Yawezekana Afande Sele yupo Sahihi?

Yawezekana Afande Sele yupo Sahihi?

Hizi issues za imani huwa ni mantanange kweli kweli, watu walishalishwa yamini kuwatoa ni changamoto la jua la saa 7pm!
 
Umeongelea uislam na uKristo sasa vipi kuhusu wanaoabudu ng'ombe, nyoka, mbuzi, vinyago, bangi na migomba etc?
 
Hawana tofauti na wakristo na waislamu
 
Mwanafunzi mwingine wa Kiranga.

Afande kasema anaabudu migomba yake au bangi zake.

Sasa huyo mtu nzima kweli?
Sasa migomba inatofauti gani na hili dubwasha hapa ambalo makanisani limewekwa?

IMG_20210405_140912.jpg

Mtu kabisa na akili zako timamu utamuona afande sele ni mjinga kwa kuabudu migomba na bangi halafu huyu anayepigia magoti hilo lizege la mifuko miwili ya cement mixer concrete awe na akili timamu?

Angalia kundi lingine hili zaidi ya maelfu ya watu hapa wameinama kulisujudia lakini unakuta watu hawa nao wanaungana kuponda migomba ya afande sele

1617621361175.png

Tuwe serious sometimes hata kama tupo kipindi cha april fools
 
Yeye ameumbwa na hiyo dhana! Bangi tu zunamsumbua
 
Kingine sitarajii kupambana na hali yangu baada ya kufa!
Naamini nikifa ntakuwa kama nilivyokuwa kabla sijazaliwa.
SAWA, KWANI WEWE UNA TATIZO NA WENYE IMANI KUWA MUNGU YUPO NA WATAISHI BAADA YA KUFA? AU UNGEPENDELEA WOTE TUFANANE NA WEWE? HAITAKAA ITOKEE.

Wewe unaamini hakuna MUNGU/PAGANI kwa sababu zako na hakuna atakayekukataza, na unaamini kuwa baada ya wewe kufa hutakuwepo tena ndo mwisho wako. SAWA.

KILA MTU NA AAMINI ANACHOAMINI NA ITAPENDEZA KAMA MWISHO UTAKUWA KULINGANA NA IMANI.
 
Wanajamii,

Umofia kwenu.

Baada ya msiba wa mzee Magufuli, mwimbaji wa zamani wa mziki wa kizazi kipya maarufu kama Afande Sele/mkali wa rhymes alijitokeza na kutoa maneno mengi yaliyotafsiriwa kama kashfa au matusi kwa Mungu na watu wengi.

Msanii huyo mantiki yake ilionekana kudai Mungu ni dhana tu hayupo kama angekuwepo asingemuondoa Magufuli mapema kiasi hiki wakati bado anahitajika.

Hoja yangu ni kwamba, vipi kama ni kweli Afande Sele yupo Sahihi?

Kwanini...

Mosi, Dini nyingi sana. Haiwezekani Huyu Mungu anayempenda mwanadamu alete utitili wa dini halafu aweke masharti ya kwamba ukikosea unachomwa moto. Ni sawa na uwe mgonjwa uende kwa daktari halafu huyo dk amwage dawa zaidi ya 4000 mbele yako then akulazimishe kuchagua dawa moja sahihi, na adhabu pale tu utakapokosea.

Pili. Mwingiliano wa vitabu. Qur'an na Biblia kuna mwingiliano wa visa vinavyofanana, pamoja na wahusika. Mfano Mariamu, Issa(yesu) Musa, Ibrahim pamoja na wengine wengi. Hii sio kufanana kwa bahati nasibu tu ila kuna mmoja alinakili kutoka kwa mwenzake na/ kulingana na mazingira yanayofanana basi hivi ni visa vya kubuni ambavyo ilikuwa haiwezekani kuvikwepa, ni sawa na ngano za Kiafrika ambavyo huwezi kumkwepa mhusika "zimwi".

Eti, Mungu anajuwa yote (Omnipotence), kwanini hakugundua mapema kama shetani angeleta zogo kwa Adam na Hawa? Baada ya Ibilisi kupambana na majeshi ya Mungu akashindwa alitupwa duniani, then anamuumba mwanadamu anamweka duniani. Anaweza kumwacha mwanao unaemoenda alale chumba kimoja na chatu? Kwanini asingetuweka hata sayari ya Mars.

Mungu na shetani sio maadui.

Hii inajidhihirisha pale anapopiga stori na Shetani, mwanzoni kabisa mwa kitabu cha Ayubu.
"Shetani akiwa anatembea zake duniani akiwa anapunga upepo, alikutana na Mungu, Mungu akamuuliza ... Umenionea mtumishi wangu Ayubu...."

Kwa muktadha wa mazungumzo hayo, viumbe hawa hawawezi kuwa maadui.

Tano, kama Mungu anabusara asingeweza kumwacha shetani akae pamoja na mwanadamu.

Kumbuka shetani alikuwa malaika, ambaye licha ya uwezo wa jeshi tiifu la Mungu alifanikiwa kupambana nalo kwa muda mrefu, mwanadamu angewezaje kukaa na jeshi la Shetani sasa, au Mungu hakujua.

Mungu pia hufa kutokana na maendeleo ya wanadamu.

Wanadamu wamekuwa na miungu wengi sana ambao kulingana na wakati na maendeleo ya sayansi hao miungu hufa na kupotea, mfano ni NIKE Mungu wa vita, ATLAS mungu aliyeshikilia/beba mabegani dunia hewani isiporomoke, VULCA, mungu wa moto na hasira aliyekuwa akikasirika hufuka moto toka ardhini. (Ambaye kwaye tumepata neno Volcano)

Je, unahakika huyu Mungu unayemwamini sasa hatakufa kutokana na wakati?

