Yona na Mramba: Mashtaka na yatokanayo

Yona na Mramba: Mashtaka na yatokanayo

FMES, umechanganya hawa akina Yona hapa. Yona unayemzungumzia baba yake Candy (Kande) siyo huyu Yona wa Hazina. Mmoja Yona ni jina la kwanza na mwingine Yona ni jina la mwisho. Wote ni wa-Pare ila hawana undugu. Huyu Yona fisadi binti yake mkubwa yuko kwenye late 20s au early 30s sasa hivi.

Pia huyu Yona fisadi kahamia Makongo Juu si muda sana (less than 5 years), jirani ya dada mmoja wa Tanga.

Huyo Candy yuko kwenye early 40s na alisoma na sister Morogoro kipindi hivi.

Mkuu wewe ndio kidogo unachanganya hapa,
Napenda kusema kuwa FMES yuko right!
Huyu Yona ndio babake Kandi ( Marylin) na Daniel junior na Chichi.Amekaa Makongo juu for more than 20 yrs...amefanya THB na other Banks .Pia kama consultant nje ( nadhani Mauritius na west africa )kwenye masuala ya nyumba/ real estate.Hatimaye akaingia kwenye siasa na kufanikiwa kupata ubunge na uwaziri kwenye kipindi cha Mkapa.
 
Bail saga ends as: Heavyweights come to Mramba`s rescue: And Yona fronts personal assets worth over 3bn/-
THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

A TOP local executive linked to an international gold mining company, along with a local firm involved in tanzanite mining, were amongst benefactors who yesterday helped former finance minister Basil Mramba to fulfill tough bail conditions and at last gain release from remand prison after spending a total of seven nights behind bars.

On the other hand, former energy and minerals minister Daniel Yona needed no such help, producing personal asset title deeds of sufficient value to obtain his own release after spending the same number of nights in remand prison.

And after a protracted battle against the legal odds against them, the two prominent ex-ministers in the third phase government of ex-president Benjamin Mkapa thus yesterday managed to walk out of the Kisutu Resident Magistrate's Court in Dar es Salaam as free men once more � pending formal hearing and determination of their trial.

Mramba (68) and Yona (67) are jointly charged with abuse of public office and causing a loss of more than 11.75bn/- to the nation by allegedly illegally extending the government's contract with Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation and granting dubious tax exemptions to the gold auditing company.

In order to meet their bail conditions, each was required to produce at least 2.9bn/- in cash, or alternatively surrender documentation for immovable assets worth at least that amount.

Those who came to the rescue of the 68-year- old Mramba included the country manager for AngloGold Ashanti which owns the Geita Gold Mine in Mwanza Region, Hatibu Senkoro, and large-scale tanzanite producing company Kilimanjaro Mines Limited which is based at Mirelani in Simanjiro District, Manyara Region.

The Geita Gold Mine is the largest of AngloGold Ashanti�s eight open-pit mines in Africa, and is the group's only operation in Tanzania. In favour of Mramba's bail, the AngloGold Ashanti country boss surrendered title deed number 42578 for a house worth 397m/- in Dar es Salaam.

At the same time, Kilimanjaro Mines Ltd, operating at Block A in the Mirelani tanzanite-producing area, submitted to the court title deed number 7217 for a building located on plot number 53 in Msasani, Dar es Salaam, valued at 976.42m/- .

Also in favour of Mramba's bail, another person identified as Harun Mohamed surrendered title deed number 44755 for an immovable asset valued at 1.229bn/-, while the ex-finance minister came up with title deed number 4268 for his own personal house located in the city's Kawe suburb, valued at 547.4m/-.

In total, the assets produced by Mramba and his friends were valued at more than 3.1bn/-, which is at least 200m/- over and above the amount set in the revised bail conditions as approved by the High Court.

On his part, Yona produced three title deeds for his own assets worth a combined total of 3.06bn/-.

They include title deed number 59935 for his personal house located in the Makongo Juu area, close to the University of Dar es Salaam (UDSM) main campus, valued at 2.2bn/-; plus another property also in Makongo Juu, worth 420.3m/-; as well as a third asset, valued at 443m/-.

Apart from surrendering these documents, Mramba and Yona also each had to give up their passports to the court as part and parcel of the bail conditions. They are also not allowed to leave the city without the court�s permission.

After the two completed fulfilling their bail conditions to the satisfaction of the court, Kisutu Resident Magistrate Hezron Mwankenja formally declared: ''I hereby release you on bail.''

Outside the courthouse, crowds of curious onlookers had gathered to follow the judicial proceedings against the two once-powerful ministers in the Mkapa administration.

And when they finally emerged from inside the court building, both were greeted by joyful relatives and friends, as the somewhat hostile crowd appeared not at all amused by their release.

