Kutoka viwanja vya Sinoni-Arusha: Mkutano wa Mgombea Urais wa CHADEMA, Edward Lowassa - Okt 8, 2015

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,221
1,788
Leo mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya shule ya Sekondari Sinoni, Mkutano huu utarushwa live na ITV.

Maandalizi ya mkutano yamekamilika na Lowassa anatarajiwa kupokelewa katika uwanja wa ndege wa Arusha na msafara wake kuelekea uwanjani.

Mkutano wa leo utaweka msimamo na mwelekeo wa Taifa kuhusu uchaguzi kwa hizi siku zilizobaki.Mwenyekiti wa chama Taifa na kamanda wa anga Mh Freeman Mbowe atatoa mwelekeo na msimamo wa chama kabla ya siku ya uchaguzi.

Mkutano utaanza saa nane kamili.Mapokezi ya Mh Rais saa tano pale Kisongo uwanja wa Ndege

Nipo uwanjani kukuletea yale yote yanayojiri pamoja na picha

Stay tuned!!!!!!

Updates

4.jpg

Wananchi wa Arusha na viunga vyake wakiendelea kumwagika viwanjani hapa Kwa hiyari yao wenyewe. hajalipiwa mtu hapa. Hakuna Lori wala basi lililoleta mtu.

Uwanja umeshatapika na mambo ndiyo bado hata hayajaanza. Hakika Lowassa ni Rais wa awamu ya Tano.
Screenshot from 2015-10-08 17:23:40.png

Endelea kufuatilia huu Uzi Kwa updates zaidi kwani mambo ndiyo kwaaaanza bado.

Lowasaaaaaaaaa...Mabadiliko!!

Usiondoke baki hapohapo.

Updates

Taarifa za hivi punde zina sema Rais mtarajiwa Edward Ngoyai Lowassa akiwa na Timu nzima ya UKAWA watakuwa viwanjani hapa kuanzia majira ya Saa10 Jioni.

Endelea kufuatilia huu Uzi Kwa Updates zaidi...

Updates


Mkutano ameshaanza. Mbatia anazungumza.

Anasema Arusha imepewa heshima ya kuhutubiwa na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru.

Anasema Ccm wameuza hisa za TBI zenye thamani ya shilingi177Bil ili zisaidie kampeni zao

Wiki ijayo watauza tena 50% za NBC zenye dhamani ya 412bil

Jk katumia 4trilion kwa safari za nje fedha ambazo zingetosha kujenga vyuo vya ufundi 200 kwa thamani ya bil 20 kila kimoja

Ccm badala ya kufanya kampeni inabebwa na dola kwa kufanya haramu.

Kikwete amefanya ccm haramu kwa kutumia fedha za watanzania kwenye kampeni

Lowassa amesema kipaumbele chake cha kwanza hadi tatu ni elimu.

Elimu ya Lowassa itasaidia kwa kuanzisha vyuo vya ufundi ili ziweze kumsaidia.

Mkamate sana elimu usimwache aende zake maana ndiyo uzima wako. Maneno ya mithali

Tarehe 25/10 tuhakikishe rais wetu ni Lowassa.. Magufuli asipate kura hata moja

Mbowe:
Naomba nimlete kwenu mgeni wenu wa siku ya leo ambaye ana kadi namba 8 ya ccm. Anataka kuzungumza na watu wa Arusha

Watu wanashangilia babu babu babu babu babu

Tangu ccm imeanza kampeni imefanya vituko,kampeni zao zimetawaliwa na matusi,kimepoteza dira

Ccm haisemi sera tena bali kusema watu kwenye mikutano yao

Lazima mtu anayesemwa sana awe ni mtu mzito sana,ndio maana watu wazima wanamsema sana

