You are not my type

You are not my type

Kile ni kiapo tu mtu anasoma si lazima awe anatamka kutoka moyoni mwake....speaking about kiapo hivi kumbe ni wanawake tu ndio huwa wanaapa eeh? Mimi nilidhani wanaume pia huwa wanaapa maana wao ndio vinara wa usaliti. Hapo mwisho umemaliza vizuri kwamba kumbe inawezekana kushindwa, kwani mimi nimesema sitampa mwanaume yeyote? Nitawapa wengine Ila yeye sitompa.
😂😂😂 sawa mpenzi
 
Lakin kuna maneno ya kumwambia mtu si lazima useme neno ilo mtu mwenye busara anawwza kusema labda na mtu tayari au hapana siwezi kuwa nawe neno rahisi sana siyo kutoa neno ambalo kiuhalisia linaonekana kama kejeli flani
Mi lazma ntamuuliza kwahio me mjusi sindo manake? ~ in Joti's voice
 
Ninyi wanaume wa sikuhizi si mnadai hamna muda wa kupoteza kumfatilia mwanamke akikwambia NO ndio byebye.
Hii ni kweli mtu kakuambia 'NO'. Kwa miaka hii , unaanza kuangalia upande mwingine...( Wengi wapo hivyo)
 
Kuna Dada alijibu hivyo mimi sio type yake, nikamuangalia nikasema Hiii.
Akakutana na mjanja,akampa mimba,akazalia kwao,hajakaa vizuri mimba yapili MTU mwingine,mimi namuangalia tu nasema Hiii
Sasa hivi analia lia kuomba msamaha eti anaomba tuendeleee.mimi nimemjibu KWA Sasa haitowezekana.
msamehe tu
 
Wanaume na wanawake, let's say umetongoza au unampenda mtu yeye akakujibu 'You are not my type' au ukasikia anamwambia mtu kuwa you are not his/her type utalipokea vipi?

Mimi ninavyojua mtu akisema wewe sio type yake anamaanisha wewe si aina ya mtu ambaye angependa kuwa naye, haimaanishi amekudharau, amekushusha na kukuona una hadhi ya chini kuliko yeye kama wengi tunavyofikiria.

Kwenye mapenzi kila mtu kipo anachopenda iwe ni katika mwonekano au personality kiujumla. Wapo wanaume wanapenda chubby girls, wengine wanapenda English figure, wapo watu wanapenda mtu mchangamfu, anayeweza kufanya acheke muda wote lakini wengine wanapenda makauzu, kuona jino lake mwaka mpya hadi mwaka mpya. Kwa hiyo akikutana na wewe upo kinyume cha hapo ni kwamba wewe si type yake.

Japo si busara kumchana mtu live kuwa 'wewe si type yangu' lakini haina haja ya kukasirika, kuumia na kujenga chuki ukisikia kitu kama hicho. Maana wengine wakiambiwa hivyo wanaanza kuchambua demu mwenyewe miguu yote ya kushoto, sura kama anaramba ndimu anawezaje kutamka maneno kama hayo? Relax, kunywa maji then tafuta wa kufanana na wewe, yupo mahali anakusubiri.

Pengine kilichomfanya Diana asikupende ndio hichohicho kitakachomfanya Mwajuma asilale kwaajili yako.

Thanks
Majibu kama haya yanatolewa na wale wanaojudge kile wanachokiona leo. Hawajui kuwa kuna kesho, kwamba maisha hubadilika.


Huyo anayemuona ni type yako leo, mambo yakigeuka kesho utamkana. Wakati yule unayemuona si type yako kwa sasa, wakati huo wewe ndo utakuwa siyo type yake.


Let's Be Wise (especially ladies).
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom