You are not my type

You are not my type

Wanaume na wanawake, let's say umetongoza au unampenda mtu yeye akakujibu 'You are not my type' au ukasikia anamwambia mtu kuwa you are not his/her type utalipokea vipi?

Mimi ninavyojua mtu akisema wewe sio type yake anamaanisha wewe si aina ya mtu ambaye angependa kuwa naye, haimaanishi amekudharau, amekushusha na kukuona una hadhi ya chini kuliko yeye kama wengi tunavyofikiria.

Kwenye mapenzi kila mtu kipo anachopenda iwe ni katika mwonekano au personality kiujumla. Wapo wanaume wanapenda chubby girls, wengine wanapenda English figure, wapo watu wanapenda mtu mchangamfu, anayeweza kufanya acheke muda wote lakini wengine wanapenda makauzu, kuona jino lake mwaka mpya hadi mwaka mpya. Kwa hiyo akikutana na wewe upo kinyume cha hapo ni kwamba wewe si type yake.

Japo si busara kumchana mtu live kuwa 'wewe si type yangu' lakini haina haja ya kukasirika, kuumia na kujenga chuki ukisikia kitu kama hicho. Maana wengine wakiambiwa hivyo wanaanza kuchambua demu mwenyewe miguu yote ya kushoto, sura kama anaramba ndimu anawezaje kutamka maneno kama hayo? Relax, kunywa maji then tafuta wa kufanana na wewe, yupo mahali anakusubiri.

Pengine kilichomfanya Diana asikupende ndio hichohicho kitakachomfanya Mwajuma asilale kwaajili yako.

Thanks
Umenikumbusha mbali, kuna hawa walikua wanaitwa ma TX, kuna demu mmoja wa kizungu nilimtokea nikampa somo , ili niruke na ngozi nyeupe, alichoniambia ni kwamba " I am not suitable for you" Mara ya kwanza nilijua kanidharau, ila baada ya muda akanifuata mwenzake wa kiume, akaniambia " if you really wanna get that girl , stick to what you have planned " niligonga yule demu mpaka anaondoka TZ, alikua anasikitikia atakachokosa TZ.
 
unajua nini unapukua unatongoza ni kawaida kuwa vulnerable maana wewe unakua muhitaji na ambaye unamtongoza unamuona kama prize vile she is there for you to win her , sometime unakuwa na your own imagination jinsi gani perfect she is , na dhana nyingi tu za uongo zinakuwa zimekujaa kichwani , unamuona yeye ni mkamilifu sana , sasa kitendo cha yeye kusema you are not my type ni kitendo cha kuumiza hisia, maana unamjudge mtu maisha yake ndio manaa wengi wanaogopa kutongoza sio kwamba hawajui kutongoza ni swala la kupokea majibu , hiyo inakua kama hukumu inaumiza hisia za mtu haswa ukiwa kweli unamtaka na umepania kuwa naye , unaambiwa bora shambulio la kupigwa utaumia maumivu yataisha utakasirika utasahau lakini shambulio la maneno lina dumu miaka unaweza kuta mjukuu wako akaja kubeba kisasi cha maneno uliyowai kutamka na ukasahau kumbe mwinzio bado miaka yote hayo maneno yanamchoma, lakini jambo moja ambalo mwanaume inabidi kuwa nalo ni kuweza kuvumilia upumbavu ambao wanawake wanajibu na kupuuzia , lakini sio wote wanaoweza hayo
Kiukweli kaka zangu mnakutana na changamoto sana, ningekuwa mwanaume mimi sidhani kama hata ningetongoza
 
Kwa mtazamo wangu, hayo maneno siyo mabaya kutumia lkn jinsi yanavyokua presented mtu anajiskia vibaya, mfano unamjibu mtu "you're not my type" huku umebinua kidomo unampandisha na kumshusha, hapo ni dharau, na imezoeleka ukijibiwa hivo means hufikii hadhi yake

hivo kama hmtaki mtu tumia maneno mengine ya busara huwezi jua huenda akakufaa baadaye wakati utakaposhusha vigezo
Hahaha utakapokuwa kwenye bei ya promotion
 
Shida ni pale unapoambiwa sio type yangu huku likiambatanishwa na Msonyo,Kunyali, na kunithaminisha kutoka Kichwani hadi miguuni....

Tofauti na hapo hiyo ni sentensi ya kawaida sana na inaelekweka vyema.
Haha ni kweli kabisa
 
bora umpotezee kimya kimya. ...
siku za usoni unakutana naye ndio unavutiwa naye. ...utashindwa kurudisha maneno nyuma. ....
Yaaa, huo ndio uungwana, tukiongea tusimalize maneno yote, tuache na maneno ya akiba. Ili kesho tupate pa kuanzia,
 
Busara ni kitu kizuri sana endapo umejaliwa hilo maana busara nayo sio kama tako kila mtu analo

Kuna mtoto mmoja wa kike ashaniambia hivyo kipindi hiyo analiwa na wazee type ya Kina Kimei au Laswai

Nikaona isiwe ishu mama tembea na gepu

Ukapita muda huyu Mungu sio Athuman kanikuta sehemu na wa kumsaidia ni mimi alitamani ardhi ipasuke azame

Basi mie nikamsaidia hakuamini ,ndio kuanza kujipendekeza na mambo yangu elfu 15 yananisumbua naanzia wapi tena kuhangaika naye nikafunga vioo na mimi nikatambaa na gepu langu

Naimani alijifunza kitu japo ilishakuwa too late .
 
Ninyi wanaume wa sikuhizi si mnadai hamna muda wa kupoteza kumfatilia mwanamke akikwambia NO ndio byebye.
Naam siye ukimpenda mrembo kwa akili na moyo wako wote huwa hatukatishwi tamaa na kauli kama hizo over my dead body, you’re not my type etc. Unaendelea kuzoza tu mpaka kieleweke na maneno kama hayo kwa baadhi ni motisha tosha kabisa ya kumfukuzia mrembo kwa juhudi zote.
 
hapo mwisho hapoo
Kwa mtazamo wangu, hayo maneno siyo mabaya kutumia lkn jinsi yanavyokua presented mtu anajiskia vibaya, mfano unamjibu mtu "you're not my type" huku umebinua kidomo unampandisha na kumshusha, hapo ni dharau, na imezoeleka ukijibiwa hivo means hufikii hadhi yake

hivo kama hmtaki mtu tumia maneno mengine ya busara huwezi jua huenda akakufaa baadaye wakati utakaposhusha vigezo
 
See that’s what I am talking about especially if you’re in LOVE with that girl/lady.

Umenikumbusha mbali, kuna hawa walikua wanaitwa ma TX, kuna demu mmoja wa kizungu nilimtokea nikampa somo , ili niruke na ngozi nyeupe, alichoniambia ni kwamba " I am not suitable for you" Mara ya kwanza nilijua kanidharau, ila baada ya muda akanifuata mwenzake wa kiume, akaniambia " if you really wanna get that girl , stick to what you have planned " niligonga yule demu mpaka anaondoka TZ, alikua anasikitikia atakachokosa TZ.
 
Haha kwa nini unaamini hutokaa uambiwe tena?

Mara nyingi hili jibu linakuja baada ya kulazimisha sana, unajibiwa no, unaforce kuuliza kwa nini, unaambiwa basi tu, unang'ang'ania. Hilo ndilo jibu linalofata.

Sasa hivi ukinijibu no nafunga chapter, siulizi sababu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom