Yawezekana Afande Sele yupo Sahihi?

Yawezekana Afande Sele yupo Sahihi?

Huwezi ukasema Mungu hayupo wakat haumjui.Nisawasawa na umekutana na mtu kwenye sherehe,alaf unamuuliza umemwona Joseph ukumbini?anakujibu sijamwona,unamuuliza unamjua lakin? Anakujibu cmjui.unabaki kushangaa sasa amejuaje Kama Joseph hayupo ukumbini wakat hamjui.Vivohivyo hatuwezi kusema Mungu hayupo wakat hatumjui
basi ndivyo hivyo hivyo hatuwezi kusema yupo wakati hatumjui.
 
Wanajamii,

Umofia kwenu.

Baada ya msiba wa mzee Magufuli, mwimbaji wa zamani wa mziki wa kizazi kipya maarufu kama Afande Sele/mkali wa rhymes alijitokeza na kutoa maneno mengi yaliyotafsiriwa kama kashfa au matusi kwa Mungu na watu wengi.

Msanii huyo mantiki yake ilionekana kudai Mungu ni dhana tu hayupo kama angekuwepo asingemuondoa Magufuli mapema kiasi hiki wakati bado anahitajika.

Hoja yangu ni kwamba, vipi kama ni kweli Afande Sele yupo Sahihi?

Kwanini...

Mosi, Dini nyingi sana. Haiwezekani Huyu Mungu anayempenda mwanadamu alete utitili wa dini halafu aweke masharti ya kwamba ukikosea unachomwa moto. Ni sawa na uwe mgonjwa uende kwa daktari halafu huyo dk amwage dawa zaidi ya 4000 mbele yako then akulazimishe kuchagua dawa moja sahihi, na adhabu pale tu utakapokosea.

Pili. Mwingiliano wa vitabu. Qur'an na Biblia kuna mwingiliano wa visa vinavyofanana, pamoja na wahusika. Mfano Mariamu, Issa(yesu) Musa, Ibrahim pamoja na wengine wengi. Hii sio kufanana kwa bahati nasibu tu ila kuna mmoja alinakili kutoka kwa mwenzake na/ kulingana na mazingira yanayofanana basi hivi ni visa vya kubuni ambavyo ilikuwa haiwezekani kuvikwepa, ni sawa na ngano za Kiafrika ambavyo huwezi kumkwepa mhusika "zimwi".

Eti, Mungu anajuwa yote (Omnipotence), kwanini hakugundua mapema kama shetani angeleta zogo kwa Adam na Hawa? Baada ya Ibilisi kupambana na majeshi ya Mungu akashindwa alitupwa duniani, then anamuumba mwanadamu anamweka duniani. Anaweza kumwacha mwanao unaemoenda alale chumba kimoja na chatu? Kwanini asingetuweka hata sayari ya Mars.

Mungu na shetani sio maadui.

Hii inajidhihirisha pale anapopiga stori na Shetani, mwanzoni kabisa mwa kitabu cha Ayubu.
"Shetani akiwa anatembea zake duniani akiwa anapunga upepo, alikutana na Mungu, Mungu akamuuliza ... Umenionea mtumishi wangu Ayubu...."

Kwa muktadha wa mazungumzo hayo, viumbe hawa hawawezi kuwa maadui.

Tano, kama Mungu anabusara asingeweza kumwacha shetani akae pamoja na mwanadamu.

Kumbuka shetani alikuwa malaika, ambaye licha ya uwezo wa jeshi tiifu la Mungu alifanikiwa kupambana nalo kwa muda mrefu, mwanadamu angewezaje kukaa na jeshi la Shetani sasa, au Mungu hakujua.

Mungu pia hufa kutokana na maendeleo ya wanadamu.

Wanadamu wamekuwa na miungu wengi sana ambao kulingana na wakati na maendeleo ya sayansi hao miungu hufa na kupotea, mfano ni NIKE Mungu wa vita, ATLAS mungu aliyeshikilia/beba mabegani dunia hewani isiporomoke, VULCA, mungu wa moto na hasira aliyekuwa akikasirika hufuka moto toka ardhini. (Ambaye kwaye tumepata neno Volcano)

Je, unahakika huyu Mungu unayemwamini sasa hatakufa kutokana na wakati?

UNA UHAKIKA?
Mnajua jamani Bangi sio nzuri, sasa kama afande sele huyo mungu anayemuabudi anadai ana nguvu,ameshindwaje kumuomba huyo mungu wake ili amuamshe mheshimiwa.
 
Mtoa mada huenda akielimishwa akaelewa vizur tu.chukua huu mfano.

Mwalimu wako wa shule kwann anatoa mitihani ili kuwapima???!! Kwann asiwaache tu muende darasa lingine kwa kuwa wote ni wanafunzi wake????? Tafakari chukua hatua

Mungu ni mmoja tu ambae ni Allah peke yake hao miungu wengine ni miungo waliotengenezwa na fikra za binadamu baada ya kuconect dot.
 
Huwezi ukasema Mungu hayupo wakat haumjui.Nisawasawa na umekutana na mtu kwenye sherehe,alaf unamuuliza umemwona Joseph ukumbini?anakujibu sijamwona,unamuuliza unamjua lakin? Anakujibu cmjui.unabaki kushangaa sasa amejuaje Kama Joseph hayupo ukumbini wakat hamjui.Vivohivyo hatuwezi kusema Mungu hayupo wakat hatumjui
Mfano wako utaleta maana kama utataja sifa za huyo Joseph ili unayemuuliza apate kujua katika watu waliohudhuria hiyo shughuli kuna yeyote ambaye ana sifa kama za Joseph.???

Akipata mtu mwenye sifa za Joseph atakujibu yupo au hayupo kulingana na sifa ulizoziainisha..

Tukirejea katika suala la Mungu ambaye hayupo ni huyu ambaye amepewa sifa ambazo zinajipinga zenyewe kimantiki kulingana na maandiko yake ndo maana baadhi yetu tunapata mashaka inawezekana akawa hayupo Mungu wa sifa hizo zinazotajwa katika maandiko...
 
Mtoa post unajiamini nini?vitu vingine havihitaji uchambuzi unaweza ukajikuta ghafla umeumaliza mwendo....tutakukumbuka ujue ....
 
Mosi, Dini nyingi sana. Haiwezekani Huyu Mungu anayempenda mwanadamu alete utitili wa dini halafu aweke masharti ya kwamba ukikosea unachomwa moto. Ni sawa na uwe mgonjwa uende kwa daktari halafu huyo dk amwage dawa zaidi ya 4000 mbele yako then akulazimishe kuchagua dawa moja sahihi, na adhabu pale tu utakapokosea
Katika dini yangu ya Uislamu, nina amini ya kuwa tutakuja kuulizwa juu ya neema ambazo Allah aliye juu ametupa,kisha Allah akasema katika Qur'aan ya kuwa kama tukitaka kuhesabu neema alizo tujaalia katu hatuwezi kudhibiti idadi yake. Miongoni mwa neema hizo ni neema ua akili.Sitaki nikuelezee ya kuwa Akili ni nini, bali nataka nikuonyeshe ni namna gani nzuri ya kuitumia neema ya akili uliyopewa.

Mwanadamu alipoumbwa aliachwa awe huru (hapa napo kama msingepewa uhuru napo mngelia lia) . Mola aliporuhusu kuwepo kwa dini nyingi akatuonyesha dini ipi sahihi na ipi si sahihi, maana yake ukienda kinyume ujue umetaka wewe.

Mfani ulio utoa ni mfano wa uongo sababu ulicho kitolea mfano hakikingani kabisa na desturi ya Allah mtukufu, yaani umemzulia uongo, na inaonekana wazi humjui Mola wetu, lakini ajabu unamzungumzia, huu ujinga huwa nauona sana humu jf. Hali yetu sisi kwa Mola wetu si sawa na hali ya daktari na mgonjwa, kwa munasaba wa mfano wako.
 
. Mwingiliano wa vitabu. Qur'an na Biblia kuna mwingiliano wa visa vinavyofanana, pamoja na wahusika. Mfano Mariamu, Issa(yesu) Musa, Ibrahim pamoja na wengine wengi. Hii sio kufanana kwa bahati nasibu tu ila kuna mmoja alinakili kutoka kwa mwenzake na/ kulingana na mazingira yanayofanana basi hivi ni visa vya kubuni ambavyo ilikuwa haiwezekani kuvikwepa, ni sawa na ngano za Kiafrika ambavyo huwezi kumkwepa mhusika "zimwi".
Wakubwa zenu walipowahimiza kuhoji, walisahau kuwapa hii tahadhari ya kuwa "ukihoji,hoji vya maana na usihoji upumbavu". Ulichokiandika hapa ni mtazamo wako, tena uliojengeka katika ujinga uliopea kabisa.

Lazima kuwe na mfanano sababu ya asili ya maandiko hayo yanatoka katika chanzo kimoja, yaani kwa Mola muumba. Desturi ya Mola kwa mitume wake na manabii, huwa anawafunulia habari za mitume waliopita kwa lengo la kuwaliwaza waja wake hao, au kuwafunza jambo.

Sababu wewe ni mjinga, mimi nakupa kazi moja japokuwa maoni yako yamejengeka katika dhana, naomba utupe ushahidi wa nani amenakili toka kwa nani na ilikuwaje ?

Lakini jalia kwamba kuna fulani amenakili toka kwa fulani, je shida iko wapi wakati vyote hivyo vinatoka kwa mmoja ?
 
, Mungu anajuwa yote (Omnipotence), kwanini hakugundua mapema kama shetani angeleta zogo kwa Adam na Hawa? Baada ya Ibilisi kupambana na majeshi ya Mungu akashindwa alitupwa duniani, then anamuumba mwanadamu anamweka duniani. Anaweza kumwacha mwanao unaemoenda alale chumba kimoja na chatu? Kwanini asingetuweka hata sayari ya Mar
Hivi kwanini hizi habari hamzisomi kiundani na mkazijua, ili muepukane na kukosea kosea ? Lakini kama ungekisoka kisa cha Ibilisi katika vyanzo vya uhakika na visivyo kuwa na shaka, usingeandika huu ujinga. Mola wetu anajua kila kitu, ila kujua kwake hakukuzuii wewe usifanye unalo taka, sababu alisharuhusu uhuru, na huwezi kuta utaratibu wa Mola wetu muumba ni wenye kubadilika, Mola wetu hayumbi mzee. Kisa cha Adamu na Ibilisi kiko wazi sana, Adamu alipopewa ruhusa ya kuingia katika bustani hakuachwa hivi hivi, bali alipewa na tahadhari, sababu uwezo wa kuiepuka tahadhari hiyo alikuwa nayo, ila shetani akifanikiwa kumshawishi na akaingia katika makosa, ila mwisho wake Adamu alijutia kosa na kuomba toba kwa Mola wake, na Allah akamsamehe, sababu Mola wetu ni mwingi wa kusamehe.

Kingine, wapi Ibilisi alipambana na majeshi ya Mungu ? Hivi hizi hanari huwa mnazipata wapi au nyinyi ndiyo mnazitunga nini ? Maana katika vitabu vya imani zetu hasa katika Uislamu hamna hanari hizi.

Kadhalika, huwa nawaambia kila siku mnatatizo kubwa sana la kulinganisha mambo, yaani unalinganisha suala la mtoto na chatu, kwa Adamu na nyoka, huku hujatuambia mfanano uko wapi mpaka unalinganisha, maana mtoto hana uwezo wa kung'amua mambo,Adamu alikuwa mtu mzima na alipewa tahadhari na uwezo wa kushinda ule mtihani alikuwa nao, ila kwa hiari yake akakubali kushawishiwa, sasa mtoto anakuwa vipi na uwezo wa kumshinda chatu ? Je tahadhari gani una mpa mtoto huyo, sasa vipimo gani huwa mnatumia kutoa mifano mfu kama hii ?
 
Mungu na shetani sio maadui.

Hii inajidhihirisha pale anapopiga stori na Shetani, mwanzoni kabisa mwa kitabu cha Ayubu.
"Shetani akiwa anatembea zake duniani akiwa anapunga upepo, alikutana na Mungu, Mungu akamuuliza ... Umenionea mtumishi wangu Ayubu...."
Kijana unaandika ujinga mpaka napata uzito wa kukujibu, ila ngoja nikuonyeshe ujinga wako ulipo.

Shetani ni adui wa mwannadamu na amelaaniwa na Allah. Shetani ni katika majini, ambaye hapo kabla alikuwa mja mwema mwenye kusujudu sana, akaitwa Aba Saajida. Lakini hapo hapo umekiri kabisa ya kiwa hapo mwanzo walikuwa wana piga stori, ila ungekuwa mtu makini na mwenye akili timamu, ulitakiwa ujiulize kipi kimepelekea huo uadui kuwepo ? Jibu ni kuwa Shetani alifanya kiburi kwa Mola wake, na kujiona yeye ni bora kuliko Adamu.
 
Unachokifanya ni "Ad hominem Argumentum " unanishambulia kwa kuangalia akili yangu badala ushambulie hoja niliyoweka.
Hapa ndipo utakapo ona udhaifu wa "logic". Inaonekana hujui maana ya akili, sasa unaitenganisha vipi akili yako na unachokiandika ? Ukiona akili yako imeshindwa kufanya kazi yake vizuri ya kuzuia wewe usikosee katika kuhoji,basi ya kutazamwa hapo ni wewe na akili yako, hakuna Ad Hominem hapo.
 
Tukirejea katika suala la Mungu ambaye hayupo ni huyu ambaye amepewa sifa ambazo zinajipinga zenyewe kimantiki kulingana na maandiko yake ndo maana baadhi yetu tunapata mashaka inawezekana akawa hayupo Mungu wa sifa hizo zinazotajwa katika maandiko...
Nitajie sifa tatu ambazo zinajipinga kimantiki.

Kisha unahikikishie ya kuwa mantiki hukidhi vigezo vya kuujua ukweli kama ulivyo, mpaka wewe ukaufanya huo kuwa kama mzani wa kufiki hitimisho la jambo lako.

Unakubali kama Akili ina ukomo, kama jicho lilivyo na ukomo wake wa kuona ? Nasema hivi au nauliza hivi sababu msingi wa mantiki umemili katika kuifanua akili kama ndiyo kila kitu katika kuhitimisha mambo.

Ila vijana huwa mnachekesha sana, yaani mnahoji mambo juu juu na kitoto mno.
 
Angalia kundi lingine hili zaidi ya maelfu ya watu hapa wameinama kulisujudia lakini unakuta watu hawa nao wanaungana kuponda migomba ya afande sele

1617621361175.png
Hapo linasujudiwa nini ? Hivi mpaka lini akili zenu mtazichukua toka kwa wale walio washikia, tena wajinga wakubwa.
 
Sasa migomba inatofauti gani na hili dubwasha hapa ambalo makanisani limewekwa?

View attachment 1744091

Mtu kabisa na akili zako timamu utamuona afande sele ni mjinga kwa kuabudu migomba na bangi halafu huyu anayepigia magoti hilo lizege la mifuko miwili ya cement mixer concrete awe na akili timamu?

Angalia kundi lingine hili zaidi ya maelfu ya watu hapa wameinama kulisujudia lakini unakuta watu hawa nao wanaungana kuponda migomba ya afande sele

View attachment 1744092

Tuwe serious sometimes hata kama tupo kipindi cha april fools
Hivi kwanini hujishangai wewe ambaye unasema Mola hayupo wakati humjui wala huna ushahidi wa hili ? Huu ni ujinga ulioje ? Wewe ni sawa na yule ambaye anasema "Mimi sina elimu lakini hunidanganyi chochote" ? Aisee wewe wakupigwa makofi.
 
Katika dini yangu ya Uislamu, nina amini ya kuwa tutakuja kuulizwa juu ya neema ambazo Allah aliye juu ametupa,kisha Allah akasema katika Qur'aan ya kuwa kama tukitaka kuhesabu neema alizo tujaalia katu hatuwezi kudhibiti idadi yake. Miongoni mwa neema hizo ni neema ua akili.Sitaki nikuelezee ya kuwa Akili ni nini, bali nataka nikuonyeshe ni namna gani nzuri ya kuitumia neema ya akili uliyopewa.

Mwanadamu alipoumbwa aliachwa awe huru (hapa napo kama msingepewa uhuru napo mngelia lia) . Mola aliporuhusu kuwepo kwa dini nyingi akatuonyesha dini ipi sahihi na ipi si sahihi, maana yake ukienda kinyume ujue umetaka wewe.

Mfani ulio utoa ni mfano wa uongo sababu ulicho kitolea mfano hakikingani kabisa na desturi ya Allah mtukufu, yaani umemzulia uongo, na inaonekana wazi humjui Mola wetu, lakini ajabu unamzungumzia, huu ujinga huwa nauona sana humu jf. Hali yetu sisi kwa Mola wetu si sawa na hali ya daktari na mgonjwa, kwa munasaba wa mfano wako.
Swali langu kwanini unaaminishwa kuwa mungu yupo kwa lugha sio yako
na maombi na dua zako zitakubaliwa tu ukiziomba kwa lugha ngeni ya kiarabu
kwanini usisali na kuomba kwa lugha yako tu na sio kwa kiarabu

Huoni wanakushika akili uwaone wao bora zaidi kwa huyo mungu ila ukiomba kwa lugha yao
Labda mungu yupo, lakini utafute kwa fahamu zako na si hadithi za kusimuliwa kwenye vitabu vya wageni ambao hata ujio wao kwenu ulikuwa wa maovu ya kuwatumia kama watumwa wa kuwafanya kuwa sio binadmu kamili mwenye fahamu yake.
 
Mtoa uzi kumbuka kuwa Afande Sele alishatubu, Hivyo Wewe unakula matapishi yake na kubeba hukumu ambayo mwenzako alishajinasua nayo.
 
Wanajamii,

Umofia kwenu.

Baada ya msiba wa mzee Magufuli, mwimbaji wa zamani wa mziki wa kizazi kipya maarufu kama Afande Sele/mkali wa rhymes alijitokeza na kutoa maneno mengi yaliyotafsiriwa kama kashfa au matusi kwa Mungu na watu wengi.

Msanii huyo mantiki yake ilionekana kudai Mungu ni dhana tu hayupo kama angekuwepo asingemuondoa Magufuli mapema kiasi hiki wakati bado anahitajika.

Hoja yangu ni kwamba, vipi kama ni kweli Afande Sele yupo Sahihi?

Kwanini...

Mosi, Dini nyingi sana. Haiwezekani Huyu Mungu anayempenda mwanadamu alete utitili wa dini halafu aweke masharti ya kwamba ukikosea unachomwa moto. Ni sawa na uwe mgonjwa uende kwa daktari halafu huyo dk amwage dawa zaidi ya 4000 mbele yako then akulazimishe kuchagua dawa moja sahihi, na adhabu pale tu utakapokosea.

Pili. Mwingiliano wa vitabu. Qur'an na Biblia kuna mwingiliano wa visa vinavyofanana, pamoja na wahusika. Mfano Mariamu, Issa(yesu) Musa, Ibrahim pamoja na wengine wengi. Hii sio kufanana kwa bahati nasibu tu ila kuna mmoja alinakili kutoka kwa mwenzake na/ kulingana na mazingira yanayofanana basi hivi ni visa vya kubuni ambavyo ilikuwa haiwezekani kuvikwepa, ni sawa na ngano za Kiafrika ambavyo huwezi kumkwepa mhusika "zimwi".

Eti, Mungu anajuwa yote (Omnipotence), kwanini hakugundua mapema kama shetani angeleta zogo kwa Adam na Hawa? Baada ya Ibilisi kupambana na majeshi ya Mungu akashindwa alitupwa duniani, then anamuumba mwanadamu anamweka duniani. Anaweza kumwacha mwanao unaemoenda alale chumba kimoja na chatu? Kwanini asingetuweka hata sayari ya Mars.

Mungu na shetani sio maadui.

Hii inajidhihirisha pale anapopiga stori na Shetani, mwanzoni kabisa mwa kitabu cha Ayubu.
"Shetani akiwa anatembea zake duniani akiwa anapunga upepo, alikutana na Mungu, Mungu akamuuliza ... Umenionea mtumishi wangu Ayubu...."

Kwa muktadha wa mazungumzo hayo, viumbe hawa hawawezi kuwa maadui.

Tano, kama Mungu anabusara asingeweza kumwacha shetani akae pamoja na mwanadamu.

Kumbuka shetani alikuwa malaika, ambaye licha ya uwezo wa jeshi tiifu la Mungu alifanikiwa kupambana nalo kwa muda mrefu, mwanadamu angewezaje kukaa na jeshi la Shetani sasa, au Mungu hakujua.

Mungu pia hufa kutokana na maendeleo ya wanadamu.

Wanadamu wamekuwa na miungu wengi sana ambao kulingana na wakati na maendeleo ya sayansi hao miungu hufa na kupotea, mfano ni NIKE Mungu wa vita, ATLAS mungu aliyeshikilia/beba mabegani dunia hewani isiporomoke, VULCA, mungu wa moto na hasira aliyekuwa akikasirika hufuka moto toka ardhini. (Ambaye kwaye tumepata neno Volcano)

Je, unahakika huyu Mungu unayemwamini sasa hatakufa kutokana na wakati?

UNA UHAKIKA?
Tuseme tu kusema mtu asiye amini kwamba Mungu hayupo ni MPUMBAVU kama wewe mtoa mada.
 
Back
Top Bottom