Ushirombo
JF-Expert Member
- Jan 22, 2013
- 3,558
- 2,711
Mbowe: CHADEMA ni mpango wa Mungu, lazima kifanye kazi ya kukomboa nchi hii
Amen. Yametimia
Mbowe: CHADEMA ni mpango wa Mungu, lazima kifanye kazi ya kukomboa nchi hii
Hakika hii ni faraja. Hata kwa kupigwa mabomu lakini hawakati tamaa bado umati umejaa. Upande wa siasa uliopanga uhalifu huu na uone aibu sana. kweli uroho wa siasa na madaraka unakufanya uondoe roho ya binadamu. Shame!!View attachment 98024Hizi ndo picha za leo
Taarifa mpya mbaya aliyotoa Mbowe ni kuwa mmoja wa majeruhi aliyekuwa kalazwa Mount Meru Hospital na jana akahamishiwa Selian Hospital aitwaye Amiri Ally amefariki leo mchana!
Wajikumbushe jinsi ambavyo Mungu alivyomkataa Sauli baada ya kuendelea kutenda maovu mengi dhidi ya wananchi wa Israel. Kuweweseka kwa kauli zao kutatusaidia kujua mbivu na mbichi, bora wangenyamaza. Makamanda tujuzeni ili ikiwezekana tuchukue hatua za dhati, maana hata Misri ilianza kidogo kidogo hawa hawafai kusubiriwa mpaka 2015.
Muda wa CCM kukaa madarakani umetosha wakakae segerea na Ukonga tu, Ukimwona Mwigulu na Wassira unaona kabisa nafsi zao zinawashtaki
Hao morani waliompiga nao ni ngumu kuwakamata?Nassari aliumizwa akisimamia uchaguzi makuyuni, na hivi sasa amelazwa Seliani, ana matatizo kwenye mgongo
Kwanza ni nani amemkabidhi Lukuvi ripoti ya mlipuko?,muuaji mkubwa huyo.
Kamanda Mbowe haya mambo mnaratibu na kuyapanga nyie wenyewe; unamlaumu Lukuvi kwa lipi nyie kama mna uchungu na watanzania wanaopoteza maisha yao kwa sababu za kipuuzi kama hizi mnayapangia nini? Mnatafuta mchawi nyumba ya jirani wakati mchawi mnalala naye chumba kimoja!
Ubarikiwe ndugu! Ila kumbuka kwamba "MCHEKA KOVU ASIYE FIKIWA NA JERAHA".
Mwenyezi Mungu amrehemuTaarifa mpya mbaya aliyotoa Mbowe ni kuwa mmoja wa majeruhi aliyekuwa kalazwa Mount Meru Hospital na jana akahamishiwa Selian Hospital aitwaye Amiri Ally amefariki leo mchana!
mbowe:
Katika eneo la tukio zimetumika silaha tatu.
Silaha ya kwanza ni bomu. Aliyerusha bomu tunamjua.
Silaha ya pili ni bunduki aina ya smg. Silaha ya tatu ni bastola.
Mauaji haya yalipangwa. Nimezungumza na igp pamoja na chagonja. Tumewaambia tuwajua, na waliochafua amani ni jeshi la polisi.
Lukuvi anatoa kauli bungeni kwa kudanganya wananchi kuwa wananchi waliwashambulia polisi. Uwongo.
Nilikuwa wa mwisho kuondoka eneo la tukio nikiwa na lema. Majeruhi wote makamanda wa chadema waliwabeba siyo polisi.
Lukuvi anazungumzia tukio la arusha utadhani waliokufa arusha ni kuku.
Mmbarikiwe nyie mlio mahodari wa kujipangia majanga na kuua watu wasio na hatia!
Ulipotokea mlipiko kanisani arusha kila kiongozi na familia yak walibebana kutoa pole eti ni ugaidi. hili waliloliandalia wao si ugaidi? tunasubiri tuone watakavyofanya - walitegemea tungekuwa na msiba wa Lema na Mbowe.............. mungu azilaze pema peponi roho za marehemu kwani imewatokea kwa kuwa karibu na walengwa. ploeni sana wafiwa!
Tunasubiri viongozi kumiminika Arusha na rambi rambi zao kama walivyofanya bomu lilipolipuka kanisani. Ama kwa sababu labda mpango mzima aliujua ndo maana hata hawakushtuka?
We bahau jiheshimu,hii thread kwanza haikuhusu kama una-comment acha masiara wakati watu wanaomboleza..Mmbarikiwe nyie mlio mahodari wa kujipangia majanga na kuua watu wasio na hatia!
tatizo kila mtu anajifanya yy ni mr clean mi naomba chadema waonyeshe mkanda wavideo ambao utaonyesha kila kitu hata muharifu alipokuwa anajiandaa kurusha bomu na nadhani waandishi wa habari wa habari walikuwepo nao watusaidie km video ya mwangosi kuuwawa ilipatikana kwa nini ktk hili lishindikane? Msitufanye akili za watz vimeshikwa na lukuvi au mbowe