Yanga bingwa tena msimu huu wa 2023/2024 , wanasimba tujiandae kisaikolojia

Mkono Mmoja

JF-Expert Member
Jan 26, 2019
1,932
4,086
Nikiwa kama shabiki kindakindaki wa klabu ya Simba sc ,nathubutu kusema kwa kinywa kipana kuwa Yanga atatwaa tena ubingwa wa ligi kuu ya NBC msimu wa 2023/2024.

Naitazama Yanga kwa jicho la kimpira naona kabisa kuwa wameizidi simba kwa vitu vingi sana. Wachezaji wa Yanga wana ari na shauku ya kuipambania klabu yao tofauti na wachezaji wa timu yetu ya Simba.

Wachezaji wetu wanaonekana hawana ile shauku na ari ya kupambana kabisa. Tunapopata goli moja tunaridhika kabisa na kujiaminisha kuwa tumeshi da mechi tofauti na Yanga ambayo hata ikiongoza kwa bao mbili bado utaiona inawasha moto.

Mwisho nitoe wito kwa wanasimba wenzangu kuwa tujiandae kabisa kisaikolojia kuwa hatutaweza kupata ubingwa kwa msimu huu kutokana na wapinzani wetu kuwa bora zaidi yetu. Tuwe wakweli kuwa chama letu halichezi kibingwa .
 
Hilo lipo wazi
 
Sisi mashabiki wa Simba tunataka Robertinho arudi, heri papatu papatu ya matokeo kuliko hii ya kuwekana roho juu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom