Yaliyojiri katika Uchaguzi Serikali za Mitaa - Dec 14, 2014

Yaliyojiri katika Uchaguzi Serikali za Mitaa - Dec 14, 2014

LIVE UPDATE UCHAGUZI SERIKALI ZA MTAA PWANI na DAR ES SALAAM (CALL CENTER CHADEMA)

hali ni mbaya sehemu kubwa ya Dar es salaam sehemu nyingi uchaguzi humehairishwa kwa mapungufu mengi kama watu kukamatwa wanapiga kura mara mbili,vifaa kukosekana,wasimamizi kutofika..... VINGUNGUTI,KIWALANI,KINYEREZI UMEHAIRISHWA...........MIKOCHENI B UCHAGUZI UMESIMAMA BAADA YA WATU KUKAMATWA WANAPIGA KURA MARA MBILI
 
...

Rombo kimenuka fujo zimeaanza baada ya vifaa vya kupigia kura kuchelewa kwenye vituo SOURCE sunrise Radio inasemekana ni vituo vingi sana mpaka sasa hawajaanza kupiga kura

Mpaka muda huu havijafika?
 
Hapa mtaa wa SUSUNI Nyakato MWANZA jamaa wa CCM katolewa mbiyo na kifurushi cha kura feki.
Vijana, kinamama na wazee wakiongozwa na mwasisi wa CHADEMA mzee MASINDE kwa wingi wamejikusanya kuzunguka kituo cha kupigia kura ili wasichakachuliwe.

Leo ndiyo nimejihakikishia kwa macho CCM huwa wanaiba kura, huwa hawashindi kwa haki!!!
Hali ya MAGAMBA ni ngumu sana jiji zima la MWANZA.
 
Johnson kutoka Sumbawanga anaripoti kuwa Mtaa wa Nyanya Kata ya Musua Sumbawanga mjini mpaka sasa wasimamizi hawajafika wapo mawakala na mlinzi tu na hata majina hayajabandikwa.
10641156_315209392006368_3419519143227662928_n.jpg
 
Mkuu Manning...Bunda ni disaster ....ukiacha karukekere...uliza ya hunyari,mihale,kunzugu,bukore kote ni shida hapo bado hujasimuliwa vurugu za Msoma mjini usiku wa jana.
Huko salama wananchi wanasubiri masanduku full equiped na visu...matochi..mapanga n.k....
Alafu ukiwauliza watendaji,wawakilishi wa tume na viongozi wengine wa serikali wanatoa majibu mepesi yanayochochea hasira.
 
Taarifa kutoka Nzega zinaripoti:
Ndala kijiji cha Buhemeli hadi sasa bado hawajapiga kura na wala hawajaambiwa chochote

10351394_315213878672586_7362419471726576815_n.jpg
 
Mbozi kata ya Mloo Mratibu wa ccm wilaya
amekamatwa na masanduku ya kura
 
ccm wamebaka huu uchaguzi mapingamizi kila kona na sasa vifaa havitoshi ,,,,hell u ccm
 
Kutoka Sumbawanga anaripoti kuwa Mtaa wa Nyanya Kata ya Musua Sumbawanga mjini mpaka sasa wasimamizi hawajafika wapo mawakala na mlinzi tu na hata majina hayajabandikwa.

10641156_315209392006368_3419519143227662928_n.jpg


LHRC
 
Wilaya Mbozi kata ya Mloo katika kituo cha kupiga kura, Mratibu Kata amekamatwa na kura, anashikiliwa na police. Bado taarifa inafuatiliwa zaidi.

10857725_315208078673166_2407385649655011796_n.jpg


LHRC
 
Hivi matokeo kwa kawaida yanatangazwa leo leo? Tujuzeni yaliopo kwenye maeneo yenu huko
 
Kutoka kata ya kaloleni manispaa ya moshi mjini, zoezi linaendelea na kuna vituo viwili vyote vimejaa inaonyesha jinsi wananchi walivyojitokeza kupiga kura..ingawa wananchi wanapomaliza kupiga kura bado wanaendelea kuwepo eneo la kupiga kura kinyume na utaratibu wa kanuni.

10685404_315195495341091_889895406656812147_n.jpg
 
Huu ni uchaguzi au kiini macho, validity yake unazidiwa na ule wa kumchagua kiranja mkuu au monita wa darasa. Unapiga kura kwa kuchagua jina tu kwenye mbao, huulizwi japo kitu chochote cha kuthibitisha kwamba ni wewe mwenye jina au mkazi wa eneo,kwa hali hii mtu anaweza kupiga kura hata mara 5, hovyo kabisa, kujisifia ndo kwingi lakini mambo yenyewe ni madudu tu, nahisi hizi kasoro zinaachwa makusudi ili ziweze kuokoa jahazi baadae kwa chama tawala
 
Back
Top Bottom