Yaliyojiri kesi ya Mbowe 01/02/2022. Luteni Denis Urio amaliza kutoa ushahidi wake. Shahidi wa 13 kuanza 04/02/2022

Dogo Urio kateseka sana. Kasahau mke, mtoto, baba, mama, paroko, makomando wenzake.

Kuna tatizo kubwa sana.

Bado anashikiliwa lkn anawaamini police?

Mie naamini angetumia mahakama kuwamwaga police na aseme mbele ya jaji kuwa nimekaririshwa na kulazimishwa tu.

Angekuwa poa sana
 
Dogo Urio kateseka sana. Kasahau mke, mtoto, baba, mama, paroko, makomando wenzake.

Kuna tatizo kubwa sana.

Bado anashikiliwa lkn anawaamini police?

Mie naamini angetumia mahakama kuwamwaga police na aseme mbele ya jaji kuwa nimekaririshwa na kulazimishwa tu.

Angekuwa poa sana
Malize mchezo tu yaishe
 
Hawezi rudi jeshini yule.Hapa ni kuwahurumia tu jamaa wako gerezani.kwa sasa hata wakimfunga Mbowe hakuna impact yoyote.wananchi na Chadema wataendelea na maisha na kama imeandikwa ccm kutoka madarakani muda ukifika watatoka tu.Chadema wameishazoea bila Mbowe, Lissu na Lema.
Sahihi na maisha yanaendelea
 
Habari Wakuu,

Leo 01/ 02/ 2022 shahidi wa 12 Denis Urio amemaliza kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3.

Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki: Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi Februari 01, 2022

UPDATES

04:00 Jaji ameingia

- Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Jamuhuri Dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu.

Wakili wa Serikali Robert Kidando, Ikupendeze Mheshimiwa Jaji naitwa Robert Kidando nipo pamoja na
  • wakili Pius
  • Hilla Abdallah
  • Chavula Jenitreza
  • Kitali Nassoro
  • Katuga Esther
  • Martin Ignasi Mwinuka
  • Tulimanywa Majige
Peter Kibatala Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja
  • Khadija Aron
  • Michael Mwangasa
  • Maria Mushi
  • Dickson Matata
  • Alex Massaba
  • Seleman Matauka
  • Michael Mwangasa
  • Nashon Nkungu
  • Wakili Lusako Mwaiseke anayeshika mikoba ya Wakili John Mallya kwa Leo
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na tupo tayari Kuendelea

Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi tupo tayari Kuendelea.

Kibatala: Shahidi Habari ya toka Jana

Shahidi: Nzuri

Kibatala: Uliwahi Kufahamishwa Katika Kesi hii Kabla ya Kuendelea Kuliwahi Kufanyika Kesi Ndogo Mbili

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Kwa hiyo hufahamu Kwamba Mshitakiwa Adam Kasekwa na Mshtakiwa Mohammed Ling'wenya walisema katika Ushahidi Wao Kuwa Wewe Ulikuwa Mmoja wapo ya Watu waliokamatwa

Shahidi: Ndiyo nasikia Kutoka Kwako.

Kibatala: naomba Unikumbushe tena nani aliyekupa Taarifa wewe Kuja Kutoa Ushahidi

Wakili wa Serikali: Mhe Jaji Jana Ulisema Kuwa Maswali yasirudiwe

Kibatala: Wacha Niulize Kwa Namna Nyingine, Shahidi Ulishawahi Kukutana na Wakili wa Serikali Robert Kidando kabla ya Kutoa Ushahidi Wako

Shahidi: Nilienda Kuriport Ofisi ya DCI, Baada ya Hapo Jumatano ni kariport hapa na Kukutana na Mawakili Wa Serikali

Kibatala: Kwa Maana hiyo Shahidi hujawahi Kuzungumzia Lolote Kuwa wewe hujawahi Kukamatwa na Maafisa wa Polisi akiwemo Jumanne Malangahe, Pamoja na Goodluck.

Shahidi: Nasemaje Wakati bado Sijakamatwa, Siwezi Kutoa Taarifa ambazo hazijanitokea

Kibatala: Katika Ushahidi Wako hujawahi Kupinga Kuwa hujawahi Kufikishiwa Katika Kituo cha Polisi Tazara

Shahidi: Yangekuwa yamenitokea ningemwambia Jaji

Kibatala: Kwa Maana hiyo pia hujawahi Kusema Kuwa hjawahi Kufikishiwa Katika Kituo cha Polisi Mbweni Siku ya Tarehe 09.

Shahidi: Sijawahi Kufikishiwa Popote Kituo cha Polisi wala Kuhojiwa

Kibatala: Wewe Una Ugomvi wowote na Adamoo au Ling'wenya?

Shahidi: Sijawahi Kugombana nao

Kibatala: Unaweza Kutusaidia Kwanini Watu hawa wawili Watunge Uongo Wa Namna hiyo Wenye Detail zote dhidi yako?

Shahidi: Mimi sifahamu

Kibatala: Na nilikuuliza detail ya kwamba wewe Uliwekwa katika Cell ya polisi Mbweni ambayo ilikuwa kabla ya Cell ya Mohammed Ling'wenya?

Shahidi: Kwanini unaniwekea maneno jamani?

Kibatala: Jibu swali ndugu shahidi usinikasirikie!

Kibatala: Unafahamu Kwanini nilikiwa nakuuliza Kuhusu Sehemu Unayo Sali na Paroko Wako?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Baada ya Wao Kuhojiwa Kwamba nani aliwaunganisha Wao na Kiongozi Wa Upinzani Freeman Mbowe, Wao Baada ya Mateso Walikutaja wao, Baada ya Hapo Ukakamatwa.

Shahidi: Jana nilisha Jibu Kuwa nilikuwa Kamanda wa QRF Wakati huo

Kibatala: Katika Ushahidi Wako Ulimtaja Ex Commando anaitwa Khalid?

Shahidi: Simfahamu

Kibatala: Katika Ushahidi Wako Ulimtaja Ex Commando anaitwa Gabriel Mhina

Shahidi: Simfahamu

Kibatala: Unaugomvi na hawa nilio wataja?

Shahidi: Sina

Kibatala: Unafahamu Maana ya Mdepo

Shahidi: Intake mates

Kibatala: Khalid anasema Wewe ni Mdepo Mwezake

Shahidi: Simfahamu Mtu huyo

Kibatala: Khalid ana sababu ya Kutunga Uongo Juu yako

Shahidi: Sijui.

Kibatala: Kwa kuwa wewe Ulikuwa unazungumza na Kingai, Je alishawahi Kukwambia Kuwa kuna Washtakiwa Wengine Makomandoo Wawili

Shahidi: hajawahi Kuniambia

Kibatala: Kwa hiyo Ulikuwa pia hufahamu kuwa katika hii Kesi Palikuwa na Makomandoo Wawili ambao walikuwa Washtakiwa.

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Khalid anasema kuwa, Baada ya Kumuona Bwire anamlinda Freeman Mbowe, ulimuuliza Kuhusu Kazi akasema akuulize wewe, Akakutafuta kwa Mtandao Wa Facebook

Shahidi: Sasa nawasiliana na Khalid Wangapi.

Kibatala: Mwanzo umesema Hakuna Khalid Unayemfahamu ambaye ni Ex Commando Wa 92 KJ

Shahidi: Simfahamu Ndiyo Khalid Yoyote Kibatala: Khalid anasema Baada ya KuKutafuta wewe, Ulimwambia utamtafuta Kuhusu Kazi ya Mgodini

Shahidi: Huyo Khalid Simfahamu.

Kibatala: na Baada ya Wakina Admin na Ling'wenya Kukamatwa Ukasema Kwamba Ile Kazi imebumburuka Kwa hiyo huwezi tena

Shahidi: Simfahamu Khalid, Nihoji watu ambao nimetolea Ushahidi.

Kibatala: Unafahamu Kwamba Kuna Afisa wa Polisi ambaye anaitwa Jumanne alikuja hapa Mahakamani na Kukiri Kuwa kamata Gabriel na Khalid

Shahidi: Sifahamu Kuhusu Jumanne, na simfahamu Jumanne.

Kibatala: Unafahamu Kwamba Siyo Kawaida Kwa Mtu Kusikilizwa Vifaa Vyake kwa zaidi ya Mwaka Mmoja

Shahidi: Inategemea Sasa na suala Lenyewe

Kibatala: Kwa Vifaa Vyako ni Mazingira

Shahidi: Nilienda Kuuliza Mwaka Mmoja Uliopita Wakasema bado Uchunguzi Unaendelea.

Kibatala: Unamfahamu mtu anaitwa John Urio

Shahidi: ambaye ni nani

Kibatala: Ambaye ni Baba yako Mdogo

Shahidi: Simfahamu

Kibatala: Unakumbuka Nilikuuliza Kuhusu Gari yako la Silver

Shahidi: Nakumbuka

Kibatala: Nakakuuliza Kuhusu Hotel uliyofikia

Shahidi: Nakumbuka

Kibatala: Nikisema Kwamba wewe Upo Chini ya Ulinzi Haupo huru

Shahidi: Nashangaa sana Kufikiria hivyo

Kibatala: Unafahamu Gari yako ni Mke wako Ndiye aliyefuatilia na Kuitoa kwa muda Mrefu Kwa Viongozi Wa Jeshi

Shahidi: Ni Uongo

Kibatala: Gari yako imeenda Kihonda lini

Shahidi: haijawahi Kufika kihonda

Kibatala: una Cornfirm Hapa Kwamba Gari hiyo imepakiwa Kambini Kizuka?

Shahidi: Na Cornfirm, Na Siku ya Kwanza Ndivyo Nilivyo Jibu.

Kibatala: Tukitaka Kujua wewe Upo katika Active Duty hujafukuzwa Kazi, Kwa Kosa la Kuwasiliana na Kiongozi Wa Upinzani

Shahidi: Unaangalia Kitambulisho na Kumuuliza Mwajiri Wangu

Kibatala: Hakuna Duty Roaster?

Shahidi: Ipo wewe Unauliza Duty Roaster ya kazini kwangu Kwanini?

Kibatala: Wewe Jibu swali Kwamba Moja ya Uthibitisho Wako Kuwa upo Active Jeshini, ni kutazama Duty Roaster?

Shahidi: Ni kweli

Kibatala: Ni Nyaraka Ipi Unathibitisha Kwamba wewe Ulipewa hiyo QRF Kamanda

Shahidi: Nilisema Kwamba kuanzia Tarehe 03 nilikuwa QRF kamanda

Kibatala: Kwa hiyo Nikukuombea Hairisho Uende Ukalete Karatasi Linalosema wewe Upo katika Active Duty.

Shahidi: Wewe si Unajua Taratibu za Ofisi, Naenda Kuomba Nyaraka Kama nani

Kibatala: Nasema tena Mahakama Ikakupq Hairisho Kwamba Ukalete Karatasi ambalo Lita thibitisha Kuwa Upo Katika Active Duty Utaenda Kuleta

Shahidi: Andikeni Barua, Ndiyo Watanipa Mimi sina Mamlaka.

Kibatala: Kwa hiyo Niliona Kwa Mahakama na Mahakama Ikatafakari Ukalete unaweza Kuleta hilo Karatasi

Shahidi: Ndiyo Kwa Barua naweza Kwenda

Kibatala: Na huo Mchakato Unaweza Kuchukua Siku Ngapi, Kwa Makadirio

Shahidi: Siwezi Kujua Kwa sababu Ofisi inaweza kutafakari na Kujibu

Kibatala: Shahidi Ni kweli au siyo Kweli Mtoto Wako Jackson alipozaliwa, Uliletewa Huko ulipo Kuwa huko Mafichoni umuone?

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji Swali limeshaulizwa

Jaji: Kuhusu Kupelekewa Mtoto Kumuona halijaulizwa

Kibatala: Shahidi Ni kweli au siyo Kweli, Mtoto Wako Jackson alipozaliwa Uliletewa Mtoto ulipokuwa Mafichoni umuone?

Shahidi: Yaani Mtoto azaliwe halafu niletewe Kizuizini, Jaribu Ku' think Kidogo Wakili Msomi, Who are you by the Way?

Kibatala: Shahidi Jibu swali usikasirike.

Kibatala: Ni kweli hata mama yako alikuja Kukuona Ulipokuwa Kizuizini huko Mafichoni?

Shahidi: Sijawahi Kuwa kizuizini

Kibatala: Ni kweli au si kweli hata unapokuja hapa Mahakamani Unasindikzwa na Maafisa Wa Jeshi Wenye silaha?

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shahidi Kila Saa anasema hayupo Kizuizini, Wakili aulize Maswali yenye Mantiki, Sioni Kwanini atoe allegations.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Sijatoa Allegations, Sisi tunauliza Maswali tukileta Mashahidi mbao watayathibitisha Kuwa Shahidi alikuwa Kizuizini, Isionekane hatukuuliza.. Kama Wakili Wa Serikali anachagua Swali la Kuuliza na namna ya Kujitetea, Basi wasiwe Wanaleta Kesi Mahakamani.

Jaji: Swali linahusu Knowledge sioni Kama Kuna tatizo Shahidi Kujibu.. Shahidi Jibu swali hilo.

Kibatala: Ni kweli si Kweli Kwamba Shahidi unapokuja Mahakamani Upo Kizuizini na Unasindikzwa na Maafisa Wa Usalama Wenye Silaha

Shahidi: Sipo Kizuizini, Mawakili Wananipitia Kila Siku Hotelini

Kibatala: Magari yanayo kupitia Huko Hotelini ni Magari Yao Binafsi au Ya Serikali (hao Mawakili Unasema ni wa Kwako)

Shahidi: Sijui Kama ni Magari Yao au Ya Serikali labda niende Kuyakagua.

Kibatala: Je Jibu lako Kwamba Mawakili Wako (Mawakili wa Serikali) inaoanisha Vipi na Jibu la Kwamba Unakutana nao Asubuhi Mahakamani.. Je hizo Dhana Mbili zinaoana?

Shahidi: Narudia tena, Siku ya Kwanza nimekuja Kukutana na Mawakili hapa Mahakamani, Baada ya Hapo Kila Siku nakuja nao na Kuondoka nao

Kibatala: Sawa kazi yangu ni Kuuliza Maswali

Kibatala: Unafahamu Shahidi Mwingine ambaye anapitiwa Hotelini na Mawakili Wa Serikali Kuletwa Mahakamani

Shahidi: sijui Kuhusu Shahidi Mwingine

Kibatala: Ni sahihi Utaratibu Wa Kupitiwa Hotelini na Kurudishwa Hotelini

Shahidi: Siyo Kila Siku, Kuna Siku napewa Mtu wa Kukupeleka

Kibatala: Kama lini Vile

Shahidi: Hata Ijumaa

Kibatala: Uliondoka na Gari gani

Shahidi: Gari Ndogo

Kibatala: Ni Mtu Binafsi au Mtu wa Usalama

Shahidi: Ni Mtu Binafsi

Kibatala: Lakini Ujamwambia Mheshimiwa Jaji Kuwa Gari hilo ni Taksi au Mali ya Mtu Binafsi

Shahidi: Nitamwambiaje Jaji Kuhusu Maswala yangu Binafsi

Kibatala: Kwani hujaambiwa Kuwa hapa Kwenye Ushahidi Kila Kitu ni hadharani, labda iwe Jaji kaona linavunja Haki zako?

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Shahidi Unafahamu Kwamba Viongozi Wote wa Serikali Wamehamia Dodoma Kutoka angalau Mwaka 2018

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba Ofisi za DCI, IGP, CDF wote Wamehamia Dodoma

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba DCI alikwambia Yupo Dar es Salaam Kikazi Mnaweza Kuonana

Shahidi: Sijazungumzia

Kibatala: Unafahamu Kwamba DCI Kahamia Dodoma na Shughuli Zote za Ofisi ya DCI yana fanyika Dodoma

Shahidi: Siwezi Kuzungumzia Kuhusu Ofisi ya DCI.