Mimi ni mtu wa mabadiliko

Ninaamini kwa dhati ya moyo wangu kuwa mabadiliko Tanzania ni sasa

Wakati tunaanzisha TANU tulikuwa tunatafuta chombo cha kumkomboa Mtanganyika

ASP na TANU vimefanya jitihada kubwa kuboresha maisha ya watanzania,na kwa kuwa viliamini katika mabadiliko viliungana

Tunaendelea na mabadiliko hadi sasa,lakini katika awamu hii ya nne,kuna dalili kuwa baada ya ccm kukaa madarakani kwa nusu karne imeishiwa pumzi

Ccm ilirithi pumzi ya asp na Tanu ila sasa pumzi imekwisha

Mkapa alichukua kutoka kwa Mwinyi wakati uchumi ukikuwa kwa 4%

Kikwete karithi unaokuwa kwa 7asilimia,miaka 10 baadae na kwa taarifa za serikali yenyewe uchumi unakuwa chini ya 7%

Maana yake ni kwa miaka 10 hii tumeganda!

Ili kuondoa umasikini lazima uchumi ukue kwa 10%kitaalam
Kwa miaka kumi ccm uchumi umekuwa kwa single digit

Uchaguzi ni kura,sio maneno

Tarehe 25 kazi ni moja tu,unachukua kichinjio unaweka Lowasa

Naomba marafiki zangu wa ccm,wengine tangu wakati wa kupigania uhuru,wasibabaike,sijawaacha kwa sababu nawachukia,nimeondoka kwa sababu sikubaliani na uongozi unaovunja katiba ya chama,taratibu,na kanuni.

Uongozi unaodhalilisha wagombea Urais wa chama chao,na wanaendelea kana kwanba hakuna lililotokea

Anaaga wanachi kwa kumtia moyo.

Nawatakieni mafanikio katika harakati za kuleta mabadiliko

Uwanja unalipuka Kwa kushangilia. babu babu babu babu.

Sumaye
Watanzania wameamua kuwa sasa ni mwaka wa mabadiliko

Wameamua hivyo kwa kuwa ccm imeshindwa kuleta maisha bora

Watoto hawatibiwi bure

Ccm imeahidi vijana ajira,na kikwete aliahidi vijana kuwa tatizo la ajira litakuwa ajira,Je tatizo hilo limeisha?

Elimu imeharibiwa na ccm

Wananchi wanajibu kuwa hakuna haja ya kuchagua ccm tena

Rais lazima awe mwadilifu,awe mtumishi mwema,na awe kimbilio la watu

Kwenye mizani kuna rushwa kubwa,wizara ya magufuli imenunua bot ya miaka 30 kwa gharama ya boti mpya

Wizara ya ujenzi inaongoza kwa ufisadi,Je ni Magufuli ni mwadilifu?

Ameshindwa kupambana na ufisadi wizarani kwake ataweza kwa nchi?

Lazima rais awe msikivu,je Magufuli ni msikivu?

Kigamboni aliwaambia watu wapige mbizi Maana yake wafe.

Hatutaki Rais mbambe

Sumaye anamaliza Kwa kushangiliwa vilivyo.

Sasa Lowassa anataka kuzungumza na Watanzania.

Wimbo unapigwa anacheza

Lowassa

Namshukuru sana mzee Ngombale ndie aliyekuwa nguzo ya ccm,kuondoka kwake ni pigo kwa ccm

Nimekuja kuomba kura

Wananchi wanaitikia Kwa shangwe. Umepataaaaaaa. Uwanja mzima kelele na vifijo

Wananchi wanaimba Rais Rais Rais Rais Lowassa

Kwa huu umati ikulu nimefika

Kwanini nagombea urais

Nimechoshwa na umaskini

Naomba kura nyingi ili niweze kushinda.

Nimeomba kuwa rais kwasababu nimechoka na umaskini.

Nitaanza na elimu ili kuondoa hali ya umaskini. Vipaumbele vyangu vya kwanza elimu pili elimu tatu elimu. Ukimpa mtoto wako elimu umemsaidia kimaisha. Nimesema elimu kuanzia nursery hadi chuo kikuu bure.