Groups of animated youths could be heard shouting 'Thieves!' as a smiling Mramba was whisked away in a Toyota Land Cruiser (T 521 AFS) while Yona sped off in a new-model Suzuki Vitara sports utility vehicle (T 822 ANR).

Both vehicles left the Kisutu court premises at abnormally high speed, ostensibly in a bid to avoid the frenzy of reporters, media cameras and curious onlookers in the vicinity.

Prosecutors said investigations into the case have not been concluded. The case was adjourned until January 2 next year, when it comes up for its next mention.
 
Hivi mtu ukiwa na hela/mali nyingi hivyo unazifanyia nini? Mtu kama Yona anaishije material-wise yaani? I just want to try to imagine how he spends his wealth nijue what I might be in for incase I stumble into such one day
 
Date::12/2/2008
Masha atetea Magereza kuhusu Mramba, Yona

Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

KITENDO cha mawaziri wawili wa zamani kutolewa gerezani bila ya hati ya kuitwa mahakamani kimezua mjadala mkubwa kwa wadau mbalimbali, lakini Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha amelitetea Jeshi la Magereza kuwa halikuwapeleka mahakamani watuhumiwa hao.

Hakimu Hezron Mwankenja juzi alikataa kushughulikia dhamana ya mawaziri hao, Basil Mramba na Daniel Yona akidai kuwa walipelekwa mahakamani bila ya amri ya dharura ya kupelekwa mahakamani kwa ajili ya kushughulikiwa dhamana yao na hivyo kuwafanya vigogo hao kurejeshwa gerezani.

Wakati Hakimu Mwankenja akikataa kushughulikia dhamana hiyo, Mramba na Yona walikuwa kwenye gari lililokuwa nje ya mahakama wakisubiri kuitwa ndani, lakini wakajikuta wakirejeshwa tena rumande, hali iliyozua majadala juu ya nani aliwatoa vigogo hao Gereza la Keko na kuwasafirisha hadi Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu.

Jana, Waziri Masha, ambaye alitembelea gereza la Keko siku moja baada ya mawaziri hao kulazwa humo akisema kuwa alikuwa kwenye moja ya shughuli zake za kikazi licha ya kwamba alitumia gari binafsi, alisema watuhumiwa hao walikwenda Kisutu kuunganishwa na wenzao ili warudishwe Keko.

"Naomba ieleweke wazi kwamba, watuhumiwa hawakuwa wamepelekwa Kisutu kupandishwa kizimbani, walifikishwa pale ili waunganishwe na wenzao kurejea Keko... ninachosema magereza iko makini, ina mfumo imara haiwezi kutoa watuhumiwa bila taratibu," alifafanua Masha.

Waziri Masha alikiri kwamba watuhumiwa hao hawakuwa na kibali cha kuwafikisha mahakamani Kisutu kwani haikuwa siku ya kusikilizwa dhamana yao.

Hata hivyo, akifafanua zaidi alisema watuhumiwa hao walikuwa na kibali cha kufikishwa Mahakama Kuu kwa ajili ya taratibu za kumaliza dhamana zao.

"Kama mnavyojua, bado kuna taratibu za dhamana zilikuwa hazijakamilika Mahakama Kuu, sasa wao walikuwa na kibali cha Mahakama Kuu na si Kisutu," alifafanua waziri huyo.

Waziri Masha alisema uamuzi wa hakimu (Hezron Mwaikenja), kusema hakukuwa na kibali cha kuwafikisha watuhumiwa hao mahakamani hapo, ulikuwa sahihi.

"Ndiyo maana hakimu akasema hakukuwa na kibali cha kuwafikisha watuhumiwa hao mahakamani hapo, ni sahihi kwani hawakuwa wamekwenda kupandishwa kizimbani," alisisitiza Masha.

Afisa habari wa Magereza, Omar Mtiga alisema uamuzi wa kuwapeleka akina Mramba na Daniel Yona, si mpya.

Mtiga alifafanua kuwa kutokana na uhaba wa magari, si rahisi kumsafirisha kila mtuhumiwa ndiyo maana waliwachukua watuhumiwa hao na kuwapeleka Kisutu ili wakaunganishwe na wenzao ambao wanatuhumiwa kama mtandao wa wizi katika mabenki.

"Si mara ya kwanza, wakati mwingine watuhumiwa wa Kinondoni wanaletwa Kisutu kusubiri wenzao, sasa sijui hii imechukuliwaje lakini hawa hawakwenda kupanda kizimbani," alifafanua.

Aliongeza kwamba ndiyo maana watuhumiwa hao walikuwa katika chumba maalumu si kizimbani na hata hakimu hakusema kizimbani.

Wakati Masha na Magereza wakijisafisha, duru huru za habari kutoka serikalini zilisema suala hilo lilitikisa ndani ya serikali hadi Ikulu kutaka ufafanuzi.

Kwa mujibu wa duru hizo, Magereza ilipaswa kutoa maelezo kuhusu nini hasa kilitokea katika shitaka hilo.

"Hapa Ikulu imehitaji taarifa, wakuu wa Magereza wanaandaa kuipeleka Ikulu kueleza nini hasa kilitokea," zilisema duru huru.

Alipoulizwa Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo hakuwa tayari kuzungumzia na kuongeza: "Mimi siwezi chochote."

Mramba, ambaye alishika wizara nyeti katika serikali za awamu zote nne, na Yona, ambaye alikuwa waziri wa Wizara ya Madini katika serikali ya awamu ya tatu, wanatuhumiwa kutumia vibaya ofisi kwa kuipa kampuni ya M/S Alex Stewart ya Uingereza mkataba wa kudhibiti madini ya dhahabu kinyume cha sheria.

Kutokana na tuhuma hizo, wawili hao wanadaiwa kulisababishia taifa hasara ya Sh11.9 bilioni.

Wakati maofisa hao wa serikali wakitetea kitendo hicho, wadau mbalimbali wametoa maoni yao kuhusu uamuzi wa kuwapeleka mahakamani bila ya hati hiyo ya kuitwa (remove order).

Baadhi ya wananchi waliongea na Mwananchi walionyeshwa kushangazwa na kitendo hicho na kusema kuwa hali hiyo inaashiria kuna jambo fulani dhidi ya watuhumiwa hao.

“Ninavyojua mimi ni kwamba mahabusu hawezi kutolewa nje bila kibali hata kama ni kwa ajili ya kupelekwa mahakamani. Utaratibu ni kwamba askari anayekwenda kumtoa ni lazima awe na kibali cha mahakama ambacho anatakiwa kukionyesha kwanza kwa mkuu wa gereza,” alisema Clement Msumi mkazi wa Mabibo Makuburi.

Msumi alisema askari Magereza ni watu makini sana na kwamba hata mtoto mdogo hawezi kuelewa kuwa watuhumiwa walitolewa kimakosa, huku akisisitiza kuwa kwa vyovyote vile aliyetoa agizo la kutolewa kwao rumande na kupelekwa mahakamani atakuwa ni mtu mzito.

Naye Jackson Lyimo alisema askari wasingeweza kuwatoa mahabusu hao bila kibali kwa kuwa hata wao wanajua kuwa kitendo hicho ni hatari kwani ikitokea bahati mbaya wakapata ajali ama wakafa au wakatoroka mzigo huo unakuwa juu yao.
 
Hapa kuna kamchezo kalifanyika ndiyo maana Ikulu ilishtuka na kutaka maelezo.Mengine ni blah blah.
 
Jamani hawa waliokuwa watumishi wa umma wanapata wapi uwezo wa kuwa na mali za mabilioni????
 
Jamani hawa waliokuwa watumishi wa umma wanapata wapi uwezo wa kuwa na mali za mabilioni????

USISHANGAE sana ndugu yangu.
waliwezeshwa.Nyumba ya msasani kwa mfano unaweza kukuta ni kati ya zile nyumba za serikali walizouziwa bei poa na kupewa marupurupu ya kuwawezesha kulipia! Ole kwa wale wasiokuwa na nyumba za thamani! Siku ikifika itakuwa patashika maana dhamana za siku hizi masharti yake si mchezo!
 
Japo ana mashtaka ya kifisadi, Yona (na watoto) amekuwa kwenye biashara ya Real Estate kwa muda mrefu sana, hata kabla hajawa waziri. Kwa jinsi hali ya bei za nyumba zilivyo tu, hiyo Bilioni 3 ni kama nyumba sita tu za milioni 500 kila moja. Pesa anayo, cha kujiuliza ni kuwa ni zipi alizipata isivyo halali tangu alipokuwa waziri na pamoja na mali zote alizonazo, analipa kodi kama inavyostahili?
 
jamani hawa waliokuwa watumishi wa umma wanapata wapi uwezo wa kuwa na mali za mabilioni????

jamani hawa wakuu wetu wamejitahidi kutupatia picha kuwa katika hawa wakulu wawili mmoja wao ashakuwa balozi mkazi wa ghana na keshafanya kazi nyingi za ushauri ktk nchi mbalimbali, it means huyu mtu alikuwa ktk nchi ya kijamaa lakini akiishi ktk network ya kibepari huko ughaibuni na hapa ndani, huyu yonah hakuingia siasa akiwa lofa hata kidogo, tunakubali ndani miaka 10 ya ben amenufaika hasa ukizingatia tayari alishakuwa mjasiliamali longtime.

