Yawezekana Afande Sele yupo Sahihi?

Yawezekana Afande Sele yupo Sahihi?

Dini zaidi ya 2000 we umewwzaje kusoma vitabu vyote hivyo na ukajua ni uwongo?
Inaonekana husomi, tafuta kitabu hiki usome.
IMG-20210323-WA0011.jpg

Sisi tunasoma nyinyi mnaokoteza. Hiki kitabu kimeelezea vyanzo vya Dini,makundi na mfano wa hayo.
Well, ila haya pia yanaelezeka bila kuhusisha mungu wala dini
Tatizo siyo kuelezeka tatizo yanayo elezwa ni ya kweli au la. Mara ngapi tumeambiwa ya kuwa chanzo cha dunia ni "Kishindo kikubwa", wanafalsafa wa kale wamagharibi walisema chanzo cha maisha ni hewa, wengine wakasema maji, wengine wakasema ni jua. Wote hawa walieleza. Lakini wanasayansi wanatuambia ya kuwa kuwepo kwa usiku na mchana ni matokeo ya Dunia kuzunguka katika muhimili. Wote wanaelezea haya mambo, swali ni je wanayoyasema ni kweli ? Kwahiyo hii si hoja, hoja ni je hayo maelezo ni ya kweli au uongo.
Kwa maana hiyo wewe unayeabudu unseen God unajiona upo salama kwasababu swali hilo kwako linajibika?

Kwa maana hiyo wale wote wanaoabudu miungu mingine isiyoonekana kama wako watakuwa sahihi kusema Mungu wao kaumba ulimwengu?
Mola wetu amejielezea kupitia vitabu na kuna chain ambayo haijakatika.

Tunamuabudu Mola ambaye haonekani Ulimwenguni ila kuna muda ataonekana kama tunavyoliona jua la saa sita mchana. Lakini Mola huyu huyu hakutuacha hivi hivi baada ya kutuumba bali alituwekea ishara za kuona na kujua uwepo wake.
kwasababu ya ulimwengu na vilivyomo kwasababu kila dini imeelezea ukweli wa vitabu vyao kwa kuonesha ulimwengu na vilivyomo kua ndio mfano)
Soma aya ya 35 katika sura ya 52, nilikuwekea huko nyuma.
Hata wewe mungu wako hana sifa za kuitwa Mungu katika dini zingine. Hivyo unabidi utambue kuwa katika dini nyingine mungu wako anahesabika kama "miungu" kama ambavyo wewe umekuwa ukiita miungu inayoabudiwa na dini nyingine
Thibitisha ya hilo. Hapa nakupa mfano. Makafiri wa kiarabu walikuwa wana miungu 360, lakini kuna muda mambo yalipokuwa yanawazidia wanarudi kwa Mola wa ulimwengu. Sasa sharti lazima Mungu huyo ajielezee na kuwe na ushahidi.
 
Kwani kila kilichopo lazima kiwe na chanzo?

Usitumie fallacy yako kusema "kila kitu kinachanzo isipokuwa"

Kama hakuna ulazima wa chanzo basi hakuna haja ya kusema ulimwengu unachanzo
Unaposema hii ni fallacy, kazima uonyeshe hilo.

Kila kitu kina chanzo ila Mola pekee,vipi aliyeumba awe na chanzo ? Usiulize maswali ambayo majibu yake yako wazi.
 
Nimekuuliza swali

Unawezaje kusujudu bila kupiga magoti?

We unakuja kuniambia sijui kupiga magoti sharti kiwili wili kiwe kimefanyaje na blah blah kibao.

Kupiga magoti kuna involve magoti hatuangalii namna mwili unavyoonekana

Kwa hiyo hao pichani wako wima au wamesimamia tumbo?

Au wamepiga nne?
Inaonekana hujui maana ya kusujudu na kupiga magoti. Unaweza kusujudu bila kupiga magoti, kwani kupiga magoti ni sharti kiwili wili kiwe wima. Ndiyo maana ikawa kupiga magoti si sawa na kusujudu.

Hao pichani wamesujudu i
 
Uwepo wa ulimwengu unaonesha ulimwengu upo
Imekuwaje ukawepo ? Hili ndiyo swali la msingi. Hata wewe kuwepo kwako kunaonyesha upo ila baada ya mchakato maalumu.
Kifo kinajulikana na kinaelezeka vyema na kuthibitishika. Roho ni hadithi za dini ambayo inatumika kama ngao pale hoja ngumu zinapotolewa na kipindi hiki roho imekua ikihusishwa hadi kufanya dhurma

Mchungaji anatapeli watu kwa kuwaambia roho wa mungu kaniambia waumini mnichangie milion kumi ninunue gari ya kutembelea

Roho sio tu ni uzushi nje ya dini bali hata kwenye dini humo humo habari zake zimejaa ukakasi sana.

Wewe ukikaa na mkristo muanze kuzungumzia mada ya roho hamuwezi mkafika hitimisho bila kuhitilafiana hiyo inaonesha jinsi gani wote hamuwezi kua sahihi japokua kila mmoja atavutia upande wake kua yuko sahihi ila mwenzake amepotoka
Kifo kinajulikana,ila tunatofautiana katika kukielezea. Katika kutofautiana huko yupo mkweli. Ukitaka kuona ya kusa hujui hakika ya kifo. Tuambie kifo ni nini ?

Haya mchungaji uongo wake wazi kabisa, no vile tu Wakristo si watu wa kuhoji na kuwabana wakubwa wao. Laiti kama wangekuwa ni watuwa kuhoji, Ukristo ungebakia vitabuni tu.

Ukwei kuhusu Roho uko wazi, na ndiyo maana Moa wetu akasema ya kuwa ametupa elimu ndogo sana kuhusu Roho, huki nyingine kubwa ikibakia kwake. Roho ni kitu kisicho onekana ambacho kwacho humpa uhai mwanadamu, Roho ni katika vitu miongoni mwa vitu vyenye mwanzo ila havina mwisho.

Hakuna tamko "dhurma" sahihi ni "dhulma".

Nithibitishie ya kuwa Roho ni hadithi za dini tum
 
Unajuaje labda ni clone?
Usilete dhana, weka jibi la uhakika. Clone inajulikana wazi. Sasa unaposema labda ni clone, inaonekana hujui clone ni nini na hujui unachokielezea.
 
Hilo swali linahitaji explanations

Je chanzo ni muhimu ili kitu kiwepo?

Je kilichopo ni lazima kiwe na chanzo?

Kumbuka jibu hapo lisiseme kua "kila kitu kina chanzo isipokua jambo flani"

Kama hakuna lazima wa chanzo basi hakuna haja ya kuhangaika kujua chanzo cha ulimwengu kwasababu tutahitimisha tu kua hauna chanzo

Ila kama kila killichopo kina chanzo mtuambie huyo mungu aliumbwa na nani/nini?
Chanzo hakiepukiki na chanozo ni lazima, na ndiyo maana huwa kinatafutwa. Sasa usiulize swali la kijinga.

Moa ni necessary being, haihitaji kuwa na chanzo, bali yeye ni chanzo na kuuliza chanzo cha Mola ni ugonjwa wa akili.

Unakubali kuna infinity series ?
 
Hujaelewa hoja yangu, hoja yangu ilikuwa inajaribu ku challenge dhana yako ya self evident truth kupitia mfano wako ambao hauendani na kile kitu ulicho ki propose mwanzo

Ulisema mungu yupo kupitia kielelezo cha uwepo wa ulimwengu kua hiyo ni self evident truth

Halafu ukaja na mfano wa baba na mimi, kwamba sihitaji uthibitisho wa kujua baba ni mkubwa kwangu. Sasa huu mfano wako hauendani na hilo dai lako la kwanza, kwasababu mtoto na baba wote wapo na wanathibitishika, ukija katika hoja yako inaonesha ulimwengu upo na unathibitishika ila huyo mungu hayupo na unayaka kumthibitisha kupitia ulimwengu jambo ambalo ni uongo
Mfano wangu ni sahihi na una ukingano kwa kile nilichokipigia mfano.

Ndiyo maana nikakuuliza ya kuwa ulimwengu umejiumba au umetokea from nothing ? Hukujibi swali hili. Sasa uongo uko wapi na huku unashindwa kukosa ninacho kiandika.
 
Mawazo yangu katika huu ulimwengu yamejikita katika kuangalia uthibitisho ambao ni testable sio maoni ya kundi fulani walio share mitazamo yao
Hujajibu swali, usahihi wake unaujuaje.

Sasa tuelezee ithibati yako juu ya ulimwengu huu.
 
Tulikua wawili tumekaa sehemu moja tukapata ajali ya kukandamizwa na behewa lilojaa mizigo tani 50 lilipo tolewa behewa hilo mwanzangu alikufa hapohapo mimi nikapona kabisa hata alama wala dalili sina mpaka leo naishi.
Naomba unipe law of nature ilofanya mwenzangu afe mie nipone pasina kubakia hata na kilema au mkwarozo wowote?
So madai yako ni kua hilo tukio ni muujiza siyo?

Muujiza ni jambo ambalo mtu kahusika halafu kakosa maelezo sahihi kuelezea mechanism ya hilo jambo lilivyotokea. Mtu huishia kusema mungu ndio kafanya

Mtu ameugua kansa kwa akiwa katika hali mbaya huku matibabu akafanikiwa kupona. Record inaonesha watu 99% walioumwa kansa ya aina hiyo wote walikufa

je huo ni muujiza?

hapana nafikiri kuna sababu yenye mashiko yenye kuonesha kwanini mtu huyo apone wakati wenzake waliopata ugonjwa huo walikufa. Ila tukawa hatuna tecnolojia ya kubaini hilo kwa muda huu, haijalishi tuna technology ya kiasi gani kumbuka bado hatupo katika uwanja wa kujua kila kitu

Pengine miaka ya mbele jambo hilo likatafutiwa ufumbuzi kwanini mtu huyo ali survive ugonjwa ule kutokana na genes ndogo alizonazo ambazo ilikuwa ngumu kugundulika kwa vifaa vya kipindi hicho

So inawezekana kuna maelezo mazuri na sahihi kwenye mkasa wako uliokutokea kuonesha kwanini ulipona, lakini watu wengi tunaishi kimazoea kuita muujiza yale ambayo hatuyaelewi

Katika mapito ya maisha ya binadamu mambo mengi kwa miaka mingi yalikuwa yakitajwa kua ni miujiza mpaka pale sayansi ilipoanza kutafiti kujua kwanini vitu hivi vinatokea.

Kiukweli wigo wa kuhusisha Mungu katika vitu vinavyofanyika umezidi kupungua kuwa mdogo zaidi na zaidi. Watu walikuwa wakifikiri kua mvua na upepo ni miujiza inaletwa na mungu, lakini saizi tunaweza kuelezea process nzima kwanini mvua zina nyesha pamoja na kutabiri ni lini na saa ngapi mvua itanyesha bila kuhusisha Mungu wala muujiza

Miaka ya nyuma kuna jamii zilikuwa zikiamini radi ni ishara ya mungu kakasirika, lakini leo hii tunajua radi sio hasira za mungu ni kitu kingine tofauti kinachoelezeka bila mungu
 
Wanajamii,

Umofia kwenu.

Baada ya msiba wa mzee Magufuli, mwimbaji wa zamani wa mziki wa kizazi kipya maarufu kama Afande Sele/mkali wa rhymes alijitokeza na kutoa maneno mengi yaliyotafsiriwa kama kashfa au matusi kwa Mungu na watu wengi.

