Uchaguzi 2020 Yaliyojiri katika Ufunguzi wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) - Uwanja wa Jamhuri, Dodoma (Agosti 29, 2020)

Na mtaji wa chadema mbona jana hatujauona. Unaambiwa nyomi la zarkiem mpaka kamanda lissu kasahau sera
Screenshot_20200829_070343.jpg
 
Lengo ni kujaza bila kujali wamejaa jaa vipi. Wakishajaa watasikiliza na huwezi sema ushindi si halali wakati mikutano ilijaa. Watanzania kama wamechoka na hawaitaki basi wasiende bila kujali watakachokosa. Wakijaa bila kujali njia iliyotumika basi wimbo ule ule tuliouzoea unaweza kurudiwa 2020.
Wakijaa kwa Lissu oooh! wamekuja kumwangalia tuu wakijaa kwa Magufuli hao ndio wapiga kura!
 
Kama ni kodi zetu, imekuwaje deni la taifa limepanda kwa 15t+ ndani ya hii miaka mitano tu. Miradi ya SGR & SG, inakadiriwa itagharimu 15t, lakini yote miwili haijala 7t mpaka sasa. Ndege ni 2t, kadirio ni 9t. Vituo vya afya nchi nzima havifiki 500b, madaraja yote makubwa Busisi nk hayavuki1.5. ukiangalia hiyo ni 11t, elimu bure mpaka kufikia sasa ndani ya hii miaka mitano ni kama1t. 3t ni mengineyo. Sasa hela yetu hapo ni ipi?
Ni upigaji mtupu ile 10% inatumaliza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna dawa hapa. Anazidi kuwaudhi wapiga kura. Hakuna atakaye mchagua huyu.
Atuambie
Gwanda yuko wapi?
Saa 8 yuko wapi?
Nani alimpiga risasi Lisu?
Kwannaliyemtoleea Nape bunduki hajakqmtwa?
Watu wamepotea na matukio yapo mengi tokea kuumbwa kwa Dunia, tena isijekua mlifanya haya yote kama mlivyochoma ofisi zenu
 
Madaraja yanamsaidia hata mama yako kuvula ili aende kuuza ndizi zake.
Kwahiyo kabla ya madaraja ya magufuli alikua hauzi ndizi?
Saaizi watu wamekua masikini zaidi hata hizo ndizi haziuziki tena
 
Leo chama tawala (CCM) kinafungua kampeni zake uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kuomba ridhaa ya wananchi kurejea kwenye utawala baada ya ngwe ya kwanza ya miaka mitano ya serikali ya awamu ya tano kuisha.



Dkt. John Magufuli Rais anayemaliza awamu yake ya kwanza amepewa ridhaa ya chama hicho kukiwakilisha kuwania ngazi ya Urais kwa mara nyingine huku makamu Rais akiwa Samia Suluhu Hassan.

Kuwa nami nikujuze yatakayojiri kwenye viwanja vya Jamhuri na viunga vya mji wa Dodoma kwenye siku ya leo.

========

11:10 Asubuhi: Viongozi mbalimbali wameshafika viwanja vya Jamhuri akiwemo Rais mstaafu wa awamu ya nne na mwenyekiti mstaafu wa CCM, Jakaya Mrisho Kikwete. Pia amefika Mgombea Urais Zanzibar kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi, Hussein Mwinyi. Mjumbe wa kamati kuu na waziri mkuu, Kassim Majaliwa. Makamu mwenyekiti mstaafu, Pius Msekwa. Mjumbe wa kamati kuu na spika wa Bunge, Job Ndugai.

Sasa anaingia Edward Lowassa na anasalimiana kwa bashasha na Rais mstaafu, Jakaya Kiwete. Pia yumo Mizengo Pinda na mama Samia Suluhu Hassan.

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi na mgombea Urais kupitia chama cha Mapinduzi, John Magufuli amewasili uwanja wa Jamhuri.

Sasa anaongea katibu mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally na anaanza kwa kuwataja wageni waliohudhuria mkutano wa leo wa Ufunguzi wa kampeni.

Bashiru: Kabla ya leo, Wamachinga walileta mchango wa shilingi milioni tano kwa ajili ya mafuta ya kampeni na wako hapa wameshanikabidhi kwa sababu ya Ratiba naomba upokee kwa naiba yao mbele ya hadhara hii.

Pia nnao mchango wa wauza ndizi nilipozaliwa, ambao tulioza wote ndizi miaka ya 90 kutoka Bukoba kwenda Mwanza, wamechanga shilingi milioni moja kama shukrani ya kazi tuliyowahi kufanya ya kuwarahisishia kazi ya kusafirisha ndizi kwa bei nafuu.

Hadhara hii unayoiona inaonyesha moyo wa kujitolea na wengi wameanza kuingia hapa saa 12 na wakati tunachukua fomu ilianza kuingia michango ua kukuunga mkono, tumepokea jumla ya milioni 110 kutoka kwa wapenzi wa CCM na wanachama nchi nzima.

MAELEZO MAFUPI YA MAUDHUI YA ILANI YA CCM
Bashiru:
Ilani ya uchaguzi 2020 ina kurasa zaidi ya 300 ikibainisha tulivyotekeleza ilani ama ahadi za uchaguzi wa 2015 na mafanikio makubwa tuliyoyapata lakini pia tukitoa ahadi mpya kwa miaka mingine mitano ijayo na inapatikana kwenye tovuti ya chama na katika ofisi zetu za mikoa na tutaendelea kuinadi. Nitatumia muda mchache kutoa muhtasari kwa ufupi tuendane na ratiba.

CCM kimejengwa kwenye misingi ya ujama na kujitegemea na imeimarishwa chini ya uongozi wako, CCM inaahidi itaendelea kusimamia serikali zake kuhakikisha misingi hii inalindwa.

Kupitia uongozi wako mwenyekiti, CCM kimekuwa chama cha kutoa matumaini mapya kwa watanzania hasa vijana na kinamama. Hivi sasa chama chetu kinaaminika zaidi kama unavyoona kwa sababu tukiahidi tunatekeleza.

Sisi ni chama cha ahadi na kutekeleza ndio maana kauli mbiu ya ya ilani yetu mwaka huu inasema tumetekeleza kwa kishindo na tunasonga mbele pamoja. Katika miaka mitano ijayo, CCM itahahakisha Tanzania inaendelea kulinda uhuru wake, kudumisha mapinduzi matukufu ya Zanzibar na kuimarisha muungano wetu wa serikali mbili.

Hussein Mwinyi: Ndugu zangu tuhakikishe tunailinda amani tuliyokuwa nayo, bila amani hakuna maendeleo. Vipo viashiria vilivyoanza kujitokeza kutokana na kauli zinazotolewa na baadhi ya watu.

Tusikubali kupelekwa katika jambo lolote litakalohatarisha amani ya nchi yetu, leo tuko hapa tunafanya kazi za maendeleo, tuinafanya ibada zetu ni kwa sababu ya amani tuliyokuwa nayo. Amani ya nchi inaletwa na wananchi wake.

Bashiru: Taarifa ya tume ya Taifa ya uchaguzi ya Ijumaa Tarehe 28, chama cha Mapinduzi kinao kibindoni wabunge 18 wateule, kwa furaha niliyonayo kuhusu matokeo ya mitambo ya ushindi niwatambulishe kwa kuwasoma majina ili ujumbe huu ufike na wewe kama daktari uliowaandalia wale tunaoshindana nao iingie Barabara.

Tunazo kata kibindoni za wagombea wa CCM zaidi ya 400 nchi nzima. Mitambo ya ushindi imeanza kufanya kazi na moto uliowashwa atakaebabuka tusilaumiane.

Kibajaji: Mimi nina mambo machache ya kuzungumza mbele ya hadhara hii, jambo la kwanza tunamshukuru sana Mungu kwa ajili ya maisha yako na kwa sisi wakristo, Biblia inasema ukimaliza kazi utavishwa Taji na mwaka huu tunaenda kukuvisha taji la ushindi ambalo hujawahi pata katika mkoa huu.

View attachment 1551789

Ndugai: Nakukishukuru chama changu kwa kuniamini kusamama nafasi ya mbunge Kongwa bila kuwasahau wajume maana mnajua mwaka huu walifananaje.

Wanadodoma tunayo kila sababu ya kumchagua Magufuli, kubwa zaidi ni mwenzetu, ni miongoni mwetu anaishi nasi hapa Dodoma. Sasa nani huwa anaacha wa nyumbani alafu anakwenda ugenini?

Kampeni yetu ya safari hii iwe ya Rais na iwe ya nyumba kwa nyumba, tumeelewana? Hapa Dodoma kaya kwa kaya.

Kama spika nina mawili ya kusema, katika demokrasia ya kibunge suala sio ujuzi wa kusema bungeni au ujuzi wa kupanga hoja. Ni muhimu lakini si muhimu kihivyo.

Katika demokrasia ya kibunge, umuhimu ni uwezo wa kuamua mwisho wa siku. Ili tuwe na uezo wa kuamua ni muhimu sana wabunge wa CCM wakazidi theluthi mbili ya wabunge ili tuweze kuamua jambo lolote litakaloletwa bungeni na serikali yetu.

Na wale wengine lazima niwape ripoti, kazi yao ni kununa, kuzira, kazi yao ni kutoka nje bungeni. Sidhani kama wananchi wa Tanzania mnachagua watu kwenda bungeni au kwenda kutoka bungeni.

Pili mheshimiwa, mimi ndio muundaaji wa Bunge la kumi na mbili, nikuambie mapema kwamba maandalizi yetu ya bunge la 12 ambalo litakuwa la kisasa zaidikuliko la 11 yako zaidi ya asilimia 80, tuchague vizuri.

View attachment 1551657

Dkt. John Magufuli: Leo Dodoma imefurika, uwanja umejaa lakini hata kule nje nako kumejaa, hii inanipa changamoto kwamba mara nitakapochaguliwa kuwa Rais ni lazima nijenge uwanja mkubwa sana kuliko huu uliopo na hio ndio itakuwa kazi yangu ya kwanza ili wananchi wa Dodoma wakiingia kwenye uwanja wanatosha, Dodma ni jiji.

Mungu wetu anatupenda ndio maana Mataifa mengine hata mkiangalia kwenye TV Corona bado ipo, ila sisi kwetu Mungu amejibu maombi yetu, sisi tupo salama, Watoto wetu wanaenda shule, Wanamichezo wanacheza, Wasanii wanaendelea, Ibada na harusi zinafanyika.

Wananchi wengi wamejitokeza hii inadhihirisha kuwa CCM ni Baba lao na ni Mama lao na nikimaliza hotuba nabaki hapa niendelee kutazama burudani za wasanii na nitacheza kwelikweli maana leo ni siku ya furaha

Tumejitahidi sana kuimarisha nidhamu kwenye utumishi wa umma, tumejitahidi kupambana na rushwa, tumefungua jumla ya mashauri 2,256 ya rushwa ambapo serikali imeshinda mashauri 1013 kati ya mashauri 1926 yaliyoamuliwa na wengi waliofikishwa mahakamani na kuhukumiwa ni samaki wakubwa na sio dagaa.

Tumeimarisha usimamizi wa rasilimali za nchi yetu na kuhakikisha zinatumika kwa manufaa ya watanzania wote. Mtakumbuka tulizuia utoroshaji wa rasimali zetu ikiwemo mchanga wa madini.

View attachment 1551829

Magufuli: Mtakumbuka tulipoanza kuchukua hatua hizi, baadhi ya watu wakiwemo watanzania wenzetu ambao hivi sasa mnawajua walitubeza na kututisha kwamba tutashtakiwa na kufikishwa mahakamani lakini sisi tukasema rasilimali hizi ni zetu, tumepewa na mwenyezi Mungu ili tunufaike nazo hivyo hatuwezi kumuogopa mtu yeyote. Naamini wale waliotubeza sasa wameaibika.

Tumefanikiwa kupunguza matumizi ya serikali, tangu nimekuwa Rais nimetembelea nchi nane tu zote za Afrika. Najua baadhi ya watu wanadai kwamba kwa sababu ya mimi kutosafiri sana, uhusiano wetu kimataifa na ushawishi wetu wakidiplomasia umepungua, hiyo si kweli.
Lete picha
 
Naomba summary ya ilani ya ccm kwa maana nimesikia machache sana mfano kutengeneza ajira milioni8, ndege ya mizigo
 
Back
Top Bottom