Yawezekana Afande Sele yupo Sahihi?

moghasa

JF-Expert Member
May 7, 2013
1,084
1,251
Wanajamii,

Umofia kwenu.

Baada ya msiba wa mzee Magufuli, mwimbaji wa zamani wa mziki wa kizazi kipya maarufu kama Afande Sele/mkali wa rhymes alijitokeza na kutoa maneno mengi yaliyotafsiriwa kama kashfa au matusi kwa Mungu na watu wengi.

Msanii huyo mantiki yake ilionekana kudai Mungu ni dhana tu hayupo kama angekuwepo asingemuondoa Magufuli mapema kiasi hiki wakati bado anahitajika.

Hoja yangu ni kwamba, vipi kama ni kweli Afande Sele yupo Sahihi?

Kwanini...

Mosi, Dini nyingi sana. Haiwezekani Huyu Mungu anayempenda mwanadamu alete utitili wa dini halafu aweke masharti ya kwamba ukikosea unachomwa moto. Ni sawa na uwe mgonjwa uende kwa daktari halafu huyo dk amwage dawa zaidi ya 4000 mbele yako then akulazimishe kuchagua dawa moja sahihi, na adhabu pale tu utakapokosea.

Pili. Mwingiliano wa vitabu. Qur'an na Biblia kuna mwingiliano wa visa vinavyofanana, pamoja na wahusika. Mfano Mariamu, Issa(yesu) Musa, Ibrahim pamoja na wengine wengi. Hii sio kufanana kwa bahati nasibu tu ila kuna mmoja alinakili kutoka kwa mwenzake na/ kulingana na mazingira yanayofanana basi hivi ni visa vya kubuni ambavyo ilikuwa haiwezekani kuvikwepa, ni sawa na ngano za Kiafrika ambavyo huwezi kumkwepa mhusika "zimwi".

Eti, Mungu anajuwa yote (Omnipotence), kwanini hakugundua mapema kama shetani angeleta zogo kwa Adam na Hawa? Baada ya Ibilisi kupambana na majeshi ya Mungu akashindwa alitupwa duniani, then anamuumba mwanadamu anamweka duniani. Anaweza kumwacha mwanao unaemoenda alale chumba kimoja na chatu? Kwanini asingetuweka hata sayari ya Mars.

Mungu na shetani sio maadui.

Hii inajidhihirisha pale anapopiga stori na Shetani, mwanzoni kabisa mwa kitabu cha Ayubu.
"Shetani akiwa anatembea zake duniani akiwa anapunga upepo, alikutana na Mungu, Mungu akamuuliza ... Umenionea mtumishi wangu Ayubu...."

Kwa muktadha wa mazungumzo hayo, viumbe hawa hawawezi kuwa maadui.

Tano, kama Mungu anabusara asingeweza kumwacha shetani akae pamoja na mwanadamu.

Kumbuka shetani alikuwa malaika, ambaye licha ya uwezo wa jeshi tiifu la Mungu alifanikiwa kupambana nalo kwa muda mrefu, mwanadamu angewezaje kukaa na jeshi la Shetani sasa, au Mungu hakujua.

Mungu pia hufa kutokana na maendeleo ya wanadamu.

Wanadamu wamekuwa na miungu wengi sana ambao kulingana na wakati na maendeleo ya sayansi hao miungu hufa na kupotea, mfano ni NIKE Mungu wa vita, ATLAS mungu aliyeshikilia/beba mabegani dunia hewani isiporomoke, VULCA, mungu wa moto na hasira aliyekuwa akikasirika hufuka moto toka ardhini. (Ambaye kwaye tumepata neno Volcano)

Je, unahakika huyu Mungu unayemwamini sasa hatakufa kutokana na wakati?

UNA UHAKIKA?
 
Mwanafunzi mwingine wa Kiranga ..

Afande kasema anaabudu migomba yake au bangi zake.....
Sasa huyo mtu nzima kweli?
Amesema hivyo kwasababu ya hasira yake juu ya Mungu wenu akiwa na maana ya kumlinganisha na bangi pamoja na migomba! Downsizing intent !
 
Waebrania 13:8 Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele.

Basi hakuna kuongeza wala KUPUNGUZA
Nje ya biblia unajua pia kuna Qur'an, Talmud, venda,.... Kinachokufanya hoja zako uegemee kwenye biblia ni nini?

Kinachokufanya uamini kwamba mpango wa Mungu wako ni mwanadamu nini, vipi kama ng'ombe ndio viumbe teule wa Mungu kama kweli yupo. Au kwavile ng'ombe lugha yao hatuelewi
 
Nje ya biblia unajua pia kuna Qur'an, Talmud, venda,.... Kinachokufanya hoja zako uegemee kwenye biblia ni nini?

Kinachokufanya uamini kwamba mpango wa Mungu wako ni mwanadamu nini, vipi kama ng'ombe ndio viumbe teule wa Mungu kama kweli yupo. Au kwavile ng'ombe lugha yao hatuelewi
Kwasababu mambo yanadhihirika kwenye maisha yangu
 
Ndiyo maana naipenda sana biblia. Ilijua kuna watu hawamwamini Mungu. Kwa hiyo yawaita wapumbavu 😂😂😂

“Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.” Zaburi 14:1

“Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza, Hakuna atendaye mema.” Zaburi 53:1
 
Kwa mujibu wa maneno yako hapa itakuwa sio rahisi kuelewa hata nikikuelezea akili yako tayari inamajibu
Unachokifanya ni "Ad hominem Argumentum " unanishambulia kwa kuangalia akili yangu badala ushambulie hoja niliyoweka.
 
Hatari mijadala ya dini maana inaleta mipasuko.
Swali la zamani zaidi hapa duniani " .... Tumetoka wapi?" Hii ni katika kutafakari sisi ni nani na kwanini tuko hapa!

Sina lengo la kuleta mpasuko, lakini pia nataka akili yangu ifanye suluhu na Afande Sele!
 
Back
Top Bottom