Ya Polisi na vyama vya siasa Tanzania

Ya Polisi na vyama vya siasa Tanzania

Picha yaonyesha wavuta bange, na maneno yako haya uliandika wakati umeisha vuta au bado ?


Na wewe kama huna la kusema usikoment jamaa kaweka point wewe unajifanya wajua, just let ur fingers do other things
 
Kwani ndiyo mwanzo polisi wetu kuuwa raia katika shughuli za siasa na maandamano kwa ujumla?

Soma:
Mwaka 1993 walimwuua mwana-CUF kule Shumba Mjini, Zanzibar kwa amri ya OCD kwa kosa la kupandisha bendera ya CUF katika tawi alilolianzisha. Si OCD wal;a polisi aliyepiga risasi walipandishwa kizimbani.

Mwaka 1998 polisi waliwaua kwa kuwapiga risasi wapita njia wanne kwa maelekezo ya ofisa wa usalama. Hii ilikuwa katika vurugu za Mwembechai. ITV wanayo footage hiyo. Si polisi aliyefyatua risasi wala yule mwanausalama
walifikishwa mahakamani. Waliofikishwa mahakamani ni viongozi wa dini.

Mwaka 2001 huko Chake, Pemba polisi hao hao wa CCM waliwapiga risasi na kuwaua makumi ya wana-CUF. Hakuna polisi aliyefikishwa mahakamani kwa makosa hayo. Waliofikishwa mahakamani ni viongozi wa wana-CUF walioandamana.

Jana polisi wamewaua wanachadema wawili huko Arusha. Wanaofikishwa mahakamani ni viongozi wa Chadema.

Nawaambia CCM nchi hii si kisiwa cha amani kama mnavyopenda kuimba. Amani haiimbwi majukwaani -- inajengwa kwa misingi imara ya dhati na ya haki, si vinginevyo.

You have reached the end of your tether. Please GO, CCM, GO away before it's too late.
 
Jamani hebu tupeni habri za uhakika maana huku kupitia mtandao radio one taarifa inasema ni watu wawili na sio watu kumi. Ila hata ingekuwa mtu mmoja tu vitendo hivyo vya Polisi kutumia nguvu inabidi vikemewe sana maana hiyo inaweza kuharibu ajira ya kuwa Polisi maana watachinjwa mitaani, wakumbuke wanaishi jirani na hao wanaowaua. Lingine wapelekwe shule ili kufundishwa ustaarabu, wafanye kama wenzao huku nje ya nchi ambao hawatumii silaha za moto kwa watu wasio na silaha yoyote. Poleni sana wafamilia zilizopoteza wapendwa wao. Jibu liko njiani linakuja msihofu.
 
Jamani hebu tupeni habri za uhakika maana huku kupitia mtandao radio one taarifa inasema ni watu wawili na sio watu kumi. Ila hata ingekuwa mtu mmoja tu vitendo hivyo vya Polisi kutumia nguvu inabidi vikemewe sana maana hiyo inaweza kuharibu ajira ya kuwa Polisi maana watachinjwa mitaani, wakumbuke wanaishi jirani na hao wanaowaua. Lingine wapelekwe shule ili kufundishwa ustaarabu, wafanye kama wenzao huku nje ya nchi ambao hawatumii silaha za moto kwa watu wasio na silaha yoyote. Poleni sana wafamilia zilizopoteza wapendwa wao. Jibu liko njiani linakuja msihofu.

Habari zenyewe ni kwamba wameuwawa watu 5, miongoni mwao polisi 4 na raia mmoja.
 
Aluta continua, together we stand. Our blood will nourish the tree that will bear the fruits of the freedom.
 
Habari zenyewe ni kwamba wameuwawa watu 5, miongoni mwao polisi 4 na raia mmoja.

Hapa kweli ni kuchanganyana, watu 10 mara 3 mara 2 sasa 5; hivi vyombo vya habari mbona sio reliable jamani???
 
SASA ONJENI SHUBIRI HIYO NA MJUE SERIKALI IPO. NGOMA IKILIA SANA MWISHOWE HUPASUKA.

Nadhani ni bora kuangalia kuwa waliokufa ni watanzania wenzetu waliokuwa wakipinga ugandamizi waliouona. Hamna haja ya kukebehi kwani "ukiona mwenzio ananyolewa......"
"ukiona kwa mwenzio kunafuka moshi...."
 
Ndio demokrasia tanzania hiyo..alisema Lowassa katibu mkuu darasa la nne akapuuza..ndio matokeo hayo!
 
Kwani viongozi wa CDM walipokuwa wanawaamrisha wafuasi wao haya hawakutegemea ? wao ndio wabebe lawama kwa waliyo tokea kwa kutafuta umaarufu usio na tija. Huwezi shindana na dola, na hii imeonyesha kuwa dola ipo na inafanya kazi, next time watatia akili kichwani

Nani kakudanganya kwamba huwezi kushindana na dola? Kitu pekee usichoweza kushindana nacho ni nguvu ya umma kwa kuwa wenyewe ndio unaiweka hiyo dola!
 
Mimi naona kua Polisi hawajapigana kwa muda mrefu tokea ile vita ya Nduli Idd Amin sasa wameamua kufanya mazoezi kwenye miili ya wapenda a mageuzi na mado! Hatukubali ALUTA CONTINUE!
 
Hii habari nimeipata BBC ila imenisikitisha sana nilipoona hiyo last para ambayo ni mistali miwili hii hapa:, nikasema hata mie ningekuwa Arusha ningeshiriki kwenye Maandamano hayo kwa nguvu zote! Peoplees Powerrrrrrr!!!

The country boasts East Africa's second-biggest economy, although more than 50% of Tanzanians still live below the poverty line.


