Yanga wanajua hizi Sh bilioni 5+ wanazokusanya GSM? Propaganda za Haji Manara zinaamsha wengi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Simba walisaini mkataba na Vunja Bei wenye thamani ya shilingi bilioni 2 kwa miaka miwili, ikiwa na maana kuwa kila mwaka au kila msimu Simba wanaingiza bilioni moja katika mauzo ya jezi.

Sina kumbukumbu za hivi karibuni na nimejaribu kutafuta lakini sijapata kama Yanga na GSM waliwahi kusema hadharani kuhusu thamani ya mkataba wao wa jezi na bidhaa nyingine zenye nembo ya Yanga, bali ninachokumbuka GSM walisema watatoa kiasi fulani kwa klabu hiyo kwa kila mauzo ya jezi.

Haji Manara amejinadi kuwa klabu yao ya Yanga inaongoza kwa mauzo ya jezi mara tano ya klabu nyingine zote Tanzania.

Najua ni porojo za mabosi wake wa GSM ili tu ionekane wanafanya biashara, wakati wameanza kupunguza mauzo ya jezi ili mzigo utoke.

Tuachane na hilo kwa sababu siyo hoja ya msingi, jambo la kujiuliza ambalo linaweza kuanza kwa mfano.

Simba wanaingiza Sh bilioni moja kwa mwaka kwa mauzo ya jezi, kama Yanga wanauza jezi mara tano ya klabu nyingine zote, tuanze na Simba ambao mkataba wao upo wazi na ndiyo wanaoonekana kuwa na takwimu za wazi za kimkataba, hiyo inaaanisha kuwa Yanga wanaingiza zaidi ya shilingi bilioni tano kwa mwaka?

Tangu GSM wameanza kuidhamini Yanga inamaana wameingiza bilioni ngapi mpaka sasa? Zimeinufaisha zaidi pande gani, Yanga au GSM?

Viongozi wa Yanga, mashabiki na wanachama wanajua kuhusu hizo bilioni tano za kila mwaka?

Je, vipi kuhusu zile bidhaa nyingine ambazo GSM wanauza kwa nembo ya Yanga (Club Merchandise) zikiwemo traki suti, t-shirts, vikombe, saa, kofia, viatu (raba na sandozi), bracelets na nyingine nyingi ambazo zilianza kuuzwa kuwanzia mwaka jana (2021), mahesabu yake yanajulikana?

Yanga.jpg
 
Hizo propaganda zilianza zamani sana, kipindi wana release kwa mara ya kwanza walitangaza kuwa package ya jersey 1M ishakuwa sold out

Na hapo ilikuwa ni siku chache kuelekea siku ya mwananchi, watu tulitegemea kuona asilimia kubwa ya mashabiki watakao hudhuria uwanjani watapiga uzi mpya ambao wameununua sana

Lakini haikuwa hivyo kwani 85% waliohudhuria pale kwa mkapa walivaa old jersey na 12% walivaa nguo za kawaida halafu 3% ndo walivaa hizo jezi mpya

Sasa kama hiyo haikutosha kumpuuza manara pamoja na wenzake unataka mpaka ifanyike sensa ndo umpuuze?
 
Hizo propaganda zilianza zamani sana, kipindi wana release kwa mara ya kwanza walitangaza kuwa package ya jersey 1M ishakuwa sold out....
Mkuu umetumia methodology gani kuziibua hizi statistic zako?
 
Simba walisaini mkataba na Vunja Bei wenye thamani ya shilingi bilioni 2 kwa miaka miwili, ikiwa na maana kuwa kila mwaka au kila msimu Simba wanaingiza bilioni moja katika mauzo ya jezi.

Sina kumbukumbu za hivi karibuni na nimejaribu kutafuta lakini sijapata kama Yanga na GSM waliwahi kusema hadharani kuhusu thamani ya mkataba wao wa jezi na bidhaa nyingine zenye nembo ya Yanga, bali ninachokumbuka GSM walisema watatoa kiasi fulani kwa klabu hiyo kwa kila mauzo ya jezi.

