Yona na Mramba: Mashtaka na yatokanayo

Yona na Mramba: Mashtaka na yatokanayo

Sawa kabisa mhe. Mwankenja hakuna kupinda sheria eti tu kwa sababu ni vigogo/ mafisadi. sijui amri za kijeshi (magereza) zinasemaje katika hili - nani aliruhusu hawa watuhumiwa wapelekwa mahakamani bili removal order?! hivi bado hajachukuliwa hatua?
 
Ewe MCHAGA na kama ndugu wao hao watu, unaombwa kufika ROMBO BAR katika harambee ya kumchangia Mramba kupata dhamana. Tatiso hili si la Warombo peke yao ila ni la wachaga wote- Machame, Kiboso, Uru, Old Moshi na Marangu. Tusaidiane maana tatiso la kupenda lipo kwenye damu. Kimaro, Kimario, Lema, Massewe, Shirima, Moshi, Mushi, wote wameshafika. Au tuma mchango wako kwenye akaunti 85755758 NMB.
Kumbuka: TANSANI BILA WACHAGA HAIWESEKANI.............
 
..mramba na yona wametumia madaraka vibaya....na kusababisha hasara..tatizo hapa mashtaka hayajaweka wazi kuiba..,tofauti na kina JEETU patel ambao wameiba live,.....imekuwaje wale wa EPA wamekubaliwa kuweka bond hadi mali zisizoamishika...na kwa hawa kuinakuwa na kigugumizi.....

thats why pamoja na uamuzi huu ambao utakuwa funzo kwa wanasiasa wetu....nachelea kusema pia ndani ya hii kesi kuna hidden agenda vile vile..ningependa kusubiri hadi mwisho...nione.Lakini labda tutahadharishe tu kuwa kama kuna nguvu ya ziada inatumika chini kwa chini ..iachwe kwani ita jeopedise ..good will ya president...katika hii vita!!..,mwisho itasababisha sympethisers kuona kama kuna kukomoana kwenye hii kesi...

na pia la muhimu rais tunamtegemea sana kwenye kuwashughulikia waliotutia hasara ya RICHMOND...kwani ushahidi wake ni wa moto zaidi na wa kuaminika .....


Bado sijatulia na hii kesi, nahisi kuna underground nyingi tu na usanii ndani yake! Yona kwanini ashitakiwe kwa haya tu, what about OUR LOVELY KIWIRA?

I doubt the earnestness of these move!
 
Ewe MCHAGA na kama ndugu wao hao watu, unaombwa kufika ROMBO BAR katika harambee ya kumchangia Mramba kupata dhamana. Tatiso hili si la Warombo peke yao ila ni la wachaga wote- Machame, Kiboso, Uru, Old Moshi na Marangu. Tusaidiane maana tatiso la kupenda lipo kwenye damu. Kimaro, Kimario, Lema, Massewe, Shirima, Moshi, Mushi, wote wameshafika. Au tuma mchango wako kwenye akaunti 85755758 NMB.
Kumbuka: TANSANI BILA WACHAGA HAIWESEKANI.............

Mchaga kajiunga humu leo tu kuja kututapeli. Haya Mangi tutakuwekea mchango wetu kwenye hiyo account yako.

Kwa hiyo mwenzetu unaposema ni tatizo la wachaga wote una maana gani, au ndiyo kusema JK kawakalia vibaya safari hii. Anyway, usijali sana kwani mwanae ameoa uchagani.
 
wewe na mimi hatukuwepo wakati mramba na yona wakifanya madudu yaliyowafikisha mahakamani, ila tumemtwaa tu-try kwa sheria zetu, kwa sheria iliyoko yule ni mtuhumiwa tu na hajawa convicted, kwa hiyo anayo haki ya dhamana.

inapotokea hakimu anamkomoa mtu anyemtuhumu kwa kuzima simu na kukimbil;ia bagamoyo ili asiandike removal order tumsifu kwa lipi? kama yeye ameshawahukumu ya nini sasa waendelee kuitwa watuhumiwa? nadhani huyu hakimu ni mkomoaji, na hastahili kuitwa mtoa haki, yeye ni sawa na mafisadi wengine, tofauti tu yeye anaifisadi sheria tuliyoitunga wenyewe(kwa kuwakilishwa na bunge letu)

asipotenda haki kwa hawa una hakika gani kuwa atatenda haki kwa mjomba wako aliyekamatwa na kubambikiziwa kesi na polisi? au siku kikwete atakapombakizia kesi dr slaa akapelekwa kwake una hakika gani atatenda haki?

