Yanga wanaendelea kutumia mbinu za Shirikisho kwenye Klabu Bingwa

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,136
7,903
Jana nilisikia kuwa Yanga baada ya mechi yao na Medeama, walizungumza na mshambuliaji wao hatari aliyewasumbua sana Jonathan Sowah kwa nia ya kumsajili.

Nakumbuka msimu uliopita katika mashindano ya shirikisho, karibia kila timu iliyokuwa inacheza na Yanga, baada ya mechi ya kwanza na timu hiyo, kabla hata ya kurudiana walikuwa wanaonyesha waziwazi interest na wachezaji walioonekana hatari wa timu pinzani na kuwaahidi kuwasajili. Nakumbuka walifanya hivyo kwa TP Mazembe, walifanya hivyo kwa AS Bamako. Walipokutana na Monastir, ghafla tawi lao Singida Big Stars wakaingia ushirikiano na Monastir. Tulio na jicho la tatu tulihoji haya mambo toka kipindi kile. Baada ya mission katika shirikisho kufanikiwa hakuna mchezaji wa TP Mazembe wala Bamako aliyesajiliwa Yanga msimu huu wala ule ushirikiano na SBS hatujausikia tena.

Kwa mtazamo wangu hizi ni mbinu chafu zisizo za kiungwana na kimichezo za kurubuni wachezaji ili kuwapunguza makali kabla ya mechi ya marudiano, ili mchezaji asicheze kwa kiwango chake akidhani atakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga baada ya muda mfupi. Mbinu hii pia siyo fair kwa timu yake ya sasa inayomlipa mshahara wake. Mara nyingine unakuta timu inaamua hata kutompanga huyo mchezaji katika mechi ya marudiano wakiwa na wasiwasi hatacheza kwa bidii.

Embu waza Yanga wangefanyiwa kitu kama hicho kwa timu pinzani kuonyesha interest waziwazi kwa kuongea direct na mchezaji wa Yanga katikati ya mashindano bila kwanza kwenda kwa uongozi wa timu. Naamini wote tunajua jinsi malalamiko yao yangekuwa maana tuliyaona wakati wa sakata la Feisal na Azam. Hizi ni janja janja za muda mfupi na mwisho wa siku zinagonga mwamba maana sitegemei kama wataweza kufanya hivyo kwa wachezaji wanaojitambua wa CRB au wa Al Ahly.

Nawasilisha.
 
Unajua wewe ni kiumbe wa ajabu sana, unatuletea habari za ''Nasikia" alafu unashutumu kitu ambacho auna uhakika nacho!

Leta uthibitisho wa yanga kuongea na uyo mchezaji na hao wengine unaowataja! Unaokota taarifa za mitandaoni uko watu wanataka wauze magazeti na kusaka followers ndio unatuletea hapa?

Kama ni ivyo basi yanga imeongea na lundo la wachezaji si chini ya 100 kwa maana wanaoandikwa ni wengi!

Halafu wewe unalalamika Kama nani?

Simba kaenda kumbeba kocha wa vipers wakati wanajiandaa kucheza nao aukuona?

Miltoni karisa aliyehusishwa na Simba wakati mnaenda kucheza nao aukuona mbona ukuandika?
 
Umebwabwaja bila kuleta ushahidi wowote, hao Yanga wanaela gani ya kuwarubuni wachezaji 11 wa Medeama, wachezaji 11 wa Belouizdad, wachezaji 11 wa Al Ahly. Hivi wewe ni mwehu kiasi hiki.

Unajua wewe ni kiumbe wa ajabu sana, unatuletea habari za ''Nasikia" alafu unashutumu kitu ambacho auna uhakika nacho...
Kwani unadhani tumesahau baada ya mechi na Mazembe jinsi Hersi alivyoshuka kutoka jukwaani na kwenda moja kwa moja kuzungumza na mchezaji wa Mazembe aliyewasumbua siku ile na mkasema waziwazi mnataka kumchukua? Na alifanya vile bila woga wala aibu.
 
Kucheza mpira acheze Bingwa wako wa makombe mengi TZ na mbabe wa kukugonga mechi nyingi duniani na mbinguni afu uteseke wewe Makolokolo SC fan

Sema tu hujazigusa pia zile timu alizozifunga goli 5 kwenye ligi. Huenda na kwenyewe alitumia mbinu hiyo hiyo.

