JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,314
- 5,478
Simba walisaini mkataba na Vunja Bei wenye thamani ya shilingi bilioni 2 kwa miaka miwili, ikiwa na maana kuwa kila mwaka au kila msimu Simba wanaingiza bilioni moja katika mauzo ya jezi.
Sina kumbukumbu za hivi karibuni na nimejaribu kutafuta lakini sijapata kama Yanga na GSM waliwahi kusema hadharani kuhusu thamani ya mkataba wao wa jezi na bidhaa nyingine zenye nembo ya Yanga, bali ninachokumbuka GSM walisema watatoa kiasi fulani kwa klabu hiyo kwa kila mauzo ya jezi.
Haji Manara amejinadi kuwa klabu yao ya Yanga inaongoza kwa mauzo ya jezi mara tano ya klabu nyingine zote Tanzania.
Najua ni porojo za mabosi wake wa GSM ili tu ionekane wanafanya biashara, wakati wameanza kupunguza mauzo ya jezi ili mzigo utoke.
Tuachane na hilo kwa sababu siyo hoja ya msingi, jambo la kujiuliza ambalo linaweza kuanza kwa mfano.
Simba wanaingiza Sh bilioni moja kwa mwaka kwa mauzo ya jezi, kama Yanga wanauza jezi mara tano ya klabu nyingine zote, tuanze na Simba ambao mkataba wao upo wazi na ndiyo wanaoonekana kuwa na takwimu za wazi za kimkataba, hiyo inaaanisha kuwa Yanga wanaingiza zaidi ya shilingi bilioni tano kwa mwaka?
Tangu GSM wameanza kuidhamini Yanga inamaana wameingiza bilioni ngapi mpaka sasa? Zimeinufaisha zaidi pande gani, Yanga au GSM?
Viongozi wa Yanga, mashabiki na wanachama wanajua kuhusu hizo bilioni tano za kila mwaka?
Je, vipi kuhusu zile bidhaa nyingine ambazo GSM wanauza kwa nembo ya Yanga (Club Merchandise) zikiwemo traki suti, t-shirts, vikombe, saa, kofia, viatu (raba na sandozi), bracelets na nyingine nyingi ambazo zilianza kuuzwa kuwanzia mwaka jana (2021), mahesabu yake yanajulikana?