You are not my type

You are not my type

Wanaume na wanawake, let's say umetongoza au unampenda mtu yeye akakujibu 'You are not my type' au ukasikia anamwambia mtu kuwa you are not his/her type utalipokea vipi?

Mimi ninavyojua mtu akisema wewe sio type yake anamaanisha wewe si aina ya mtu ambaye angependa kuwa naye, haimaanishi amekudharau, amekushusha na kukuona una hadhi ya chini kuliko yeye kama wengi tunavyofikiria.

Kwenye mapenzi kila mtu kipo anachopenda iwe ni katika mwonekano au personality kiujumla. Wapo wanaume wanapenda chubby girls, wengine wanapenda English figure, wapo watu wanapenda mtu mchangamfu, anayeweza kufanya acheke muda wote lakini wengine wanapenda makauzu, kuona jino lake mwaka mpya hadi mwaka mpya. Kwa hiyo akikutana na wewe upo kinyume cha hapo ni kwamba wewe si type yake.

Japo si busara kumchana mtu live kuwa 'wewe si type yangu' lakini haina haja ya kukasirika, kuumia na kujenga chuki ukisikia kitu kama hicho. Maana wengine wakiambiwa hivyo wanaanza kuchambua demu mwenyewe miguu yote ya kushoto, sura kama anaramba ndimu anawezaje kutamka maneno kama hayo? Relax, kunywa maji then tafuta wa kufanana na wewe, yupo mahali anakusubiri.

Pengine kilichomfanya Diana asikupende ndio hichohicho kitakachomfanya Mwajuma asilale kwaajili yako.

Thanks
Hapo shida ni pesa tu.. Akiwa hana pesa hawezi kuwa type yako ila akishanyaka maneno yanabadilika kutoka kanyaboya mpaka HONEY
 
Mushi unaabudu sana pesa eeh?
Tufanye assumption ndogo tu... Hivi unafikiri kwa mfano, ni wanawake wangapi wanaweza kutoa hiyo kauli kwa mtu mwenye pesa? - assume mtoto wa Mengi hapo halafu unamwambia wewe sio type yangu... unadhani ni kitu ambacho ni possible and practical???
 
Hilo jibu inabidi liwe moyoni tu kwamba huyu mtu hana vigezo hitajika, ila unamtafutia jibu lingine lolote ambalo hatoumia kuliskia, tena ukimpata kaka amejipindia ukamjibu hivo, atakushushua hadharani mpk ujute, utaskia "wewe Dada mwenyewe unahadhi gani wewe na pua yako kubwa kama umeweka tonge la ugali, miguu imefanyaje fanyaje dooh, aibuuu

🤣🤣🤣🤣 nakumbuka tulikua mahali jamaa akawa anavuta fegi, dada mmoja akamwambia kaka moshi huo... jamaa alimshushia matusi akammalizia na “ukimwi unaukatikia mauno afu unanibania pua kaka moshiii (huku kabana pua)”, kila mtu alicheka aiseee

mtu kama huyu ukisema umjibu namna hii utafurahi na roho yako
 
Rejection ni rejection tu.
Sema kupunguza ukali wa maneno, mtu anaweza kukuambia kwamba nina mtu au hata akakuchana ukweli kwamba moyo wake hauna hisia na wewe.
Ila wewe sio wa type yangu imekaa kimatako matako sana.
 
Kichwa huongoza mwili, nacho huponzwa na ulimi, hauna ushuru mdomo so chunga ulimi usilete mgogoro - fid Q

Hayo majibu huwa wanajibiwa wale wanaume wasumbufu sana, wale wenye sifa sana Otherwise ni masela tu tunakuwa tunawatokea mademu wenye nature ya Dharau. Hio kauli ni Dharau 100%, hata ikisemwa kwa upole.
 
Hili neno linachoma sana, sijawahi kukutana nalo ila kuna mchizi lilimpa hasira ya kutafuta maisha, mwanamke mwenyewe alikuja kuchoka vibaya kutoka kwenye nyodo hadi kuuza afu jamaa mambo yamemnyookea jamaa alikuja kumsaidia kumpatia kazi

Kabla ya kutamka neno, fikiri mara mbili
Hii ndio hali halisi yaani hakuna kingine ambacho mwanamke anaweza kukukataa nacho zaidi ya hali duni kwa mfano mimi Demu aliyenitamkia hivyo tuko marafiki kabisa na ni kama tunaelewana sana labda sababu ya umaskini wangu tuu japo nafanya kazi na ninalipwa tena kipato kizuri tu zaidi ya milion ila sidhani kama yeye anajua, inashangaza lakini ndio hivyo inaniuma sana kwa kweli. Nafanya kazi usiku na mchana nikimbiane na umaskini nije nimuoneshe yule manzi kwamba nilikua na ndoto kubwa sana na ndio maana nikampenda binti mrembo na mwenye akili nyingi kama yeye. Anyway ni mipango ya Mungu wakati mwingine ila inauma sana kukataliwa na mtu unayempenda sababu unakua na mipango lukuki kichwani sema ndio mwisho wa siku zote zinabaki kuwa ndoto zisizo kuwa na tumaini lolote.
 
Kuna Dada alijibu hivyo mimi sio type yake, nikamuangalia nikasema Hiii.
Akakutana na mjanja,akampa mimba,akazalia kwao,hajakaa vizuri mimba yapili MTU mwingine,mimi namuangalia tu nasema Hiii
Sasa hivi analia lia kuomba msamaha eti anaomba tuendeleee.mimi nimemjibu KWA Sasa haitowezekana.
 
Tufanye assumption ndogo tu... Hivi unafikiri kwa mfano, ni wanawake wangapi wanaweza kutoa hiyo kauli kwa mtu mwenye pesa? - assume mtoto wa Mengi hapo halafu unamwambia wewe sio type yangu... unadhani ni kitu ambacho ni possible and practical???
Haha sasa mtoto wa Mengi hata kama sio type yako si kuna cha kujipoozea
 
Hii ndio hali halisi yaani hakuna kingine ambacho mwanamke anaweza kukukataa nacho zaidi ya hali duni kwa mfano mimi Demu aliyenitamkia hivyo tuko marafiki kabisa na ni kama tunaelewana sana labda sababu ya umaskini wangu tuu japo nafanya kazi na ninalipwa tena kipato kizuri tu zaidi ya milion ila sidhani kama yeye anajua, inashangaza lakini ndio hivyo inaniuma sana kwa kweli. Nafanya kazi usiku na mchana nikimbiane na umaskini nije nimuoneshe yule manzi kwamba nilikua na ndoto kubwa sana na ndio maana nikampenda binti mrembo na mwenye akili nyingi kama yeye. Anyway ni mipango ya Mungu wakati mwingine ila inauma sana kukataliwa na mtu unayempenda sababu unakua na mipango lukuki kichwani sema ndio mwisho wa siku zote zinabaki kuwa ndoto zisizo kuwa na tumaini lolote.
Mkuu hapo mwanzoni hauko sahihi kabisa, kwamba hakuna ambacho mwanamke anaweza kukukataa nacho zaidi ya umasikini? Sio kweli kabisa ingekuwa hivyo maskini wasingekuwa na wapenzi au ndoa
 
Kwani kuna haja ya kumweleza hayo maneno maisha yanazunguka kuna siku atakuwa type yako huwezi jua maisha haya. Kama humtaki mtu tumia neno la busara achana naye. Kwa mtazamo wangu
Jibu zuri sana
 
Mkuu hapo mwanzoni hauko sahihi kabisa, kwamba hakuna ambacho mwanamke anaweza kukukataa nacho zaidi ya umasikini? Sio kweli kabisa ingekuwa hivyo maskini wasingekuwa na wapenzi au ndoa
Masikini wanapata wapenzi kwasababu ya namba yao tu lakini hamna mwanamke anayependa mwanaume maskini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom