Yaliyojiri katika Uchaguzi Serikali za Mitaa - Dec 14, 2014

Yaliyojiri katika Uchaguzi Serikali za Mitaa - Dec 14, 2014

Kutoka kata ya kaloleni manispaa ya moshi mjini, zoezi linaendelea na kuna vituo viwili vyote vimejaa inaonyesha jinsi wananchi walivyojitokeza kupiga kura..ingawa wananchi wanapomaliza kupiga kura bado wanaendelea kuwepo eneo la kupiga kura kinyume na utaratibu wa kanuni.
10685404_315195495341091_889895406656812147_n.jpg
 
Naungana na mleta mada hata huku Dar. Hali niliyoiona asubuhi kwenye jimbo la mnyika ccm wanachinjwa vibaya
 
Masud akiwa Kigoma ana ripoti:


uchaguzi umeahirishwa katika kata ya Kagunga mwambao mwa ziwa Tanganyika yenye vijiji viwili vya Kagunga na Zashe, na: jumla ya vitongoji 11 yenye jumla ya watu 5029. Sabubu ya kuahirisha ni kutolewa kwa wagombea wa ACT, baada ya kamati ya rufaa ya halmashauri ya wilaya ya kigoma kuwakuta na makosa ya kukosea kujaza fomu na kua na uanachama zaidi ya chama kimoja . Baada ya kutangazwa kuahirishwa kwa uchaguzi huo, vurugu kubwa zimeibuka, na tayari Askari 16 wa FFU wameagizwa kwenda kutuliza gasia.
 
ccm ndio watakao leta machafuko nchi hii; muda hauko mbali sana haya kujiri.

hadi sasa naandika uzi huu vijiji vya salama kati,salama a,na kurusanga wananchi hajaanza kupiga kura.
Tatizo ni kucheleweshwa kwa masanduku ya kupigia kura.
Ziko taarifa ccm wanafanya hujuma kuvuruga uchaguzi kwa maslahi yao binafsi kwani ushahidi wa mazingira unaonesha ukawa wanaongoza kura za maoni kama ilivyo kwenye kata za msoma mjini na serengeti.
Nawaomba wananchi,serikali,tume ya uchaguzi pamoja na wadau wote wa amani na maendeleo ya taifa letu kupigia kelele na kukomesha hujuma zozote dhidi ya haki mahali popote kunakofanyika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Aidha kwa umhimu mkubwa niwasihi wananchi wa kata ya salama kuwa wavumilivu ili kuepusha machafuko kwani mpaka sasa kuna kila dalili za ukosefu wa utulivu wa kisiasa.
 
Tayari jamani nimeshaweka alama ya vema kwa Chadema..

Kuna mamluki wa CCM waliletwa hapa kituoni
lakini nimefurahi sana.
mkuu wa uchaguzi hapa amewatema..
Makada wachache wa CCM kitongoji hiki wanahaha sana.

People's powerrrrrrrr

Umesoma vizuri jina la mgombea?
 
Wanasema Karatasi za kupigia kura zimepelea,kwa hiyo tangu asubuhi mpaka sasa wamezifuata Kiomboi

Cha ajabu baadhi ya vijiji na vitongoji vimeshapiga kura katani,na karatasi wamezichukuliwa hapa hapa katani Tulya,katika kijiji cha Tulya!

Na gari ya halmashauri ilizileta karatasi hizo jana pamoja na maboksi ya kura saa mbili usiku !

Cha kustajabisha hata kijijini Tulya(headquater of the district)uchaguzi bado

Vijiji vilivyo fanya uchaguzi mpaka sasa ni:
1)Doromoni
2)Migilango

N.B:Hata Kata ya Shelui bado!

CCM WANATAPATAPA!
 
Uchaguzi wa kijiji cha kagunga kigoma kaskazini umefutwa hafi siku nyingine baada ya mtendaji wa kata kusema act imefutwa lakini msimamizi mkuu amesema anafuta uchaguzi hadi watakapotangaza
 
Leo uchaguzi wa serikali za mitaa slaa yupo karatu na mbowe yupo ujerumani wote hao hawapigi kura alafu wana taka chadema ishinde kila siku mtabaki na ngonjera kuwa ccm imewaibia kura
 
hapa Bunda mjini hamasa ni kubwa sana katika vituo vya shule za msingi balili na kabarimu. vijana ni wengi sana na wana ari kubwa ya mabadiliko. hapa kabarimu kijana mmoja ambaye ni katibu wa mgombea wa ccm ambaye ni diwani kidogo aleta hali ya kutokuelena na vijana wengine baada ya kujipa jukumu la kuwasaidia wote wasiojua kusoma. vijana ambao ni wengi sana walikataa jamba ambalo lingehatarisha utulivu wa kituo. busara za wasimamizi na polis kumuondoa zimesaidia na zoezi linaendelea vizuri. watu ni wengi na imebidi zoezi la mistari lisitishwe na hivyo watu wanaitwa majina ili kuokoa muda. nitaendelea kuwajuza kinachoendelea hapa Bunda mjini.
 
Nimeshapiga kura

Nyie ccm acheni wizi wa kiboya....
Kuna vijana wamekuta majina yao yashapigiwa kura....yaani watu wamepiga kura kwa kutumia majina ya watu....wenyewe walivyokuja ni tafrani nimeshindwa kupiga picha kwasbb police walikuwa washatinga ....
 
Huku kidete mkoani morogoro mawakala wa wa ccm ni wagombea na na wazimamizi wameshindwa kuwaondoa je, ni haki.
 
Kaka acha kuongopa na kudanganya watu, mh. Mbowe tuko naye huku Machame tangu jana kwenye harakati za kufunga kampeni.
 
…niko kwenye mstari nasubiri kupiga kura yangu kumchagua mwenyekiti wa mtaa…jua ni kali sana na foleni ni ndefu na nisogea pole pole sana…liwake ama inyeshe nitabaki hapa hadi kieleweke…kura ni siri lakini kura yangu, ya mke wangu,pamoja na shemeji yangu na dada wa kazi kura zetu sio siri,kura zetu ni kwa UKAWA… MUNGU IBARIKI TANGANYIKA, MUNGU IBARIKI UKAWA
"UKAWA TUMAINI LETU"…

Amina! Hakikisha kura zote mlizopiga zina uzito wa nyangumi ili magamba yasiweze kuchakachua. Ukawa daima
 
Bado kidogo karibu utapata faili Mirembe Hospitali. Unajua kabisa hawapo nchini kwa majukumu ya kitaifa bado unataka kuwahusisha na mambo ambayo waliopo wanatosha kuyafanya.
 
Kutoka kigoma, kijiji cha kalinzi
jamaa yangu anaripoti kuwa kuna vitingoji kama 5 hivi uchaguzi umeahirishwa, kwa sababu wagombea wa chadema woote majina yao hayapo... Nchii hii ccm imekuwa ni janga la kitaifa katika kutenda haki.,
 
Back
Top Bottom