Kibatala: Aliyeleta Masuala ya Kufika Ofisi Ya DCI

Shahidi: Ni Mimi

Kibatala: Shahidi Unafahamu Kuhusu Neno "CIMIC"

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Unajua Kirefu Chake

Shahidi: Sijui ila najua Maana yake ni nini

Kibatala: Nikisema Kwamba ni CIVIC AND MILLITARY COORDINATION utakubali au Utakataa

Shahidi: Siwezi Kukubali au Kukataa

Kibatala: Nikisema Maana yake ni taratibu za Jeshi kuratibi Mahusiano na Raia au Taasisi zingine za Kijeshi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kwa Tanzania ipo hiyo CIMIC

Shahidi: Haipo, Ipo katika Active Operation, Kama Nchi Zenye Vita.

Kibatala: Kwa Maana yake Tanzania Hakuna Utaratibu Wa Jeshi Kushea Taarifa na Jeshi Kama la Polisi

Shahidi: Utaratibu huo upo

Kibatala: kwa Maana hiyo CIMIC ipo

Shahidi: Ndiyo ipo

Kibatala: Kwa Maana hiyo Jeshi wanaweza Kumkamata Mtu na Bangi kisha Jeshi likaona ni swala la Polisi, Wakampeleka Polisi

Shahidi: Ndiyo.

Kibatala: Hata Kama siyo Kazi ya Jeshi Kuchunguza Ugaidi, Chini ya Mwamvuli wa CIMIC Jeshi siwanaweza Kumkamata na Kumpeleka Polisi

Shahidi: Hapo unampeleka Polisi

Kibatala: Na Kinyume Chake Taasisi Za Kiraia zinaweza Kuona Mtu Kwa Taarifa zake, Wana weza Kumkabidhi kwa Jeshi Kwa Tuhuma zake

Shahidi: Hakuna Kitu Kama hicho

Kibatala: Kwani Coordination Maana yake nini Under CIMIC

Shahidi: Mahusiano Kwa ajili ya Ku badirishana Taarifa.

Kibatala: Unafahamu Kuhusu Presence Patrols

Shahidi: Ndiyo nafahamu, Lakini haifanyiki Mara Kwa Mara

Kibatala: Hata Kama Mara 3 au 2, Jeshi lina fanya au halifanyi

Shahidi: Linafanya.

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Majuzi Ulitoa Uamuzi Mdogo Kuhusu Taarifa za Kijeshi, Naomba Wakili Peter Kibatala azuiwe asijadili Taarifa Za Operation za Kijeshi, Maana anakuoenda si Pazuri.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Wakati Uamuzi Unatolewa nilikuwepo na Nilisikia, Sijauliza Kuhusu Vifaru Vingapi wala Silaha ni Ngapi. Wakili wa Serikali Labda Hajui Kuhusu Presence Control, Presence Control Maana yake ni kwamba Jeshi Lina chukua Askari Wake Wanapita Mtaani iwe Kwa sababu za Kiusalama au Kwa sababu ya Taharuki, Labda hata Wanasiasa wakitoa Matamko Jeshi Wakati fulani hata Tanzania lilipitisha Wanajeshi Na MAGARI Mtaani Baada ya Tamko la Maandamano, Lakini Mheshimiwa Jaji Ukisema niache nitaacha.

Jaji: Basi Kuhusu Frequently Msifike, Kama Idadi ya Mara ngapi

Kibatala: Sawa Mheshimiwa Jaji.

Kibatala: Shahidi Ni sahihi Presence Patrols Inafanyila Kuonyesha Maadui Kuwa Jeshi Lipo

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Ni sahihi Katika Tanzania Kumefanyika Presence Patrols

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Je kunapotokea Tishio la Ugaidi, Jeshi lina husika au halihusiki

Shahidi: Kuna Level of Protocols, Mpaka Wanaohusika Wa Declare Kuwa Jeshi Lije Kuongeza Nguvu.

Kibatala: Unafahamu Jeshini Kuna Kitu Kinaitwa kwa Jina la Utani OFFICE NUMBER 10

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Kila Kikosi au Kambi ya Jeshi ina intelligence office

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Kazi yake Kudeal na Masuala Mtambuka

Shahidi: Ipo specific siyo suala Mtambuka.

Kibatala: Kuna Sehemu Umetaja Spray ya Sumu au Powder ya Sumu

Shahidi: Sikusema

Kibatala: Hukusema Kwa sababu Bwire Hakukwambia Kuhusu Spray ya Sumu au Powder Ya Sumu

Shahidi: Jaji Mbona ananiwekea Majibu Mdomoni

Kibatala: Jibu swali Langu

Shahidi: Sijjazungumzia kabisa

Kibatala: Unamfahamu Tundu Lissu?

Shahidi: Ndiyo Namfahamu

Kibatala: unafahamu Kwamba Khalfani Bwire na Wenzake Walihusika Kulinda Tundu Lissu Wakati anawasili Tanzania

Shahidi: Rais Mwenyewe halindwi na Komandoo

Kibatala: Jibu swali Langu

Shahidi: Sifahamu Kama Walimlimda

Kibatala: Shahidi Unafahamu Kwamba Moja ya Jukumu ulilo waitia Ilikuwa Kumlinda Tundu Lissu

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba Tundu Lissu kwa Madhira aliyo Pata alikuwa anataka Ulinzi wa Hali ya Juu

Shahidi: Najua Kazi ya Ulinzi Kwa Mgombea ni Kazi ya Polisi

Kibatala: Kwani we Unajua Kuwa Mgombea analindwa na Polisi Wangapi

Shahidi: Sifahamu Kibatala: wewe Uliongea na Polisi Kuhusu Walinzi Wa wagombea

Shahidi: Sijawahi

Kibatala: Ulishawahi Kumlinda Mgombea wa Urais

Shahidi: Sijawahi

Kibatala: Ulishawahi Kumlinda hata Katibu kata

Shahidi: Sijawahi

Kibatala: Sasa Unaongelea Mambo ya Polisi, Yanakuhsu Nini wewe?

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Kibatala: Je unafahamu Kwamba Jeshi la Polisi Pamoja na Kulinda Raia, lakini Lissu alipigwa Risasi zaidi ya 30

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba Mpaka Leo Jeshi la Polisi Hawajamkamata Mtu hata Mmoja Mpaka Leo

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Unafahamu Kwamba Freeman Mbowe alikuwa na Mlinzi Wake anaitwa Allan Bhujo na Hapa Mahakamani yupo

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Mtu anaitwa Ben Saa Nane ( Talking about Security Threats)

Shahidi: Simfahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba Mbowe (Homeboy Wako) Msaidizi Wake Ben Focas Rabiu SaaNane Kapotea Mpaka Leo hajulikani Halipo

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Je Mpaka hapo huoni Kwamba Mtu alikuwa anahitaji Walinzi (Ulinzi)

Shahidi: suala la Walinzi ni Swala Binafsi la Mtu.

Kibatala: Je Kwa wewe Kuwasiliana na Freeman Mbowe, Je Jeshi longe fahamu, au Wakubwa zako au Office namba 10 Je Wangejua unawasiliana na Freeman Mbowe Kiongozi Wa Upinzani limhekuwa Kosa au Siyo Kosa

Shahidi: Siyo Kosa.

Kibatala: Je Kwa Ufahamu Wako wewe Mwanajeshi na Afisa wa Jeshi, Kanuni, Miongozo na Sera, Je Afisa Wa Jeshi anaruhusiwa Kuwa na Mahusiano Ya Moja kwa Moja na Kiongozi Wa Kisiasa?

Shahidi: Personal anaruhusiwa

Kibatala: Kisiasa Je?

Shahidi: Haruhusiwi.

Kibatala: Je Kwa Afisa Wa Jeshi Kama wewe Kumtafutia Kiongozi wa Upinzani Walinzi, inaruhusiwa Kijeshi

Shahidi: Haikuwa Kwa Bahati Mbaya Ndiyo Maana Mpaka Leo Sijashtakiwa

Kibatala: Nani anaamua Kuwa hili ni Kosa la Kinidhamu au siyo Kosa la Kinidhamu

Shahidi: Ni Mimi Mwenyewe

Kibatala: Unafahamu au Hufamu Kwamba Hawa Walinzi, Moja wapo ya Majukumu Waliyo kuwa wanayafanya Kama Walinzi Wa Freeman Mbowe na Chadema ikiwemo Katika Vikao Vya Ndani Vya Chadema.

Shahidi: Sifahamu, Miymi najua Mbowe aliwashawishi Kwenda Kumdhuru Sabaya Moshi baada ya hapo Waje Kulipua Vituo Vya Mafuta Dar es Salaam

Kibatala: Unafahamu Kwamba Adamoo na Ling'wenya Walipoenda Moshi Walipokelewa na Gari yanye Chata na Bendera ya Chadema?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Je unafahamu Kwamba Siku Wanakuja Kumpokea Lissu Walikuja Kutoka Moshi Kwa Kusafiri na Gari ya Chadema

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Je Uliwa uliza

Shahidi: Siwezi Kuwa uliza Kila Saa Watashtuka.

Kibatala: Tarehe 26, Kabla hamjakata Mawasiliano, Je ulikuwa Unawa Monitor Kwa Details Kama hizo

Shahidi: Ndiyo Maana Khalfani Bwire Ali confess Kwangu Kuwa Wamekengeuka

Kibatala: Adamoo Ali confess kwako

Shahidi: Hapana

Kibatala: Ling'wenya Ali confess Kwako

Shahidi: Hapana

Kibatala: Shahidi unafahamu Maana ya Dimina

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Unajua Kuwa Moja yake ni Kama hiyo ya Kuulizwa Kingine na Kuji fanya ujaelewa

Shahidi: Nimesema Kwamba Niliwa uliza

Kibatala: Walikwambia nini

Shahidi: Waliniambia Kuwa walikuwa Wa nasubiri Kuajiriwa.

Kibatala: Siku Wa Nakwambia Wanasubiri Kuajiriwa ilikuwa Tarehe ngapi

Shahidi: Siwezi Kukumbuka.

Kibatala: Nilisikia kwamba Mbowe alikwambia atashiriki Uchaguzi

Shahidi: Hakuniambia Kuhusu Uchaguzi, aliniambia Kuwa Wamepanga Kuchukua Dola Kwa namna yoyote

Kibatala: Kwa hiyo Hapa Mahakamani Hakuna Maneno Kwamba Katika Uchunguzi huu, Chama Chake kimejipanga Kuchukua Dola Kwa namna yoyote

Shahidi: Yapo,

Kibatala: Sasa Mbona Unakataa.

Shahidi: alisema Chama Changu Kimepanga Kuchukua Dola

Kibatala: Unafahamu kwamba Chadema ilikuwa na Wagombea Ubunge Nchi Nzima

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba Chadema Ilikuwa na Mgombea Urais

Shahidi: Nafahamu.

Kibatala: Je Kwamba Mgombea Urais Kuzunguka Nchi Nzima, Kufanya Kampeni

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Kwakuwa wewe Ulikuwa Na Mawasiliano nao Kama Sehemu Ya kuwa Monitor, Je unafahamu Kwamba Moja ya Majukumu yao Ilikuwa Kulinda Makao Makuu Ya Chadema, Mtaa wa Ufipa

Shahidi: Sikuwahi Kufahamu.

Kibatala: Freeman Mbowe Katika Ushahidi Wako aliwahi Kukwambia Katika Mpango huo Kuna Kiongozi Yoyote Wa Chadema ambaye anahusika au Kushiriki

Shahidi: Hakuwahi Kuniambia

Kibatala: Je Unafahamu Kuwa Zile pesa zilikuwa ni Za Freeman Mbowe Binafsi au Za Chama ambazo zilitoka kwa Kufuata Utaratibu wote?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba Suala la Kutafuta Walinzi lilikuwa Maamuzi Ya Chama

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba Freeman Mbowe jawezi Kuleta Walinzi Mpaka Makao Makuu Waje Kulinda bila Idhini ya Chama

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Shahidi Unafahamu Kwamba Hawa Walinzi Waliajiriwa Kutoka Katokana Mapendekezo ya Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama ya Chadema.

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba hata wanamuziki kama Diamond au Wacheza Mpira wana Ma' bodyguards

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Mtu akiwa Discharged Jeshini Kuna zuio la Kufanya Kazi Nyingine?

Shahidi: Hakuna, Msingi afuate sheria

Kibatala: Hata Kunywa Bia lazima Ufuate Sheria, Ndiyo Maana inatakiwa uwe above 18. Je Kiongozi Wako wa Kambi Ulimwambia Kwamba wewe Uliwa' Recruit hawa Walinzi?

Shahidi: Ndiyo nilimwambia

Kibatala: Kwahiyo Ofisi Inafahamu wewe Ukiwa Recruit hawa

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ilikuwa Ofisini au Nyumbani

Shahidi: Ilikuwa Ofisini

Kibatala: Kwahiyo tuliomba Taarifa hiyo Katika Ofisi tutapata

Shahidi: Siwezi Kujua

Kibatala: Katika Hati ya Mashitaka, Hapa Kwanini uliamua Kuwa Mkutane Morogoro

Shahidi: Kwasababu ndiyo Centre

Kibatala: Je Ulisema lolote Kuhusu Kufanya Kikao Mwanza

Shahidi: Hapana

Kibatala: Kuhusu Mwanza

Shahidi: Hapana

Kibatala: Kuhusu Arusha

Shahidi: Hapana.

Kibatala: Wakati Unatoa Taarifa ulimwambia Kuwa Matukio yalitokea tarehe ngapi ya Wewe na Mbowe

Shahidi: Kati ya Tarehe 1 July mpaka Tarehe 10

Kibatala: Sasa Kwenye Hati Ya Mashtaka Wenzetu wameandika Tarehe 1 May, hujamwambia Wewe

Shahidi: Sijasema hivyo mimi.

Kibatala: Unafahamu Kwamba Aishi Protea Machame Hotel Wakati huo Ilikuwa tayari imeshakodishwa

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Uliwahi Kufahamu kama Mbowe aliwahi Kusafiri Nje ya Nchi baada ya Kukwambia Taarifa hizo

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unamfahamu Godbless Lema

Shahidi: Ndiyo Namfahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba Yupo uhamishoni

Shahidi: Sina Taarifa

Kibatala: Unafahamu Lissu anaishi uhamishoni

Shahidi: Sijui Kama yupo Uhamishoni au Kaenda Kutalii

Kibatala: Unafahamu Kwamba Kama hawa Vijana Watatu Wasinge kamatwa, Tundu Lissu angebakia Nchini.. Tundu Lissu Kanyang'anywa Walinzi Wake, Na wapo Mahakamani Wanashitakiwa

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu kwamba hata Godbless Lema Kukimbilia uhamishoni ni Kwa sababu Kijana Mmoja hapa alikuwa amepangiwa Kumlinda Godbless Lema

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba kuishia hapa Kwa shahidi huyu, ASANTE SANA

Wakili wa Serikali: Shahidi Umeulizwa Hapa Kuhusu Mtu Kuwa na Ambao ni Specialized Walinzi ni Swala lake Binafsi, Ulikuwa Unamaanisha nini

Shahidi: Kuna Ma Kampuni Mengi Binafsi Yanatoa huduma, Ila Kimsingi Suala La Ulinzi wa Watanzania Lipo Chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali Kuhusiana Kama Jeshi lingejua kuwa una Mahusiano na Freeman Mbowe, Ukasema Hakuna Tatizo

Shahidi: Ndiyo Kwa sababu Hakuna Mtu anazuiwa Kuwa na Mahusiano na Mtu Mwingine, Kama ni personal

Wakili wa Serikali: Eleza taratibu.

Shahidi: Kufahamiana na Mtu siyo Kosa, Kama tuh Mwanasiasa kijiingiza katika Siasa zake ndiyo kosa

Wakili wa Serikali: Umeulizwa Hapa Kama wewe ni Mtu Muhimu au siyo Mtu Muhimu

Kibatala: OBJECTION Hakuna Mtu aliulizwa swali hilo, Shahidi alivolunteer Mwenyewe.

Wakili wa Serikali: Sawa Shahidi Kwanini Unasema wewe siyo Mtu Muhimu

Shahidi: Hakuna Mtanzania ambaye ni Mtu Muhimu Kuliko Mwingine.

Wakili wa Serikali: Vile Vile Jana Ulipewa Kifungu Kimoja cha Kwenye Biblia Kuhusu Daniel, halafu Mwisho Wa Siku Ukaambiwa Kosa cha Daniel na akina Ling'wenya Ukasema ni tofauti, fafanua

Shahidi: Kwa Daniel Zilitungwa Sheria Kwa sababu alikuwa anaabudu Mara tatu, Wakili anataka Kufananiisha na Suala la kina Bwire, Hawa ni Watu wazima, Ndiyo Maana Wali Confess Kwa Kutaka Kumdhuru Sabaya na Kuja Kulipua Kituo cha Mafuta.

Wakili wa Serikali: Na Uliulizwa Masuala Kuhusiana na Mzazi Wake Ling'wenya, Baada ya Kukupigia Wewe, wewe Ukasema Mpigie Boss wake, Fafanua

Shahidi: Ni kweli Mzazi Wake alinipigia, Ni kweli Nilimwambia kwamba Mpigie Boss Wao, Kama akimkosa Bwire.

Kibatala: OBJECTION Suala la Kupigiwa Bwire ni Jipya

Wakili wa Serikali: Shahidi Suala la Kumpigia Boss wake Ulikuwa Unamaanisha Nini

Shahidi: ampigie Freeman Mbowe ndiyo Boss wake KAMA Kuna Jambo limempata yeye Ndiyo anajua

Wakili wa Serikali: Suala la Simu Siyo Salama, Niwezeshe nikutane nao, Fafanua

Shahidi: Kukutana Pamoja na Kuongea Pamoja ni sahihi zaidi, Simu si salama ndiyo Maana Nikaomba aniwezeshe

Wakili wa Serikali: Kingine ni swala la Meseji ya Saa 2 na Dakika 24 Siku ya Tarehe 22 July 2020, Kwamba atumie namba za Wasaidizi Wake au Wakala.

Shahidi: Nilikuwa nakwepa Kuonekana na Mtega, Nikataka Kujenga Uaminifu, Mbowe aliniambia Simu Siyo Sahihi Wakili Dickson

Matata: OBJECTION Hakuna Maeneo Ambayo alisema Kuwa Simu Siyo Sahihi, atoe hayo Maneno.

Jaji: Wakili Kibatala tusaidie hilo, Nakumbuka Uliuliza swali Kuhusu hilo

Kibatala: Mhe Jaji naomba shahidi ajibu swali Kwanza

Jaji: amesha Jibu

Kibatala: Kwa Ruhusa Yako

Jaji: amejibu Kuwa alikwambia Kuwa atumie Simu ya Wasaidizi Wake au Wakala kwa Lengo la Ku win Trust

Kibatala: Sawa tumuache aendelee

Wakili wa Serikali: Kuna lingine Kwenye sms hapa ya Tarehe 22 July 2020, Meseji ya Saa 12 na Dakika 27 Ulinukuliwa hapa Ukisema Kwamba Ikiwezekana uwe unanitumia Fedha ya kuwa Mobilise, Ulimaanisha nini?

Shahidi: Nilikuwa namaanisha Kwamba anitumie Pesa ya Kuwa Mobilise huko Walipo, niwafanyie Vetting Kwa ajili ya Kuja Kufanya Jukumu lao..

Wakili wa Serikali: Kuna Swala Umeulizwa hapo Kuhusiana na Fedha, Ka Ulitumiwa kuwa siyo za Kigaidi au Ugaidi na wewe Ukaafiki siyo kwa ajili ya Ugaidi.

Shahidi: Nilikuwa namaanisha Kwamba Pesa zilitumwa Kwa Malengo ya Ugaidi, ila Wapokeajoli walikuwa hawajui Kuwa walikuwa wa napokea kwa ajili ya Matukio ya Ugaidi.

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Hapa, Ukasema hukushangaa Kusikia Khalfani Bwire amekamatwa, Ulikuwa Umemaanisha nini

Shahidi: Kwa sababu nliwaambia Mnaenda Kufanya Kazi ILA Matukio Ya Uhalifu Mniambie, Wao wakanyamaza, Baadae Khalfani Bwire akaniambia Bro nimekengeuka Wale Madogo Wapo Ground, Ndiyo Maana Siku shangaa kwa sababu Taarifa alinipa too late Ikiwa Wameshaingia Kwenye Uhalifu. Nisingeweza Kukutana na Mtu Siku ya Kwanza alafu nimpe Details zangu zote, Ni swala la Kiusalama

Wakili wa Serikali: Umeulizwa tena Swala lingine hapa Kwamba Wale Watu (Washtakiwa) Waende Wakafanye Kazi ya Ulinzi Waambatane naye Kuchukua Dola, Ulikuwa Unamaanisha Nini?

Shahidi: Nilikuwa namaanisha Kwamba Freeman Mbowe alikuwa anatafuta watu Kwa ajili ya Kuchua Dola, Katika Kuchukua Dola huko alikuwa anataka Experts Katika Kuchukua Dola huko kwa ajili ya Kukata Miti na Kulipua Vituo Vya Mafuta.

Wakili wa Serikali: Ulionyeshwa Hapa Maelezo ambayo Uliyaandika Ukiwa Polisi, Kuna Maeneo ambayo katika Maelezo Umezungumza Kifupi ila hapa Umezungumza Kirefu, Kwanini imetokea.

Shahidi: Kwa Sababu aliyekuwa anaandika siyo Maneno Yote alikuwa anaandika hapa Naongea Sababu nipo Free, Kwa hiyo siyo Maneno Yote Kaandika Mle.

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Huyo Ndiye Shahidi tukiyekuwa naye kwa Leo na hatuna Shahidi Mwingine, Hivyo tunaomba hairisho la. Siku 2 kwa Maana ya Tarehe 2 na Tarehe 3 ili tuweze Kuendelea Ijumaa Tarehe 4 Ndipo tutakuwa Tume Procure Shahidi Mwingine.

Kwa sababu Shahidi ambaye tulipanga baada ya Shahidi huyu hakuwezi Kufika Kwa sababu Ya Sababu zilizo Nje ya Uwezo Wetu hivyo Katika Mazingira Hayo na ili Kupata Uhakika Wa Kuendelea Ijumaa, Tunaomba Hairisho Ili hata kama kama tukishindwa tuweze Kupata Shahidi Mwingine.

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Sisi kwa kweli bila tunakosewa sana na hawa Wenzetu Hatuoni sababu ya airisho.. Kwenye Commital Bundle Wameorodhesha Mashahidi Wengi sana, Inawezekana Vipi Kukosa Mashahidi?

Kama nilivyosema Mwanzo, Kwamba Wateja Wetu Wana Haki ya Kujua Hatima yao, Tunatamani Kesi iendelee leo. Tunapinga Kuhairisha kesi, Tunaomba Mahakama Iwaelekeze Walete Mashahidi. Ukizingatia Wengine Address (anuani) zao ni Dar es Salaam.

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Tumesikia Hoja ya Kupinga airisho Kutoka Kwa Wenzetu ila tunaona Kwamba wamekuwa too emotional Kuliko Kuleta Hoja za Kisheria. Kuita Mashahidi Kuna Masuala Mengi Sana, Si Jambo Rahisi na Mengine hatuwezi Kuyasema hapa. Ukiangalia Shahidi huyu ameanza Kuwa Cross Examined Kuanzia Alhamisi.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji hii ni Rejoinder au Hoja Mpya, ajibu Hoja zetu,

Jaji: Nisaidie kijibu Hoja ya Siku Mbili, Wao wanasema kwamba Waje Kesho, Je tu assume Mpaka Kesho Kutwa huwezi Kupata Shahidi.

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Naweza Kusema Alhamisi tukaja Kupoteza Resources hapa, Mheshimiwa Jaji Naomba hata KAMA Kuna alternative iwe Ijumaa basi.

- Jaji anaandika Kidogo

Mahakama ipo Kimyaaaa

Jaji: Katika Kutolea Uamuzi Wa hoja Ya airisho, Kuhusu Kuhairisha Mpaka Tarehe 04, Nafahamu Kwamba ipo Sheria ainayowabana Upande wa Mashtaka katika kuleta Mashahidi.. Lakini Upande wa Mashtaka Wemetoa Hoja ambayo inawalizimu Kuleta Mashahidi Tarehe 04. Upande wa Utetezi Hoja yao Kuwa Shauri Lipo katika Mode ya Speed Trial, Na Kwamba ni Shauri ambalo linatakiwa kuisha Haraka.. Lakini Mahakama Inaona ni Busara hata Kama ikilazimisha Kama Mashahidi hawapo Mahakama haitoweza Kuendelea.

Kwa sababu hiyo naairisha Mahakama Mpaka Ijumaa Tarehe 4 February 2022. Washitakiwa wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Mpaka hiyo Ijumaa.

07:00 Koooooooorti Jaji anatoka

- Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio amaliza ushahisi wake, kesi kuendelea tarehe 04/02/2022 -
HII HAJAKUWA EDITED WALA HAINA UCHADEMA

Kidando: Shauri linakuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi kwa shahidi kuhojiwa na upande wa utetezi nasi tupo tayari

Jaji: Upande wa utetezi?

Kibatala: Nasi tupo tayari Mheshimiwa jaji

Kibatala: Shahidi habari za tangu Jana

Shahidi: Nzuri

Kibatala:Uliwahi kufahamishwa kuwa kuliwahi kufanyika kesi ndogo mbili ndani ya kesi kubwa ya msingi?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Adamu na Lingw'enya walisema wewe ulikuwa ni sehemu ya watu waliokamatwa, ni sahihi?

Soma zaidi: Kibatala amng’ang’ania Luteni Urio kesi ya kina Mbowe

Shahidi: Nasikia kutoka kwako.

Kibatala: Uliwahi kukutana na mawakili wa Serikali ikiwemo Mr Kidando kabla ya kuja kutoa ushahidi mahakamani hapa?

Shahidi: Kwa maelekezo niliambiwa nieenda kuripoti kwa DCI ndio nikaletwa hapa.

Kibatala: Kwa maelekezo yako hujasema kama uliwahi kukamatwa na maafisa wa Polisi hasa Jumanne Malangahe na Goodluck?

Shahidi: Sasa nitasemaje wakati sijakamatwa?

Kibalata: Relax shahidi

Kibatala: Katika ushahidi wako hujawahi kusema kuwa hujawahi kutifikishwa kituo cha Polisi cha Tazara tarehe 8 au 9 ya mwezi wa Saba, mwaka 2020?

Shahidi: Sijawahi kufikishwa

Kibatala: Pia hujawahi kusema Kama ulifikishwa kituo cha Polisi Mbweni katika tarehe hiyo.

Shahidi: Sijawahi kufikishwa kituo chochote cha Polisi, narudia tena mimi sijawahi kufika kituo chochote cha Polisi Mbweni

Kibatala: Wewe una ugomvi na Adamoo na? Lingw'enya?

Shahadi: Sijawahi kuwa na ugomvi nao.

Shahidi: Narudia tena sijawahi kufikishwa kituo cha Polisi Mbweni, mbona unaniwekea maneno mdomoni?

Kibatala: Shahidi usikasirike

Kibataka: Unafahamu sababu ya mimi kukuuuliza maswali kuhusu wapi unasali na paroko wako ni nani?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Sasa baada ya kukamatwa Adamo na Lingw'enya na kuteswa walipohojiwa walikutaja kuwa wewe ndio uliwaunganisha kwa Mbowe na wewe ulikamatwa ni sahihi?

Shahidi: Sijawahi kukamatwa

Kibatala: Katika ushahidi wako ulimtaja komando aitwaye Gabriel Mhina?

Shahidi: Sifahamu

Kibataka: Una ugomvi na watu niliyokutajia?

Shahidi: Sina ugomvi nao

Kibatala: Afande Kingai aliwahi kukuambia kuwa kuna komando wengine walikamatwa?

Shahidi: Hajawahi kuniambia

Kibatala: Ex- Komando Halid alimuuliza Bwire nani aliyekuunganisha katika kazi hii ya ulinzi? Akasema ni wewe ni sahihi?

Shahidi: Halid ni nani? Mimi simfahamu Halid na wala hapa katika ushahidi wangu sijamtaja

Kibatala: Huyo halidi pia, baada ya kukutafuta kwenye mtandao wa Facebook, ulimwambia utamuunganisha na kazi ya ulinzi migodini, ni sahihi?

Shahadi: Simfahamu Halidi wala sina Access huko migodini

Kibatala: Unamfahamu baba yako mdogo mzee John Urio?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu mke wako ndio aliyefanya juhudi za kuitoa gari yako Rav4 rangi ya silver pale kwenye parking na kwenda kuipark Kihonda ni Sahihi? Kwa sababu wewe mpaka sasa upo chini ya ulinzi, ni sahihi?

Shahidi: Sio sahihi? Gari haijawahi kuzuiliwa na hata nakuja hapa kutoa ushahidi gari nilipaki.

Kibatala:Tukitaka kuangalia upo kwenye active duties kwenye Military Service tunatakiwa kuangalia nyaraka zipi?

Shahidi: Ni kuangalia identity card na kuhakiki kwa mwajiri wake.

Kibatala:Ni kweli ili kudhibitisha kuwa wewe hujafukuzwa kazi unatakiwa kuangalia duties Roster?

Shahidi: Ni kweli

Kibatala: Kama tunafikiria kuiomba ahirisho kwa Mahakama kwa ajili ya kukupa nafasi ya kufuatilia nyaraka ya udhibitisho kuwa wewe upo kazini, unaweza kufahamu mchakato huo utachukua siku ngapi? Ili upate nyaraka hiyo?

Shahidi: Sijui itachukua muda gani.

Kibatala: Ni sahihi mtoto wako mdogo Jackson wakati anazaliwa wewe ulikuwa mafichoni umefichwa?

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Pius Hilla ananyanyuka na kumueleza Jaji kuwa suala la mtoto, lisiwekwa kwenye rekodi kwa sababu hajalitolea ushahidi.

Jaji: Sawa

Shahidi: Hili swali nimeshakujibu wakili halafu wewe ni wakili msomi....Sasa sitaki uniulize tena? Sawa? Wewe ni wakili msomi? Alaah

Mahakama: Kichekoo hahaha hahaha hahaha

Kibatala: Shahidi hebu Relax basi

Shahidi: Mimi nimelax

Kibatala: Ni kweli shahidi hata mama yako mzazi ilibidi aje kukuona ukiwa kizuizini?

Shahidi: Narudia tena sijawahi kuwekwa kizuizini.

Kibatala: Ni kweli au sio kweli kwa kuwa upo kizuizini kwa sasa unasindikizwa na maofisa usalama wenye silaha?

Shahidi: Kwanza naomba uondoe neno kizuizi kwa sababu unanichafulia...mimi sijawahi kuletwa na maofisa usalama wenye silaha.


Shahidi: Mimi nakuja na mawakili wangu (wa upande wa mashtaka) ambao hunipitia hotelini na magari yao.

Kibatala: Kwa magari ya Serikali? Usinitajie namba zake kwa sababu ni masuala ya kiusalama.

Shahidi: Labda unipe task nikayakague

Kibataka: Hivi hizo dhana mbili zinaoana kweli?

Shahidi: Dhana zipi?

Soma zaidi:Luteni Urio: Sikuona umuhimu kurekodi mazungumzo yangu na Mbowe

Kibatala: Ulisema uliripoti kwa DCI ndio ukaletwa hapa mahakamani na leo umetueleza kuwa unapitiwa na mawakili wako kuletwa hapa mahakamani.

Shahidi: Hujanielewa ...siku ya kwanza nililipoti kwa DCI na baada ya hapo nikawa nachukuliwa na mawakili wa Serikali kuletwa mahakamani.

Kibatala: Shahidi Ndio utaratibu wako wa kila siku unapitiwa na mawakili wako?

Shahidi: Ndio wenyeji wangu.

Kibatala: Okay

Shahidi: Karibu

Kibatala: Unafahamu DCI, IGP na wengine wamehamia Dodoma?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Sasa unafahamu kwa sababu ofisi mama ya DCI imehamia Dodoma?.

