Yona na Mramba: Mashtaka na yatokanayo

Yona na Mramba: Mashtaka na yatokanayo

Aiseeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!usiniambie yule mama aliezirai jana mke wa daniel yona anafungua zile shampeni saa izi!!!!haya wapeni pole zao wacha tuwafariji jamani!!
 
Kama hakimu huyu alisimama kidete kulinda taratibu/sheria bila shinikizo lo lote basi nampa tano za fastafasta.
 
Mimi faraja yangu nimewaona wamepanda karandinga walilo pitisha bajeti wao wenyewe yanunuliwe safi sana hii na ninafrahi sana wamekaa takribani siku 7 au zaidi hili nalo safi sana.Nacho frahi zaidi ni kwamba mahabusu si kwa walala hoi pekee hata watu wenye mipesa yao wanaweza wakawekwa huko safi sana.
Haya wazee mkapumnzike mjipange kupangua mashtaka juu yenu huku tukiandaa mashtaka mengine juu yenu.
 
hakimu huyu tutaendelea kumpenda kwa kuwa tu tuna uchungu na wanaoitwa mafisadi, lakini kama tuko makini na utawala wa sheria, kitendo alichowafanyia watuhumiwa hawa si cha kuunga mkono, kwa kuwa angepaswa kuitumia sheria iliyo wazi, kumbukeni kuwa leo ni mramba , kesho ni slaa na pengine wewe, inapokuwa swala la kufuata sheria tujitahidi kuondoa jazba na ushabiki. huko uganda idd amin alianza kama mwankenza, akasifiwa sana baadaye akaitumbukiza nchi mahali wote tunapajua.

ningependa mramba na yona wahukumiwe kwa sheria na haki na wala si si kwa ubabaishaji anaoufanya mwankenza

nani anajua kama mwankenja anatumiwa na watu kama lowasa au rostam kutupumbuza kwenye swla la mramba? wewe na mimi hatujui bali tunategemea siku zote mahakama ndo mahali pekee pa kupata haki kwa nkia halali, na wababaishaji kama akinamwankenja pale si mahali pao
 
MPYA KUTOKA KISUTU:
Mramba na Yona wameachiwa kwa dhamana. Mramba amewasilisha hati tatu za nyumba zenye majina tofauti ambazo thamani yake inafikia sh bil 3 na Yona amewasilisha hati tatu zote zikiwa na majina yake na thamani ya kama sh bil 3
 
tuna cha kushangaa hapa? yona ni mbia wa mgodi wa mult billions, mramba naye si haba kibo hotel nk,
 
kwenu wananchi na wapenda amani!!yah tunajua kuna swala la
v.i.p jela lakini inapofika swala la kuvunja sheria za nchi wacha tu watanzanie
wote tujue!!tuna ndugu zetu awajasomewa mashtaka wana mwaka sasa
kesi zinachunguzwa zinachunguzwa!!!iweje leo hii mh mramba na yona .
watolewe gerezani mpaka mahakamani nakurudi bila kusomewa mashtaka!!je

maswali mengi ambayo watanzani tulazimishe kujua kusaidia ndugu zetu hapo baadae ni

1))JE POLISI WA MAGEREZA WALICHUKUA HONGO

2))SHERIA ILIKIUKWA KWA MAKUSUDI KUTOKANA NA VYEO WALIVYOKUWA NAVYO

3))NANI AWAJIBISHWE KWA HILI

4))NA KAMA SHERIA IPO RASMI TWAWEZA WENGINE KUJUA VIPENGELE

AHSANTENI,TUNAITAJI MSAADA WA SHERIA HAPO!@@@@@@

MCHANA MWEMA
 
wamepelekwa mahakama ya kisutu na wote wameachiliwa kwa dhamana. Yona kaweka dhamana kwa viwanja vyake mwenyewe vyenye thamani ya zaidi ya bilioni tatu na Mramba kaweka vya jamaa zake na kimoja cha kwake na kingine cha kampuni ambyo nadhani anamiliki yeye.

