Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Mwanzo mwanzoni nitamke wazi kuwa mimi ni mshabiki wa Yanga tangu utoto wangu. Lakini, kila ninapotazama mechi ya mpira(nilianza kufuatilia tangu miaka ya 90), huwa nauweka ushabiki wangu pembeni.
Daima huwa naitazama mechi kiufundi na kunasa cha kuondoka nacho, achilia mbali matokeo. Huwa naondoka na hali ya maandalizi; mbinu za benchi la ufundi; uwezo wa wachezaji; figisu zitokeazo na kadhalika. Kinapofanyika kila kitu na timu kukosa matokeo mazuri huwa naumia lakini nafarijika.
Yanga imetoa somo la kuwa matokeo ya soka yanaweza kupatikana popote-nyumbani au ugenini. Msimu huu wa Kombe la Shirikisho Afrika Yanga imesare, imeshinda na kushindwa nyumbani na ugenini. Lakini, rekodi yake ya kushinda ugenini imetamalaki.
Yanga imeshinda kwenye viwanja vigumu kupata matokeo. Ilishinda kwa Rivers ambako Wydad alipotea. Ikashinda kwa Marumo ambako Pyramids aliuwawa; ikashinda kwa USMA ambako hata sare kabla ya jana haikutoka. Nimeacha pale Lubumbashi kwa Mazembe makusudi.
Yanga imetoa somo na kutuma ujumbe kwa wapinzani wajao wa michuano ya CAF. Kuwa hakuna cha nyumbani wala ugenini watakapokutana na Yanga. Simba wajifunze. Wafike mbali zaidi na zaidi.
Najua na nakiri kuwa rekodi ya Simba kwenye Klabu Bingwa Afrika ni kubwa kuliko ya Yanga. Ila wanapaswa kuvuka robo fainali kwa somo la Yanga. Waachane na kufukua mambo bishani ya 1974 na mengineyo. La kweli ni la fainali ya CAF mwaka 1993 na walizabwa 2 kwa 0 Uwanja wa Uhuru baada ya sare ya kule Abidjan. Wakaponzwa na uwanja wa nyumbani.
Pamoja na figisu za jana za USMA, Yanga wakalipa kisasi cha kufungwa nyumbani. Uongozi wa CAF ulikuwepo na kuona ukali wa Yanga. Waarabu wanakuwa wanaiogopa Yanga popote watakapokutana nayo.
Wachambuzi walichambua na kutisha kwa rekodi za nyumbani za wapinzani wa Yanga kila mechi. Yanga proved them wrong. Mpira hauna nyumbani wala ugenini. Ni kiwango na maandalizi tu. Faraja yetu ni kuwa tumemaliza mashindano ya Afroka kwa ushindi. Na tumekuwa Makamu Bingwa wa Shirikisho tukitoa Mfungaji bora na Golikipa bora wa mashindano hayo. Tukutane msimu ujao wa michuano ya CAF!