Yona na Mramba hawana kesi ya kujibu maana katika katiba yetu ya Tanzania kahuna sheria au kifungu chochote binding kinachomtaka Waziri au Niabu Waziri kufuata ushauri fulani katika kutoa maamuzi , ndio maana kuna collective cabinet responsibilities hivyo kama hawa walikosea, ni Cabinet nzima na Rais wao-Mkapa walikosea na kuitia serikali hasara hizo, pia hawawezi kufanywa scape goats maana sheria ina-operate uniformly btn citizens hivyo hata wengineo walioboronga inabidi waletwe mbele ya Pilato mkuu as soon as practically is possible. Labda akina yona na Mramba wa-argue hili ili watanzania wainuliwe macho..
Case hii ni Nzuri kama DPP akiishinda maana ina na ita-set precedent kwa wengineo kufanyiwa kweli, sio Magufuri, Megji (sorry spelling), kalamagi na hata Mkapa Mwenyewe.
Kinachotakiwa ni DPP na wanasheria wake wawapeleke wote waliokuwa kwenye cabinet ya mkapa na waishitaki cabinet nzima ya mkapa-Kikwete akiwemo pia kwamba- wali-abuse powers as collective responsibility na pia kwamba wananchi wa Tz hawakuwatuma kwenda kufanya criminal activities bali ku-excute sheria zilizomo ndani ya katiba yetu.
Evidence zipo za akina Mwakyembe na Dr Slaa, kwa nini kusua sua, witness wapo na affidavits nyingine zipo sasa kwanini kuogopa ogopa kama kuku anayechinjwa?
Kama DPP anasua sua hata yeye mwenyewe ana harufu ya ka-ufisadi maana walikuwepo wakati haya yanatokea in some capacities, na tunachohitaji ni kuwa na independent judiciary iliyo kama federal Court ya USA kwamba Rais aweze kuwachagua majaji lakini asiwe na uwezo wa kuwafuta baada ya bunge kuwathibitisha, wao wawe independent na excutives pia legislature.. hii itasaidia kuwafikisha mahakamani wale wote wanaofanya uharifu.
1. Dpp alisema kwamba ma-fisadi wote wakipelekwa mahakamani , nchi itayumba, basi afanye amnest kwa masharti ya kwamba mali zao zote zitaifishwe na ziletwe kwenye ujenzi wa taifa pia mafisadi hao badala ya kuachwa kwenda huru, waisadie serikali katika kutumia akili zao kuziba mianya ya ufisadi maana wao wanazifaham loopholes za grand corrption haswa.
SMP- LLM London