Utaasisi wa Chama Cha Mapinduzi katika Kuisimamia Serikali katika Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,862
930

UTAASISI WA CHAMA CHA MAPINDUZI KATIKA KUISIMAMIA SERIKALI KATIKA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI
Nyandi Raphael Jr.
K/UVCCM [M]SHINYANGA
0718695061

November 26,2023.

CHAMA CHA MAPINDUZI ni Miungoni mwa Vyama Vikongwe vya Ukombozi wa Ukoloni Nchini na Africa.
Haina Mashaka katika Uhiriki wake katika Ukombozi wa Nchi mbalimbali kutoka Utumwa wa wakoloni katika Bara la Africa. Nchi kama Angola,Africa Kusini,Zimbabwe,Nambia na Msumbiji zilikombolewa kwa Juhudi Mahususi na VIONGOZI wa Chama cha MAPINDUZI waliokuwa Madarakani kwa Serikali ya JMT.

Mbali na Ukombozi wa utumwa kutoka kwa wakoloni,Chama cha MAPINDUZI kimekuwa Mkombozi wa Maendeleo ya watanzania katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi kuanzia awamu ya Kwanza mpaka sasa awamu ya Sita chini ya Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN.

Itakumbukwa katika ziara ya Katibu wa NE-ITIKADI,UENEZI NA MAFUNZO Ndg. MAKONDA,P.C katika Mikoa ya Kanda ya ziwa,kuliibuka baadhi ya VIOJA juu ya namna anavyochukua hatua Mathubuti juu ya Serikali katika kuwahudumia Wananchi.

Ni Ukweli usipingika kwamba,Chama lazima kiisimamie vyema Serikali yake kwani Serikali inatekeleza Mkataba Baina ya CCM na Wananchi. Inapobidi Chama hakina budi kuchukua hatua kali na Mathubuti kwa Maslahi ya Mkataba na Wananchi. Kutokuchua hatua kali kwa watendaji wa Serikali ni kukiweka Rehani Chama cha MAPINDUZI kwa Wananchi.

Kwa mujibu wa Katiba ya Nchi,ni sheria na Utaratibu kwamba Chama kitakapokuwa kimeshinda ,Ilani yake itakuwa imeshinda endapo kitafanikiwa Kupata wa Kutosha Kuunda SERIKALI.

Katiba inatupa angalizo Kuu,kwamba kushinda UCHAGUZI ni Jambo moja na Kuunda SERIKALI ni Jambo jingine.

Katika Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Ibara ya 51(1) na (2) zikisomwa pamoja na Ibara 33 na 34(1) zinaainisha Mamlaka ya Rais,Serikali na Utaratibu wa Kuunda Serikali. SERIKALI itaundwa na Rais pale Rais kwa mujibu wa Katiba anapomteua WAZIRI MKUU, na Waziri Mkuu hatashika Madaraka yake mpaka atakapokuwa ameapa Mbele ya Rais kwa Kiapo kinachohusika.

Lakini pia,Katiba imeweka wazi Utaratibu wa Mbunge aliyeteuliwa Kutoka miongoni mwa wabunge waliochaguliwa anayetokana na Chama chenye wabunge wengi,hatashika madaraka ya Uwaziri Mkuu mpaka atakapothibitishwa na Bunge la JMT kwa azimio litakaloungwa Mkono na wabunge walio wengi ([Ibara 51(1-2)]

Kimsingi kwa Mujibu wa Katiba,Chama chenye Wabunge wengi ndicho kinachounda Serikali na kwa Tanzania tangu kuanza kwa Mfumo wa vyama vingi vya siasa kuanza mwaka 1992 ni CCM imekuwa inashinda kwa kishindo nafasi ya URAIS na Kuunda Serikali.

Wakati tunatafuta kujibu Baadhi ya Vioja na Maswali mbalimbali juu ya kwanini Chama cha MAPINDUZI lazima kisimame kidete katika Kusimamia Ilani ya Uchaguzi kiliyoinadi wakati wa Uchaguzi. Tunapokwenda katika Uchaguzi kila Chama kinakuwa na Ilani yake. Katika Ilani ndimo Kuna mambo ya Msingi ambayo ni Ushawishi kwa Wananchi Kukichagua.

Kwa sababu ya Ilani,Chama ndicho hugombea na Kushinda au Kushindwa kisha humkabidhi Mgombea Ilani kwa ajili ya Utekelezaji.

