Yaliyojiri katika Uchaguzi Serikali za Mitaa - Dec 14, 2014

Yaliyojiri katika Uchaguzi Serikali za Mitaa - Dec 14, 2014

Leo uchaguzi wa serikali za mitaa slaa yupo karatu na mbowe yupo ujerumani wote hao hawapigi kura alafu wana taka chadema ishinde kila siku mtabaki na ngonjera kuwa ccm imewaibia kura
Wakupimwa ww sio bure
 
Mkuu wangu na ndugu yangu kipenzi Ngongoseke kiukweli hamu ya mabidiliko kwa vijana wengi ni kubwa sana hasa ukizingatia wakati kama huu nchi hii imezidi kuzama katika kila aina ya unyonyaji kwa wananchi wake lakini hawa tunaowaita wanamabadiliko wenyewe wapohoi bin taabani aka wasakatonge walilokosa tonge hilo kutoka CCM au wanaosaka chanci ya kuwapiga watz kama watawala wanavyofanya. Kwa mtindo huu tutake tusitake bado sana mpaka kuja kuwang'oa CCM.

Nimekuwapo hivi karibuni maeneo ya kusini mwa nchi hii ambako angalau kwamba CUF inapigapiga kelele lakini nimeshuhudia maisha ya watu huko niya mashaka sana na wengi wao wanachagua viongozi hasa kutokana na kidogo kitu wanachopata.

Safari ni ndefu sana ukizingatia waendeshaji wenyewe wa harakati hizi si wamoja.

Hawezi kukuelewa huyo. Hao ndo wale wakiendaga marekani kwa mwezi mmoja wakirudi wanajifanya eti wamesahau kiswahili! Anadhani tz ya 92 ni ya leo! Anakazana tu kwamba eti mbinu ni zilezile akisahau harakati za akina mwigulu madelu kuua upinzani! Jamaa namshangaa sana na ili niepuke ban nimemwacha na maujinga yake!
 
Last edited by a moderator:
Kutoka Mkuranga; Uchaguzi wa serikali za mitaa kwa wilaya yote ya Mkuranga umeairishwa mpaka Jumamosi ya tarehe 20/12/2014


Kutoka Moshi, Kilimanjaro;

[15:12, 14/12/2014]: Kutoka Wilaya ya SIHA Kata ya kiruwa kituo cha wanri kati kura haijapigwa wapiga kura wameambiwa waondoke mana kiongozi alishapita kwa kura za maoni.

[15:13, 14/12/2014]: Kutoka Wilaya ya Hai Uchaguzi wa M.kiti wa kijijii Sadala umeahirishwa ila uchaguzi wa vitongoji unaendelea kama kawaida.

[15:15, 14/12/2014]: Kata ya sanya juu vituo vya kilingi kati,kikuyuni,shule ya msingi na sekondari fomu za kujaza matokeo mpaka sasa bado hazijafika.

[15:17, 14/12/2014]: Kutoka Wilaya ya SIHA P20.A.2.7- Vituo vyote kilingi kati na kikuyuni ambapo ndo kuna upinzani kwa maana ya kuwa wananchi wanakuja wamelewa na kutamka hadharani chama wanachokitaka.

Chanzo:LHRC‬
 
Hapa kwenye kijiji chetu wameengua jina moja la mgombea wa chadema kwenye wajumbe mchanganyiko na jina la mjumbe viti maalumu , hivyo kwa kanuni ikipigia wajumbe wawili tu na viti maalumu mmoja kura yako inakuwa imeharibika.
CCM ni wezi na wauaji kabisa.
 
Asubuhi ya leo nimeamka kwenda kupiga kura ili kutimiza haki yangu. Nilipofika pale nikaambiwa kasome jina lako ni namba ngapi. Nilipoenda kupitia jina langu nikakuta makaratsi yalikwishabandikwa kama siku tano zilizopita na kunyeshewa mvua. Nimetumia muda mrefu sana kupata namba yangu na hii imetokana kuwa najua kusoma. Kuna akina Mama ambao kwa kweli hawajui kusoma na imekuwa vigumu sana kupata namba zao licha ya wingi wa watu waliokuwa pale.
Pili, sehemu ya kura nimepata masanduku matatu matatu yamewekwa ndani sehemu tofauti na watu ni wengi humo ndani. Unakabidhiwa makaratsi matatu ya kupigia kura na mle ndani watu wako wengi na kuna hatari sana ya akina Mama kurubuniwa ili ampigie fulani kwa sababu mle ndani tumetawanyika kila mtu kuweka vema kwenye karatasi alizopewa.
Tatu, kwa utaratibu unapomaliza kupiga kura lazima upakwe wino ambao utaonyesha kuwa ulikwisha piga kura na usirudie tena. Lakini cha ajabu nilipoulizia kupakwa wino nikaelelezwa kuwa wino hamna. Kuna Mama mmoja wa CCM amekuja na orodha ya watu watano eti anataka kuwapigia kura, bila watu kuchachamaa basi huyu Mama angeruhusiwa kupiga kura.
Tujiulize maswali yafuatayo:- Kwa nini siku ya kujiandikisha hawakumpa kila mtu akariri namba yake?. Pili kwa nini upigaji kura unakuwa ovyo ovyo?. Tatu, kwa nini hakuna wino unatakiwa kupakwa baada ya kupiga kura?.
 
basi wewe utakuwa choko hasa.tuulize wakongwe tukujuze huyo mleta mada ni kada kiasi gani?hauna hata akili ya kumfuatilia
Mkuu tatixo CCM iyetu imeingiliwa na watu wa maslahi, hawasikii cha muadhhini wa,a mpiga kengele.
Wakitonywa kujisahihisha wao wanafikiria tu kutetea tonge , lao sasa CCM ni synonymous na wizi mkubwa mkubwa ulioenea nchini.
 
Mkuranga hapa mpaka sasa hivi saa 7 mchana zoezi la upigaji kura halijaanza.Vifaa vimeletwa saa 6:54 mchana.

Nahisi hizi ni mbinu chafu tu.Kwa nini vifaa vichelewe wakati uchaguzi umeandaliwa kwa muda mrefu tu?

Mkuu huko mkuranga tayari uchaguzi umeahirishwa
 
Hapa kwenye kijiji chetu wameengua jina moja la mgombea wa chadema kwenye wajumbe mchanganyiko na jina la mjumbe viti maalumu , hivyo kwa kanuni ikipigia wajumbe wawili tu na viti maalumu mmoja kura yako inakuwa imeharibika.
CCM ni wezi na wauaji kabisa.

Unge tick majina yote
 
Siasa za bongo ni upumbavu mtupu, inakuwaje mgombea wa chama kimoja awe na uwezo wa kupitisha wapiga kura bila kufuata utaratibu? Kila mgombea akiamua kupitisha wapiga kura wake kutakarika kweli? Wanasiasa kuwe wastaarabu japo mara moja moja.
 
Back
Top Bottom