tusimame kwenye haki na tujue kuwa mahakama ni mahali pekee panapotolewa haki, hakutakiwi watu wanaoendeshwa kwa utashi na ushabiki wao kama mwankenja bali wenye uadilifu na kuifuta sheria

Mwikimbi hakai mbali!
Maamuzi ya Jaji yalikuwa ijumaa jioni, jumatatu asubuhi watuhumiwa wanaletwa mahakamani! ni kwa amri ya nani? By the time Jaji anamaliza kumake decision tayari muda ushakwenda arijojo! Na usisahau pia kuwa Mwakenja kama Mwakenja anao utaratibu wa kazi zake kama ambavyo anavyopewa mwongozo na bosi wake. Angekuwa mtovu wa nidhamu kutokwenda kule amabko bosi wake amemtuma eti kwa sababu tu kuna fununu kuwa Mramba na Yona wataletwa mahakamani. Nasema fununu kwa kuwa kama angekuwa amesaini removal order angekuwa na taarifa za kuletwa kwao mahakamani siku hiyo na hapo ndo tungemwita mkomoaji kwa sababu alikuwa na taarifa! Pia hakuzima simu kwa ajili ya hao, kama wewe uliwahi kuhudhuria semina au warsha ambazo sio za kihuni utakubaliana na mimi kuwa unapoingia ukumbini unazima simu yako ili usidraw attension ya mtu au watu wanapoconcentrate kwenye issue sensitive. Mwisho hakuana utashi wala ushabiki hapo ila ni kwa matakwa ya sheria na niliwahi kusema kuwa sheria zinatibu sheria nyingine. Kipengele fulani kinatengua kifungu fulani cha sheria! Hii ndo sheria, kama sio fani yako basi tuwaachie wenye fani zao wacheze nazo.
 
hatimaye Mh.Hezron Mwankenja ameridhia dhamana na tayari wanajiandaa kuiacha Kisutu na kuelekea nyumbani muda huu, magaereza wana clea umati wa umma uliofika kushuhudia tukio hilo.
 
hatimaye Mh.Hezron Mwankenja ameridhia dhamana na tayari wanajiandaa kuiacha Kisutu na kuelekea nyumbani muda huu, magaereza wana clea umati wa umma uliofika kushuhudia tukio hilo.

Hawatamsahau Mwakenja maisha yao yote. Hii ndiyo inayoitwa sheria an si vinginevyo. Cheers Mhe. Mwakenja!
 
mwikimbi hakai mbali!
Maamuzi ya jaji yalikuwa ijumaa jioni, jumatatu asubuhi watuhumiwa wanaletwa mahakamani! Ni kwa amri ya nani? By the time jaji anamaliza kumake decision tayari muda ushakwenda arijojo! Na usisahau pia kuwa mwakenja kama mwakenja anao utaratibu wa kazi zake kama ambavyo anavyopewa mwongozo na bosi wake. Angekuwa mtovu wa nidhamu kutokwenda kule amabko bosi wake amemtuma eti kwa sababu tu kuna fununu kuwa mramba na yona wataletwa mahakamani. Nasema fununu kwa kuwa kama angekuwa amesaini removal order angekuwa na taarifa za kuletwa kwao mahakamani siku hiyo na hapo ndo tungemwita mkomoaji kwa sababu alikuwa na taarifa! Pia hakuzima simu kwa ajili ya hao, kama wewe uliwahi kuhudhuria semina au warsha ambazo sio za kihuni utakubaliana na mimi kuwa unapoingia ukumbini unazima simu yako ili usidraw attension ya mtu au watu wanapoconcentrate kwenye issue sensitive. Mwisho hakuana utashi wala ushabiki hapo ila ni kwa matakwa ya sheria na niliwahi kusema kuwa sheria zinatibu sheria nyingine. Kipengele fulani kinatengua kifungu fulani cha sheria! Hii ndo sheria, kama sio fani yako basi tuwaachie wenye fani zao wacheze nazo.
mkuu ninakusaidia kitu kimoja ktk ku conclude kuwa mzee hezron mwankenja hakutenda haki, unapotumwa kwenda sehemu na senior wako huondoki na ofisi ila ninakuhakikishia kuwa licha ya kujua atakuwa bagamoyo siku ile lakini hakumkabidhi kaimu incharge wake, utaratibu ni wazi kuwa kama kuna issue pending au kesi za kuja mbele yake anapaswa kuzikabidhi kwa kuahirishwa/ kutoa dhamana kwa mujibu wa masharti yako/ au yale wa senior wako baada ya anayeoomba dhamana kufuata taratibu kwa hiyo ijumaa remove order ilikuwa ya high court na dhamana ni kwa masharti yao ila kesi kuu iko kwa mwankenja hivyo ilikuwa ni lazima wahamie kisutu ku finalize hata kama mwankenja asingelikuwepo, above all kusingelikuwa na any harm ktk taratibu za mahakama.

