Yanayojiri Katika Uwanja wa Soweto Jijini Arusha

Wana Jf,

Tupo hapa uwanja wa Soweto Kaloleni, uwanja ambao tukio la bomu lilitokea.

Muda huu viongozi wa chama wakiongozwa na kamanda wa anga Freemen Mbowe, Mbunge Godbless Lema wameingia uwanjani.
Uwanja umefurika sana watu ni wengi.

Usalama wa wananchi ulikuwa chini ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania.
Polisi walifika lakini walizomewa na kufukuzwa na raia. Polisi wana ugomvi na raia na chadema
View attachment 98029
View attachment 98031
Kama CCM kuwauwa watanzania kwenye mkutano wa chadema mlidhani mtawatisha basi imekula kwenu kwani leo watu walikuwa wengi sana na hawakutangaziwa mkutano wowote hali iliyopelekea wanajeshi wa JWTZ kuja kuwalinda badala ya wapumbavu waliokubali kutumika...

IMG-20130617-WA000.jpg
Wakati nchi ikiyumba, FastJet anauza sura.....
 
R.I.P marehemu wote ,damu yenu itawaandama chama cha mauaji (ccm) na vizazi vyao mpaka ukombozi wa ukweli wa Taifa hili utakapopatikana.
 
Mungu awape pumziko la milele wale wote waliopoteza maisha yao ktk tukio hilo.Kwa kweli ni jambo la kusikitisha mno mno,ila nasema tusihuzunike sana kwa kuwa Mungu amesikia kilio cha watu wake,na kwa kuwa Mungu ni mwenye haki hakika hatutachelewa kupata majibu.
 
Poleni sana wakuu.
Bahati mbaya nunino yupo anapiga misele...anatembelea tutoto huko sunderland, then atatinga QPR kujikusanyia jezi zaidi!
 
Mbowe:
Anawapongeza Jeshi la wananchi kuwa tunawapenda sana, na tunatambua na kuiheshimu kazi yao. Ameomba wananchi wawasaidie kurahisisha kazi yao.
Amesema tuna mgogoro na jeshi la polisi.
Jeshi la polisi linaundwa na binadamu.
Miongoni mwa binadamu hawa wapo wanaotutendea vitendo viovu.
Polisi wale ambao wanaheshimu haki pia tunawapongeza. Lakini wale ambao wanafanya uhalifu dhidi ya raia ndiyo tuna ugomvi nao
 
Poleni sana Mkuu Mungi!! lakini pia ningeomba utujuishe nasi kwa picha kama upenyo unaruhusu!!
 
Mbowe:
Katika eneo la tukio zimetumika silaha tatu.
Silaha ya kwanza ni bomu. Aliyerusha bomu tunamjua.
Silaha ya pili ni bunduki aina ya smg. Silaha ya tatu ni bastola.
Mauaji haya yalipangwa. Nimezungumza na IGP pamoja na Chagonja. Tumewaambia tuwajua, na waliochafua amani ni jeshi la polisi.
Lukuvi anatoa kauli bungeni kwa kudanganya wananchi kuwa wananchi waliwashambulia polisi. Uwongo.
Nilikuwa wa mwisho kuondoka eneo la tukio nikiwa na lema. Majeruhi wote makamanda wa chadema waliwabeba siyo polisi.
Lukuvi anazungumzia tukio la arusha utadhani waliokufa arusha ni kuku.
 
Mungi Hongera sana kwa kutupatia hbr hii kadri unavyoweza kupata.
Nipo mbali na mji kwa muda huu.
 
Last edited by a moderator:
Tuwasamehe Bure Polisi hawana jinsi, kuna habari kwamba ukienda tofauti na matakwa ya viongozi waliopo madarakani unajiingiza kwenye matatizo sana, hebu fikilia ndugu yangu kulikuwa kuna habari kwamba Imrani Kombe alishiriki katika kufanya kilichompata Horace Kolimba, na kuna habari pia kilichomtokea Imrani Kombe kilitokana na kujua Siri za Kifo cha Horace Kolimba au umewahi kujiuliza kilichompata Balali kwasababu tu ya kujua siri zoote za BOT. Ndiyo maana nawaonea huruma sana watu walio Usalama wa Taifa, Polisi na baadhi ya Watumishi wa umma.

Hapana sio kila unachoambiwa unatekeleza pamoja na kuwa hawana la kufanya wakiamuliwa wanakila sababu ya kujiuliza na sio wakiambiwa songambele wao ni kwenda tu unajiuliza nasonga mpaka wapi!resoning is very important,inatajwa kuwa Afrika Misri wanaongoza kwa jeshi kubwa na bora lakini Hosni Mubarak alipo amuru jeshi la nchi hiyo kutoka ili kupiga raia wasio na hatia walijihoji na kutafakari kuwa hata sie tuna watoto,wazazi,shangazi na wajomba wanahitaji elimu bora,afya nzuri,mazingira mazuri ya kufanyia kazi,je nini tatizo kwa majeshi yetu hawayaoni ambayo wenzao tunayaona tunahitaji second independence in this country.
 
Mbowe:
Matumaini yetu jana ilikuwa nikumaliza postmoterm, na kupanga mipango ya mazishi, kwa namna ratiba ilivyo, ni dhahiri kuwa kazi hii haitamalizika leo.
Tulio hili lisihusishwe na dini yoyote, tukio hili ni la kisiasa.
Tunawaomba serikali mkijaribu kuwatetea wahuni hawa wanaovuruga amani ya nchi, tukiwaka msilalamike!
 
Nassari aliumizwa akisimamia uchaguzi makuyuni, na hivi sasa amelazwa Seliani, ana matatizo kwenye mgongo
 
Back
Top Bottom