Msanii huyo mantiki yake ilionekana kudai Mungu ni dhana tu hayupo kama angekuwepo asingemuondoa Magufuli mapema kiasi hiki wakati bado anahitajika.

Hoja yangu ni kwamba, vipi kama ni kweli Afande Sele yupo Sahihi?

Kwanini...

Mosi, Dini nyingi sana. Haiwezekani Huyu Mungu anayempenda mwanadamu alete utitili wa dini halafu aweke masharti ya kwamba ukikosea unachomwa moto. Ni sawa na uwe mgonjwa uende kwa daktari halafu huyo dk amwage dawa zaidi ya 4000 mbele yako then akulazimishe kuchagua dawa moja sahihi, na adhabu pale tu utakapokosea.

Pili. Mwingiliano wa vitabu. Qur'an na Biblia kuna mwingiliano wa visa vinavyofanana, pamoja na wahusika. Mfano Mariamu, Issa(yesu) Musa, Ibrahim pamoja na wengine wengi. Hii sio kufanana kwa bahati nasibu tu ila kuna mmoja alinakili kutoka kwa mwenzake na/ kulingana na mazingira yanayofanana basi hivi ni visa vya kubuni ambavyo ilikuwa haiwezekani kuvikwepa, ni sawa na ngano za Kiafrika ambavyo huwezi kumkwepa mhusika "zimwi".

Eti, Mungu anajuwa yote (Omnipotence), kwanini hakugundua mapema kama shetani angeleta zogo kwa Adam na Hawa? Baada ya Ibilisi kupambana na majeshi ya Mungu akashindwa alitupwa duniani, then anamuumba mwanadamu anamweka duniani. Anaweza kumwacha mwanao unaemoenda alale chumba kimoja na chatu? Kwanini asingetuweka hata sayari ya Mars.

Mungu na shetani sio maadui.

Hii inajidhihirisha pale anapopiga stori na Shetani, mwanzoni kabisa mwa kitabu cha Ayubu.
"Shetani akiwa anatembea zake duniani akiwa anapunga upepo, alikutana na Mungu, Mungu akamuuliza ... Umenionea mtumishi wangu Ayubu...."

Kwa muktadha wa mazungumzo hayo, viumbe hawa hawawezi kuwa maadui.

Tano, kama Mungu anabusara asingeweza kumwacha shetani akae pamoja na mwanadamu.

Kumbuka shetani alikuwa malaika, ambaye licha ya uwezo wa jeshi tiifu la Mungu alifanikiwa kupambana nalo kwa muda mrefu, mwanadamu angewezaje kukaa na jeshi la Shetani sasa, au Mungu hakujua.

Mungu pia hufa kutokana na maendeleo ya wanadamu.

Wanadamu wamekuwa na miungu wengi sana ambao kulingana na wakati na maendeleo ya sayansi hao miungu hufa na kupotea, mfano ni NIKE Mungu wa vita, ATLAS mungu aliyeshikilia/beba mabegani dunia hewani isiporomoke, VULCA, mungu wa moto na hasira aliyekuwa akikasirika hufuka moto toka ardhini. (Ambaye kwaye tumepata neno Volcano)

Je, unahakika huyu Mungu unayemwamini sasa hatakufa kutokana na wakati?

UNA UHAKIKA?
Mwanangu hapa una hoja hata kama wakikushambulia wale mbumbumbu walioharibiwa na dhana hii usijali we kaza buti. Watakaokusakama wambie wamuachia aliyekashfiwa au wamtafutie wakili akafungue kesi mahakamani ambapo tutamtaka mteja wake kujitokeza ili tujue yupo au la.
 
Ndiyo maana naipenda sana biblia. Ilijua kuna watu hawamwamini Mungu. Kwa hiyo yawaita wapumbavu [emoji23][emoji23][emoji23]

“Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.” Zaburi 14:1

“Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza, Hakuna atendaye mema.” Zaburi 53:1
Bado hyo ni maneno ya kuambiw weka ushahid wako ktk maisha ya kawaida
 
Back
Top Bottom