Ya Polisi na vyama vya siasa Tanzania

Ya Polisi na vyama vya siasa Tanzania

Tanzanian officers have shot dead two people during an anti-government protest in Arusha, police say.

Nine people were injured, including three police officers, the city's police chief Tobias Andengenye said.

The unrest started after the chairman of opposition party Chadema, Freeman Mbowe, was detained, ahead of a rally against government corruption.

Police fired tear gas to disperse the crowd of several thousand people, who demanded Mr Mbowe's release.

Mr Andengenye said 49 Chadema officials were also arrested in total in the northern city.

"They overstepped the authorisation we gave them," AFP news agency quotes the police chief as saying.

"They tried to invade police headquarters to free the people who had just been arrested."

Three senior opposition leaders, including Mr Mbowe and Chadema's secretary general and presidential candidate in elections last year, Willibrod Slaa, are to appear in court on Thursday, the party's spokesman told the BBC.

President Jakaya Kikwete of the CCM was returned to office in November with more than 61% of the vote.

The country boasts East Africa's second-biggest economy, although more than 50% of Tanzanians still live below the poverty line.

http://www.bbc.co.uk/news/world-africa-12126861
 
"Nipigeni niueni nitakufa kwa ajili ya kutetea wananchi wengi walio maskini na wanyonge. Kama nchi imefikia hivi hali si nzuri …mnanipiga kiasi hiki wakati nimeshaawambia nina ujauzito … hakuna neno damu mliyoimwaga haitaenda bure lazima matunda yake yatapatikana, kwani wananchi watapata haki zao. Hata huyo dereva mnayemtoa sadaka damu yake haitaenda bure," Haya ni maneno ya Josephine wakati alipokuwa amesimama huku damu zikimchuruzika kutoka kichwani na kusambaa mwilini.
Maneno haya ni makali sana na yanatia simanzi. Hayatapotea bure ipo siku yataleta matunda yanayotegemewa (Democrasia na usawa).

Kweli mafisadi wa CCM na polisi wao wamechanganyikiwa. Tayari wameshaanza kumhofia 'Slaa mdogo' ambaye bado yupo tumboni mwa mama'ake (Josephine).
 
Hapa ndipo busara za Lowasa katika hile la umeya zinapoonekana.....Lowasa aliwaonya CCM na CDM kuwa wakae wayamalize kwani mvutano uliopo ungeiharibu sifa ya arusha na kuiathiri kiuchumi. Arusha inategememea sana watalii, hizi vurugu zitawafanya watalii na hata wawekezaji wengine kuanza kufikiria kutafuta sehemu nyingine, wale wenye biashara hizi wanakumbuka athari za kukosekana kwa watalii hasa hasa enzi zile za mgogoro wa uchumi......tatizo la hili ni kuwa hawa watalii na wageni wengine wataambiana arusha si shwari na ndipo hapo hofu ya Lowasa itakapokuja kuwa dhahiri.......ccm wanashindwa kukubali ukweli kuwa kwa sasa wananchi wamebalika na kile kizazi za zidumu fikra za mwenykt wa chama zimekwisha
 
Haya, dunia nzima sasa inajua Tanzania si kisima cha amani tena...


Kwani ndiyo mwanzo polisi wetu kuuwa raia katika shughuli za siasa na maandamano kwa ujumla?

Soma:
Mwaka 1993 walimwuua mwana-CUF kule Shumba Mjini, Zanzibar kwa amri ya OCD kwa kosa la kupandisha bendera ya CUF katika tawi alilolianzisha. Si OCD wal;a polisi aliyepiga risasi walipandishwa kizimbani.

Mwaka 1998 polisi waliwaua kwa kuwapiga risasi wapita njia wanne kwa maelekezo ya ofisa wa usalama. Hii ilikuwa katika vurugu za Mwembechai. ITV wanayo footage hiyo. Si polisi aliyefyatua risasi wala yule mwanausalama
walifikishwa mahakamani. Waliofikishwa mahakamani ni viongozi wa dini.

Mwaka 2001 huko Chake, Pemba polisi hao hao wa CCM waliwapiga risasi na kuwaua makumi ya wana-CUF. Hakuna polisi aliyefikishwa mahakamani kwa makosa hayo. Waliofikishwa mahakamani ni viongozi wa wana-CUF walioandamana.

Jana polisi wamewaua wanachadema wawili huko Arusha. Wanaofikishwa mahakamani ni viongozi wa Chadema.

Nawaambia CCM nchi hii si kisiwa cha amani kama mnavyopenda kuimba. Amani haiimbwi majukwaani -- inajengwa kwa misingi imara ya dhati na ya haki, si vinginevyo.

You have reached the end of your tether. Please GO, CCM, GO away before it's too late.
 
"Nipigeni niueni nitakufa kwa ajili ya kutetea wananchi wengi walio maskini na wanyonge. Kama nchi imefikia hivi hali si nzuri …mnanipiga kiasi hiki wakati nimeshaawambia nina ujauzito … hakuna neno damu mliyoimwaga haitaenda bure lazima matunda yake yatapatikana, kwani wananchi watapata haki zao. Hata huyo dereva mnayemtoa sadaka damu yake haitaenda bure," Haya ni maneno ya Josephine wakati alipokuwa amesimama huku damu zikimchuruzika kutoka kichwani na kusambaa mwilini.
Maneno haya ni makali sana na yanatia simanzi. Hayatapotea bure ipo siku yataleta matunda yanayotegemewa (Democrasia na usawa).

Duh, kumbe padri nae ameisha mpa mke wa mtu ujauzito wakati sio mkewe halali, makubwa !
 
Kwani ndiyo mwanzo polisi wetu kuuwa raia katika shughuli za siasa na maandamano kwa ujumla?

Soma:
Mwaka 1993 walimwuua mwana-CUF kule Shumba Mjini, Zanzibar kwa amri ya OCD kwa kosa la kupandisha bendera ya CUF katika tawi alilolianzisha. Si OCD wal;a polisi aliyepiga risasi walipandishwa kizimbani.

Mwaka 1998 polisi waliwaua kwa kuwapiga risasi wapita njia wanne kwa maelekezo ya ofisa wa usalama. Hii ilikuwa katika vurugu za Mwembechai. ITV wanayo footage hiyo. Si polisi aliyefyatua risasi wala yule mwanausalama
walifikishwa mahakamani. Waliofikishwa mahakamani ni viongozi wa dini.

Mwaka 2001 huko Chake, Pemba polisi hao hao wa CCM waliwapiga risasi na kuwaua makumi ya wana-CUF. Hakuna polisi aliyefikishwa mahakamani kwa makosa hayo. Waliofikishwa mahakamani ni viongozi wa wana-CUF walioandamana.

Jana polisi wamewaua wanachadema wawili huko Arusha. Wanaofikishwa mahakamani ni viongozi wa Chadema.

Nawaambia CCM nchi hii si kisiwa cha amani kama mnavyopenda kuimba. Amani haiimbwi majukwaani -- inajengwa kwa misingi imara ya dhati na ya haki, si vinginevyo.

You have reached the end of your tether. Please GO, CCM, GO away before it's too late.

Picha yaonyesha wavuta bange, na maneno yako haya uliandika wakati umeisha vuta au bado ?
 
facebook.jpg



Kibunango rekebisha hii haraka. WATU WAMEISHAPOTEZA MAISHA NA WEWE UNASEMA GOOD.
Tunakujua vilivyo, kwa hiyo na wewe ulikuwa unaomba watu wafe? Be carefull. and watch yourself. Kauli zingine zitakuponza wewe na familia yako.

Thanks Mchonga. Wasaliti kama hawa wanatakiwa wajulikane.......liangalie lilivyo desparate: he hardly earns anything kwa CCM zaidi ya kupewa vijisent vya kulewea.....
 
Ripoti laini kabisa haina hata impact yeyote !!!! nchi inaendelea tu.
 
Hivi ni kweli waliouawa katika sakata hili ni wawili tu?

Official statement ya polisi ni kuwa so far wamefariki watu wawili. Polisi walipiga risasi watu kama 10. Wawili wamekufa, wengine wako hospitali na majeraha ya risasi. Vijana waliopigwa risasi walipoenda hospitali wakaambiwa hawawezi kutibiwa bila ya fomu ya PF3 kutoka kwa polisi. Walipoenda polisi kuomba PF3 wakawekwa ndani badala ya kupelekwa hospitali. Wengi wametoka damu nyingi, walipokuwa serious ndiyo wakapelekwa hospitali. Wengine kadhaa waliopigwa risasi waliogopa kwenda kufata PF3 polisi watakamatwa.