Ilani inyoshinda ndiyo hutekelezwa nchi nzima.
Kuna baadhi ya watu wamekuwa na ugoigoi katika kulielewa na kulielimisha hili kwa Umma.

Hakuna Ilani tofauti kwa Maeneo tofauti kutokana na dhana tu ya ushindi wa vyama tofauti haswa kwenye Serikali za Mitaa.

Tangu Mwaka 1995 hadi Sasa,Ilani ya CCM inashinda katika Uchaguzi na kutekelezwa Nchi nzima.
Idadi ya wabunge, madiwani wanaotokana na vyama Pinzani inazidi kuongezeka kila Uchaguzi.
Hii ni dalili njema ya Ukuaji wa Demokrasia NCHINI na ni msingi tunaoujenga kwamba kwa Utanzania wetu,baada ya Uchaguzi ni kufanya kazi ya waliopewa dhamana kupitia Ilani yao.

Serikali hiyo imeundwa kwa mujibu wa sheria,katiba na kanuni. Na kwa mujibu wa sheria hizo na Katiba,Ilani ya CCM ndio mwongozo Mkuu wa Utendaji kazi wa Serikali ya Jamhuri wa Muungano, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali za Mitaa upande wa Bara na Zanzibar.

Naomba ifahamike wazi kwamba,Katika Majimbo yaliyopo chini ya vyama vya upinzani kote wanatekeleza Ilani ya CCM. Hii ina Maana kwamba, Chama chenye Ilani iliyoshinda kinayo Mamlaka Makuu kwa Serikali zote na hakuna Ilani nyingine inyotekelezwa zaidi ya hiyo.

KUTEUA MAKADA

Najaribu kuwaeljmisha na kuwafahamisha vyema juu ya hoja ya kwanini anateua Makada wa Chama kushika nyadhifa za Ukuu wa Mkoa na WILAYA. Ni jambo rahisi sana kwamba, ili kutekeleza Kwa ufanisi Ilani ya Uchaguzi iliyoshinda wazo kuu ni kuteua Maofisa wa kusimamia wanaokifahamu vyema Chama,wanaoweza kuiishi na kuelezea vyema Ilani ya Uchaguzi. Kutakufanya hivyo ni kupelekea mazingira ya kupotea kwa kushindwa kuwahudumia Wananchi [Katiba Ibara ya 8(2)]

Itakumbukwa kuwa,Madhumuni Makubwa ya vyama vya siasa Nchini ni kushinda chaguzi na kushika Dola. Hatua hii inakifanya Chama kilichoshinda kufuatilia Utekelezaji wa Ilani yake kwa Serikali kwa yale iliyoahidi katika Uchaguzi kupitia Ilani yake.

Chama lazima kifuatilie na kusimamia vyema Utekelezaji wa Ilani kisije kuhukumiwa endapo Ilani hiyi haitatekelezwa ipasavyo.

Katika hatua hii ,Ilani inakuwa inamilikiwa na umma. Umma una wajibu wa kufuatilia na kukumbusha Utekelezaji wa Ahadi za Serikali iliyopo Madarakani.

Katika Kipindi cha 2020-2025 Ilani inayotekelezwa ni ya CCM na ni wajibu wa serikali kuwahudumia Wananchi kwa mujibu wa Ilani hiyo maana hakuna Mwongozo mwingine unatoa Maelejezo ya Utekelezaji wa Ilani isipokuwa CCM.

Chama cha MAPINDUZI katika Awamu zote tangu awamu ya Kwanza ya Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius KAMBARAGE NYERERE mpaka sasa Awamu ya Sita Chini ya Mwanamama Mahili na Shupavu Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN Rais wa Serikali ya JMT na Dkt. Hussein MWINYI Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kwa Utekelezaji huu wa Ilani ya Uchaguzi kwa JMT na SMZ Chama cha MAPINDUZI kitabaki kuwa Chama chenye Mapinduzi ya kweli kwa MAENDELEO ya watanzania katika nyanja mbalimbali za Maendeleo.
Na huu ndio Utaasisi Imara katika Kusimamia Ilani ya Uchaguzi kwa Serikali.

Mungu Ibariki Africa
Mungu Ibariki Tanzania 🇹🇿
 

Attachments

  • NYANDI 4.JPG
    NYANDI 4.JPG
    1.6 MB · Views: 4
Back
Top Bottom