Yawezekana Afande Sele yupo Sahihi?

Yawezekana Afande Sele yupo Sahihi?

Sasa migomba inatofauti gani na hili dubwasha hapa ambalo makanisani limewekwa?

View attachment 1744091

Mtu kabisa na akili zako timamu utamuona afande sele ni mjinga kwa kuabudu migomba na bangi halafu huyu anayepigia magoti hilo lizege la mifuko miwili ya cement mixer concrete awe na akili timamu?

Angalia kundi lingine hili zaidi ya maelfu ya watu hapa wameinama kulisujudia lakini unakuta watu hawa nao wanaungana kuponda migomba ya afande sele

View attachment 1744092

Tuwe serious sometimes hata kama tupo kipindi cha april fools
Scars usiniharibie siku,Wewe unaita dubwasha???,Aisee ungekuwa karibu ningekutukia nikaishughulikia shingo yako hiyo Hadi Dunia ilivyo chungu na nisingeiachia haki ya nani, hata Sasa nikijua ulipo na kufuata nikutafune mzima mzima.
 
Wanajamii,

Umofia kwenu.

Baada ya msiba wa mzee Magufuli, mwimbaji wa zamani wa mziki wa kizazi kipya maarufu kama Afande Sele/mkali wa rhymes alijitokeza na kutoa maneno mengi yaliyotafsiriwa kama kashfa au matusi kwa Mungu na watu wengi.

Msanii huyo mantiki yake ilionekana kudai Mungu ni dhana tu hayupo kama angekuwepo asingemuondoa Magufuli mapema kiasi hiki wakati bado anahitajika.

Hoja yangu ni kwamba, vipi kama ni kweli Afande Sele yupo Sahihi?

Kwanini...

Mosi, Dini nyingi sana. Haiwezekani Huyu Mungu anayempenda mwanadamu alete utitili wa dini halafu aweke masharti ya kwamba ukikosea unachomwa moto. Ni sawa na uwe mgonjwa uende kwa daktari halafu huyo dk amwage dawa zaidi ya 4000 mbele yako then akulazimishe kuchagua dawa moja sahihi, na adhabu pale tu utakapokosea.

Pili. Mwingiliano wa vitabu. Qur'an na Biblia kuna mwingiliano wa visa vinavyofanana, pamoja na wahusika. Mfano Mariamu, Issa(yesu) Musa, Ibrahim pamoja na wengine wengi. Hii sio kufanana kwa bahati nasibu tu ila kuna mmoja alinakili kutoka kwa mwenzake na/ kulingana na mazingira yanayofanana basi hivi ni visa vya kubuni ambavyo ilikuwa haiwezekani kuvikwepa, ni sawa na ngano za Kiafrika ambavyo huwezi kumkwepa mhusika "zimwi".

Eti, Mungu anajuwa yote (Omnipotence), kwanini hakugundua mapema kama shetani angeleta zogo kwa Adam na Hawa? Baada ya Ibilisi kupambana na majeshi ya Mungu akashindwa alitupwa duniani, then anamuumba mwanadamu anamweka duniani. Anaweza kumwacha mwanao unaemoenda alale chumba kimoja na chatu? Kwanini asingetuweka hata sayari ya Mars.

Mungu na shetani sio maadui.

Hii inajidhihirisha pale anapopiga stori na Shetani, mwanzoni kabisa mwa kitabu cha Ayubu.
"Shetani akiwa anatembea zake duniani akiwa anapunga upepo, alikutana na Mungu, Mungu akamuuliza ... Umenionea mtumishi wangu Ayubu...."

Kwa muktadha wa mazungumzo hayo, viumbe hawa hawawezi kuwa maadui.

Tano, kama Mungu anabusara asingeweza kumwacha shetani akae pamoja na mwanadamu.

Kumbuka shetani alikuwa malaika, ambaye licha ya uwezo wa jeshi tiifu la Mungu alifanikiwa kupambana nalo kwa muda mrefu, mwanadamu angewezaje kukaa na jeshi la Shetani sasa, au Mungu hakujua.

Mungu pia hufa kutokana na maendeleo ya wanadamu.

Wanadamu wamekuwa na miungu wengi sana ambao kulingana na wakati na maendeleo ya sayansi hao miungu hufa na kupotea, mfano ni NIKE Mungu wa vita, ATLAS mungu aliyeshikilia/beba mabegani dunia hewani isiporomoke, VULCA, mungu wa moto na hasira aliyekuwa akikasirika hufuka moto toka ardhini. (Ambaye kwaye tumepata neno Volcano)

Je, unahakika huyu Mungu unayemwamini sasa hatakufa kutokana na wakati?

UNA UHAKIKA?
Zaburi 14:1
Mpumbavu husema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.
 
Afande alitakiwa kujenga hoja sio kutukana kama alivyofanya
 
Scars usiniharibie siku,Wewe unaita dubwasha???,Aisee ungekuwa karibu ningekutukia nikaishughulikia shingo yako hiyo Hadi Dunia ilivyo chungu na nisingeiachia haki ya nani, hata Sasa nikijua ulipo na kufuata nikutafune mzima mzima.
Piga dua allah akupe ip adress yangu ujue nilipo
 
Hapo linasujudiwa nini ? Hivi mpaka lini akili zenu mtazichukua toka kwa wale walio washikia, tena wajinga wakubwa.
unazungumzia picha ya kwanza au ya pili?
 
Hivi kwanini hujishangai wewe ambaye unasema Mola hayupo wakati humjui wala huna ushahidi wa hili ? Huu ni ujinga ulioje ? Wewe ni sawa na yule ambaye anasema "Mimi sina elimu lakini hunidanganyi chochote" ? Aisee wewe wakupigwa makofi.
Unajikanganya

Dhana ya kuwapo mungu ni idea ya kufikirika tu, na ndio maana hata wewe unayejipambanua unamjua huwezi kuthibitisha yupo

Unaweza? Thibitisha
 
Mwanafunzi mwingine wa Kiranga.

Afande kasema anaabudu migomba yake au bangi zake.

Sasa huyo mtu nzima kweli?
Ni mzima, that's y tuna Uhuru wa kuabudu. Huwezi amini dini yako ni sahihi na ya mwenzako sio sahihi.
 
Sasa migomba inatofauti gani na hili dubwasha hapa ambalo makanisani limewekwa?

View attachment 1744091

Mtu kabisa na akili zako timamu utamuona afande sele ni mjinga kwa kuabudu migomba na bangi halafu huyu anayepigia magoti hilo lizege la mifuko miwili ya cement mixer concrete awe na akili timamu?

Angalia kundi lingine hili zaidi ya maelfu ya watu hapa wameinama kulisujudia lakini unakuta watu hawa nao wanaungana kuponda migomba ya afande sele

View attachment 1744092

Tuwe serious sometimes hata kama tupo kipindi cha april fools
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] aisee we mtu umenifanya nimecheka sana
 
Unajikanganya

Dhana ya kuwapo mungu ni idea ya kufikirika tu, na ndio maana hata wewe unayejipambanua unamjua huwezi kuthibitisha yupo

Unaweza? Thibitisha
Sasa wewe si mpagani uthibitisho wa nn wakati huamini katika MUNGU?

Kwangu mm Uthibitisho kuwa MUNGU yupo ni uwepo wa ulimwengu na viumbe hai maana sijawahi ona vitu vinatokea from no where lazima viundwe.
Sasa wewe thibitisha kuwa hayupo.

HIVI HATUWEZI KUKUBALIANA NA HALI?

WEWE PAGANI UACHWE NA ANAYEAMINI MUNGU AACHWE.

KILA MTU APAMBANE NA HALI YAKE, KILA MTU NA ALE ALIPOLEKA MBOGA.
 
Swali langu kwanini unaaminishwa kuwa mungu yupo kwa lugha sio yako
na maombi na dua zako zitakubaliwa tu ukiziomba kwa lugha ngeni ya kiarabu
kwanini usisali na kuomba kwa lugha yako tu na sio kwa kiarabu
Mpaka najiuliza inakuwaja mna hoja dhaifu namna hii kushinda hata nyumba za bui bui. Lugha ngeni siyo kikwazo wala si tatizo, ndiyo maana unakuta katika wanazuoni wakubwa mno wa ugha ya kiarabu kiasili si Waarabu. Hii hoja dhaifu sana, sababu Mola wetu ametupa uwezo wa kujifunza mambo na tukayaelewa kwa lugha yoyote ile.

Kuhusu maombi si kweli, lugha ya kiarabu inatumika tu katika sala, ila katika kuomba dua nje ya Sala, unatumia lugja yoyote sababu Allah anazijua lugha zote hizo, na yeyw ndiyo amejaalia ziwe. Huu ni utaratibu kama zilivyo taratibu taratibu nyingine, na angetaka sote tutumie lugha ya Kiarabu bila kujifunza hilo kwake dogo sana.
 
Huoni wanakushika akili uwaone wao bora zaidi kwa huyo mungu ila ukiomba kwa lugha yao
Labda mungu yupo, lakini utafute kwa fahamu zako na si hadithi za kusimuliwa kwenye vitabu vya wageni ambao hata ujio wao kwenu ulikuwa wa maovu ya kuwatumia kama watumwa wa kuwafanya kuwa sio binadmu kamili mwenye fahamu yake.
Mjifunze kujenga hoja na msiwasemee watu kwa mambo ambayo hamna elimu nayo. Hakuna cha maana ulichokiandika katika hili.
 