Kuna uwezekano hii death toll ya mauwaji ya Arusha itaongezeka.
 
Hapa ndipo busara za Lowasa katika hile la umeya zinapoonekana.....Lowasa aliwaonya CCM na CDM kuwa wakae wayamalize kwani mvutano uliopo ungeiharibu sifa ya arusha na kuiathiri kiuchumi. Arusha inategememea sana watalii, hizi vurugu zitawafanya watalii na hata wawekezaji wengine kuanza kufikiria kutafuta sehemu nyingine, wale wenye biashara hizi wanakumbuka athari za kukosekana kwa watalii hasa hasa enzi zile za mgogoro wa uchumi......tatizo la hili ni kuwa hawa watalii na wageni wengine wataambiana arusha si shwari na ndipo hapo hofu ya Lowasa itakapokuja kuwa dhahiri.......ccm wanashindwa kukubali ukweli kuwa kwa sasa wananchi wamebalika na kile kizazi za zidumu fikra za mwenykt wa chama zimekwisha

Huyo ndiye muasisis wa siasa za ufisadi....hastahili sifa ya kuwa na busara hata kidogo....
 
Polisi yaua wawili Tanzania



Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Kikosi cha Kuzuia Fujo nchini Tanzania

Polisi ya Tanzania yathibitisha kuwa watu wawili wamekufa baada ya mapambano kati yake na waandamanaji wa chama kikuu cha upinzani nchini humo, Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).





Kwa uchache watu wawili wamekufa baada ya kupigwa risasi na Polisi wa Tanzania katika mji wa Kaskazini wa Arusha na wengine wengi wanashikiliwa na jeshi hilo hadi sasa.
Miongoni mwa waliokamatwa na viongozi 10 wa chama cha CHADEMA, akiwemo aliyekuwa mgombea wa urais wa chama hicho katika uchaguzi uliopita, Dkt. Wilbrod Slaa na mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, pamoja na wabunge wa eneo hilo.
Chanzo cha maandamano hayo ni kuupinga uchaguzi wa meya wa Arusha kwa madai kwamba idadi ya madiwani wanaoviwakilisha vyama vya CCM na CHADEMA inafanana ila walizuiwa kupiga kura. Mwandishi wetu wa Arusha, Nicodemus Ikonko, amekifuatilia kisa hicho na hii hapa taarifa yake.
Mwandishi: Nikodemus Ikonko
Mhariri: Josephat Charo
 
“Nipigeni niueni nitakufa kwa ajili ya kutetea wananchi wengi walio maskini na wanyonge. Kama nchi imefikia hivi hali si nzuri …mnanipiga kiasi hiki wakati nimeshaawambia nina ujauzito … hakuna neno damu mliyoimwaga haitaenda bure lazima matunda yake yatapatikana, kwani wananchi watapata haki zao. Hata huyo dereva mnayemtoa sadaka damu yake haitaenda bure,” Haya ni maneno ya Josephine wakati alipokuwa amesimama huku damu zikimchuruzika kutoka kichwani na kusambaa mwilini.
Maneno haya ni makali sana na yanatia simanzi. Hayatapotea bure ipo siku yataleta matunda yanayotegemewa (Democrasia na usawa).

Mama watalipa! mkwere na wenzako mtalipa damu iliyomwagika, haki ya mtu haipotei na damu ya mtu haiendi bure. Ndo tatizo la kuongozwa na mkwere!
 
sio kumi tena?au ndio tayari polisi washaziba mashimo.


Wawili wauwawa kwenye ghasia Arusha


100721174848_wilbroad_slaa_226x170_nocredit.jpg
Dr Wilbroad Slaa naye pia amekamatwa


Polisi wamethibitisha watu wawili wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mji wa Arusha Tanzania, kwenye makabiliano baina ya Polisi na wafuasi wa chama cha upinzani cha CHADEMA.
Ghasia zilianza baada ya Polisi kumkamata Mwenyekiti wa kitaifa wa chama hicho Freeman Mbowe na mbunge wa Arusha mjini Godbless Jonathan Lema, wakiwa wanaelekea kuhutubia mkutano wa kisiasa.
Baadaye polisi pia walimkamata aliyekuwa mgombea wa chama hicho cha CHADEMA kwenye uchaguzi wa Urais uliofanyika mwezi Oktoba, Dr Wilbroad Slaa.
Taarifa zinasema biashara kadhaa zilichomwa moto kwenye vurugu hizo.
Kwa mujibu wa waandishi wa habari mjini Arusha, Polisi walikuwa wamewakataza viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao kufanya maandamanao kabla ya mkutano wa kisiasa wa Jumatano, lakini mamia ya wafuasi wa chama hicho wakawafuata viongozi hao walipokuwa wanaelekea eneo la mkutano.
Dr. Slaa amenukuliwa akisema maandamano hayo yalikuwa ya kupinga ufisadi katika serikali mpya ya Rais Jakaya Kikwete.
Polisi walifyatua risasi hewani mara kadhaa kutoa tahadhari kwa maelfu ya wafuasi waliokwenda kutaka viongozi wao waachiwe huru, na baadaye wakafyatua gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya.
Walioshuhudia wanasema Polisi waliendelea kufyatua risasi mchana kutwa, huku wafuasi wa CHADEMA wakiendelea kukabiliana na askari Polisi katika maeneo mbali mbali ya mji wa Arusha.
Kwenye mkutano huo wa kisiasa, Dr Slaa aliwataka Polisi kumwachilia huru Bwana Mbowe na wengine, na pia akamtaka Rais Kikwete kujiuzulu.
Hadi kufikia Jumatano jioni hakuna taarifa iliyokuwa imetolewa na serikali kuhusu mzozo huo.
Kumekuwa na mvutano wa kisiasa nchini Tanzania tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Urais ambao vyama vya upinzani vinadai ulikuwa na udanganyifu.
Kufuatia uchaguzi huo shinikizo zinaendelea za kutaka Tanzania iwe na katiba mpya tofauti na iliyopo sasa, ambayo hairuhusu matokeo ya uchaguzi wa Urais kupingwa mahakamani yanapotangazwa na tume ya uchaguzi.


BBC Swahili - Habari - Wawili wauwawa kwenye ghasia Arusha
 
Hili jambo sio la kisiasa tena wala kichama ni haki ya wananchi kuujua ukweli kuhusu mauaji ya ndugu zao yaliyotokea Arusha mpaka taarifa za uhakika kabisa na ambazo hazina ubabaisha ambapo mpaka baadhi ya wanausalama wamekiri kuwa watu wameuawa na Polisi na kusababisha hasira kwa wananchi kupelekea na wao kuchukua sheria mkononi na kupelekea askari mmoja kuchinjwa na wengine wawili kupigwa mpaka kufa huku mmoja akipigwa risasi kwa bahati mbaya na mwenzake na kupoteza maisha.
Swali langu ni kwa nini serikali haitaki kusema ukweli kuhusu hili na hata kuwahonga na kuwafukuza baadhi ya waandishi wa hapa nchini kwetu ili wasitoe taarifa hizo ambazo zitaleta picha kamili nini kinatokea kwenye nchi yetu tunayosema ni ya kidemokrasia.

Na kwa nini maiti zao zinafichwa wapi na kwa nini wanaficha ukweli na hata maiti kama ni ukweli umeshajulikana muda mrefu kuwa serikali hii haikushinda zaidi ya wizi wanaficha nini tena?

HII INAUMA SANA NA WASIJIDANGANYE KUWA HALI HII IMEPOA AU ITATULIA ZAIDI WANAZIDI KUWASHA MOTO AMBAO WATAKUJA KUSHINDWA KUUZIMA.
 
JK mikono yako imetapakaa damu za watz wasiokuwa na hatia.Damu yao inakulilia popote utakapokwenda. UMEHARIBU SANA CV YAKO NA UTAENDELEA KUJICHAFUA MPAKA MWILI WAKO WOTE UTATAPAKAA DAMU, USIJE SEMA HATUKUKUONYA, ACHANA NA MAFISADI SIKIA KILIO CHA MAMILIONI YA WATANZANIA

Are you serious? JK na Mafisadi unawatenganishaje?
Pole sana!
 
Picha yaonyesha wavuta bange, na maneno yako haya uliandika wakati umeisha vuta au bado ?


Hata hivyo, kwani aliyosema ni uongo? Ni ukweli mtupu na ona nilivyomgongea!! Kazi kubwa ya CCM ni ufisadi na kubwabwaja majukwaani eti hiki ni kisiwa cha amani. Amani my foot!!!
 
Back
Top Bottom