kejeli za wananchi wenye hasira za mgao wa umeme zimekua nyingi.Na nyingi zikijielekeza na kukumbushia miaka 5 ya Magufuli kuwa umeme haukukatika na hata kama ulikatika sio kwa kiasi hiki.

Mimi sio mtaalam wa umeme ila ntatoa hoja yangu kisiasa zaidi, inajulikana wazi Makamba ni mwanasiasa kijana ambaye yuko very ambitious, sihitaji kukumbushia nafasi yake katika mbio za urais za 2015,na wengi tunaamini mbio zake za urais hazijakoma ingawa kwa miaka 5 iliyopita mambo hayakuwa marais kwake.

Amekuja mama Samia na kumrudisha uwanjani baada ya kukaa benchi mda mrefu.hii ni fursa hadhim kwake kufufua ndoto na matarajio yake. Kwa kawaida mchezaji anayetoka benchi anakuwa na nguvu mpya bila kuacha makeke mengi.

Sio rahisi mchezaji anayetoka benchi na kuona makosa mengi ya wachezaji wenzake aanze kwa kujifunga goli la makusudi kabisa ukichukulia mtu kama Makamba ni mwanasiasa aliyetoka kwenye familia ya wanasiasa wakongwe.

Naamini kabisa kinachoendelea kuhusu umeme ni kama jumba bovu lililomwangukia Makamba mara tu baada ya kuingia kama mpangaji mpya.

Nikirejea kauli yake ya kuwapa TANESCO wiki mbili na ile ya mitambo kutofanyiwa matengenezo kwa uoga wa watu,naamini kabisa kuna sababu iko nje ya uwezo wake inayosababisha umeme kukatika.

Nawasilisha
 
Huo ndio ukweli, sababu zilizo nje ya uwezo wake ndio hasa zinazo mkwamisha, Mvua zimegoma kunyesha, na nchi yetu inatumia umeme wa mabwawa ya maji kwa kiasi kikubwa, na hayo marekebisho, mfano morogoro tanesco pale msamvu kuna kituo cha kupooza umeme ambacho kina changamoto mara kwa mara na kusababisha shida ya huduma
 
Huo ndio ukweli, sababu zilizo nje ya uwezo wake ndio hasa zinazo mkwamisha,
Mvua zimegoma kunyesha, na nchi yetu inatumia umeme wa mabwawa ya maji kwa kiasi kikubwa, na hayo marekebisho, mfano morogoro tanesco pale msamvu kuna kituo cha kupooza umeme ambacho kina changamoto mara kwa mara na kusababisha shida ya huduma
Hakuna lolote amefeli kabisa na hilo lilijionyesha tangu siku ya kwanza ameingia wizarani.
 
Tatizo wanasiasa wanakurupuka kubadilisha watu bila kuwauliza wataalamu mitazamo yao kuhusu hali na ufanisi wa shirika na kitu gani wanapendekeza..........akiingia huyu anataka aweke timu yake, akiingia yule naye aweke timu yake, yaani ni shaghalabaghala.....
 
Nimepita kwenye account za Januari Makamba,Matusi na kejeli za wananchi wenye hasira za mgao wa umeme zimekua nyingi.Na nyingi zikijielekeza na kukumbushia miaka 5 ya Magufuli kuwa umeme haukukatika na hata kama ulikatika sio kwa kiasi hiki.

Mimi sio mtaalam wa umeme ila ntatoa hoja yangu kisiasa zaidi, inajulikana wazi Makamba ni mwanasiasa kijana ambaye yuko very ambitious, sihitaji kukumbushia nafasi yake katika mbio za urais za 2015,na wengi tunaamini mbio zake za urais hazijakoma ingawa kwa miaka 5 iliyopita mambo hayakuwa marais kwake.

Amekuja mama Samia na kumrudisha uwanjani baada ya kukaa benchi mda mrefu.hii ni fursa hadhim kwake kufufua ndoto na matarajio yake. Kwa kawaida mchezaji anayetoka benchi anakuwa na nguvu mpya bila kuacha makeke mengi.

Sio rahisi mchezaji anayetoka benchi na kuona makosa mengi ya wachezaji wenzake aanze kwa kujifunga goli la makusudi kabisa ukichukulia mtu kama Makamba ni mwanasiasa aliyetoka kwenye familia ya wanasiasa wakongwe.

Naamini kabisa kinachoendelea kuhusu umeme ni kama jumba bovu lililomwangukia Makamba mara tu baada ya kuingia kama mpangaji mpya.

Nikirejea kauli yake ya kuwapa TANESCO wiki mbili na ile ya mitambo kutofanyiwa matengenezo kwa uoga wa watu,naamini kabisa kuna sababu iko nje ya uwezo wake inayosababisha umeme kukatika.

Nawasilisha
Familia ya wanasiasa wakongwe!!??
Familia ya Makamba ni ya wanasiasa wakongwe!!???
 
Back
Top Bottom