Unajikanganya

Dhana ya kuwapo mungu ni idea ya kufikirika tu, na ndio maana hata wewe unayejipambanua unamjua huwezi kuthibitisha yupo

Unaweza? Thibitisha
Kwanza kabisa naomba uonyeshe wapi nilipojichanganya,ukiwaza naacha kujadiliana juu mambo haya.

Sijawahi kushindwa kuthibitisha hili, na nimeshalithibitisha zaidi ya mara moja humu, ila kwa masikitiko makubwa ni kwenu ambao mnadai Mola hayupo na huku hamuwezi kuthibitisha hilo.

Ithibati ya kwanza ni "self evident truth". Ithibati ya nyingine ni "Contingent fact". Uwepo wa ulimwengu na vyote vilivyomo huthibitisha uwepo wa Mola sababu vyote hivyo haviwezi kutoa pasi na chochote au kujiumba vyenyewe.
 
Sasa wewe si mpagani uthibitisho wa nn wakati huamini katika MUNGU?

Kwangu mm Uthibitisho kuwa MUNGU yupo ni uwepo wa ulimwengu na viumbe hai maana sijawahi ona vitu vinatokea from no where lazima viundwe.
Sasa wewe thibitisha kuwa hayupo.

HIVI HATUWEZI KUKUBALIANA NA HALI?

WEWE PAGANI UACHWE NA ANAYEAMINI MUNGU AACHWE.

KILA MTU APAMBANE NA HALI YAKE, KILA MTU NA ALE ALIPOLEKA MBOGA.
Mi sio mpagani, mpagani ni yule anayeabudu miungu tofauti na dini za abraham

Kusema uwepo wa ulimwengu ndio uthibitisho wa uwepo wa mungu hiyo ni fallacy na hilo ni dai ambalo linahitaji uthibitisho.

Kuna maswali mengi yanaibuka

1. Kuna idadi zaidi ya 5000 ya Mungu inayoabudiwa na watu duniani na kila dini imemtaja Mungu wake kwamba ndio muumbaji wa ulimwengu.

Unahakika gani kua mungu wako ndo muumbaji wa ulimwengu na sio Mungu wa dini nyingine tofauti na yako?

2. Umesema hujawahi ona vitu vinatoka from nowhere (na huu ndio msingi wako wa swali), so unakubali kwamba hata huyo Mungu naye kuna chanzo chake kilichomfanya awepo?

Kama Mungu wako hatahitaji chanzo basi mpaka hapo tutajua kua chanzo si muhimu ili kingine kiwepo. Kwa fact hiyo tusingeweza hata kuhoji chanzo cha ulimwengu ambao upo na unathibitishika kwa kutafuta majibu ya kufikirika (Mungu) kuwa ndio chanzo. Wote tungejua ulimwengu hauna chanzo na hivyo nafasi ya Mungu ni useless

Umeniambia nithibitishe Mungu hayupo

Kiukweli mimi siwezi kuthibitisha Mungu yupo. Ila nataka nijue ni Mungu gani kati ya hao 5000 ambaye wewe unamuabudu

Nikishajua Mungu wako unayemuabudu kati ya hao nitataka unithibitishie hao 4,999 kua hawapo halafu nitatumia njia hizo hizo kukuthibitishia Mungu wako hayupo
 
Umeninukuu katika post yenye picha mbili
Kijana mbona una kichwa kigumu mno ? Kuna picha mbili hapo,moja ni mdau amepiga magoti nyingine watu wanasujudu, na mimi nimeongelea kuhusu kusujudu, wewe unauliza tena mambo ya picha mbili. Kwa uzembe huu lazima uone ya kuwa Mola hayupo.
 
Afande Sele katusababishia mtufiano mkubwa sana.

Ramadhani inakaribia ni lini (kwa mujibu wa Shehe) atakufa ili mtifuano Huu uishe.
 
Sasa wewe si mpagani uthibitisho wa nn wakati huamini katika MUNGU?

Kwangu mm Uthibitisho kuwa MUNGU yupo ni uwepo wa ulimwengu na viumbe hai maana sijawahi ona vitu vinatokea from no where lazima viundwe.
Sasa wewe thibitisha kuwa hayupo.

HIVI HATUWEZI KUKUBALIANA NA HALI?

WEWE PAGANI UACHWE NA ANAYEAMINI MUNGU AACHWE.

KILA MTU APAMBANE NA HALI YAKE, KILA MTU NA ALE ALIPOLEKA MBOGA.

Hujawahi ona vitu vinatokea from nowhere lazima viundwe.
Mungu ameumbwa na nani?
 
Back
Top Bottom