Shahidi: Siwezi kuzungumzia ofisi ya DCI

Kibataka: Shahidi unafahamu kitu kiitwacho Civico?

Shahidi Nafahamu.

Kibatala: Cimico ni Civic and Military Coordination?

Shahidi: Ndio,

Kibatala: Hii maana yake ni mahusiano ya kubadilishana taarifa kati ya taasisi za Jeshi na jamii.

Shahidi: Ni sahihi.

Kibatala: Unafahamu Presence Patrol?

Shahidi: Nafahamu.

Kibatala: Shahidi ni sahihi zimeshawahi kufanyika Presence Patrol hapa Tanzania inapofanyika uchaguzi au kunapotokea matukio tata?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Shahidi limetoka tishio la kuripua madaraja makubwa hapa nchini, ni kweli Jeshi letu haliwezi kufanya Presence Patrol?

Shahidi: Sijaelewa unaenda wapi.

Kibatala: Nisikilize swali langu.

Shahidi: Nimelielewa swali.

Kibatala: Shahidi nakuuliza spry ya sumu, je Uliwahi kuiongelea katika ushahidi wako?

Shahidi: Sijasema...halafu usinilishe maneno mdomo..vipi wewe rafiki yangu bwanaa...hebu relax

Kibatala: Una mfahamu Bwire.

Shahidi: Namfahamu.

Kibatala: Unafahamu jukumu la Bwire lilikuwa ni kwenda kumlinda Tundu Lissu?

Shahidi: Hata raisi mwenyewe halindwi na Komando.

Kibatala: Unafahamu Tundu Lissu Kama mgombea urais alitaka mlinzi Maalum kwa kuwa alishashambuliwa na risasi?

Shahidi: Kila mgombea anapewa mlinzi

Kibatala: Unafahamu mgombea urais anapewa walinzi wangapi?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Unafahamu Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi kwenye viwanja vya bunge ?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Unafahamu hadi leo Jeshi la Polisi halijakama mtu hata mmoja, alihusika na kumshambulia Lissu.

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Ni kosa mtu kujiimalisha kwa kuwa na walinzi wake?

Shahidi: Sio kosa

Kibatala: Unafahamu Ben Sanane alikuwa ni msaidizi binafsi wa Mbowe amepotea na hajajulika alipo hadi leo?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Kwa mujibu wa kanuni za Jeshi na miongozo ya jeshi,ofisa wa Jeshi anaruhusiwa kuwa na mahusiano na kiongozi wa chama cha upinzani? Ni kosa au sio kweli?

Shahidi: Si kosa kama ni mahusiano ya Kawaida lakini sio ya siasa.

Kibatala: Ulimfahamu ama hufahamu ...moja wapo ya majukumu ya Bwire na Lingw'enya ni kumsindikiza Mbowe kwenye mikutano yake ya kisiasa ikiwemo ule uliofanyika ukumbi wa kanisa Katoliki.

Shahidi: Sifahamu, nachojua walienda kutekeleza uhalifu.

Kibatala: Unafahamu Julai 26, 2020 Adamoo na Lingw'enya siku hiyo walipanda magari ya Chadema yenye nembo za M4C kwenda kwenye mikutano?

Shahidi: Walishawishiwa kuingia katika uhalifu na kukataa mawasiliano na mimi.

Kibatala: Kabla ya kukataa mawasiliano baina ya Adamoo na Lingw'enya, hukuwauliza?

Shahidi: Waliniambia wanataka kuajiliwa.

Soma zaidi: Shahidi muhimu kuhojiwa siku ya tatu kesi ya kina Mbowe

Kibatala: Big answer

Shahidi: Ndio ulikuwa unataka hilo.

Mahakama: Kicheko.

Kibatala: Shahidi ulipoongea na Mbowe alijicommit akisema anapanga kushiriki uchaguzi?

Shahidi: Alisema chama changu kimejipanga kuchukua dola

Shahidi: Alisema chama changu kimejipanga kuchukua dola kwa njia yoyote.

Kibatala: Unafahamu chama cha Chadema kilisimamisha wagombea katika ngazi zote?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Unafahamu alifanya kampeni?

Shahidi: Sikufuatilia sana.

Kibatala: Hata kama ulifuatilia kwa mbali ulijua?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu zile pesa ulizotumiwa na Mbowe zilikuwa ni za Mbowe au za chama?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Unafahamu jukumu la kutafuta walinzi ni jukumu lililoidhinishwa na chama?

Shahidi: Sifahamu.

Soma zaidi:Luteni Urio asoma mawasiliano yake na Mbowe mahakamani

Kibatala: Mtu alishtakiwa discharge ana mipaka ya kufanya kazi?

Shahidi: Ili mradi afuate sheria.

Kibatala: Unafahamu hata kina Diamond Platinum ana bordguard?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Shahidi naomba utusaidie kwanini ulichagua kukutana na Moses Lijenje eneo la Morogoro na sio sehemu nyingine?

Shahidi: Kwa sababu ndio center

Kibatala: Center ya Nini?

Shahidi: kwa sababu ndio sehemu ya karibu.

Kibatala: Uliwahi kufahamu Mbowe alisafiri nje ya nchi?



Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unamfahamu Godless Lema?

Shahidi: Namsikia

Kibatala: Unafahamu Lema anaishi uhamishoni kwa sababu ya matishio ya maisha ya usalama wake?

Shahidi: Sijui Kama anaiishi uhamishoni kwa sababu ya matishio ya maisha yake.

Kibatala: Unafahamu Kama Tundu Lissu anaishi uhamishoni kwa sababu ya matishio ya usalama wa maisha yake?

Shahidi: Sijui kama ni uhamishoni au amekwenda kitalii.

Soma zaidi: Urio aeleza alivyomtafutia Mbowe makomandoo na kuahidiwa cheo

Kibatala: Unafahamu kama hawa vijana wasingekamatwa, Lissu asingeondoka hapa nchini?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu kama hawa vijana wasingekamatwa, Lema asingeondoka hapa nchini?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba kuishia hapa...yangu ni hayo tu.

Kibatala amemaliza kumhoji Luteni Urio na sasa upande wa mashtaka wanatakiwa kumfanyia re- examination ( mawakili wa Serikali kumuuliza shahidi kwa ajili ya kupata ufafanuzi kuhusiana na ushahidi alioutoa wakati anahojiwa na mawakili wa upande wa utetezi).

Wakili Chavula: Hebu ifafanulie mahakama ni Kwanini ulimwambia Freeman Mbowe atumie wakala au msaidizi wake kutuma pesa bada ya kutumia namba yake ini salama zaidi

Shahidi: Nilimwambia atumie Wakala au msaidizi wake ili niweze kuwini Trust.

Wakili: Kuna swali uliulizwa kuhusu kukamatwa kwa kina Bwire ukasema hukushangaa ulivyosikia wamekamatwa.

Shahidi: Sikushangaa kwa sababu walinipa taarifa wakiwa wameshapanga.

Wakili: Licha ya wewe kuwa na cheo na kumwambia Freeman Mbowe kuwa huna cheo hebu ifafanulie mahakama kwanini ulisema jibu hilo wewe ulikuwa mkweli.

Shahidi: Kwa mara ya kwanza ndio nakutana na Freeman Mbowe anataka kujua cheo changu nilimjibu hivyo kwa ajili ya usalama.

Wakili: Ulisikika uliieleza mahakama ukisema uliwaambia washtakiwa wakafanye kazi ya ulinzi na kuambatana nae katika kuchukua dola ulikuwa unamaanisha nini

Shahidi: Dhumuni kubwa la Mbowe kuwahitaji hao watu ilikuwa ni kwa ajili ya kukata miti, kuchoma vituo vya mafuta pamoja na kumdhuru viongozi.

Wakili Chavula:Mheshimiwa Jaji ni hayo tu.



Wakili Kidando: Mheshimiwa Jaji hatuna shahidi mwingine kwa leo tunaomba ahirisho la siku mbili Shahidi tuliyekuwa tunategemea hadi jana tulikuwa hatujampata alikuwa kasafiri.

Katika mazingira hayo hata kama tutakuwa hatujampata tutaendelea na Shahidi mwingine.

Ni hayo tu.

Wakili Kibatala: Bila kuwakosea wenzetu hatujaona sababu ya kuahirisha katika mashahidi kadhaa waliotajwa hata kibinadamu yenyewe tunaomba wenzetu kesho walete Shahidi kwa kuwa tumebrek mapema muda wa kumuandaa upo.

Wakili Kidando: Tumewasikia wenzetu kuita mashahidi hata kama ni wengi kiasi gani inacost kusubiri na wengine hawapo Dar es Salaam.

Jaji: Tujikite hiyo hoja ya siku mbili hao wamesema kwa nini iwe hadi Ijumaa.
Jifunze namna ya kuanzisha thread kijana naona threads zako mods wanazifuta kwakuwa unaandika ujinga ujinga mwingi.
ACHA UMBEYA
 
Yes. Kibatala hakutaka kuingia sana ndani. Labda sheria hairuhusu kuhoji sana private issues. Lakini kaweka foundation ambayo anaweza baadaye akaleta ushahidi wa kumbana zaidi Urio.
Itakuwa lini sasa hapo maana Urio kesha maliza
 
Huyu shahidi anatupa tabu sana akina sisi tusokuwa na uelewa wowote....yaan kuwa Freemn alitaka kuchukua nchi kwa kukata miti 🤭🤭🤭 na hiyo ndo huitwa terrorism..kheee! Haya mambo yangefanyw kule vijijn na raia wakigombea shamba ingetia sense. Lkn kwa wakubwa kabsa wa nchi aaah cyooo!! Ilitupasa hata ss kuwa tunatawaliwa,tena na waarabu mizee ya kutufunga minyororo😂😂😂😂😂😂😂😂😂labda tungetia akil kichwan
Screenshot_20220201-184825~2.png
 
Kama wewe ni mtaalam kweli, na naomba niamini wewe ni Mtaalam, huwezi kusuggest Key Witness aulizwe maswali mawili matatu wakati upande wa mashtaka ulimleta kama silaha ya maangamizi. Sijaona swali jepesi Kati ya maswali aliyoulizwa labda Yale yaliyolenga kumtoa Shahidi relini kama lile la kuletewa Mtoto wake akiwa mahabusu na yeye akaprovoke na kuuliza "Who are you by the way?" Swali kama ulionana na DCI tarehe ngapi hulioni umuhimu wake wakati mashahidi wote wameshindwa kulijibu? Swali ulionana na DCI wapi hulioni uzito wake wakati unajua Wazi 2020 ofisi zote zilishahamia Dodoma? Swali umetokea wapi kuja hapa na yeye kujieleza kwamba anachukuliwa na Mawakili kuletwa mahakamani huoni uzito wake?
Nimesema awali kama humpendi Mtu siyo tiketi ya kudharau kazi yake. Nakuhakikishia Kidando na wenzake wanajua ndo maana Re-examination ilikuwa fupi baada ya kuona ufafanuzi anaoutoa unaharibu zaidi.
Kama kawaida ya watanzania

Ukiishiwa hoja unabakia kulilia kuchukiwa.

Nani ana chuki na wakili wa upande wa utetezi.

Anyways ngoja nijikalie kimya hapa maana kuna watu hawataki kukosolewa .

Hakuna mtu perfect kila mtu anakosea hata mimi nakosea.

So unapokosolewa angalia hoja inayotumika kukukosoa kuifanyia kazi.
 
Wakili wa Serikali: Ulionyeshwa Hapa Maelezo ambayo Uliyaandika Ukiwa Polisi, Kuna Maeneo ambayo katika Maelezo Umezungumza Kifupi ila hapa Umezungumza Kirefu, Kwanini imetokea.

Shahidi: Kwa Sababu aliyekuwa anaandika siyo Maneno Yote alikuwa anaandika hapa Naongea Sababu nipo Free, Kwa hiyo siyo Maneno Yote Kaandika Mle.

Mawakili wa Serikali Wanateta Kwa Chini chini

Maswali Yamesimama hapa kwa muda

Mawakili wa kiserikali Wanamuomba Jaji Samahani Kidogo Asubirie, wanajadiliana.

Wakili wa Serikali Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji sisi hatuna Maswali sanaaaa, Nafikiri Yanatosha. 😀😀😀😀
 
Jibu la mwisho la shahidi wa 12 wa Jamhuri. Luteni Denis Urio leo wakati
wa Re-examination akifanyiwa n wakili
wa serikali. Jibu limefanya maswali yakaishia hapo. Maana yake ni kwamba, Urio alitoa maelezo yake ya onyo akiwa chini ya ulinzi. Leo alikuwa free. kashikiliwa mateka?


WS: Ulionyeshwa Hapa Maelezo
ambayo Uliyaandika Ukiwa Polisi, Kuna Maeneo ambayo katika Maelezo Umezungumza Kifupi ila hapa Umezungumza Kirefu, Kwanini imetokea

Shahidi: Kwa Sababu aliyekuwa anaandika siyo Maneno Yote alikuwa anaandika hapa Naongea Sababu nipo Free, Kwa hiyo siyo Maneno Yote
Kaandika Mle.
 
Huyu Shahidi wa leo ndio alikuwa Shahidi Tegemeo Namba 1 wa Jamuhuri maana Kwa mujibu wa hii kesi yeye ndio alianzish hii kesi lakini kajichanganya sana kwasababu kalishwa

Shahidi wa 12 wa Jamhuri, ambaye
ndiye mtoa taarifa, Luteni Denis Urio
anasema wakati anatoa taarifa kwa DCI
alimueleza Mbowe alikula njama za
ugaidi kati ya 1-10 July 2020 lakini hati
ya mashtaka wameandika matukio hayo
yalitokea 1 May 2020. Hii kesi ina ujinga
na uonevu sana.

Kibatala: Wakati Unatoa Taarifa
ulimwambia Kuwa Matukio yalitokea
tarehe ngapi ya Wewe na Mbowe
Shahidi: Kati ya Tarehe 1 July mpaka
Tarehe 10

Kibatala: Sasa Kwenye Hati Ya Mashtaka
Wenzetu wameandika Tarehe 1 May,
hujamwambia Wewe

Shahidi: Sijasema hivyo mimi
 
Wakili wa Serikali: Ulionyeshwa Hapa Maelezo ambayo Uliyaandika Ukiwa Polisi, Kuna Maeneo ambayo katika Maelezo Umezungumza Kifupi ila hapa Umezungumza Kirefu, Kwanini imetokea.

Shahidi: Kwa Sababu aliyekuwa anaandika siyo Maneno Yote alikuwa anaandika hapa Naongea Sababu nipo Free, Kwa hiyo siyo Maneno Yote Kaandika Mle.

Mawakili wa Serikali Wanateta Kwa Chini chini

Maswali Yamesimama hapa kwa muda

Mawakili wa kiserikali Wanamuomba Jaji Samahani Kidogo Asubirie, wanajadiliana.

Wakili wa Serikali Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji sisi hatuna Maswali sanaaaa, Nafikiri Yanatosha. 😀😀😀😀
ina maana Urio ni mateka aliyeteseka siku nyingi... wameona mengi yatafichuka heri waustiri utupu wao japo kwa manyasi!!
 
Uzi umeingiliwa na vijana wasio na ustarabu,ni mwendo wa lugha mbovu tu
Hao si suala la ustaarabu Tena. Ni wajinga ambao wameadvance na kuwa wapumbavu wa viwango vya juu.

It's aju nini na mtu km Comte, sijui Elitwege, mwingine anajiita mjinga mimi lkn hajui tyari ni mpumbavu.

Ni majitu tu ya hovyo hovyo yasiyo na tija kwa jamii wala familia zao.
 
"Hapa naongea niko free"

Halafu akiambiwa aliteswa kituo cha polisi ni kina Adamoo anakataa, sasa kitu gani kilichomfanya asiwe free wakati anatoa maelezo yake mwanzoya kama sio alitishwa?

Ameshaambiwa truth shall set him free, lakini namuona bado anajipotezea muda tu wa kuwa huru.
 
Back
Top Bottom