Nadhani tusipoteze muda wetu kudadisi ukwasi wa watu hapa tena ktk issue iliyo genuine kuwa siasa ya nchi hii sasa imejaa matajiri.
 
Hii ni quote kutoka web ya mwananchi Mwananchi Read News Ukisoma yote unaweza kucheka sana, na kushindwa kuamini kuwa mtu huyu amepewa wizara kama hii. Huyu Mheshimiwa anaprove kiwango cha chini kwa kuongea anayoongea, i wonder kama mwandishi amekosea, au ni kweli alisema haya. Kama alisema haya, basi ni afadhali awe anakaa kimya kuliko kuongea na kuunga mkono hata mambo yasiyofaa.

mkuu nimesoma ni vichekesho kama si aibu kabisa mkulu
sijui jama aanabeba viongozi wa aina gani!!!???
 
Hii ni quote kutoka web ya mwananchi Mwananchi Read News Ukisoma yote unaweza kucheka sana, na kushindwa kuamini kuwa mtu huyu amepewa wizara kama hii. Huyu Mheshimiwa anaprove kiwango cha chini kwa kuongea anayoongea, i wonder kama mwandishi amekosea, au ni kweli alisema haya. Kama alisema haya, basi ni afadhali awe anakaa kimya kuliko kuongea na kuunga mkono hata mambo yasiyofaa.

mkuu nimesoma ni vichekesho kama si aibu kabisa mkulu
sijui jama aanabeba viongozi wa aina gani!!!???

Serikali ya kishikaji, unategemea nini? Kama cheo mtu anapewa si kulingana na uwezo ama CV yake bali na fdhila na maelngo mengineyo hayo ndo tuyategemee siku zote!.

By the way nadhani suruhisho ni kubadili kaiba na kumpunguzia mamlaka raisi walau akichagua mawaziri wathibitishwe na bunge period!
 
Hii ni quote kutoka web ya mwananchi Mwananchi Read News Ukisoma yote unaweza kucheka sana, na kushindwa kuamini kuwa mtu huyu amepewa wizara kama hii. Huyu Mheshimiwa anaprove kiwango cha chini kwa kuongea anayoongea, i wonder kama mwandishi amekosea, au ni kweli alisema haya. Kama alisema haya, basi ni afadhali awe anakaa kimya kuliko kuongea na kuunga mkono hata mambo yasiyofaa.

mkuu nimesoma ni vichekesho kama si aibu kabisa mkulu
sijui jama aanabeba viongozi wa aina gani!!!???

Serikali ya kishikaji, unategemea nini? Kama cheo mtu anapewa si kulingana na uwezo ama CV yake bali na fdhila na maelngo mengineyo hayo ndo tuyategemee siku zote!.

By the way nadhani suruhisho ni kubadili kaiba na kumpunguzia mamlaka raisi walau akichagua mawaziri wathibitishwe na bunge period! Na hapo jukumu letu wananchi ni kuhakikisha tunakuwa na bunge lenye meno lenye uwakilishi wa uwiano wa chama tawala na upinzani.
 
Wakuu enzi za waziri Daniel Yona akiwa waziri wa nishati na madini alikwapua bilioni 2 pesa za wananch, wananchi wa wilaya ya Kasulu. Ni baada ya wananchi kufanikiwa kupata fedha za mradi wa umeme wa maji kutoka serikali na Denamark kupitia shirika lake la misaada DANIDA, wananchi wakiongozwa na Mzee maarufu Mzee Ntiruka walipata Bilioni 2 pesa za kitanzania, kwa ajiri ya mradi wa umeme wa nguvu za maji kutoka chanzo cha mto katika kijiji kimoja huko, kwaani mmisionari wa kanisa la katoriki aliweza kufanikiwa kutengeneza umeme wa nguvu za maji.

Wanachi walitakiwa kuchangia milioni 100. Katika ziara ya waziri wakati huo (Daniel Yona) alishawishi pesa zile zipelekwe wizarani eti ataongeza fungu zaidi nguvu iwekwe kwenye grid ya taifa na kupeleka umeme katika mkoa mzima wa Kigoma badala ya wilaya moja ya Kasulu, lakini bahati mbaya pesa ile iliishia mikononi mwa waziri na kutafunwa.

Wananchi waliwahi kumfikishia malalamiko kwa Mheshimiwa Rais Kikwete Kikwete katika ziara za mwanzo katika mkoa wa Kigoma, alimwelekeza mbunge wakati ule Daniel Nsanzugwanko alishughurikie lakini mpaka sasa hakuna jibu la pesa hizo. Serikali ya CCM inarudisha maendeleo ya wananchi kwa kuwakatisha tamaa.
 
ulikuwa wapi kuleta haya miaka hiyo kadhaa imepita sasa, au umekumbuka nini leo?
 
Back
Top Bottom