Yaliyojiri katika Uchaguzi Serikali za Mitaa - Dec 14, 2014

Yaliyojiri katika Uchaguzi Serikali za Mitaa - Dec 14, 2014

Hizo ni njama na kumtambua mtu itakuwa ni vigumu sana kwa wakala ..hivi chukulia mijini wakala anaweza kuwatambua hata waliohamia jana mtaani hapo ama ndo usanii
 
Nipo hapa sinza block C mugabe shule, nilijiandikisha namba 65 na jina serikali ya mtaa
Kwenye list lipo mpaka sasa cha ajabu kituoni halipo naona jina tofauti pia hapa ccm wanawatu wao
Wamewapa namba wanaingia na vikaratasi huku wameshikwa mkono nimeshindwa
Kwa kulalamika hakuna kiongozi zaidi ya polisi ambao hawana msaada wowote
Udanganyifu ni mkubwa kwakweli.
 
Niliamka mapema asubuhi ili nikaipigie kura chama changu CHADEMA haki ambayo nimeitimiza lakini ghafla nikamwona kada wa ccm anakuja na kundi la walevi, wakiwemo vijana, kina mama na baba wakiwa chakari, kweli ule usemi wa "tutatawala kwa ridhaa ya wajinga walio wengi" nimeuona leo. Na hao watu nawafahamu ni wapenzi wa ccm hapa mtaani huwa wanalewa mpaka wanavua nguo.
 
Ni saa tatu na dkk kibao upigaji kura hado haujaanza hapa Kakola mkoani Shinyanga.Ni mji mkubwa na ni ngome ya Chadema.Nasikia watawala wamefanya makusudi ili kukibeba kile chama cha mafisadi.Chondechonde watawala,acheni haki itendeke.
 
Mkuu hapa kidole gumba kimeshachafuka na wino kuashiria kuwa nimeshatimiza wajibu. Naamini maeskrow mtaani kwetu yatalia leo

kilio kinaanza leo mkuu kama yanga jana
 
Sumbawanga mjini- kata majengo, msua, katandala, katuma, kisiwani vituo bado vimefungwa na sasa no saa 9:17 a.m
 
Kwa nini kila siku tunamkemea shetan kwa kusema toka pepo
kwa nn leo tusiseme toka ccm?
 
mpaka mda huu, hapa kahama, shinyanga mtaa wa Nyahanga shuleni watu bado hawajaanza kupiga kura. Watu wamejitokeza kwa wingi sana hasa vijana, waeendesha pikipiki wapo wakisubili kupiga kura ni jambo la faraja kuona nao vijana sasa wamehamasika kupiga kura. kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini.

2014-12-14 08.43.41.jpg
2014-12-14 08.44.59.jpg
 
Chadema ikipata mitaa hata kumi tu, Nitatembea uchi Kariakoo.
Kwa kuwa wewe ni ccm hatutashangaa kutembea uchi kariakoo.Huoni Fedrick werema,Muhongo,Tibaijuka na wengine wako uchi lakini bado wanaingia ofisini.
 
Hatimaye nimepiga kura kwa mara ya kwanza... Nashukuru sijaona vurugu mpaka muda huu. Ila kitaeleweka2 na mshindi atajulikana mana nimesikiliza sera zao nikapata wa kumchagua.
 
Back
Top Bottom