Yaliyojiri katika Uchaguzi Serikali za Mitaa - Dec 14, 2014

Yaliyojiri katika Uchaguzi Serikali za Mitaa - Dec 14, 2014

Ndoto za alinacha
hivi ndugu huamini CCM inaweza kuanguka? Rais Mkapa aliacha misingi mizuri sana ya uchumi wa nchi. Professor Kikwete ameivunja yote. Leo hii tunavyoongea shilingi ya tanzania imeporomoka Kwa mujibu wa tovuti ya Benki kuu ya Tanzania dola moja ni shilingi 1718. Hii ni mbaya sana kwa uchumi wa nchi. Ufisadi unaofumbiwa macho umesababisha wahisani kuzuia dola 449 million na majuzi tu Serikali ya marekani imetangaza ku freeze msaada wa MCC takribani dola million 700....Professor kikwete alijipambanua sana kutegemea wahisani badala ya kujenga misingi ya kujitegemea kwenye bajeti. Leo hii ni vigumu kwa serikali kufanya matumizi ya kila siku...inalazimika kutumia ubabe kukopa kwenye mabenki ya ndani ili kulipa mishahara na matumizi mengine. Haya yote yanatokana na misingi mibovu na utawala mbovu wa Professor Kikwete. Kuna siku aliwahi kwenda kufanyiwa check up New York halaf siku anarudi wasaidizi waka wakamshauri aende kutembelea wagonjwa muhimbili. Haya yote wananchi wanayaona na kwa kuwa technolojia ya habari imekua watu hawadanganyiki tena! David kafulia aliinuka bungeni na kusema serikali ya marekani imesitisha msaada, waziri wa fedha bila chembe ya aibu anainuka na hijabu yake kusema si kweli...leo hii balozi wa marekani anathibitisha...Katibu mkuu kiongozi anasema ni jambo la kawaida duniani kote......hakika Professor Kikwete ameiharibu kabisa nchi hii.......
 
Mungu tujaalie uchaguzi uishe kwa amani na matokeo yatangazwe...
Wakuu, leo, Disemba 14, 2014 Watanzania wanapiga kura kuchagua viongozi wao wa Serikali za Mitaa, Tanzania Bara (Tanganyika).

Viongozi wanaochaguliwa leo ni katika nafasi za Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Wenyeviti wa Vitongoji, Wajumbe 6 wa Serikali ya Mtaa (Halmashauri) na wajumbe wa Viti Maalum wa Mtaa/Kijiji.

Kama ilivyo ada JamiiForums itakuwa ikikujuza yanayojiri, katika uzi huu utapata/utaleta updates zinazohusiana na uchaguzi huu.

Karibuni sana

========
UPDATES MUHIMU:

attachment.php

attachment.php

Hapa ni Mtaa wa Kijitonyama
- Eneo la Shariff Shamba, Ilala jijini Dar uchaguzi umeahirishwa mpaka Jumapili ijayo baada ya vifaa kutopatikana ndani ya muda. Vyama vyote vinavyoshiriki vimeafikiana

- Mgombea wa CHADEMA Kijiji cha Darajani huko Liwale, M. Manakwa amepigwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo, amelazwa hospitali

-Mkuu wa Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, Suleiman Liwowa ametangaza kuwa katika vitongoji 613 vya Wilaya hiyo vyama vya Upinzani vimeshindwa kusimamisha wagombea.