Wanasema haiwezekani mimi nasema inawezekana kabisa tuna fedha nyingi sana nchi hii kuanzia gesi mpaka madini na utalii. Hakuna mwanafunzi kulipa mchango wa aina yoyote. Nitazingatia maslahi ya mwalimu ili awe na moyo na kazi yake.

Eneo la pili ni eneo la kilimo nitaiboresha na mkulima akitaka kuuza mazao yake popote auze. Tuwape wananchi uhuru wafurahie matunda ya nchi yao wakale raha.

Eneo la tatu ndugu zangu wa bodaboda, mama ntilie na machinga watakuwa rafiki wa serikali yangu. Naahidi nikiingia ikulu baada ya wiki moja atakayewasumbua nakula nao sahani moa. Nitaanzisha benki kwa ajili wa wamama kupata mikopo.

Nikichaguliwa kuwa rais kila wilaya kutakuwa na hospitali za rufaa zenye vifaa vya kisasa kuwasaidia wagonjwa.

Nimekusudia kuongoza Tanzania kwakuwa nia ninayo sababu ninayo na uwezo ninao. Serikali yangu itakuwa ya mchakamchaka

Lema

Kamanda Lema, Kiboko ya CCM Arusha anazungumza sasa.

Wananchi wanamshangilia Lema Lema Jembe Jembe.

Lema anazungumza

Mh rais hawa watu ni watu wangu wananipenda nami nawapenda sana. Nimekamatwa na kuteswa kwa ajili a watu hawa, nimeenda jela kwa ajili ya watu hawa, nimejenga hospitali bado tunawapigania watu wangu.

Nakuhakikishia tayari tuna kura laki mbili na sitini na tayari hao walikusainia wakati wa udhamini. Mh rais una kura nyingi sana.

Nakuomba uwasiliane na Lubuva umwambie mpango wa kuchelewesha vifaa ukome tunahitaji kura za haki.


Wakuu mkutano imeisha na watu wanaanza kuondoka viwanjani hapa.

Ni dhahiri shahiri CCM wana kazi nzito kuanzia ngazi ya Udiwani mpaka Urais ndani na nje ya Arusha.

WanaArusha wameionyesha Arusha na Tanzania kwamba Mabadiliko hayakwepeki na CCM lazima itoke.



Shukrani za dhati ziwafikie makamanda Kwa kuwezesha Updates za Leo.

chakii Mungi Molemo Emma sweetlady Filipo Crashwise na wengine wote walioshiriki.


Tukutane Oktoba 25.

==========================

MWANASIASA mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru, jana kwa mara ya kwanza alipanda jukwaani kumnadi mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa na kusema mabadiliko ni lazima.

Kingunge aliyasema hayo jijini Arusha kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Sinoni.

Kingunge alihutubia huku mvua ikinyesha, lakini wananchi waliokuwa eneo hilo hawakuondoka.

"Historia yangu, nimeshiriki katika kuleta mabadiliko na ninaamini kwa dhati ya moyo wangu kwamba kwa sasa mabadiliko katika Tanzania ni lazima, sisi tumekuwa huru kwa miaka 54 sasa.

"Tulivyounda Tanu tulitaka chombo cha mabadiliko na Zanzibar walivyounda Afro Shirazi walitaka kuwakomboa Waafrika wenzao, vyama vyote viwili vilitaka Watanzania tupate mabadiliko na baadaye kwakuwa waliamini katika mabadiliko, waliunganisha vyama na baadaye nchi, na mimi nilikuwa kwenye kamati ya watu 20 kuanzisha CCM.

"CCM katika miaka ya karibuni kimekuwa na dalili zote kwamba baada ya kuwa madarakani kwa nusu karne kimeishiwa pumzi," alisema Kingunge na kushangiliwa.

