mkutano ulikua unaboa, majigambo mengi na matusi toka kwa lema, kwenda kwa mkuu wa mkoa, polisi na usalama wa taifa, kweli lema bado anaogopa polisi yaani anaongea huku akiangalia pa kukimbilia jamaa wakija...Ole milya maskini ya Mungu anaongea vapor tu, hakuna jipya alilosema zaidi ya pipoooz, wengi walitegemea kusikia mapya lakini hata lema mwenyewe hakuwa na jipya la kuwaaambia wana Arusha, inasikitisha kuwakusanya watu wote hao kuwapotezea mda wao. Wagombea wa Udiwani nao ni vapor tu, wamepaukaa, sijui kama wana arusha wakiwapa uongozi watasalimika, maana mpaka watoe vitambi mji utakua umebakia magofu tu, kwa ujumla wake hakukua na jipya ...lema aliwasili muda wa saa saba na nusu, kukagua uwanja akiwa na gari aina ya nissan yenye vioo vyeusi lenye namba za Kidiplomasia mara nyingi hutumika na wafanyakazi wa UN...cha ajabu kwa mbunge kuwa na access na magari kama haya, inaonyesha hajiamini, sijui tatizo lake nini wakati amejitangazia ufalme wa mji, ebanaee, jamaa kasifia mke wake mnoo, hayo ndiyo yaliyojiri