Haji Manara amejinadi kuwa klabu yao ya Yanga inaongoza kwa mauzo ya jezi mara tano ya klabu nyingine zote Tanzania.

Najua ni porojo za mabosi wake wa GSM ili tu ionekane wanafanya biashara, wakati wameanza kupunguza mauzo ya jezi ili mzigo utoke.

Tuachane na hilo kwa sababu siyo hoja ya msingi, jambo la kujiuliza ambalo linaweza kuanza kwa mfano.

Simba wanaingiza Sh bilioni moja kwa mwaka kwa mauzo ya jezi, kama Yanga wanauza jezi mara tano ya klabu nyingine zote, tuanze na Simba ambao mkataba wao upo wazi na ndiyo wanaoonekana kuwa na takwimu za wazi za kimkataba, hiyo inaaanisha kuwa Yanga wanaingiza zaidi ya shilingi bilioni tano kwa mwaka?

Tangu GSM wameanza kuidhamini Yanga inamaana wameingiza bilioni ngapi mpaka sasa? Zimeinufaisha zaidi pande gani, Yanga au GSM?

Viongozi wa Yanga, mashabiki na wanachama wanajua kuhusu hizo bilioni tano za kila mwaka?

Je, vipi kuhusu zile bidhaa nyingine ambazo GSM wanauza kwa nembo ya Yanga (Club Merchandise) zikiwemo traki suti, t-shirts, vikombe, saa, kofia, viatu (raba na sandozi), bracelets na nyingine nyingi ambazo zilianza kuuzwa kuwanzia mwaka jana (2021), mahesabu yake yanajulikana?

View attachment 2126891
Manara mwenyewe alishasema ; kule utopoloni mwenye akili ni baba yake tu. Ila akaongezea kwa kusema ; " kidogo na Kikwete tu" Sasa unategemea hawa mazuzu wengine waliobaki wang'amue kitu cha namna hiyo?Ndiyo Maana Manara anaongea linalokuja kwenye ulimi wake halafu mazuzu wanakenua meno na kushangilia tu .
 
Tuambie Mo alipoweka zile fedha tulizochanga za kujenga uwanja baada ya Babra kupigana uwanjani.
 
Kweli nyani haoni....., Sasa mmejua vunjabei ameuza jersey ngapi? Na kwa msimu mzima kauza ngapi? Yeye faida yake ni shilingi ngapi pale Simba inapopewa bil moja tu?
Yanga na Simba hakuna wa kumcheka mwingine
Lakini mchakato wa mabadiliko ukikamilika pengine Yanga itakuwa bora zaidi na huenda Simba wakapitia kipindi kigumu sana kwa sababu ya mambo ya mwekezaji wake
 
Mkataba wa Vunja Bei na Simba hauhitaji kujua zimeuzwa Jersey ngapi. Idadi yoyote atakayouza ye anatakiwa apeleke TZS 2bil ndani ya miaka miwili.

Lakini mkataba wa Yanga na GSM ni kua kwenye kila Jersey moja, Yanga apate 1,300/-. So ili asidhulumiwe Yanga inabid ajue GSM kauza ngapi ili adai chake.

Uwe unaelewa hizi mambo kwanza ndo uweze kuleta hoja hapa. Otherwise tunaonekana kama JF hatujui vitu pale watu wa nje wanaposoma comments zetu.
 
Manara mwenyewe alishasema ; kule utopoloni mwenye akili ni baba yake tu. Ila akaongezea kwa kusema ; " kidogo na Kikwete tu" Sasa unategemea hawa mazuzu wengine waliobaki wang'amue kitu cha namna hiyo?Ndiyo Maana Manara anaongea linalokuja kwenye ulimi wake halafu mazuzu wanakenua meno na kushangilia tu .
🤣🤣🤣🤣

Hata yeye mwenyewe Manara hayumo kwenye orodha ya wale wawili wenye akili.
 
Yanga Ni:-

Kapu La Mjinga, Mwerevu Gharibu Said Mohammed Anatia Mkono Anajichotea Cash Anatembea Mbio

Back
Top Bottom