Ili kutuliza watu hao, mkongwe huyo wa siasa kwa mara ya kwanza alilazimika kutumia salamu maarufu ya Chadema ya "peoples" hatua iliyofanya umati huo ulipuke zaidi kwa shangwe na kelele na kujibu "power".

Kingunge alisema maendeleo ya watu ni sawa na kupanda mlima, hivyo kuhitaji pumzi ya kutosha jambo ambalo CCM hawana.

"Lazima uwe na pumzi kila unapozidi kwenda mbele, ni wale tu wenye pumzi ndio watafika kileleni, CCM sasa pumzi imekwisha.

"Tanzania imefikia asilimia 7, Rais Kikwete alipokea nchi wakati uchumi ukiwa na asilimia 7, miaka 10 baadaye kwa taarifa za Serikali uchumi unakua kwa kasi ndogo sana, kidogo, chini ya asilimia 7, maana yake uchumi umeganda huku wenye mahitaji wakizidi kuongezeka, hivyo tunahitaji mabadiliko.

"Lazima ipatikane timu nyingine ya Watanzania hawa hawa, na timu hiyo ipo, wakabidhiwe dola wachochee mabadiliko ili kupambana na umasikini, lazima mfumo wa uchumi ukue kwa zaidi ya asilimia 10, CCM kwa miaka 10 wamebaki kwenye asilimia 7.

"Kwahiyo nasema wapo watu Tanzania wanaoweza kutupeleka mbele hata ya asilimia 10, lazima tumpate kiongozi atakayeweza kutupeleka mbele, kiongozi huyo yupo, nyie mnamjua," alisema na kuhoji "Ni nani?" wananchi wakajibu "Lowassa". Akasema "Semeni tena", wakajibu tena "Lowassa".

"Ndiyo maana mimi nipo hapa, na nilikuwapo siku ile Lowassa alipotangaza nia, nilikuwa naye sambamba, mimi ninaamini ana sifa za kutuondoa hapa, mtu hawezi kufanya miujiza ya kutuondoa hapa kama hana watu.

"Ndiyo maana nilisema pale, sifa ya kwanza kubwa ni je, ana watu nyuma yake? Na Baba wa Taifa alituambia, ‘mnapotafuta kiongozi wa nchi msikae kwenye vikao vyenu mkaamua, sikilizeni watu wanasema nini'.

"Hayo ni maoni ya Watanzania na ndiyo maoni yangu. Na huu (umati uliokuwa uwanjani hapo) ni ushahidi kwamba ana watu nyuma yake, Mwalimu alisema katika mazingira ya vyama vingi tupingane bila kupigana, ni wananchi, sasa tunaenda kwenye uchaguzi tarehe 25 kufanya maamuzi na wanaofanya maamuzi ni wananchi wa Tanzania.

"Ikulu ni kura siyo maneno, mazungumzo ya uwanjani hayatupi rais, kura zinatupa rais, kwahiyo tudhamirie tarehe 25 Oktoba twende kwenye vituo vya uchaguzi, kazi yetu iwe moja tu, msikubali kubabaishwa, kazi yenyewe ni kila mmoja ukifika pale, unachukua, unaweka Lowassa.

"Nawaomba sana, rafiki zangu wa CCM nimekuwa nao, wasibabaike, uamuzi wa kuchagua anayefaa unao wewe, na ninyi ndugu zangu niliowaacha CCM sikuwaacha kwa sababu nawachukia, mimi napenda Watanzania wote, nimeondoka kwa sababu sikubaliani na uongozi unaovunja katiba ya chama, taratibu za chama," alisema.

Kingunge ambaye alipanda jukwaani saa 10:53 jioni na kushuka saa 11:27, alisema amekuwa akifuatilia mikutano ya kampeni ya vyama vyote na amefurahishwa na Ukawa kuendesha kampeni zao kistarabu bila kumtukana mtu.