UNA UHAKIKA?
Nanukunukuu kipengele hiki
[emoji116][emoji116]

Mungu Anakujibu
[emoji116][emoji116]
ISA. 55:8-9 Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.

Umebakia kwa nini kwa nini
Mtu ana shamba lake! Kapanda nyanya, mihogo, bange...kama Ilivyo Mpende Mwenyewe [emoji123][emoji106]
ww unahoji kwa nini kwa nini umepanda 1 2 6...
Kwani shamba lako??
Kama una ubavu umba shamba lako ufanye utakavyo!
 
Huwezi ukasema Mungu hayupo wakat haumjui.Nisawasawa na umekutana na mtu kwenye sherehe,alaf unamuuliza umemwona Joseph ukumbini?anakujibu sijamwona,unamuuliza unamjua lakin? Anakujibu cmjui.unabaki kushangaa sasa amejuaje Kama Joseph hayupo ukumbini wakat hamjui.Vivohivyo hatuwezi kusema Mungu hayupo wakat hatumjui
 
Msanii huyo mantiki yake ilionekana kudai Mungu ni dhana tu hayupo kama angekuwepo asingemuondoa Magufuli mapema kiasi hiki wakati bado anahitajika.
Umemnukuu tofauti Sele kwani yeye alimtukana Mungu, hakusema Mungu hayupo. Huwezi kutukana kitu ambacho hakipo. Kwa kuwa umemnukuu tofauti, maelezo yako yoote pamoja na wingi wake, hayana maana yoyote kwani yanaelezea kitu tofauti na kilichozua mjadala. Na kwa kuwa upo nje kabisa ya mada, basi uzi wako ufungwe, vinginevyo labda umnukuu mtu mwingine
 
je' tangu uyu ibilisi alivyoasi uko mbinguni enzi izo hakuna malaika mwingine yeyote aliyekengeuka au ndio ngano za warumi
 
Wanajamii,

Umofia kwenu.

Baada ya msiba wa mzee Magufuli, mwimbaji wa zamani wa mziki wa kizazi kipya maarufu kama Afande Sele/mkali wa rhymes alijitokeza na kutoa maneno mengi yaliyotafsiriwa kama kashfa au matusi kwa Mungu na watu wengi.

Msanii huyo mantiki yake ilionekana kudai Mungu ni dhana tu hayupo kama angekuwepo asingemuondoa Magufuli mapema kiasi hiki wakati bado anahitajika.

Hoja yangu ni kwamba, vipi kama ni kweli Afande Sele yupo Sahihi?

Kwanini...

Mosi, Dini nyingi sana. Haiwezekani Huyu Mungu anayempenda mwanadamu alete utitili wa dini halafu aweke masharti ya kwamba ukikosea unachomwa moto. Ni sawa na uwe mgonjwa uende kwa daktari halafu huyo dk amwage dawa zaidi ya 4000 mbele yako then akulazimishe kuchagua dawa moja sahihi, na adhabu pale tu utakapokosea.

Pili. Mwingiliano wa vitabu. Qur'an na Biblia kuna mwingiliano wa visa vinavyofanana, pamoja na wahusika. Mfano Mariamu, Issa(yesu) Musa, Ibrahim pamoja na wengine wengi. Hii sio kufanana kwa bahati nasibu tu ila kuna mmoja alinakili kutoka kwa mwenzake na/ kulingana na mazingira yanayofanana basi hivi ni visa vya kubuni ambavyo ilikuwa haiwezekani kuvikwepa, ni sawa na ngano za Kiafrika ambavyo huwezi kumkwepa mhusika "zimwi".

Eti, Mungu anajuwa yote (Omnipotence), kwanini hakugundua mapema kama shetani angeleta zogo kwa Adam na Hawa? Baada ya Ibilisi kupambana na majeshi ya Mungu akashindwa alitupwa duniani, then anamuumba mwanadamu anamweka duniani. Anaweza kumwacha mwanao unaemoenda alale chumba kimoja na chatu? Kwanini asingetuweka hata sayari ya Mars.

Mungu na shetani sio maadui.

Hii inajidhihirisha pale anapopiga stori na Shetani, mwanzoni kabisa mwa kitabu cha Ayubu.
"Shetani akiwa anatembea zake duniani akiwa anapunga upepo, alikutana na Mungu, Mungu akamuuliza ... Umenionea mtumishi wangu Ayubu...."

Kwa muktadha wa mazungumzo hayo, viumbe hawa hawawezi kuwa maadui.

Tano, kama Mungu anabusara asingeweza kumwacha shetani akae pamoja na mwanadamu.

Kumbuka shetani alikuwa malaika, ambaye licha ya uwezo wa jeshi tiifu la Mungu alifanikiwa kupambana nalo kwa muda mrefu, mwanadamu angewezaje kukaa na jeshi la Shetani sasa, au Mungu hakujua.

Mungu pia hufa kutokana na maendeleo ya wanadamu.

Wanadamu wamekuwa na miungu wengi sana ambao kulingana na wakati na maendeleo ya sayansi hao miungu hufa na kupotea, mfano ni NIKE Mungu wa vita, ATLAS mungu aliyeshikilia/beba mabegani dunia hewani isiporomoke, VULCA, mungu wa moto na hasira aliyekuwa akikasirika hufuka moto toka ardhini. (Ambaye kwaye tumepata neno Volcano)

Je, unahakika huyu Mungu unayemwamini sasa hatakufa kutokana na wakati?

UNA UHAKIKA?
Hivi unapokuwa na kiatu chako huwa kinakuamulia cha kufanya au wewe ndo mwenye maamuzi
 
Tatizo hiki kitabu unachosema, watu wengi hukitazama na kukipa nafasi tofauti na kitabu cha hesabu!!!
 
Back
Top Bottom