Huu hapa ukweli wa Yanga Sc kutinga robo fainali Mara tatu kwenye michuano Ya klabu bingwa Africa kabla ya kubadilishwa jina michuano hiyo

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,206
12,726
Niliona Makaburi yamefukuliwa baada ya Yanga Sc kutinga fainali ya shirikisho, Simba sc (mashabiki ) walitumia nguvu Kubwa Kufukua Makaburi ili tu nao waonekane kuwa walifika fainali.

Ndiyo Leo NALIA NGWENA nawaletea historia inayoonesha Yanga Sc ilitinga Robo Mara tatu katika michuano hii ya kimataifa na kama Kuna mtu hatotaka kukubaliana na hii historia basi zifutwe na fainali ya Simba sc.

Ukifuatilia CAF wanasema Simba sc hawajawahi kufika Fainali na hata Yanga Sc pia CAF walipost kuwa ni Mara Yao ya kwanza kufika Robo.

Ukweli ni huu hapa kwa Yanga sc kutinga Robo Mara tatu kwenye michuano ya kimataifa kabla haijabadilishwa jina.

Na NALIA NGWENA

Katika mfumo wa sasa ‘Ligi ya mabingwa Afrika’ hii itakuwa ni michuano ya 10 kwa mabingwa mara 24 wa Tanzania Bara, timu ya Yanga SC. Miaka ya nyuma michuano ya mabingwa Afrika ilikuwa ikifahamika kama klabu bingwa Afrika.

Timu zilikuwa zikishindana kwa mtindo wa mechi mbili za mtoano (nyumbani na ugenini) kuanzia mwanzo hadi mwisho alipokuwa akipatikana bingwa. Katika utaratibu huo Yanga ilifanikiwa kuiwakilisha Tanzania mara 11 hadi mwaka 1996 ilipobadilika kidogo na kuwekwa hatua ya makundi mawili kufikia timu nane bora na hivyo kuanzia mwaka 1997 michuano hiyo ilibadilika na kuwa ligi ya mabingwa Afrika.

Kihistoria katika mara 20 zilizopita katika ushiriki wa Yanga katika michuano hiyo wameweza kufika nane bora mara 3. Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 1969 waliweza kuwa miongoni mwa klabu nane bora katika michuano hiyo.

Wakarejea tena mwaka uliofuata (1970) wakafika hatua ya robo fainali kwa mara ya pili mfululizo. Baada ya hapo ni mara mbili tu waliweza kufika raundi ya pili (1975 na 1982.) Mara ya tano waliishia raundi ya kwanza ( 1972, 1973, 1984, 1988 na 1992.) Mara mbili waliishia raundi ya awali ( 1971 na 1996).

LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Kufikia mwaka 1997, Shirikisho la soka Afrika, CAF lilibadilisha mfumo wa michuano na timu 8 bora zilipangwa katika makundi mawili na timu mbili za juu katika kila kundi zimekuwa zikifuzu kwa hatua ya nusu fainali. Yanga ilikuwa timu ya kwanza ya Tanzania kucheza michuano ya mabingwa Afrika.

Baada ya kutolewa kwa jumla ya goli 1-0 na Express Red Eagles ya Uganda katika raundi ya awali mwaka 1997, ‘Timu ya wananchi’ ilifanikiwa kutinga nane bora ya michuano ya mwaka 1998. Licha ya kwamba hawakubahatika kushinda hata mchezo mmoja katika hatua ya makundi lakini waliweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza kutoka Afrika Mashariki kucheza ligi ya mabingwa Afrika.

Hii ni historia fupi tu katika mapito ya Yanga Sc Kama Kuna mtu atabisha basi akabishane na maktaba/tunza kumbukumbu.

Kila la heri.
 
Yanga imecheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa 1969,1970, (1998 top 8), 2024.

Imecheza robo fainali kombe la washindi mara 1, mwaka 1995.

Imecheza CAF Confederation hatua ya makundi 2016 (top 8)=robo.
Imecheza hatua ya makundi (top 16)
Mwaka 2016.
Imecheza fainali ya CAF Confederation cup 2023.
 
Ukipindua msimamo wa kundi, utaona pia mwaka 1998 pia Uto ilifika robo na pia kuweka historia ya timu ya kwanza kutoka Tanzania kufungwa 6-0 kwenye mashindano haya na Raja Casablanca
 
Yanga imecheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa 1969,1970, (1998 top 8), 2024.

Imecheza robo fainali kombe la washindi mara 1, mwaka 1995.

Imecheza CAF Confederation hatua ya makundi 2016 (top 8)=robo.
Imecheza hatua ya makundi (top 16)
Mwaka 2016.
Imecheza fainali ya CAF Confederation cup 2023.
SHUKURANI MKUU KWA KUJAZIA NYAMA
 
Ukipindua msimamo wa kundi, utaona pia mwaka 1998 pia Uto ilifika robo na pia kuweka historia ya timu ya kwanza kutoka Tanzania kufungwa 6-0 kwenye mashindano haya na Raja Casablanca
HAKUNA CHA AJABU MZEE.
MBONA SIMBA IKIWA YA MOTO ILIPIGWA 5-0 NA AL AHLY JUZI TU HAPO.
 
Mwaka 1969 na 1970 we ulikuwa na umri gani,usituletee historia ya enzi za makaa ya mawe
Ndugu mbumbumbu Ina maana History ya Simba Ina anzia wewe ulipozaliwa mwaka 2000!! matokeo yote waliyopata Simba yanakua ya Historia ya zama za mawe?
 
Back
Top Bottom