Nimecheka sana,sasa umejuaje kama hayupo
Kwani kisichokuwepo kinajulikanaje hakipo?
?
Nani amekwambia kisichokuwepo hakithibitishiki?
Niletee uthibitisho wa kutokuwepo spiderman
Kama yuko nje ya hadithi na idea, kwa hakika mpaka jambo kuhusu Mola kingekuwa si lenye kutajika.
Spiderman anatajika. Kwa hiyo unakubali yupo?
Hivi huwa unakitafakari unachokiandika kijana ? Maana naona unakinzana na unachokiandika na kile unachokidai.
Maneno ya Qur'aan ni ukweli na uhalisia ndiyo maana nayarejea na si madai. Mfano wa wa ukweli huo, ni hili swali toka katika sura 52 aya ya 35.
Hayo ni mafunzo ya kiimani ambayo si lazima yahitaji uthibitisho. Mi nahoji uthibitisho
Anasema Allah aliye juu :
Anasema allah au ni maandishi ya kuran yameandika kuwa allah anasema?
Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji? ( At-home Tur : 35 ).
Quran inaelewa umuhimu wa chanzo ili kilichopo kiweze kiwepo?
Usiniambie "isipokuwa" kwasababu tunaweza kutumia sheria hiyo hiyo ku describe vingine
Maneno ya vitabu vingine yana uongo mwingi kuliko usahihi wake,kwahiyo hayana nafasi na haya kishi haja. Sababu hayatoki kwa Mola muumba.
Dini zaidi ya 2000 we umewwzaje kusoma vitabu vyote hivyo na ukajua ni uwongo?
Qur'aan haidhani bali inasema ukweli.
Ukweli kwa uthibitisho upi? (usiniambie kwasababu ya ulimwengu na vilivyomo kwasababu kila dini imeelezea ukweli wa vitabu vyao kwa kuonesha ulimwengu na vilivyomo kua ndio mfano)
Suala la chanzo ni la ulazima na halikwe
peki sababu huo ndiyo uhalisia. Sababu hakuna kisichokuwa na chanzo ila Mola tu.
Mpaka hapo chanzo sio lazima.
Kumbe tunaweza kusema kila kitu ndani ya ulimwengu kinachanzo isipokuwa ulimwengu na bado tukawa sahihi
Inawezekana ila ambaye hana chanzo ni Mola pekee na vingine vyote vinarejea kwake. Sasa nikuulize wewe kipi kingine ambacho hakina chanzo na ututhibitishie ukweli wa unachokidai.
Kisichokua na chanzo ni ulimwengu.ila vingine vyooote vina chanzo
Kitabu hakian dhana, ndiyo maana kinachoyasema hamuwezi kuyapinga kileimu zaidi ya dhana kama unavyofanya hapa.
Yap siwezi Kama ambavyo wewe huwezi kupinga kielimu dini 2000 zilizopo duniani lakinj bado ukaendelea kuziona za uwongo
kwa uthibitisho wa kuwa kila kitu kipo katika nidhamu na utaratibu usio ingiliana na kingine. Tazama mwendo wa jua kila siku linachomoza kutoka Mashariki na kuzama Magharibi, kuna usiku na mchana, kuna cha kiume na cha kike, kuna kutegemeana na mfano wa hivyo.
Well, ila haya pia yanaelezeka bila kuhusisha mungu wala dini
Nakuonyesha ya kuwa huyo mwingine hawezi, yule anae abudu ng'ombe anaweza kusema ya kuwa ng'ombe ameumba dunia na vilivyomo ?
Kwa maana hiyo wewe unayeabudu unseen God unajiona upo salama kwasababu swali hilo kwako linajibika?
Kwa maana hiyo wale wote wanaoabudu miungu mingine isiyoonekana kama wako watakuwa sahihi kusema Mungu wao kaumba ulimwengu?
Inakuwaje unaukiza swali la kitoto nana hii, hao mpaka wanaabudu hiyo miungu yao ujue ipo ila haina sifa ya kuitwa Mungu. Sasa utathibitisha vipi kutokuwe po kwa Ng'ombe wakati kila siku tuna mla nyama ? Jenga hoja kijana acha wasi wasi na uoga.
Hata wewe mungu wako hana sifa za kuitwa Mungu katika dini zingine. Hivyo unabidi utambue kuwa katika dini nyingine mungu wako anahesabika kama "miungu" kama ambavyo wewe umekuwa ukiita miungu inayoabudiwa na dini nyingine
Asili haiko hivyo hatuendi kwa dhana wala hatubahatishi. Wewe kuwepo kwako hakuthibitishi ya kuwa una baba au ulikuwa na baba au mama?
Unajuaje labda ni clone?
Ndiyo maana vitabu vya dini vimeshatoa majibu, na kuwauliza nyinyi ya kuwa sisi tumetokana pasi na chochote su sisi ndiyo tumejiumba ? Kuna vitu havina kinyume chake mzee.
Hilo swali linahitaji explanations
Je chanzo ni muhimu ili kitu kiwepo?
Je kilichopo ni lazima kiwe na chanzo?
Kumbuka jibu hapo lisiseme kua "kila kitu kina chanzo isipokua jambo flani"
Kama hakuna lazima wa chanzo basi hakuna haja ya kuhangaika kujua chanzo cha ulimwengu kwasababu tutahitimisha tu kua hauna chanzo
Ila kama kila killichopo kina chanzo mtuambie huyo mungu aliumbwa na nani/nini?
Ni ujinga ulioje kudai uongo wa njia fulani bila kuonyesha uongo huo na kukosoa njia hiyo.
Nikikuambia hiyo ni self evident truth inayojionesha yenyewe utakubali?
Kosoa njia hii na uonyeshe uongo wake. Kila mtu akiaumua kusema anasema tu, shida inakuja katika uthibitisho, ndiyo hapa huwa mnakimbia na kuleta dhana.
Kama ambavyo kila mtu akiamua kukwepa hoja anaweza kuweka madai yake na kusema kuwa ni self ecident truth na kuwataka watu wakubali bila uthibitisho.
Vipi nikikuambia kila nilichokiandika hapa ni self evident truth, utaridhika na jibu langu?
Sasa unakataa nini na unakubali nini ? Kuwepo kwako kunathibitisha hilo. Sasa turudi kwenye ulimwengu, kuwepo kwa ulimwengu kunaonyesha kutokuwepo kwa aliye umba ulimwengu au kunaonyesha ya kuwa ulimwengu umetokea tu pasi na chochote au ulimwengu umejiumba ?
Uwepo wa ulimwengu unaonesha ulimwengu upo
Sasa huu mjadala wa wewe kukataa ya kuwa Mola yupo kunatoka wapi kama unakubali ya kuwa uwepo wako wewe "automatically" huthibitisha juu ya uwepo wa wazazi wako ?
Hujaelewa hoja yangu, hoja yangu ilikuwa inajaribu ku challenge dhana yako ya self evident truth kupitia mfano wako ambao hauendani na kile kitu ulicho ki propose mwanzo
Ulisema mungu yupo kupitia kielelezo cha uwepo wa ulimwengu kua hiyo ni self evident truth
Halafu ukaja na mfano wa baba na mimi, kwamba sihitaji uthibitisho wa kujua baba ni mkubwa kwangu. Sasa huu mfano wako hauendani na hilo dai lako la kwanza, kwasababu mtoto na baba wote wapo na wanathibitishika, ukija katika hoja yako inaonesha ulimwengu upo na unathibitishika ila huyo mungu hayupo na unayaka kumthibitisha kupitia ulimwengu jambo ambalo ni uongo