Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 576
- 1,626
Kontena zaidi ya mbili zenye jezi feki za Simba, Yanga na Taifa Stars zinazokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Tsh. bilioni mbili zimekamatwa kwenye ghala moja lililopo eneo la Chang’ombe Jijini Dar es salaam huku Mtu aliyeziingiza nchini pamoja na Mmiliki wa ghala lililokutwa na jezi wakitokomea na hadi sasa Mmiliki wa jezi hizo feki hajafahamika.
Maafisa wa Idara mbalimbali za Serikali wameonekana wakifanya tathmini ya mzigo huo ili kujua makadirio ya thamani yake halisi na hasara iliyopatikana pamoja na viwango na ubora wake, huku Mmiliki akishindwa kufika eneo hilo wala kubainika hadi kufikia asubuhi hii.
Licha ya uwepo wa Maafisa wa Serikali, wengine waliokuwa katika eneo hilo hadi usiku wa manane ni pamoja na Viongozi wa Simba na Yanga pamoja na Wawakilishi kutoka GSM na Sandaland ambao walionekana kufuatilia kwa ukaribu kila kilichoendelea.
Viongozi wa Taasisi za Serikali hawakuwa tayari kuongea huku wakiahidi kutoa taarifa leo hii lakini Mwakilishi wa Kampuni ya GSM amesema kuwa uwepo wa jezi feki hizo unakwamisha jezi original kuuzwa na amewataka Mashabiki kununua jezi halisi kwenye maduka yaliyotangazwa kwakuwa kunua jezi feki kunaua mpira wa Tanzania na kuwatia hasara wanaowekeza pesa zao kutengeneza na kusambaza jezi original
Ayo TV