Ame prove kuwa yeye radical ktk mahakama un necesarily,tunajiuliza nyuma yake kuna nani anayemuongoza maana kama ni yesu wengi wanae na hawako hivyo au mzee pesambili alimfisadi huko nyuma?? Maana naye mwankenja ni mkongwe ktk mahakama, tunatarajia kwa kesi hii anaweza kujipatia wadhifa mkubwa siku za usoni kitu ambacho ni hatari kuliko ufisadi.
 
Mwikimbi hakai mbali!
Maamuzi ya Jaji yalikuwa ijumaa jioni, jumatatu asubuhi watuhumiwa wanaletwa mahakamani! ni kwa amri ya nani? By the time Jaji anamaliza kumake decision tayari muda ushakwenda arijojo! Na usisahau pia kuwa Mwakenja kama Mwakenja anao utaratibu wa kazi zake kama ambavyo anavyopewa mwongozo na bosi wake. Angekuwa mtovu wa nidhamu kutokwenda kule amabko bosi wake amemtuma eti kwa sababu tu kuna fununu kuwa Mramba na Yona wataletwa mahakamani. Nasema fununu kwa kuwa kama angekuwa amesaini removal order angekuwa na taarifa za kuletwa kwao mahakamani siku hiyo na hapo ndo tungemwita mkomoaji kwa sababu alikuwa na taarifa! Pia hakuzima simu kwa ajili ya hao, kama wewe uliwahi kuhudhuria semina au warsha ambazo sio za kihuni utakubaliana na mimi kuwa unapoingia ukumbini unazima simu yako ili usidraw attension ya mtu au watu wanapoconcentrate kwenye issue sensitive. Mwisho hakuana utashi wala ushabiki hapo ila ni kwa matakwa ya sheria na niliwahi kusema kuwa sheria zinatibu sheria nyingine. Kipengele fulani kinatengua kifungu fulani cha sheria! Hii ndo sheria, kama sio fani yako basi tuwaachie wenye fani zao wacheze nazo.


Hapa umefafanua vizuri sana


kwa njia yoyote mtuhumiwa anapotolewa magereza kunakuwa na remove order ambayo inapaswa hakimu au judge anayehusika aisaini kuwa yule mtuhumiwa aletwe mahakamani ili kusomewa shtaka lake au kesi yake kusikilizwa hata kama ni kuja kupewa dhamana na hiyo order ni lazima isainiwe pia na msimamizi wa gereza/ mahabusu ambamo mtuhumiwa huyo anatolewa.

Hakimu Mwankenja yuko sahihi kabisa kukataa kusikiliza shauri la hawa watu kwa kuwa hakusaini hiyo order ya watu hawa kuletwa mahakamani.

Hakimu au judge anapofika mahakamani anakuwa ameshapangiwa mashauri ya kusikiliza na yule Magistrate in Charge or Judge in Charge wa mahakama husika na hapaswi kusikiliza shauri ambalo halipo kwenye ratiba yake ya siku hiyo.

La kujiuliza hapa ni nani aliyeamuru watu hao watolewe rumande na kuletwa mahakamani bila Remove Order ya Hakimu.
 
Nani kawatoa mahakamani ?

Kwa kweli bila hiyo kiutaratibu huwa magereza hawaruhusu mtu kutolewa, sasa nani aliwatoa bila ruhusa, hiyo ni kashifa. Ila Hakimu alikuwa sahihi kiutaratibu," alisema Bw. Ndumbaro ambaye amekuwa kwenye jopo la utetezi katika mashitaka kadhaa mashuhuriu ya jinai nchini.

Kufuatia dhamana hiyo kushindikana na watuhumiwa kurejeshwa gereza la Keko nyuso za huzuni zilitawala tena mahakamani hapo, ndugu na jamaa wa watuhumiwa hao wakiendelea kutoamini makali ya taratibu za kisheria
 
hawatamsahau mwakenja maisha yao yote. Hii ndiyo inayoitwa sheria an si vinginevyo. Cheers mhe. Mwakenja!

jaji alitoa maamuzi saa saba mchana, baada ya hapo ghafla simu yake ikapotea hewani!!! Unasemaje kuhusiana na hilo.

Ameweka rekodi ya ku detain watu illegally, kwa hilo atakumbukwa sana.
 
hunipendi ndugu yangu; kasome mwisho wa manabii unakuwaje.. nina maadui wa kutosha tu so bora nibakie hivi hivi mtu wa porini, mshamba mshamba fulani hivi. Haya ya manabii yananiogofyesha.
Mbona kijarida hiki ninashindwa ku-download naomba maelekezo mwanakijiji
 
newz just cum in...guys(Yona &mramba) have just been released....2 report back on 2nd Jan'09....
 
Mwakenja ni jina ambalo kila mtu anaefuatilia maswala ya nchi yake atakuwa analifahamu.
big up Sir! Thats kinds of lawyers we need!
 
Ama kweli watahadithia kwa jamaa zao!

_______________________
You can fool some of the people all of the time, and all of the people some of the time, but you can not fool all of the people all of the time.
Abraham Lincoln,
 
Hakimu awaduwaza Mramba na Yona



Na Grace Michael

MAWAZIRI waandamizi katika Serikali ya Awamu ya Tatu ambao wanakabiliwa na kesi ya kuliingizia Taifa hasara, Bw. Basil Mramba na Bw. Daniel Yona jana walikumbwa na bumbuwazi baada ya matarajio yao ya kutoka nje kwa dhamana baada ya wiki moja ya kukaa gereza la Keko kutoweka baada ya Hakimu kukataa kushughulikia suala lao.

Hali hiyo iliyowaduwaza ndugu, jamaa na marafiki wa mawaziri hao waliofurika kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakiwa wamejiandaa kuwalaki wapendwa wao, ilitokea katika mazingi yaliyowafanya wengi kutoamini-ilikuwa bayana kuwa baada ya kupunguziwa mashrti ya dhamana na Mahakama Kuu Ijumaa, watuhumiwa hao jana wangekuwa nje.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Bw. Hezron Mwankenja alifikia uamuzi wa kugoma kuingia mahakamani kuanza kushughulikia mchakato wa dhamana ya washitakiwa hao, baada ya kubaini kuwa Mramba na Yona walifikishwa mahakamani hapo kutoka gereza la Keko bila kuwepo hati ya kisheria ya kuwatoa watuhumkiwa walioko mahabusu kabla ya tarehe yao rasmi (removal order).

Baada ya kubainika kasoro hiyo Majira lilishuhudia vuta nikuvute kati ya mawakili wa washitakiwa na Hakimu huyo kujaribu kumshawashi akubali kuendelea kuisikiliza kesi hiyo bila mafanikio.

Habari zinasema kuwa baadaye Hakimu huyo alikubali kusikiliza kesi hiyo iwapo pamoja na kukosekana hati hiyo ya kuwatoa washitakiwa gerezani, kwenye jalada hilo la kesi kungekuwa na amri ya Jaji inayomtaka kusikiliza kesi hiyo, amri ambayo nayo ilikosekana lilipofunguliwa jalada la kesi hiyo lililitoka Mahakama Kuu.

Hakimu Mwankenja alionekana kushikilia msimamo wake huo na hivyo washitakiwa hao wakalazimika kupanda karandinga kurejea gereza la Keko, huku gari walimopanda vigogo wakiwa pia wamepanda watuhumiwa wa ujambazi ambao ulitokea kwenye taa za kuongozea magari za Ubungo, Dar es Salaam.

Akifafanua kuhusu kilichotokea hadi akafikia kuchukua uamuzi huo, Bw. Mwankenja alisema asingeweza kupindisha taratibu za kisheria kwa kuendesha kesi bila kuwepo hati hiyo ambayo alisema ndiyo inayomwongoza kutambua kuwa ana kesi kama hiyo kwa siku hiyo.

"Bila kufuata utaratibu unaotakiwa hatutaweza kufanya kazi, kitu kilichotakiwa ni wao kuandika barua ya maombi ya kuwaleta washitakiwa hao leo mahakamani na ikasainiwa, lakini bila hivyo tutakuwa tumevunja utaratibu na mbali na hilo pia hata jalada halioneshi elekezo lolote," alisisitiza Hakimu Mwankenja.

Aidha alisema kuwa hata mawakili wa upande wa utetezi walikiri kuwepo upungufu huo katika kufuata utaratibu wa kuwaleta washitakiwa hao mahakamani hapo.

Uchunguzi uliofanywa na Majira mahakamani hapo ulionesha kuwa mawakili wa Mramba na Yona walimsihi sana Hakimu huyo akubali kushughulikia dhamana hiyo bila mafanikio.

Hakimu Mwankenja alisisitiza kuwa kisheria hakuweza kutambua uhalali au sababu za washitakiwa hao kuwepo bila hati hiyo.

"Kama hao washitakiwa wapo basi watakuwa na mambo mengine sijapokea maombi yoyote yakiomba kuletwa kwao hapa lakini pia hakuna maelekezo yoyote kwa maandishi ambayo yananitaka kufanya hivyo kwa hiyo haitawezekana, kinachotakiwa ni taratibu kufuatwa kwa mujibu wa sheria," alisema Bw. Mwankenja.

Hata hivyo haikuweza kufahamika mara moja bila kuwepo hati hiyo watuhumiwa waliruhusiwa vipi kutoka gereza la Keko, kwani kiutaratibu, kanuni za magereza haziruhusu kutolewa mahabusu aliyeko gerezani kabla ya tarehe yake rasmi bila kuwepo hati hiyo.Swali ni je, washitakiwa hao jana walitolewa vipi gerezani hapo?

Akitotoa ufafanuzi wa kisheria kwa gazeti hili katika mahojiano kwa njia ya simu jana, wakili mashuhuri jijini Dar es Salaam, Bw. Damas Ndumbaro alisema kimsingi hati hiyo ya kuruhusu mahabusu atolewe gerezani haipo katika tamko lolote la kisheria za Tanzania bali ni utaratibu uliowekwa kwa siku nyingi na mahakama.

"Utaratibu huo haujatajwa katika CPA (Sheria ya Mwenendo wa Mashitaka ya Jinai) ila ni utamaduni wa muda mrefu wa kuomba mshitakiwa aliye mahabusu kufikishwa mahakamani kabla au nje ya tarehe ambayo kesi yake imepangwa katika kalenda ya kawaida ya mahakama.

"Ni hati ya muhimu sana kisheria kwa sababu inawasaidia hata watu wa magereza kwa kuwa inasainiwa na Hakimu husika au Jaji, kufahamu kuwa mahabusu fulani anatakiwa mahakamani kihalali.

Kwa kweli bila hiyo kiutaratibu huwa magereza hawaruhusu mtu kutolewa, sasa nani aliwatoa bila ruhusa, hiyo ni kashifa. Ila Hakimu alikuwa sahihi kiutaratibu," alisema Bw. Ndumbaro ambaye amekuwa kwenye jopo la utetezi katika mashitaka kadhaa mashuhuriu ya jinai nchini.

Kufuatia dhamana hiyo kushindikana na watuhumiwa kurejeshwa gereza la Keko nyuso za huzuni zilitawala tena mahakamani hapo, ndugu na jamaa wa watuhumiwa hao wakiendelea kutoamini makali ya taratibu za kisheria.

Washitakiwa watafikishwa tena leo mahakamani hapo wakati kesi yao itakapokuwa ikitajwa kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria.
 
Mama Mia hawa wakulu nasikia wamesha pata dhamana wapo out saizi.
 
Back
Top Bottom