Yawezekana Afande Sele yupo Sahihi?

Yawezekana Afande Sele yupo Sahihi?

Hapa ofisini napofanyia kazi huwa wananiona mwehu! I can't comprehend how people are so narrow minded.

Eti Joshua akasimamisha [emoji3508] jua.!
Nuhu akampakia Arctic bear [emoji199] kwenye Safina huku jangwani middle East [emoji3591].[emoji51][emoji51][emoji51][emoji51]
We know the biblical floods never occurred, kwasababu kulikuwa na watu waliokuwa wakiishi katika hicho kipindi

Watu hao walitunza records hawakutaka kukubsli upotofu kuwa they were all wiped from the face of the earth

Kipindi cha nuhu harakati za kimaisha zilikuwa zikiendelea Wachina walitunza records kupitia "Neolitic Dynasty"

Wa misri waliandika "DYNASTIES 4,5,&6" hizo ni record za kipindi hicho ambacho inasemekana gharika lilitokea lakini hakuna record ambayo iliwekwa kuonesha kuna gharika

Jamhuri ya peru nayo imetunza record katika hicho kipindi kinachodaiwa "NORTE CHICO CIVILIZATION"

Hizo references zinaonesha continous line of culture, contruction, art na record zote za kihistoria zilizofanyika katika hicho kipindi cha noah
 
Kitu cha kwanza kabisa katika mjadala wa kutaka kujua zaidi kuhusu Mungu ni kumtafuta mtu ambaye ana hamu ya kujua zaidi kuhusu Mungu...watu wa aina hii wapo zaidi open minded, na watu ambao wapo open minded ni watu wanaopenda kujisomea wao wenyewe ili kufahamu...si mtu wa kuambiwa kitu halafu akaenda kumtapikia mwingine kuwa ndio ukweli kamili...ukichunguza kwa makini maswali ya mtoa mada unaeza pata majibu mawili ya haraka...labda hakuna Mungu au Mungu yupo ila ni tofauti kabisa na tunavyomfahamu...
 
Hapo halisujudiwi hilo jengo mzee!!
Soma dini kwanza uelewe sababu sio kuropoka tu,, utakuja kuchekwa siku nyingine!!
Ungemwelewesha sasa ili asichekwe! Kuliko kumuacha hivo bila uelewa!
 
Wanajamii,

Umofia kwenu.

Baada ya msiba wa mzee Magufuli, mwimbaji wa zamani wa mziki wa kizazi kipya maarufu kama Afande Sele/mkali wa rhymes alijitokeza na kutoa maneno mengi yaliyotafsiriwa kama kashfa au matusi kwa Mungu na watu wengi.

Msanii huyo mantiki yake ilionekana kudai Mungu ni dhana tu hayupo kama angekuwepo asingemuondoa Magufuli mapema kiasi hiki wakati bado anahitajika.

Hoja yangu ni kwamba, vipi kama ni kweli Afande Sele yupo Sahihi?

Kwanini...

Mosi, Dini nyingi sana. Haiwezekani Huyu Mungu anayempenda mwanadamu alete utitili wa dini halafu aweke masharti ya kwamba ukikosea unachomwa moto. Ni sawa na uwe mgonjwa uende kwa daktari halafu huyo dk amwage dawa zaidi ya 4000 mbele yako then akulazimishe kuchagua dawa moja sahihi, na adhabu pale tu utakapokosea.

Pili. Mwingiliano wa vitabu. Qur'an na Biblia kuna mwingiliano wa visa vinavyofanana, pamoja na wahusika. Mfano Mariamu, Issa(yesu) Musa, Ibrahim pamoja na wengine wengi. Hii sio kufanana kwa bahati nasibu tu ila kuna mmoja alinakili kutoka kwa mwenzake na/ kulingana na mazingira yanayofanana basi hivi ni visa vya kubuni ambavyo ilikuwa haiwezekani kuvikwepa, ni sawa na ngano za Kiafrika ambavyo huwezi kumkwepa mhusika "zimwi".

Eti, Mungu anajuwa yote (Omnipotence), kwanini hakugundua mapema kama shetani angeleta zogo kwa Adam na Hawa? Baada ya Ibilisi kupambana na majeshi ya Mungu akashindwa alitupwa duniani, then anamuumba mwanadamu anamweka duniani. Anaweza kumwacha mwanao unaemoenda alale chumba kimoja na chatu? Kwanini asingetuweka hata sayari ya Mars.

Mungu na shetani sio maadui.

Hii inajidhihirisha pale anapopiga stori na Shetani, mwanzoni kabisa mwa kitabu cha Ayubu.
"Shetani akiwa anatembea zake duniani akiwa anapunga upepo, alikutana na Mungu, Mungu akamuuliza ... Umenionea mtumishi wangu Ayubu...."

Kwa muktadha wa mazungumzo hayo, viumbe hawa hawawezi kuwa maadui.

Tano, kama Mungu anabusara asingeweza kumwacha shetani akae pamoja na mwanadamu.

Kumbuka shetani alikuwa malaika, ambaye licha ya uwezo wa jeshi tiifu la Mungu alifanikiwa kupambana nalo kwa muda mrefu, mwanadamu angewezaje kukaa na jeshi la Shetani sasa, au Mungu hakujua.

Mungu pia hufa kutokana na maendeleo ya wanadamu.

Wanadamu wamekuwa na miungu wengi sana ambao kulingana na wakati na maendeleo ya sayansi hao miungu hufa na kupotea, mfano ni NIKE Mungu wa vita, ATLAS mungu aliyeshikilia/beba mabegani dunia hewani isiporomoke, VULCA, mungu wa moto na hasira aliyekuwa akikasirika hufuka moto toka ardhini. (Ambaye kwaye tumepata neno Volcano)

Je, unahakika huyu Mungu unayemwamini sasa hatakufa kutokana na wakati?

UNA UHAKIKA?
ninaomba nirudie kusoma hili andiko tena na tena
 
Back
Top Bottom