Redio one wametangaza mchana huu kwenye taarifa ya habari
 
hakimu huyu tutaendelea kumpenda kwa kuwa tu tuna uchungu na wanaoitwa mafisadi, lakini kama tuko makini na utawala wa sheria, kitendo alichowafanyia watuhumiwa hawa si cha kuunga mkono, kwa kuwa angepaswa kuitumia sheria iliyo wazi, kumbukeni kuwa leo ni mramba , kesho ni slaa na pengine wewe, inapokuwa swala la kufuata sheria tujitahidi kuondoa jazba na ushabiki. huko uganda idd amin alianza kama mwankenza, akasifiwa sana baadaye akaitumbukiza nchi mahali wote tunapajua.

ningependa mramba na yona wahukumiwe kwa sheria na haki na wala si si kwa ubabaishaji anaoufanya mwankenza
nani anajua kama mwankenja anatumiwa na watu kama lowasa au rostam kutupumbuza kwenye swla la mramba? wewe na mimi hatujui bali tunategemea siku zote mahakama ndo mahali pekee pa kupata haki kwa nkia halali, na wababaishaji kama akinamwankenja pale si mahali pao
Ndugu yangu Mwikimba haya ungeyasema haya kwa maelfu ya Watanzania wanaosota kwenye mahabusu mbali mbali ya nchi hii kwa miezi kama sio miaka kupata dhamana ningekuelewa sana, lakini leo kuona Mwankenja ni mbabaishaji kwa vile kadai removal order kwa siku moja kwa watuhumiwa mashuhuri walio kaa siku saba Keko! bado sijakupata mkuu kama ni kweli unazungumzia ubabaishaji kweli au kuna jingine?
 
wamepelekwa mahakama ya kisutu na wote wameachiliwa kwa dhamana. Yona kaweka dhamana kwa viwanja vyake mwenyewe vyenye thamani ya zaidi ya bilioni tatu na Mramba kaweka vya jamaa zake na kimoja cha kwake na kingine cha kampuni ambyo nadhani anamiliki yeye.

Redio one wametangaza mchana huu kwenye taarifa ya habari

Hivi hivyo viwanja vyenye thamani ya 3 billion vina nini, au ndiyo kusema vina mafuta au dhahabu??


Hizo nyumba zenye thamani ya 3 billion ziko bongo au mbinguni??
 
Mkuu kwa hili tupo pamoja kwani ukiangalia Hakimu alikosea hata kupiga hesabu za dhamana, na aka demand cash instead of immovable asset of that valueBodo tuu kesi immenda kwake tenaMbona wale mafisadi walikuwa wanaend mahakamani pindi wanapokamilisha masharti ya dhamana
Huyu hakimu lazima atakuwa fisadi

Mkuu tusichanganye mambo hapa.
1.Hakimu ana mamlaka kisheria kufanya uamuzi kama alioufanya Mwankenja. Ndio maana kuna uwezekano kukata rufaa...

2.Rufaa ilipoenda mahakama kuu, moja ya sababu za kukata rufaa ni kuwa conditions za bail zilikuwa kali mno na siyo kwa vile hakimu alikosea kuweka hizo conditions.
3. Kesi kurudi kwa hakimu yuleyule ni utaratibu wa kawaida.Hakimu au jaji anaeanza kesi ndiye ataendelea kuisikiliza maana bail hearing siyo main case.Main case itaanza kuangalia mashtaka na uthibitisho wake.
 
mm.JPG


Basil Mramba na Daniel Yona wakishuka toka chemba namba moja ya mahakama ya Kisutu baada ya kuachiwa kwa dhamana muda mfupi uliopita. (Kwa hisani ya Michuzi Blog)
 
Mkuu tusichanganye mambo hapa.
1.Hakimu ana mamlaka kisheria kufanya uamuzi kama alioufanya Mwankenja. Ndio maana kuna uwezekano kukata rufaa...

2.Rufaa ilipoenda mahakama kuu, moja ya sababu za kukata rufaa ni kuwa conditions za bail zilikuwa kali mno na siyo kwa vile hakimu alikosea kuweka hizo conditions.
3. Kesi kurudi kwa hakimu yuleyule ni utaratibu wa kawaida.Hakimu au jaji anaeanza kesi ndiye ataendelea kuisikiliza maana bail hearing siyo main case.Main case itaanza kuangalia mashtaka na uthibitisho wake.

Watanzania tunapenda sana kulalamika. Hawa ni big names na hakimu anajua macho na masikio yote ya watanzania yanamwangalia na hawachelewi kumwambia anaogopa au kapewa mlungula au anaongozwa na mkono kutoka juu!

Wanasheria hebu tuelemisheni tupunguze kulalamika kwenye kila jambo.
 
Yona kweli anatisha amejidhamini mwenyewe kwa kutumia viwanja vya makongo juu duh si mchezo....
 
Dhamana ni swala la mahakama siyo la magereza. Hakuna sheria iliyokiukwa kwani dhamana ni haki ya kikatiba ya kila mtanzani (article 13(6) (b) of the Constitution of the URT.Sheria ipo soma Criminal Procedure Act 1985, R.E 2002 section 148
 
Watanzania tunapenda sana kulalamika. Hawa ni big names na hakimu anajua macho na masikio yote ya watanzania yanamwangalia na hawachelewi kumwambia anaogopa au kapewa mlungula au anaongozwa na mkono kutoka juu!

Wanasheria hebu tuelemisheni tupunguze kulalamika kwenye kila jambo.

Kuna baadhi yetu watalalamika hata pale pasipostahili kulalamika. Hakimu alikuwa na haki zote za kufuata taratibu za mahakama, vinginevyo ingegundulika kwamba taratibu za mahakama hazikufuatwa basi tungemjia juu kwamba kishapewa cha kupewa na watuhumiwa, wenyewe wanaita takrima.
 
Yona na Mramba hawana kesi ya kujibu maana katika katiba yetu ya Tanzania kahuna sheria au kifungu chochote binding kinachomtaka Waziri au Niabu Waziri kufuata ushauri fulani katika kutoa maamuzi , ndio maana kuna collective cabinet responsibilities hivyo kama hawa walikosea, ni Cabinet nzima na Rais wao-Mkapa walikosea na kuitia serikali hasara hizo, pia hawawezi kufanywa scape goats maana sheria ina-operate uniformly btn citizens hivyo hata wengineo walioboronga inabidi waletwe mbele ya Pilato mkuu as soon as practically is possible. Labda akina yona na Mramba wa-argue hili ili watanzania wainuliwe macho..

Case hii ni Nzuri kama DPP akiishinda maana ina na ita-set precedent kwa wengineo kufanyiwa kweli, sio Magufuri, Megji (sorry spelling), kalamagi na hata Mkapa Mwenyewe.

Wanaosema kwamba tuna kinga ya Rais, nafikiri hao bado ni mbumbumbu au wavivu wa kufikiri na kutafakari mambo - kwani kinga hiyo haimkingi Rais anapofanya -criminal activities, sema kwa mfano Rais yuko likizo na katika Likizo hiyo akagombana na watu kijijini kwake au hata member wa familia yake, naye aka-mshuti, sheria itakuwa ni sheria tu haijari kama ana kinga, Lazima afikishwe kwa pilato. Au sema akiwa huko Holiday afanye tendo lolote ambalo ni criminal kama ku-mwibia nduguye chochote kile katika familia yao, na mtu huyo wa familia akamfungulia mashitaka, ni lazima ashitakiwe tu.

Nina maana ya kwamba sisi wa-Tanzania ndio wanafamilia ambao tumewathamini na kuwaweka madarakani viongozi mbalimbali wa serikali zetu. Wakati tunawaweka huko, wao waliahidi kwamba watawatumikia vema WaTanzania kwa kufutua misingi ya katiba. Sasa kwa ufupi ni kwamba wametukosea na kudai kwamba eti siku hizi wao ni wanafunzi na sio wanasiasa, hii inaonesha ni jinsi gani walivyo na madhalau ua upeo mdogo wa uelewa, na wanafikiri kwamba hata sisi pia tuko kama wao.

Kinachotakiwa ni DPP na wanasheria wake wawapeleke wote waliokuwa kwenye cabinet ya mkapa na waishitaki cabinet nzima ya mkapa-Kikwete akiwemo pia kwamba- wali-abuse powers as collective responsibility na pia kwamba wananchi wa Tz hawakuwatuma kwenda kufanya criminal activities bali ku-excute sheria zilizomo ndani ya katiba yetu.
Evidence zipo za akina Mwakyembe na Dr Slaa, kwa nini kusua sua, witness wapo na affidavits nyingine zipo sasa kwanini kuogopa ogopa kama kuku anayechinjwa?

Kama DPP anasua sua hata yeye mwenyewe ana harufu ya ka-ufisadi maana walikuwepo wakati haya yanatokea in some capacities, na tunachohitaji ni kuwa na independent judiciary iliyo kama federal Court ya USA kwamba Rais aweze kuwachagua majaji lakini asiwe na uwezo wa kuwafuta baada ya bunge kuwathibitisha, wao wawe independent na excutives pia legislature.. hii itasaidia kuwafikisha mahakamani wale wote wanaofanya uharifu. Pili ili kuthibiti Rushwa inabidi tuangaliwe wenzetu wanaipunguzaje katika mahakama na taasisi nyingine, angalia mfano wa SFO= SERIOUS FRAUD OFFICE au angalia JINSI Mapolisi wa UK wanavyokuwa wana-attend matukio na kuwahoji watu,
kWANZA huwatenganisha watu na kuchukua malelezo mbalimbali, hii inasaidia non colaboration ya ushahidi, pia hao police wa uk huwa wana vinasa sauti mpaka camera kwenye vichwa au masikio yao... kila kitu wakifanyacho kinakuwa documented hamna rushwa ndogo ndogo bwana. Pia anaglieni wenzetu China, ukipatikana na hatia ya Rushwa Lazima unyongwe tu baada ya appeal zote kufanyika, haya anagalieni Malaysia pia Singapore, if they say something they mean it. ukipitisha madawa, utanyongwa ukikamatwa, na hili linafanyika, kuna -less standard of proof katika makosa yanohusu public na this is a way to go in Tanzania sio kuanza kuwahurumia etu tume ama tunakusnya ushahidi, ushahidi waweza kukusanya mtuhumiwa akiwa rumande...

Watanzania tuamkeni na tuwachangamikie wote walioanya ufisadi na kuamua yafuatayo.

1. Dpp alisema kwamba ma-fisadi wote wakipelekwa mahakamani , nchi itayumba, basi afanye amnest kwa masharti ya kwamba mali zao zote zitaifishwe na ziletwe kwenye ujenzi wa taifa pia mafisadi hao badala ya kuachwa kwenda huru, waisadie serikali katika kutumia akili zao kuziba mianya ya ufisadi maana wao wanazifaham loopholes za grand corrption haswa.

2. Tusikubari kwamba inchi itayumba maana asemaye hivyo ni mvivu wa kufikiri naye pia ana -abuse authority yake kwa kutofanya anacholipwa afanye yaani kuwafikisha wote wahusika na watuhumiwa wa ufisadi na abuse of powers kwa mzee pilato.

3. Tufanye mchakato nchi nzima na tujue wananchi wanataka nini, maana ionekanvyo ni wabunge wachache sana wanaopigia kelele mambo hayo ya ufisadi na utendanji kazi, yawezekana labda hawajui au wamezidiwa na data na inabidi wanyamaze ili wao wanazozijua data wazilezee vizuri.

4. Nchi kama nchi inabidi iwe na malengo na kuyatimiza malengo hayo kwa muda fulani na sio endless malengo yasio isha, mfano, tunataka kuwa na motorways regardless of costs ambazo zitaunganisha mikoa yote ya Tanzania inyeshe Mvua, jua liwake barabara zipitike wakati wote, lengo hili lifanyike ndani ya miaka 5 Rais anapoingia madarakani, pia tuweze kuinua pato la mkulima kwa ku-commercialise kilimo within 3 years ya mungwana katika kazi.

4. Tuondokane na kasumba kwamba wawekezaji ndo wanaleta maendleo na ku-create jobs ingawaje hii is arguable both ways, wawekezaji hao ni lolongolongo tu maana Tanzania hatuna umeme wa uhakika, kama viwanda vyote alivyojenga nyerere, vikifufuriwa na kufanya kazi 24/7, basi hatutakuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji ya umeme, pia kwamba kamam viwanda hivyo vyote vikifanya kazi , basi kazi zenyewe zitatafuta watu na sio watu kutafuta kazi, hata hao wakimbizi waliopo Kigoma kutakuwa hakuna haja ya kuwarushisha makwao bali ni tutawatumia kwa manufaa yao na kwetu.

Ni haya tu wakuu na najua kwamba uchangiaji wangu waweza kuwa na mapungufu fulani, uboleshini na nitaupokea ushauri wenu.

SMP- LLM London
 
Watanzania tunapenda sana kulalamika. Hawa ni big names na hakimu anajua macho na masikio yote ya watanzania yanamwangalia na hawachelewi kumwambia anaogopa au kapewa mlungula au anaongozwa na mkono kutoka juu!

Wanasheria hebu tuelemisheni tupunguze kulalamika kwenye kila jambo.

Hakimu ana mamlaka yake katika utoaji wa maamuzi mbalimbali ya dhamana na ndio maana kila Mahakama imewekewa viwango vyake vya usikilizaji wa kesi

Huwezi kukuta kesi inayohusu madai ya Bilioni moja inasikilizwa Mahakama ya Mwanzo.

Hakimu alikuwa sahihi kutoa masharti ya dhamana kwa kulingana na uzito wa kosa halisi na sio kufuata umaarufu au kuogopa umaarufu wa wahusika.

Unapokuwa chini ya mikono ya sheria umaarufu wako unaishia nje pale Hakimu ana uwezo kulingana na sheria inavyomruhusu kutoa maamuzi mbalimbali juu yako yaliyo ndani ya sheria na chini ya mamlaka yake.

Hakimu Mwankenja hakukosea na ndio maana Mahakama Kuu haikutoa uamuzi kuwa kulikuwa na makosa ya maamuzi ya Hakimu Mkazi Mwankenja ila ilibadilisha masharti yale tuu yaliyokuwa yamewekwa na Mwanakenja.

Kungekuwa kuna makosa katika maamuzi ay ingekuwa Mwankenja kaamua kwa kufuata ubabe au kupewa mlungula Mahakama kuu ingetupilia mbali maamuzi yake na kuweka masharti mapya na uamuzi huo ungetamka wazi kuwa MAhakama kuu imefuta masharti ya dhamana yaliyowekwa na mahakama ya Kisutu na kuweka masharti mapya.

Tusimhukumu Mwanakenja kuwa alitenda kinyume au alipokea mlungula au alifanya maamuzi ya kibabe kuwaonea watuhumiwa hao.
 
kwa mfano Rais yuko likizo na katika Likizo hiyo akagombana na watu kijijini kwake au hata member wa familia yake, naye aka-mshuti, sheria itakuwa ni sheria tu haijari kama ana kinga,
SMP- LLM London

Nadhani kabla hujapewa nchi kuongoza au kumiliki silaha akili zitakuwa zimepimwa kama uko sawa sawa ....
 
Back
Top Bottom