Na ndiyo maana kuna baadhi ya wachezaji wa timu mojawapo iliyofungwa hizo goli 5, nasikia walishtakiwa eti kwenye kamati ya nidhamu ya timu yao!! Ila tu mpaka sasa bado hatujasikia hatma yao.
Wahenga walisema mwosha huoshwa. Wengine nao wakitumia mbinu wanazojua wao kurubuni wachezaji wenu msianze kulia lia
 
Kwani unadhani tumesahau baada ya mechi na Mazembe jinsi Hersi alivyoshuka kutoka jukwaani na kwenda moja kwa moja kuzungumza na mchezaji wa Mazembe aliyewasumbua siku ile na mkasema waziwazi mnataka kumchukua? Na alifanya vile bila woga wala aibu.
Kumbe ni baada ya mechi, naomba nipe reference kabla ya mechi ili tuone matokeo ya kufungwa kwa Tp Mazembe kumetokana na wachezaji kulaghaiwa na Hersi kabla ya mchezo.
 
Umebwabwaja bila kuleta ushahidi wowote, hao Yanga wanaela gani ya kuwarubuni wachezaji 11 wa Medeama, wachezaji 11 wa Belouizdad, wachezaji 11 wa Al Ahly. Hivi wewe ni mwehu kiasi hiki.
Ni mwehu mkuu
 
Kumbe ni baada ya mechi, naomba nipe reference kabla ya mechi ili tuone matokeo ya kufungwa kwa Tp Mazembe kumetokana na wachezaji kulaghaiwa na Hersi kabla ya mchezo.
Halina akili haeleweki ana ongea nini mara Singida na Monastir ushirikiano wao haujulikani alitaka wawe wanampa taarifa kama nani? kwani makolo hajawahi kuingia ushirikiano na timu za nje nani ana taarifa nini kina endelea?
 
Unajua wewe ni kiumbe wa ajabu sana, unatuletea habari za ''Nasikia" alafu unashutumu kitu ambacho auna uhakika nacho!

na?

Miltoni karisa aliyehusishwa na Simba wakati mnaenda kucheza nao aukuona mbona ukuandika?
Analeta habari za YouTube humu
 
Chezeni mpira acheni janja janja. Na wewe vibertz soma vizuri kabla haujajibu maana naona unatapatapa
Uzi wako ni pumba tu, yaani Yanga walaghai kuwasajili wachezaji wa kila timu hilo linawezekanaje. Propaganda za kijinga tu ambazo hata haziisaidii Simba kushinda.
 
amba maana sitegemei kama wataweza kufanya hivyo kwa wachezaji wanaojitambua wa CRB au wa Al Ahly.

Nawasilisha.
Nilichosoma kwenye akaunti ya mchezaji mwenyewe ni kwamba timu haijampigia simu na ameelekeza wanaomhitaji wawaailiane na timu yake. Hizi chuki za kishabiki zinawafanya mm iwe wazushi!!
 
Chezeni mpira acheni janja janja. Na wewe vibertz soma vizuri kabla haujajibu maana naona unatapatapa
Wewe ni Rage fc kiwango cha mwisho kabisa. Hakuna cha maana ulichoandika, bora hata ungeambatanisha na kauthibitisho kidogo uonekane kichwani unazo. Ila kumbe bogasi, hata mtoto hawezi kuwa na upeo mdogo kiasi hiki.
 
Nilichosoma kwenye akaunti ya mchezaji mwenyewe ni kwamba timu haijampigia simu na ameelekeza wanaomhitaji wawaailiane na timu yake. Hizi chuki za kishabiki zinawafanya mm iwe wazushi!!
Hakuna kitu kama hicho ulichoandika. Na chuki iko wapi hapo wakati nimetoa mtazamo wangu kutokana na kile ambacho wamekuwa wanafanya na uthibitisho upo. Hakuna nilichosema ambacho hakijafanyika au hawajakisema. Hao wanaonishambulia wanajua nimemulika nia zao ovu
 
Analeta habari za YouTube humu

Uzi wako ni pumba tu, yaani Yanga walaghai kuwasajili wachezaji wa kila timu hilo linawezekanaje. Propaganda za kijinga tu ambazo hata haziisaidii Simba kushinda.

Wewe ni Rage fc kiwango cha mwisho kabisa. Hakuna cha maana ulichoandika, bora hata ungeambatanisha na kauthibitisho kidogo uonekane kichwani unazo. Ila kumbe bogasi, hata mtoto hawezi kuwa na upeo mdogo kiasi hiki.
Hizo habari zimeripotiwa katika vyombo mbalimbali rasmi vya habari vya Tanzania na Ghana na pia narudia tena, hapa naongelea Yanga kuonyesha tu interest kwa mchezaji ili kumdhoofisha yeye na timu yake.

Nawakumbusha pia kwa ule mpira wa nguvu na rafu mlioamua kucheza nao mechi ya kwanza na mtakapocheza nao tena kwa style hiyo subirini vilio tu na baadae kuwakosa wachezaji wenu katika mechi inayofuata. Tunajua pale wakikosekana wachezaji wawili tu hamna timu.
 
Ukisikia mbwiga ndio huyu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom