Hii CCM inayofanya maongezi na balozi wa marekani bado ni Chama cha Mapinduzi?

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,425
7,213
Kwa kawaida mabalozi hawaingilii mambo ya ndani ya nchi wanapowakilisha. Bila shaka ndio taratibu. Mambo ya vyama vya siasa ni mambo ya ndani ya nchi husika. Lakinini utasikia balozi wa marekani kukutana na kiongozi wa upinzani kwenye nchi anawakilisha hasa hizi za kiafrika zenye msimamo wa kimapinduzi.

Au waziri wa marekani kwenye ziara nchi fulani kukutana na wapinzani. Wasijifanye ndio vinara wa demokrasia wakati ni vinara wa dhuluma na kuchunga maslahi yao tu. Hivi leo kinachoendelea palestina la ajabu hatujasikia kauli yoyote ya ccm au serikali yake.

Hakika kama mwanaccm sikupendezwa na uongozi huu wa kina nchimbi kinana na samia. Eti Nchimbi anamkaribisha balozi wa Marekani makao makuu ya CCM. Sijui chama cha mapinduzi wanaongea nini na vinara wa ubeberu na ukandamizaji duniani. Kwangu ni sawa na shetani kukaribishwa makao makuu ya CCM.

Tungeacha mahusiano kwenye ngazi ya serikali tu sio chama. Sidhani tunahitaji mahusiano ya karibu CCM na marekani. Huko wanakoenda huenda wengine tutahama chama maana kiitikadi tutatofautiana kabisa.

Huyo macho kumchuzi naona amewekwa kutimiza matakwa ya wamarekana kuiondoa ccm madarakani.

Demokrasia wanayotaka wamarekani ni ile ya kuwapa nafasi kutekeleza matakwa yao kuweka vibaraka wao kuongoza nchi zetu.
 
Hakika kama mwanaccm sikupendezwa na uongozi huu wa kina nchimbi kinana na samia. Eti Nchimbi anamkaribisha balozi wa Marekani makao makuu ya CCM. Sijui chama cha mapinduzi wanaongea nini na vinara wa ubeberu na ukandamizaji duniani. Kwangu ni sawa na shetani kukaribishwa makao makuu ya CCM.
Shetani kakaribishwa na wenzie
 
WaTz 2 waliuawa huko, hawatoi tamko la kulaani, wanaogopa kuchafua uhusiano na Waarab- watakosa "maokoto" ...nk
Yaani huku wanapeleka vibarua israel kutumika mashambani na huku wanauza bandari zetu uarabuni😂😂
 
Kwa kawaida mabalozi hawaingilii mambo ya ndani ya nchi wanapowakilisha. Bila shaka ndio taratibu. Mambo ya vyama vya siasa ni mambo ya ndani ya nchi husika. Lakinini utasikia balozi wa marakani kukutana na kiongozi wa upinzani kwenye nchi anawakilisha hasa hizi za kiafrika zenye msimamo wa kimapinduzi.

Au waziri wa marekani kwenye ziara nchi fulani kukutana na wapinzani. Wasijifanye ndio vinara wa demokrasia wakati ni vinara wa dhuluma na kuchunga maslahi yao tu. Hivi leo kinachoendelea palestina la ajabu hatujasikia kauli yoyote ya ccm au serikali yake.

Hakika kama mwanaccm sikupendezwa na uongozi huu wa kina nchimbi kinana na samia. Eti Nchimbi anamkaribisha balozi wa Marekani makao makuu ya CCM. Sijui chama cha mapinduzi wanaongea nini na vinara wa ubeberu na ukandamizaji duniani. Kwangu ni sawa na shetani kukaribishwa makao makuu ya CCM.

Tungeacha mahusiano kwenye ngazi ya serikali tu sio chama. Sidhani tunahitaji mahusiano ya karibu CCM na marekani. Huko wanakoenda huenda wengine tutahama chama maana kiitikadi tutatofautiana kabisa.

Huyo macho kumchuzi naona amewekwa kutimiza matakwa ya wamarekana kuiondoa ccm madarakani.

Demokrasia wanayotaka wamarekani ni ile ya kuwapa nafasi kutekeleza matakwa yao kuweka vibaraka wao kuongoza nchi.
Utakuwa na makasiriko mmcheppukko uliyeachika
 
Back
Top Bottom