Tanzania police kill two in Arusha at Chadema protest

_49772248_010510978-1.jpg
Mr Slaa, who campaigned on an anti-corruption platform last year, is among those detained
Continue reading the main story Tanzanian officers have shot dead two people during an anti-government protest in Arusha, police say.
Nine people were injured, including three police officers, the city's police chief Tobias Andengenye said.
The unrest started after the chairman of opposition party Chadema, Freeman Mbowe, was detained, ahead of a rally against government corruption.
Police fired tear gas to disperse the crowd of several thousand people, who demanded Mr Mbowe's release.
Mr Andengenye said 49 Chadema officials were also arrested in total in the northern city.
"They overstepped the authorisation we gave them," AFP news agency quotes the police chief as saying.
"They tried to invade police headquarters to free the people who had just been arrested."
Three senior opposition leaders, including Mr Mbowe and Chadema's secretary general and presidential candidate in elections last year, Willibrod Slaa, are to appear in court on Thursday, the party's spokesman told the BBC.
President Jakaya Kikwete of the CCM was returned to office in November with more than 61% of the vote.
The country boasts East Africa's second-biggest economy, although more than 50% of Tanzanians still live below the poverty line.
 

Attachments

Wadau, hadi sasa Arusha kuna tension kubwa (kwa upande wa Polisi) wamejazana makundmakundi baadhi ya maeneo na barabara ya kwenda polisi kutoka pande zote imefungwa na kusababisha msongamano mkubwa wa magari. Kwa ujumla hali ni shwari (labda) Polisi wana taarifa nyingine za kiitelijensia za kuendelea na patrol na kuwa alert.

Mimi niliyekuwepo Mkutanoni (niliondoka baada ya mkutano) na kuondoka mara baada ya Mkutano na kushuhudia jinsi Polisi walivyokuwa wanakabiliana na wananchi, NATHUBUTU kusema nguvu ya Polisi ni ndogo mno ikiwa wananchi wataamua kusimama dhidi yao! Umati wa watu haukuwa mkubwa sana kama inavyoripotiwa na wengi tuliondoka kurudi kwenye shughuli zetu baada ya mkutano ingawa ilibidi shughuli zisimame kutokana na vurugu na uporaji ulioambatana na vurugu hizo.

Labda Polisi walitaka kujipima kama wanaweza kupambana na vurugu lakini ukweli ni kuwa uwezo wa Polisi wetu ni mdogo mno! Hawana vifaa vya kutosha, 'washawasha' lao si chochote, ni zito na halina msaada, ni heri wangenunua defender/landcruisers zaidi na pengine helkopta ya maji ya kuwasha. Plosi waliokwepo jana baddhi yao inaelekea kabixsa walitoka mikoa na wilaya za jirani ; jiulize kama Moshi, Manyara, na Karatu wangeandamana jana hali ingekuwaje?. Jana iliwalazimu Polisi kutumia pick-up za watu binafsi kubeba Polisi!

Pili; Polisi walichangia sana kuhamasiha vurugu kwani walivamia mkutano wa CDM uwanjani (walipkuwa wameruhusiwa) na kuwapiga mambomu wakati wakiomba dua zao; Je, huku si kutafuta sababu ya vurugu? Lile jengo lililoungua upande limeunguzwa na mambomu ya Polisi sina hakika sababu ni nini au ni panick ama la. Lakini ubabe na kutaka kujipima uwezo wa kudhibiti umma ndiyo umeyaleta haya na kwa mawazo ya watu wengi niliowasikia mitaani, Polisi wamejivunjia heshima sana na CCM na Serikali yake watakuwa na hali mbaya zaidi baada ya vurugu za jana.

MY TAKE
Polisi hwawezi kujinasua kutoka lawama; nina hakika kabisa kama wangekuwa hawajaweka kando busara walizokuwa nazo wakati wa kampeni ambako kulikuwa na mikutano mikubwa zaidi ya wa jana pamoja na mandamano yasiyo na kibali amayo yalifanyika sehemu nyingi nchini basi maandamano ya jana wangeya-facilitate wao wenyewe kwa kuwaongoza waandamanaji na kuwasindikiza hadi uwanjani kungekuwa shwari kuu.
 
Inaumiza sana kusikia vurugu za namna hii zikitokea sehemu (Arusha) ambayo Watanzania tumekuwa tunajivunia............kupoteza maisha (kama ni kweli) ya watu bila sababu............ni kitendo very unprofessional cha jeshi letu la polisi..........
 
hakuna aliyebeza kwa harakati zao.........dont mix mambo.
 
yana mwisho, damu hizo ni lazima zilipwe wala hazitapotea hivihivi
 
Hapa mpuuzi ni wewe Mtu wa pwani kisha Zitto na Shibuda wanakufuatia kwa upuuzi

Mtu wa pwani & Hakikwanza.
Msiwaingize Zitto na Shibuda kwenye mambo yenu ya kijinga kijinga kama hapa. Msiwaite (wabunge) kuwa ni wapuuzi ikaja kuwa nyie ndio wapuuzi. Tuongelee Arusha.
 
Serikali inayomiliki jeshi la police limeua kwa makusudi baadhi ya wakazi wa Arusha.Hili limesibitishwa na mganga wa hospital ya mkoa kua kati ya watu waliokufa wawili walipigwa risasi.Hii haina tofauti sana na mauaji yaliyotokea kenya,IveryCoast n.k.Lakini kwa nini police waue raiya ambao hawana hatia?Je kuandamana tu kunatosha kutoa uhai wa mtu?Serikali ya CCM inataka kutufikisha wapi?Wangeamua kuwaacha waandamane wapunguza nini?Wananchi wawe macho na jeshi la police,badala ya kulinda amani na uhai wa watu limeamua kuua.
 
Back
Top Bottom