wakuu tupeni updates za matokeo maana muda ndo huu
 
hivi ndugu huamini CCM inaweza kuanguka? Rais Mkapa aliacha misingi mizuri sana ya uchumi wa nchi. Professor Kikwete ameivunja yote. Leo hii tunavyoongea shilingi ya tanzania imeporomoka Kwa mujibu wa tovuti ya Benki kuu ya Tanzania dola moja ni shilingi 1718. Hii ni mbaya sana kwa uchumi wa nchi. Ufisadi unaofumbiwa macho umesababisha wahisani kuzuia dola 449 million na majuzi tu Serikali ya marekani imetangaza ku freeze msaada wa MCC takribani dola million 700....Professor kikwete alijipambanua sana kutegemea wahisani badala ya kujenga misingi ya kujitegemea kwenye bajeti. Leo hii ni vigumu kwa serikali kufanya matumizi ya kila siku...inalazimika kutumia ubabe kukopa kwenye mabenki ya ndani ili kulipa mishahara na matumizi mengine. Haya yote yanatokana na misingi mibovu na utawala mbovu wa Professor Kikwete. Kuna siku aliwahi kwenda kufanyiwa check up New York halaf siku anarudi wasaidizi waka wakamshauri aende kutembelea wagonjwa muhimbili. Haya yote wananchi wanayaona na kwa kuwa technolojia ya habari imekua watu hawadanganyiki tena! David kafulia aliinuka bungeni na kusema serikali ya marekani imesitisha msaada, waziri wa fedha bila chembe ya aibu anainuka na hijabu yake kusema si kweli...leo hii balozi wa marekani anathibitisha...Katibu mkuu kiongozi anasema ni jambo la kawaida duniani kote......hakika Professor Kikwete ameiharibu kabisa nchi hii.......

Una chuki binafsi na Kikwete.Pole mtafute myamalize
 
mimi nimeshindwa kupiga kura. nimekaa foleni toka saa 6 mpk saa 9 inafika ni umati wawatu. mtu mmoja anatumia masaa mawili mpk 5 foleni.kituo kina wapiga kura 1000 wanaweka kituo kimoja tu chakupigia kura. sijapata kuona uchaguzi wa hovyo hovyo hovyo kama huu. utaratibu mbovu kabisaaa. na niliwapigia tume ya taifa ya uchaguzi. kulikuwa na kipindi maalumu chanel ten wanarusha live kuhusu uchaguzi huu wakaweka namba ya kutuma malalamiko yotote yale. nikawapigia nikawapa malalamiko yote wakasema tunasshughulikia. na hakuna lolote lililofanyika. kwa hakika mmefeli kabisaaaaaaa
 
Mungu akitaka kuwaondoa viongozi/watawala madarakani huwapiga upofu ili wasione yanaendelea na wakishakuwa vipofu hujawa na kiburi kwakuwa hawaoni huamini kuwa Wako sawa mwisho huwa Ni kuanguka Tu.

wananchi wanayataka mabadiliko siyo kuyahitaji tena "wanayataka" waliopo madarakani hawalioni hili wamepigwa upofu, CCM wataendelea na kuamini Wako sawa kwani wanatazama lakini hawaoni.
 
Urambo naona police wapo fit sijui kunani na watu niweng ktk vituo vyote
 
Habari wakuu.

Ikifahamika leo ndiyo iliyokuwa siku rasmi ya uchaguzi kwa ngazi za serikali za mtaa. Huku maeneo ya Mabibo watu wanapiga kura mpaka mara tatu kwani kama inavyofahamika mara upigapo kura basi utapakwa wino kuthibitisha kwamba umeshapiga kura lakini wino huo hautumiki badala yake mtu akishapiga kura anaondoka hivyohivyo na hii inatoa mwanya kwa mpigaji kwenda kituo kingine kupiga kura tena.

Kwa tafiti nilizofanya kituo hiki kimenunuliwa na CCM kwa hiyo kila kinachoendelea mahali hapa pamoja na kuvunjwa kwa kanuni za uchaguzi hakuna anayehoji wakiwemo wasimamizi wa uchaguzi huu.

Nayasubiria matokeo ya kupikwa yatangazwe.
 
Katika hali ya kushangaza leo chadema wanashirikiana na ccm kigoma ujiji watu wa chadema wanawaambia wananchi tena kwa kuwahonga kuliko kupigia kura act bora wachague ccm hii ni ukawa nyingine mpya
 
mods waanzishe thread ya matokeo sasa, watu tunayo matokeo ya wilaya ya mbinga ,
na songea manispaa
 
Back
Top Bottom