"Chadema na Ukawa mmetia fora, ninyi mmeonyesha ustaarabu, utulivu na heshima kwa nchi yetu, hata watazamaji wameliona hilo, pamoja na kwamba mikutano yenu inakutanisha maelfu ya watu, kuna utulivu na adabu, kwa bahati mbaya chama ambacho mimi kilikuwa chama changu, tangu waanze kampeni wamefanya maajabu na vituko.

"Wameanza na matusi ya kustaajabisha, na kwa bahati mbaya pamoja na kwamba CCM ina sera nyingi tu, hawazungumzii sera, wanazungumza mtu, watu wazima waliokuwa wamepumzika wamewachukua kuja kwenye majukwaa kumzungumzia mtu, kwahiyo ni lazima mtu anayezungumzwa sana awe mtu mzito sana," alisema.



WATU WAZIMIA

Licha ya kwamba uwanja huo ulikuwa ni mkubwa, takribani watu 50 walipoteza fahamu kutokana na kukosa hewa kulikosababishwa na msongamano kuwa mkubwa.



LOWASSA

Akihutubia wananchi hao, Lowassa aambaye anaungwa mkono na vyama vya CUF, NLD na NCCR-Mageuzi, alimshukuru Mzee Kingunge kwa kumuunga mkono huku akimtaja kwamba ni kati ya nguzo za Tanu na CCM.

"Nimefanya kazi kwa miaka mingi na Kingunge, ndiye alikuwa nguzo ya CCM na Tanu, kwahiyo watakuwa wamepata pigo sana," alisema.

Kuhusu sera zake endapo ataingia madarakani, alisema atakabiliana na matatizo mbalimbali ya Watanzania, ikiwamo sekta ya afya kwa kuhakikisha kila wilaya inakuwa na hospitali ya rufaa.



SUMAYE

Naye Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, jana alikumbushia ukaguzi uliofanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kwa mwaka wa fedha 2014/15 ambao umeibua ufisadi mkubwa katika wizara, idara, wakala za Serikali, halmashauri, taasisi na mashirika ya umma.

Alisema anashangazwa na Wizara ya Ujenzi inayoongozwa na mgombea wa CCM, John Magufuli kubainika kufanya malipo hewa ya Sh milioni 951.7 na kupoteza Sh bilioni 124.8 ambazo ni malimbikizo ya riba kutokana na kuchelewesha malipo ya wakandarasi.

"Mimi nashangaa huu uadilifu wanaosema, gazeti la MTANZANIA juzi limechapisha ripoti inasema Wizara ya Magufuli imesababisha upotevu wa Sh bilioni 125, huu ni ufisadi mkubwa," alisema.

Chanzo: Mtanzania
 
Last edited by a moderator:
Mwa mujibu wa Lema kupitia account yake ya FB amesema mkutano utakuwa live kupitia ITV.
 
Hii itasaidia kumsikia Kingunge anachotaka kuzungumza kwa dk40 kuhusu JK na CCM yetu kama alivyodai.Kumbuka Kingunge ni mwanachama wa muda mrefu sana ndani ya CCM pengine kuliko wengine waliobaki.Tunawaomba UKAWA wafanye hima mkutano uwe live

Mkutano utakuwa Live ITV
 
Vizuri Nanyaro.

Tuletee kila kinachojiri mkuu na diwani wa kata ya Levolosi hakikisha kifaa chako kina moto wa kutosha mkuu.
 
Pamoja sana kamanda nitajitahidi niskie hizo fimbo za kingunge teh teh pia picha ni muhimu zaidi
VIVA UKAWA!!!
 
Hii itasaidia kumsikia Kingunge anachotaka kuzungumza kwa dk40 kuhusu JK na CCM yetu kama alivyodai.Kumbuka Kingunge ni mwanachama wa muda mrefu sana ndani ya CCM pengine kuliko wengine waliobaki.Tunawaomba UKAWA wafanye hima mkutano uwe live

Uwe na power bank ya kuwezesha TV kuwaka
 
Back
Top Bottom